ALLAH ANASEMA KATIKA KORAN KUWA WAISLAM WOTE WATAINGIA JEHANNAM

0
7K

Jamani huu ni Msiba katika taifa la Islam kwa kushindwa kusoma aya hii ambayo ipo wazi (Quran 40:60).

Katika mada hii, nitawawekea aya kutoka Koran na simulizi za Muhammad ambazo zinatushuhudia kuwa, Waislam wote wataingia Jehanamu.

Hebu tumsome kwanza Allah katika aya aliyo iteremsha kwa Mtume wake Muhammad (Pbuh).

Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.

Mungu wa Waislam ajulikanaye kwa Jina la Allah amesema kiuwazi kabisa kuwa “wale wote ambao wanajivunia Uislam na kumuabudu Allah wataingia Motoni”


Ndugu zanguni, huu ni Msiba, tena msiba mkubwa sana katika dini na taifa la Kiislam. Allah amesha toa hukumu kwa wamfuatao na inafahamika fika kuwa, Wale wote waingiao Jehannam, hao walikuwa hawafanyi Mapenzi ya Mungu wa Biblia.  Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Huu ushaidi ndio tulio usoma katika Quran 40:60.

Sasa tuwasikilize na maswahiba wa Mtume Muhammad.

Simulizi:

Pia imesimuliwa na Ibn Jarir, iliyosimuliwa na Abu Kurayb, imesimuliwa na Ibn Yaman, imesimuliwa na Ibn Malik Maghul, imesimuliwa na Ibn Ishaq ambaye alisema, "Kila mara Abu Maysarah anapo kwenda kulala na akiwa kitandani kwake yeye husema, 'Mimi nasikia Uchungu kuzaliwa na Mama yangu. 'na kisha anaanza kulia kwa Machozi. Alipoulizwa kwa nini alikuwa akilia, alijibu ayafuatayo,' Tuliambiwa kwamba SISI WAISLAMU tutaingia Jehannamu, LAKINI HATUKUAMBIWA kwamba TUTATOLEWA HUKO JEHANNAMU NA HATUKUAMBIWA NI KIVIPI TUTATOKA HUKO'"

Mfuasi huyu wa Muhammad anaoneka kupatwa na mshtuko mkubwa, pale alipo ambiwa kuwa, Waislam wote wataingia Jehannam. Mshtuko huu umemfanya ailaani siku ambayo alizaliwa. Kitu cha kujiuliza, kwanini Allah ambaye ni mungu wa Waislam anatoa ahadi ya Jehannam na si Akhera kama wafundishavyo Waislam?

Ndugu zanguni, ningependa mfahamu kuwa, utakapo ingia Jehannam, kutakuwa hakuna tena njia nyingine ya kutoka huko. Pale Jehannam ndio mwisho wa maisha ya walio tenda dhanb. Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Je, kufanya mapenzi ya Allah ni sawa na kutenda dhanb? Je, Uislam ni dini ya haki, kama wanavyo sema wafundishaji wa dini hiyo? Jiulize tena, kwanini Allah anatoa ahadi ya Jehannam kwa wafuatayo mafundisho yake?

 

Lakini Yesu anasema haya:

Yohana 14: 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 

Ndugu zanguni, mwamini Yesu ili uwe na uzima wa milele. Yesu anakupenda. Yesu Ndie Njia Pekee. Yesu Ndie Uzima. Dini haita kupeleka kwa Baba aliye Mbingu, lakini Yesu anasema Yeye NDIE NJIA.

Mungu awabariki sana.

Căutare
Categorii
Citeste mai mult
OTHERS
Husband and wife
1 "Love your wife as Christ loved the Church." (Ephesians 5:25) Risk your life to help or save...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:54:43 0 5K
OTHERS
ALLAH NA UISLAM NI DINI YA WAFU
Ndugu msomaji, Ukisoma Biblia takatifu ambayo ndio NENO la Mungu, inasema: Mungu ni Mungu wa...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-25 11:45:06 0 7K
JOB
Verse by verse explanation of Job 34
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 23 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-03 04:14:29 0 5K
REVELATION
UFUNUO 12
MAELEZO JUU YA “UFUNUO 12” Ufunuo 12 1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni;...
By GOSPEL PREACHER 2021-10-30 11:35:41 0 5K
JONAH
YONA 1
Yona alikuwa mmoja wa manabii wa Israeli wakati wa utawala wa Yeroboamu Mfalme wa Israeli,...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-20 03:02:57 0 8K