Sadaka inayomgusa Mungu
Posted 2021-08-25 09:39:38
0
8K

Nianze kwa kuwashukuru na kuwapongeza wasomaji wa makala hii, najua kuna faida nyingi za kiroho, kihuduma na kimwili mnaendelea kuzipata kutokana na somo hili zuri tunaloendelea kujifunza. Nimekuwa nikipokea simu kutoka mikoa mbalimbali za watu wanaofaidika na somo hili la Sadaka inayomgusa Mungu, nataka nikuhakikishie tena kwamba, ukimtolea Mungu kwa uaminifu na moyo wako ukawa safi mbele zake, hakika utabarikiwa. Fuatana nami tena leo tujifunze kuhusu Zaka na Aina mbalimbali za matoleo.
ZAKA NA AINA MBALIMBALI ZA MATOLEO/SADAKA.
Malaki 3:8 “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.”
Katika andiko hili tunaona Mungu anatofautisha Zaka na Dhabihu.
Kwa hiyo sisi ni mawakili wa Mungu hapa duniani, kazi ya wakili ni kuwakilisha na kusimamia mali za mwenye mali. Mungu ameweka utaratibu wa kutumia mali alizotukabidhi, Asilimia kumi( 10%) amesema tusiitumie bali tuipeleke kwake ikiwa kamili, na asilimia tisini (90%)amesema tuitumie kwa kutoa dhabihu(matoleo mbalimbali) na matumizi yetu. Wakili anapaswa kuwa mwaminifu sana 1 Wakorintho 4:2 “Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.” Tuwe waaminifu kwa kuheshimu utaratibu aliouweka mwenye mali.
Tuanze kujifunza Zaka / Fungu la kumi.
Malaki 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Zaka ni sehemu ya kumi ya mapato yako yote ya pesa, mifugo, mazao nk. Mara nyingi nakutana na maswali haya yafuatayo kwa habari ya zaka
Katika andiko hili tunaona Mungu anatofautisha Zaka na Dhabihu.
- Zaka ni sehemu ya kumi ya mapato yetu yote.
- Dhabihu ni jumla ya sadaka/matoleo mengine mbalimbali.
Kwa hiyo sisi ni mawakili wa Mungu hapa duniani, kazi ya wakili ni kuwakilisha na kusimamia mali za mwenye mali. Mungu ameweka utaratibu wa kutumia mali alizotukabidhi, Asilimia kumi( 10%) amesema tusiitumie bali tuipeleke kwake ikiwa kamili, na asilimia tisini (90%)amesema tuitumie kwa kutoa dhabihu(matoleo mbalimbali) na matumizi yetu. Wakili anapaswa kuwa mwaminifu sana 1 Wakorintho 4:2 “Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.” Tuwe waaminifu kwa kuheshimu utaratibu aliouweka mwenye mali.
Tuanze kujifunza Zaka / Fungu la kumi.
Malaki 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Zaka ni sehemu ya kumi ya mapato yako yote ya pesa, mifugo, mazao nk. Mara nyingi nakutana na maswali haya yafuatayo kwa habari ya zaka
- Je kama mimi nimeajiriwa natakiwa kutoa zaka ya mshahara kabla ya makato au baada ya makato? Jibu ni kwamba zaka unapaswa kutoa ya mshahara wote kabla ya makato. Yale makato ni matumizi yako ila tu wanakusaidia kukulipia hayo matumizi kwa kukata mshahara wako
- Je zaka ni pesa tu au hata vitu vingine? Jibu ni kwamba mapato yako yote mfano mazao, mifugo nk unapaswa kuvitolea zaka kamili.
- Je kama ni mwanafunzi /mwanachuo nimepewa ada kamili nikalipe, nayo niilipie zaka? Jibu ni hapana maana ada umepewa tu upeleke, hiyo siyo pato lako.
- Je kama nimechukua mkopo kwa ajili ya biashara niutolee zaka ule mkopo kabla ya kuanza biashara? Jibu ni ndiyo, hii itakusaidia ili Mungu aibariki biashara yako na baadae uendelee kutoa zaka ya faida unayopata kila siku.
- Je pesa ninazopata nje ya mshahara nazo nazilipia zaka? Jibu ni ndiyo maana hayo pia ni mapato yako.
