URAIA WA MBINGUNI.

0
5K

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi;

Ni vyema tukajifunza kuhusu uraia lakini uraia wa mbinguni ambao unatofautiana na uraia tulionao sasa. Neno “raia” lina maana ya mkazi wa eneo fulani kama vile mji,kijiji,au nchi. Neno la maana hapo ni kuwa “mkazi halali wa…” Na tunafahamu haki za msingi za mtu kuwa raia halali wa eneo husika. Hata hivyo kila sehemu/nchi ina taratibu zake za kuwa raia ingawa zipo zilizo kuu ambazo hufanana fanana katika kila nchi.

  • Je uraia wa mbinguni ni nini?

Uraia wa mbinguni ni urithi wa watakatifu ambao huanzia hapa hapa duniani.Kwa maana Mungu hupendezwa na watakatifu wa Duniani (Zab.16:3Sasa watakatifu hawa pindi waendapo kwa Mungu Baba,si kana kwamba wanakwenda mbinguni kuanzisha uraia wao binafsi bali wanakwenda kurithi uraia wa mbinguni walowekewa tayari. Kumbuka hili; kuna maisha zaidi ya maisha haya. Maisha yajayo huangalia sana maisha ya sasa,kwa maana kile utakachoishi leo kitaamua maisha yako ya baadae. Fikiria wale waliomkataa Yesu leo,maisha yao ya baadae yatatofautiana na waliompokea na kumwishia.

Uraia wa mbinguni hauna mwisho wake,kwa maana kila raia anastahili kuishi milele yaani kwa muda usiokuwa na kikomo. Tofauti kabisa na uraia wa sasa,ambao unaweza kuisha muda wowote ile. Hivyo ni vyema kutamani uraia wa namna hii usiokoma. Kwa sababu hiyo,mtu anapojua thamani ya uraia wa mbinguni,basi yupo tayari hata kupoteza uraia huu wa kawaida ili kuilinda imani na apokee uraia wa mbinguni. ( Marko8:35)

Najaribu kumtafakari mtu kama Stefano ambaye alikubali kupoteza uraia wake wa kawaida kwa kupigwa kwa mawe hata kufa akisimama katika kweli /Neno la Mungu,maana bila shaka alijua kule aendako na ndio maana aliweza kuziona mbingu zimefunguka na kumwona Mwana wa Adamu amesimama amesimama mkono wa kuume wa Mungu.( Matendo 7:54-60)

  • Maisha ya kila mtu,hasa ni maisha ya umele.

Kama tujuavyo ya kwamba,duniani tupo safarini tu,na hakika tunapita. Lakini swali la msingi la kujiuliza tutakuwa wapi baada ya maisha haya kuisha? Kwa mujibu wa Neno,huonesha kwamba kuna maisha ya umilele ya baadae Luka 16:19-31,ile habari ya Lazaro na tajiri mmoja ambao wote wawili walikufa lakini stori yao ya kufa haikuishia hapo,bali tunaona mmoja akienda kwenye raha na mwingine kwenye mateso kama sehemu ya pili ya maisha yao. Huu ni mfano mzuri unaotuonesha tuna maisha mengine baada haya,kutegemea uliishi vipi,na utahukumiwa sawa sawa na ulivyoishi (Warumi 2:7)

  • Waliompokea Yesu,wakaze kwake kuna maisha mapya huko mbinguni.

Ukifuatilia mitume wa Yesu karibia wote waliuwawa wakiitetea imani ya kweli,na kulikuwa hakuna jinsi,lakini bila shaka wapo mahali salama leo. Maisha yao ya hapa duniani hayana utofauti sana na maisha yako kwa maana na wao walichaguliwa na Bwana isipokuwa wao walikaza sana hata kukataa mambo mabaya ya dunia hii,na hapo waliuwawa.

Lakini neno hili linatuhakikishia kule tuendako kama tutaendelea kuweka imani yetu kwa Kristo Yesu; “ Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; ” Waefeso 3:20 (For our citizenship is in heaven, from which we also eagerly wait for the Savior, the Lord Jesus Christ,) New King James Version (NKJV )  Neno “wenyeji wetu” ni “uraia wetu / our citizenship) Kuonesha tuna makazi mapya huko kwa Baba mbinguni. (Soma pia Yoh.14:2-3)

  • Kuna daftari la uraia.

Kama ilivyo kwenye nchi huwa kuna kitabu / documents za kutambua raia wake,na ndivyo ilivyo huko mbinguni kuna kitabu cha uzima mahali ambapo majina ya watakatifu huandikwa (Kutoka 32:31-32 huonesha kuna kitabu kilichoandikwa majina ya watu wa Mungu,waliooshwa kwa damu ya Mwana-Kondoo. Soma pia Ufunuo 20:15,Ufunuo 3:5).

  • Tiketi kubwa ya kuwa raia;

Moja ya kigezo kikubwa cha mtu kuwa raia wa nchi ni kwa kuzaliwa. Katika imani nayo iko hivyo hivyo,ili ufanyike raia halali wa mbinguni,huna budi kuokoka kwanza yaani kuzaliwa kwa mara ya pili. Kuzaliwa kwa mara ya pili,kuna kuhesabia haki bure,yaani unafanyika usiye na kosa la dhambi ya umilele. Hakuna kitu muhimu duniani kama “kuokoka” na kwa sababu shetani ni mwongo,yeye huwafunga watu wengi wasiokoke ili watumbukie kuzimu wakose uraia wa mbinguni (Yoh.3:3). “Fanya maamuzi ya kumpa Yesu maisha yako leo,uokoke.”

Căutare
Categorii
Citeste mai mult
OTHERS
UTATA KATIKA KORAN: ADAM ALIUMBWAJE?
Binadamu aliumbwa kutoka nini? Tone la Damu? Maji? Udongo? Vumbi?Jamani huu nao ni Msiba Mkubwa...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:20:59 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
MALIPIZO YA NDOA
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:40:54 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
UTHIBITISHO KUWA YESU NI MUNGU
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:47:09 0 5K
REVELATION
UFUNUO 22
Bwana wetu YESU KRISTO apewe sifa, Karibu katika mfululizo wa mwendelezo wa kitabu cha ufunuo leo...
By GOSPEL PREACHER 2021-10-30 18:55:33 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
EPUKA MOTO WA KIGENI
YALIYOMO 1. Utangulizi 2. Moto wa Kigeni 3. Hitimisho MALENGO YA FUNDISO...
By GOSPEL PREACHER 2023-06-25 01:11:44 0 8K