UMOJA

0
4K

Bwana Yesu asifiwe… Kwa ufupi; ” Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. ” Matendo 3:4

Bila shaka unakumbuka habari ya muujiza wa uponyaji wa yule kiwete tangu tumboni mwa mamaye,aliyechukuliwa na watu kisha na kumweka mlangoni mwa hekalu ili kuomba sadaka. Mtu huyu alipowaona akina Petro alitaraji kupata sadaka zao. Petro na Yohana hawakuwa na sadaka,fedha za kuwasaidia wahitaji kwa maana sio eneo lao walilohitiwa bali Bwana aliwapa kitu maalumu zaidi ya pesa,nacho ni Jina la Yesu. Kile walichonacho akina Petro na Yohana kilikuwa bora zaidi ya pesa,kwa sababu pesa hazikuwa solution/ hazikutatua tatizo la kiwete,bali zilimfanya aendelee kuomba kila siku;

Lakini kile alichopewa na Petro na Yohana kilikata kiu ya kuomba omba pesa. Hivi unajua ni vyema kumpa mtu kitu ambacho kitakata kabisa kiu ya uhitaji, Fikiria kama ndugu yako asiyekuwa na kazi na mara nyingi amekuwa akikuomba omba pesa ndogo ndogo ya kula ugali na nauli,nawe unamsaidia kila aombapo,unafikiria utamsaidia hivyo kidogo kidogo mpaka lini? kwa nini usimpatie mtaji utatue tatizo lake,ili asikujie kujie tena asije akakuchosha!!! Suluhu la kumsaidia mtu wa namna hii ni kumpa mtaji wa biashara,ili awezekuendesha biashara yake mwenyewe,“mtaji” ndio utatuzi!.

Kile alichopewa yule aliyekuwa kiwete kutoka kwa watu wengine kilikuwa kikimfanya aendelee kuwa kwenye tatizo lakini Petro na Yohana walifanikiwa kumpa mtaji katika maisha yake. Lakini kuna kitu cha ajabu kidogo kilichotamkwa na Petro na Yohana. kwa maana walisema “tutazame sisi” bila shaka maneno haya aliyasema mmoja wao,labda Petro.Kwa mujibu wa Neno,ni Petro ndiye aliyesema (Mdo 3:4).

Najiuliza kwa nini neno hili lisingelikuwa “Nitazame mimi”? Kwani kungekuwa na ubaya gani kama Petro angelisema hivyo? Lakini kwa nini kaweka wingi? Bila shaka walikuwa wawili na Yohana,lakini bado angeliweza kusema nitazame mimi. mstari huu unatufundisha “umoja ni nguvu”,Bwana anakusudia watumishi wafanye kazi pamoja,hapo ndipo kuna udhuhirisho wa kiungu wa hali ya juu kuliko mtu binafsi.

Ebu fikiria Bwana alivyoshuka kwa akina Petro na Yohana hatimaye yule kiwete akapona saa ile ile. Palipo na watumishi wa Mungu wafanyao kazi ya Mungu kwa umoja,huwa siku zote kuna upako mara dufu,na shetani analitambua hili,ndio maana tunaona leo watumishi hawataki kushirikiana pamoja,ili kuwapunguza kasi yao. Ni maombi yangu; nawe useme “tutazame sisi” kama nafasi ya kushirikiana pamoja lakini pia kama nafasi ya kukubali kile anachofanya mwenzako.

Pesquisar
Categorias
Leia Mais
Injili Ya Yesu Kristo
Ngazi ya Yakobo
Mwanzo 28:10-19 “Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani...
Por GOSPEL PREACHER 2022-03-31 14:40:12 0 6K
OTHERS
Do you think Kadhi’s courts should be part of the new Tanzanian Constitution?
The current debate is about whether or not these “Kadhi” courts should be entrenched...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 20:32:21 0 5K
NDOA KIBIBLIA
MWANAUME: SIO MKE WAKO NI WEWE
Mchungaji wangu Emmanuel Nhyama Manwele ambaye ni mwalimu wangu wa kwanza wa ndoa na maswala...
Por GOSPEL PREACHER 2021-11-08 00:15:02 0 6K
DANIEL
DANIELI 5
KUANGUKA KWA BABELI: Tukisoma katika Historia na kwenye biblia tunapata picha jinsi mji wa...
Por GOSPEL PREACHER 2021-11-05 23:50:30 0 7K
SPIRITUAL EDUCATION
KWANINI WENGINE WANYAKULIWE NA WENGINE WAACHWE
KWANINI WENGINE WANYAKULIWE NA WENGINE WAACHWE.
Por Martin Laizer 2023-10-10 18:45:10 4 7K