- Je zaka ilikuwa kipindi cha sheria tu? Jibu ni kwamba Ilianza kabla ya sheria
Mwanzo 14:20
Iliendelea kutolewa wakati wa sheria
Inaendelea hata sasa wakati wa Agano jipya.
Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote. Yakobo aliahidi kutoa zaka kabla ya sheria Mwanzo 28:22, na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Iliendelea kutolewa wakati wa sheria
Mambo ya Walawi 27:30 “Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana. Malaki 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu…”
Inaendelea hata sasa wakati wa Agano jipya.
Mathayo 23:23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Mafarisayo walitoa zaka ila kosa lao waliacha mambo ya adili, rehema na imani ndio maana Yesu anawaambia waendelee kutoa zaka bila kuacha mambo makuu ya sheria. Unapotoa zaka leo hakikisha na moyo wako umeutoa kwa BWANA.
Wiki ijayo tutajifunza sababu za kulipa zaka, mahali sahihi pa kupeleka zaka yako na faida utakazopata kwa kuwa mwaminifu katika kulipa zaka, kisha tutachambua aina mbalimbali za matoleo (dhabihu).
Wiki ijayo tutajifunza sababu za kulipa zaka, mahali sahihi pa kupeleka zaka yako na faida utakazopata kwa kuwa mwaminifu katika kulipa zaka, kisha tutachambua aina mbalimbali za matoleo (dhabihu).
Bila shaka mpaka sasa umeshajifunza mambo ya kuzingatia kabla ya kutoa sadaka. Maana tuliona moyo wa mtoaji jinsi unavyopaswa kuwa ili sadaka yake imguse Mungu, pia tukajifunza sadaka iweje ili imguse Mungu. Ni muhimu sana kwa mtoaji yoyote kuzingatia haya maeneo mawili yaani moyo wako na Sadaka unayotoa vipate kibali mbele za BWANA. Sasa fuatana nami tena leo ili tujifunze kipengele kingine cha sadaka inayomgusa Mungu.
KWA NINI TUNAMTOLEA MUNGU?
A. Tunamtolea Mungu kwa sababu tunampenda.
B. Tunatoa kwa sababu ni agizo.
C. Tunatoa kwa sababu sadaka ni Hitaji la Madhabahu.
KWA NINI TUNAMTOLEA MUNGU?
A. Tunamtolea Mungu kwa sababu tunampenda.
Upendo huu ni lazima uwe wa Agape (Upendo wa Ki-Mungu), huu ni upendo usio na ubinafsi, usiojali mambo yako mwenyewe, usio na madai ya tamaa kwamba natoa ili nami nipate kitu kwake. Upendo huu utakusukuma kumtolea Mungu kwa sababu tu unampenda.
Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee… Kilichomsukuma Mungu kutoa ni Upendo, nah ii kwa sababu Alama kubwa ya Upendo ni kutoa.
B. Tunatoa kwa sababu ni agizo.
Kutoka 34:20b, Wala hapana atakayehudhuria mbele zangu mikono mitupu. Malaki 3:8-10, Tumeagizwa kupeleka zaka na dhabihu ili kiwemo chakula nyumbani mwa BWANA. Kwa kuwa sisi ni mawakili wa Mungu hapa duniani tunapaswa kuwa waaminifu sana mbele zake maana yeye ametukabidhi vyote ili tuvitumie kwa utaratibu aliouweka yeye mwenyewe.
C. Tunatoa kwa sababu sadaka ni Hitaji la Madhabahu.
Mwanzo 8:20, Nuhu akamjengea BWANA Madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi…akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. Nuhu alipojenga tu madhabahu ilibidi atoe dhabihu katika hiyo Madhabahu ya BWANA. Madhabahu yoyote inadai vitu vitatu:
D. Tunamtolea Mungu ili kuonyesha shukrani zetu mbele zake.- Dhabihu (Sadaka)
- Ibada
- Maombi.
Zaburi 116:12-14 “Nimrudishie BWANA nini kwa ukarimu wake alionitendea…”Ni mengi mno ametutendea BWANA kwa hiyo tunapaswa kumshukuru kwa sadaka zetu. Kumbuka vyote tulivyo navyo ni yeye ametupa, ndio maana hata tukifa hatuwezi kwenda navyo.
