Yesu Kristo hajaumbwa bali alikuwepo tangu milele yote

0
5KB

Ni kweli kabisa kwamba Yesu alikuwepo tangu milele yote kabla ya kuumbwa kitu cho chote kile. Bwana Yesu kwa kauli ya kinywa chake mwenyewe anasema kwamba:

“Na sasa, Baba, unitukuze Mimi pamoja Nawe, kwa utukufu ule Mimi niliokuwa nao pamoja Nawe kabla ya ulimwengu kuwako.” (Yohana 17:5)

Neno “UTUKUFU” maana yake ni heshima, uweza, uzuri, umaarufu, nguvu, sifa na mamlaka. Mambo hayo yote Yesu alikuwa nayo kabla hata ulimwengu haujaumbwa. Yesu Kristo alikuwapo hata kabla ya kuzaliwa na Mariamu; jambo hili pia Yesu Kristo kwa kinywa Chake Yeye mwenyewe ametuthibitishia alipokuwa akiwaambia Wayahudi kwamba:

 

“Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.

 

Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo?

 

Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini Mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima Yangu. Wala mimi siutafuti utukufu Wangu; Yuko mwenye kutafuta na kuhukumu. Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akuilishika neno langu, hataonja mauti milele. Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani? Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si situ; anitukuzaye ni Baba Yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. Ibrahimu baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.

 

Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe haujapata bado miaka hamsini, nawe umemona Ibrahimu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, Mimi niko.” (Yohana 8:47-58)

 

Katika kisa tulichokisoma katika maandiko hayo (Yohana 8:47-57) tunajifunza mambo kadhaa hapo. Tumeona dhahiri jinsi ambavyo hata baadhi ya Wayahudi ilivyo wawia vigumu sana kumwelewa huyu Yesu ni nani; hata wakadiriki kusema kuwa Yesu anayo mapepo (mashetani). Hawakumwelewa kwa sababu walimtazama Yesu kibinadamu kama jinsi wao walivyo, lakini hawakujua kuwa Yesu ni alikuwepo hata kabla ya Yeye kuzaliwa na Mariamu. Huyo Ibrahimu anayeongelewa hapo ni yule ambaye habari zake tunazisoma katika kitabu cha MWANZO cha Biblia (Ibrahimu baba yake Isaka na Ishmaili). Wayahudi walishangaa; Inawezekanaje huyu Yesu aseme alimwona Ibrahimu aliyeishi na kufa miaka mingi tena zaidi ya elfu moja iliyopita, wakati huyu Yesu tumemwona utotoni mwake na hata sasa bado hajatimiza umri wa miaka hamsini? Hayo yalikuwa ni mawazo ya kibinadamu; tena inaezekana hata wewe ukawa ni miongoni mwa waliokuwa wanawaza hivyo; lakini, Yesu mwenyewe anatuthibitishia kwa kinywa Chake kwa kusema:

“...Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, Mimi niko.” (Yohana 8:58)

Pia Yesu amewaambia Wayahudi kuwa huyo ambaye wao wanamwita Mungu (YEHOVA), Yeye ndiye Baba wa Yesu; tena Yesu anamjua ingawa hao Wayahudi hawamju (Yohana 8:54,55). Vile vile tusomapo kitabu cha MITHALI tunaona habari zinazo mhusu huyu Yesu; imeandikwa kwamba:

 

“BWANA alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake. Kabla ya matendo Yake ya kale. Nalitukuka tokea milele, tangu awali, Kabla haijawako dunia. Wakati visipokuwapo vilindi nalijidhihirisha... (...I was brought forth... – NKJV)...” (Mithali 8:22-24)

Usomapo Biblia ya Kiswahili; hapo nilipoandika “...Wakati visipokuwapo vilindi NALIJIDHIHIRISHA...” utaona baadhi ya Biblia za Kiswahili zimeandika “...NALIZALIWA...” lakini maana halisi hapo ni “...I was brought forth...” ambayo tafsiri yake ni “...NALIJITOKEZA...” au “...NALIJIDHIHIRISHA...”

 

Kumbuka kuwa Wayahudi walimtambua Mungu kwa jina "YEHOVA" ambalo mara nyingi walitamka kwa kusema "BWANA." Hapo Biblia Takatifu inamtaja huyu Yesu likuwa pamoja na YEHOVA katika mwanzo wa njia za YEHOVA. Kabla ya YEHOVA kuumba cho chote (...matendo ya kale...) huyu Yesu alikuwepo. Hivyo basi; huyu Yesu alikuwapo “...tokea milele, tangu awali, Kabla haijawako dunia.” (Mithali 8:23) Neno “MILELE” maana yake ni wakati ambao hauna mwanzo wala mwisho; ni wakati usioweza kuhesabika.

 

Upo ushahidi mwingi sana ndani ya Biblia Takatifu unaotuthibitishia kuwa Yesu alikuwepo hata kabla ya kuumbwa kitu cho chote kile; kwani nao manabii pia walitabiri ujio wa Yesu ambaye alikuwepo tangu milele yote, na tena manabii hao walisema wazi wazi kuwa huyu Yesu ni Mungu. 

Rechercher
Catégories
Lire la suite
OTHERS
VLOOKUP function
Use VLOOKUP when you need to find things in a table or a range by row. For example, look up a...
Par PROSPER HABONA 2024-01-01 20:56:17 0 4KB
SPIRITUAL EDUCATION
Utakatifu ni nini kibiblia?
Utakatifu ni nini kibiblia?
Par Martin Laizer 2023-10-31 20:03:00 3 6KB
MASWALI & MAJIBU
Je! kuna dhambi kubwa na ndogo?
SWALI: Naomba kufahamu Je! Kuna dhambi kubwa na ndogo, na kama hakuna je! Mtu aliyeua na...
Par GOSPEL PREACHER 2022-06-13 00:12:35 0 5KB
HOLY BIBLE
CHAPA YA MNYAMA
CHAPA YA MNYAMA Mwinjilisti mmoja alisema kuwa kuipokea chapa ya mnyama/Alama ya Mnyama ni...
Par GOSPEL PREACHER 2021-11-05 23:36:21 0 7KB
OTHERS
NANI KAMPA UTUME NA UNABII MTUME MUHAMMAD?
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia...
Par MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 04:46:10 0 5KB