UMOJA

0
5KB

Bwana Yesu asifiwe… Kwa ufupi; ” Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. ” Matendo 3:4

Bila shaka unakumbuka habari ya muujiza wa uponyaji wa yule kiwete tangu tumboni mwa mamaye,aliyechukuliwa na watu kisha na kumweka mlangoni mwa hekalu ili kuomba sadaka. Mtu huyu alipowaona akina Petro alitaraji kupata sadaka zao. Petro na Yohana hawakuwa na sadaka,fedha za kuwasaidia wahitaji kwa maana sio eneo lao walilohitiwa bali Bwana aliwapa kitu maalumu zaidi ya pesa,nacho ni Jina la Yesu. Kile walichonacho akina Petro na Yohana kilikuwa bora zaidi ya pesa,kwa sababu pesa hazikuwa solution/ hazikutatua tatizo la kiwete,bali zilimfanya aendelee kuomba kila siku;

Lakini kile alichopewa na Petro na Yohana kilikata kiu ya kuomba omba pesa. Hivi unajua ni vyema kumpa mtu kitu ambacho kitakata kabisa kiu ya uhitaji, Fikiria kama ndugu yako asiyekuwa na kazi na mara nyingi amekuwa akikuomba omba pesa ndogo ndogo ya kula ugali na nauli,nawe unamsaidia kila aombapo,unafikiria utamsaidia hivyo kidogo kidogo mpaka lini? kwa nini usimpatie mtaji utatue tatizo lake,ili asikujie kujie tena asije akakuchosha!!! Suluhu la kumsaidia mtu wa namna hii ni kumpa mtaji wa biashara,ili awezekuendesha biashara yake mwenyewe,“mtaji” ndio utatuzi!.

Kile alichopewa yule aliyekuwa kiwete kutoka kwa watu wengine kilikuwa kikimfanya aendelee kuwa kwenye tatizo lakini Petro na Yohana walifanikiwa kumpa mtaji katika maisha yake. Lakini kuna kitu cha ajabu kidogo kilichotamkwa na Petro na Yohana. kwa maana walisema “tutazame sisi” bila shaka maneno haya aliyasema mmoja wao,labda Petro.Kwa mujibu wa Neno,ni Petro ndiye aliyesema (Mdo 3:4).

Najiuliza kwa nini neno hili lisingelikuwa “Nitazame mimi”? Kwani kungekuwa na ubaya gani kama Petro angelisema hivyo? Lakini kwa nini kaweka wingi? Bila shaka walikuwa wawili na Yohana,lakini bado angeliweza kusema nitazame mimi. mstari huu unatufundisha “umoja ni nguvu”,Bwana anakusudia watumishi wafanye kazi pamoja,hapo ndipo kuna udhuhirisho wa kiungu wa hali ya juu kuliko mtu binafsi.

Ebu fikiria Bwana alivyoshuka kwa akina Petro na Yohana hatimaye yule kiwete akapona saa ile ile. Palipo na watumishi wa Mungu wafanyao kazi ya Mungu kwa umoja,huwa siku zote kuna upako mara dufu,na shetani analitambua hili,ndio maana tunaona leo watumishi hawataki kushirikiana pamoja,ili kuwapunguza kasi yao. Ni maombi yangu; nawe useme “tutazame sisi” kama nafasi ya kushirikiana pamoja lakini pia kama nafasi ya kukubali kile anachofanya mwenzako.

Suche
Kategorien
Mehr lesen
OTHERS
JE, ISA NI JINA SAHIHI LA YESU WA BIBLIA?
Katika somo letu hili tutajifunza kuhusu jina sahihi la Yesu/Yashua na tafsiri yake katika...
Von MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:28:15 0 5KB
MASWALI & MAJIBU
Je! kuna dhambi kubwa na ndogo?
SWALI: Naomba kufahamu Je! Kuna dhambi kubwa na ndogo, na kama hakuna je! Mtu aliyeua na...
Von GOSPEL PREACHER 2022-06-13 00:12:35 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
Mafundisho kuhusu Uadilifu!
Andiko la Msingi: Tito 2:11-12 “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;...
Von GOSPEL PREACHER 2022-03-31 14:45:42 0 8KB
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 33
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 28 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-01-24 15:34:01 0 6KB
REVELATION
UFUNUO 20
Bwana wetu YESU KRISTO apewe sifa, karibu katika mwendelezo wa kitabu cha ufunuo, leo tukiwa...
Von GOSPEL PREACHER 2021-10-30 12:40:40 0 6KB