Zaburi 92:1a “Ni neno jema kumshukuru BWANA” Tunapaswa kujizoesha kumshukuru Mungu mara zote kwa kutoa mali/pesa ili kuonyesha kufurahia yale anayotutendea. Kwa mfano amekupa afya, mume, mke, watoto, kazi, umefaulu masomo, huduma yako imepata kibali, umenunua gari, umejenga nyumba nk. Hakikisha unamtolea BWANA sadaka ya shukrani.

Kama wakristo tunampenda Mungu, na tunatoa kwa sababu ni agizo, Tunatoa kwa sababu sadaka ni hitaji la Madhabahu, pia tunatoa ili kuonyesha shukrani zetu kwa Mungu. Sasa ngoja tujifunze Makundi ya watu katika kutoa sadaka. 2 Wakorintho 9:7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
Fuatana sasa nami tuone Makundi sita ya watu katika kutoa sadaka.
A. Wanaotoa kwa kulazimishwa/ kwa sheria
B. Wanaotoa kwa kufuata mkumbo/ kufuata bendera.
C. Wanaotoa kumpa Mungu rushwa.
D. Wanaotoa kwa bajeti.
E. Wanaotoa kwa kujihurumia.
F. Wanaotoa kwa kuongozwa na Roho na kulitii Neno sawa sawa.
Katika haya makundi sita tuliyojifunza, ni kundi moja tu la sita ambalo utoaji wake unamgusa Mungu daima, hiyo nakushauri ndugu msomaji wa makala hii unapotoa sadaka hakikisha upo katika kundi la sita la kutoa kwa kuongozwa na Roho na kulitii Neno sawa sawa. Uwe na moyo safi mbele za Mungu kisha utoe sadaka iliyo Bora (Ya thamani) ili sadaka yako imguse Mungu.
Kumbuka: Kanuni ya maisha ni kutoa, huwezi kuishi bila kutoa. Usipozitoa kwa Mungu lazima tu utazitoa mahali pengine kama Hospitali nk.
Mungu akubariki
Fuatana sasa nami tuone Makundi sita ya watu katika kutoa sadaka.
A. Wanaotoa kwa kulazimishwa/ kwa sheria
Hawa huwa hawatoi sadaka mpaka walazimishwe, labda mpaka Mchungaji au Mzee wa kanisa asimame awafungulie maandiko mengi, awaambie wasipotoa hawatabarikiwa, watalaaniwa hapo ndipo utaona wanainuka kwa shingo upande kwenda kutoa sadaka. Watu wa kundi hili ikitokea wamechelewa ibadani na sadaka imeshatolewa hawaumii moyoni ila wanashukuru maana hawatatoa sadaka siku hiyo. Lakini pia ndio waanzilishi wa manung’uniko wakidai sadaka/michango imekuwa mingi sana. Hawa utoaji wao kamwe haumgusi Mungu.
B. Wanaotoa kwa kufuata mkumbo/ kufuata bendera.
Hawa huwa hawatoi sadaka mpaka waone mwingine anatoa. Wakati wa kutoa sadaka yeye haendi haraka kutoa ila anaangalia kwanza kama akiona wote wameenda kutoa amebaki yeye peke yake ndipo naye ataenda, ila akiona katika mstari wake aliokaa kuna wengine hawajaenda kutoa sadaka naye haendi hata kama anayo sadaka. Kwenye michango/ahadi mbalimbali hawezi kuahidi mpaka aone wengine wote wameahidi amebaki yeye tu.
C. Wanaotoa kumpa Mungu rushwa.
Hawa hawatoi mpaka wamebanwa kwenye kona Fulani ya matatizo. Ukimwona mtu wa kundi hili anatoa sadaka na analeta zaka ujue kuna mahali amebanwa na tatizo labda ugonjwa, matatizo kazini na hali imekuwa mbaya sasa anatoa kumpa Mungu rushwa ili amtoe katika tatizo hilo. Akishatoka kwenye hilo tatizo hutamwona tena akileta zaka wala dhabihu mpaka akibanwa tena.
