UNYENYEKEVU.

0
5كيلو بايت

Bwana Yesu asifiwe...

Kwa ufupi.

” Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; “ Mathayo 11:29

“unyenyekevu”hali ya kushuka,kukubali kuonekana mdogo/mtumishi wa wote,kukubali lawama na kuvumilia. Si jambo jepesi kukubali kuwa chini hali wewe una vitu vingi. Si rahisi hata kidogo kukubali lawama. Wengi wanapenda wawe wanyenyekevu lakini hawapo tayari kushuka,kupokea lawama,kuvumilia n.k. Unyenyekevu ni ghalama mpendwa!

  • Unyenyekevu ni tabia ya Yesu. Yesu alikuwa ni mnyenyekevu wa moyo

Yesu alikuwa mnyenyekevu wa moyo,sio wa kuigiza. Alikuli mateso yote ingawa alikuwa na uwezo wa kuyakataa,lakini kwa kusudi la kutufundisha ilimbidi akubali na kwa lile kusudi la ukombozi,alikubali yote. Fikiri pale alipopelekwa mbele wa waashi na wakuu wa makuhani kisha wakamsomea mashtaka ya uongo,lakini alikaa kimya asitie neno lolote hali akijua yote yanayoendelea. Hakika mtu huyu alikuwa ni mnyenyekevu wa moyo. Najiuliza,sijui ungelikuwa mwenzangu na mimi,wewe hapo- ungelisemaje au ngelifanyeje pale unaposhtakiwa kwa maneno ya uongo? naona wewe ungerusha ngumi,au ungetukana sana kiasi kwamba mpaka wangelikuachia! lakini haikuwa hivyo kwa Yesu.

Yeye ambaye ndiye mnyenyekevu wa moyo,anakutaka na wewe usiyemnyenyekevu ukajifunze kwake huo unyenyekevu. Anakualika ujitie  “nira” yake kwa maana nira yake ni laini na mzigo wake ni mwepesi nawe utapata raha nafsini mwako. Neno “nira” ni kongwa,wanalovalishwa ngombe ili waweze kulima pamoja. ( ni kama mbao iwekwayo kwenye shingo zao,kufunga ngombe na ngombe na hatimaye mkulima mmoja uishika mbele na kuwapeleka popote atakapo,nao huenda.)Yesu ametumia piacha hiyo kutufundisha kama tukijifunga nira yake,tutaweza kumfuata popote aendapo,na tujifunze kwake unyenyekevu wake.

  • Kinyume cha unyenyekevu ni kiburi

Ikiwa mtu amekosa unyenyekevu huwa na kiburi,na kiburi ni tabia ya shetani mwenye kupenda kusifiwe. Wataalamu maandiko husema kwamba kila mwanadamu amezaliwa na tabia ya kiburi. Na ndio maana kila mtu hupenda kujisikia,kusifiwe,kuonekana n.k Lakini unyenyekevu hutoka kwa Bwana,mtu hazaliwi nao. Ukimwona mtu mnyenyekevu toka tumboni mwa mamaye hujue huyo kapewa “neema ” tu kwa maana si jambo la kawaida. Kwa hiyo utagundua kwamba unayo kazi ya kujifunza kila siku habari ya unyenyekevu wa Yesu ili kusudi uwe mnyenyekevu na utoke katika kiburi.

البحث
الأقسام
إقرأ المزيد
SPIRITUAL EDUCATION
TAMBUA NAFASI YAKO ULIOITIWA
Nafasi mbili za mkristo katika wokovu
بواسطة Martin Laizer 2023-09-28 05:37:50 0 5كيلو بايت
2 SAMUEL
Verse by verse explanation of 2 Samuel 13
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...
بواسطة THE HOLY BIBLE 2022-02-05 09:44:30 0 5كيلو بايت
2 KINGS
Verse by verse explanation of 2 Kings 3
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 33 questions at the...
بواسطة THE HOLY BIBLE 2022-03-19 19:18:19 0 5كيلو بايت
Networking
How to choose the right marketplace business model
To build a sustainable and successful marketplace platform, you need to find a business model...
بواسطة Business Academy 2022-09-17 03:32:43 0 6كيلو بايت
Injili Ya Yesu Kristo
HABARI ZA MWANA MPOTEVU
(A) MWANA MPOTEVU (MTOTO MDOGO)  LUKA 15;11-24 "Kulikuwa na mtu mmoja mwenye wana...
بواسطة GOSPEL PREACHER 2022-01-15 22:14:25 0 6كيلو بايت