D. Wanaotoa kwa bajeti.
Watu wa kundi hili sadaka zao huwa hazibadiliki, wanaweka bajeti ya sadaka kwa mwaka na inagawanywa kwa kila jpili kwa hiyo hata Roho akishuka vipi kwenye ibada bado hawezi kuongeza kiwango cha utoaji maana tayari iko kwenye bajeti ya mwaka. Anaweza kuamua labda 20% ya mshahara wake ni sadaka ya mwezi kwa hiyo ataigawa kwa familia kwa mwezi mzima. Huu ni utoaji wa bajeti ambao ni hatari maana unamwekea Roho Mtakatifu mipaka.
E. Wanaotoa kwa kujihurumia.
Hawa wanatamani kanisa zima lijue kwamba wana matatizo mengi kwa hiyo hata wakati wa kutoa sadaka au michango mbalimbali wao wasitoe. Wanajihurumia na wanapenda pia watu wawahurumie. Fahamu zao zimejengwa kupokea/kupewa misaada tu. Wakisikia kuna michango kanisani wanajitenga wakidhani kwamba haiwahusu maana hata kanisa linajua kwamba hawana uwezo. Watu wa kundi hili hawawezi kamwe kubarikiwa kwa sababu Biblia inasema wazi kwenye Mdo 20:35 “…Heri kutoa kuliko kupokea”. Ni ukweli usiopingika kwamba Maskini yeyote anayetaka kuwa tajiri ni lazima awe mstari wa mbele KUTOA.
F. Wanaotoa kwa kuongozwa na Roho na kulitii Neno sawa sawa.
Kundi hili ndilo ambalo utoaji wake unamgusa Mungu daima kwa sababu zifuatazo:
NB- Wanatoa kwa Moyo wa kupenda/ moyo wa furaha na kuchangamka 2Kor 9:7 “…Si kwa huzuni wala si kwa lazima…” 1 Nyakati 29:9 “Ndipo hao watu wakafurahi kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe…” Wanatambua kuwa kila walicho nacho ni mali ya BWANA.
- Wanatoa kilicho Bora zaidi. Mwanzo 4:4 Habili alitoa wanyama walionona. Mwanzo 8:20 “Nuhu…akatwaa katika kila mnyama aliye safi na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka…” Luka 21:1-4 “…Hakika nawaambia huyu mjane maskini ametoa zaidi kuliko wote…” alitoa sadaka iliyo bora, yenye thamani kulingana kiwango cha mapato yake, isiyo kilema.
- Wanatoa kwa moyo safi (Hakuna hila wala manung’uniko ndani yao). Kabla ya kutoa sadaka mioyo yao imeshaunganishwa na madhabahu ya Mbinguni. Mwanzo 22:12 Ibrahimu alikuwa na moyo wa kumcha Mungu hata kabla ya kumtolea Mungu sadaka
Katika haya makundi sita tuliyojifunza, ni kundi moja tu la sita ambalo utoaji wake unamgusa Mungu daima, hiyo nakushauri ndugu msomaji wa makala hii unapotoa sadaka hakikisha upo katika kundi la sita la kutoa kwa kuongozwa na Roho na kulitii Neno sawa sawa. Uwe na moyo safi mbele za Mungu kisha utoe sadaka iliyo Bora (Ya thamani) ili sadaka yako imguse Mungu.
Kumbuka: Kanuni ya maisha ni kutoa, huwezi kuishi bila kutoa. Usipozitoa kwa Mungu lazima tu utazitoa mahali pengine kama Hospitali nk.
Mungu akubariki

Search
Categories
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Read More
The Deity of the Holy Spirit
Christianity has traditionally taught that the Holy Spirit is the third Person or Hypostasis of...
Verse by verse explanation of 1 Samuel 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 44 questions at the...
Verse by verse explanation of Judges 16
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 40 questions at the...
MUHAMMAD AKIRI KUWA ALLAH SIO MUNGU WA KWENYE INJIL NA TAURAT BALI NI MUNGU WA KIPAGANI
Je, Wakristo na Waislam, wanaabudu Mungu mmoja?Je, Allah ni Mungu wa Kipagani?Ndugu wasomaji, kwa...
JINSI YA KUISHINDA DHAMBI JUMLA
Kubali Kwamba Umeitenda Hiyo Dhambi, Na Usijaribu Kutafuta ANDIKO LA KUJIHAMI, Au MTU WA...