MAPEPO (MAJINI) NI NINI HASA?

0
6KB
SEHEMU YA KWANZA
Somo:MAPEPO
Lengo Kuu: Kujua mapepo na kazi zake.
Lengo Mahsusi: Kujua namna ya kuzishinda roho za kipepo na kazi zake.

MAPEPO
Ni roho chafu, roho za mashetani, ziwaingiazo watu ili kuwatesa kwa magonjwa na mateso anuwai.
“Naye Yesu akisha kuona kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi,mimi nakuamuru mtoke huyu, wala usimwingie tena”(Marko 9:25) pia (Mt 4:24 &7:22).

Sifa kuu ya Mapepo ni kuwa, hayana umbo, nyama wala mifupa. Ni roho, na roho haiwezi kuwa na mwili wala mifupa (Luka 24:39)”....ni shikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili wala mifupa...” Isipokuwa, Huweza kuingia ndani ya mwili wa kiumbe hai na kuvaa umbo na sura yake.


Kumbuka: Hii ziyo mizimu au Roho za wafu. Mtu akishakufa, roho yake haina uwezo wa kurudi duniani. Usidanganyike. Fuatilia kisa cha tajiri na masikini, roho ya tajiri haikuweza kurudi duniani. (Luka 16:27-31)
Wala, roho hizi(mapepo) siyo malaika walioasi, kwa kuwa wao wametekwa na tayali wako kwenye kamaba zao wakingoja siku ya hukumu (Yuda 1:16,2Petro 2:4)


Swali: Je, mkuu wa mapepo ni nani? Ili kupata jibu fuatana nami.....


Biblia katika kitabu cha Marko 3:22, imeeleza wazi, aliye mkuu wa mapepo. Naye ni Beelzebuli. Hili ni dhahili, kuwa huyu ndiye mkuu wa mapepo na ndiye pepo mkuu.


Je, mapepo yanamfahamu Mungu, yanamchukuliaje?Mepepo yanafahamu fika kuwa Mungu yupo. Tena yanajua kuwa Mungu anauwezo na nguvu zaidi yao, ndiyo maana humwogopa. (Yakobo 2:19).”Wewe waamuni ya kuwa Mungu ni mmoja; watenad vema.mashetani nao wanaamini na kutetemeka”


Kama vile mapepo yanavyomogopa Mungu na hata kutetemeka, kadharika mtu asiye na roho wa Mungu, huyaogopa mapepo. Je, hujaona mtu anaogopa kulala peke yake ndani, pengine hata mchana huogopa kubaki nyumbani peke yake wengine wanapokuwa hawapo? Hata wanafunzi wa Yesu, kabla ya kumpokea Roho Mtakatifu, walikuwa waoga juu ya pepo. (Mathayo 14:26,Luka 24:37). Hivyo, watu wote, wanapaswa kuokoka na kupokea nguvu ya Roho mtakatifu ili kuwashinda mapepo na kazi zao zote.
Zingatia hili, mapepo yananao uwezo wa kutenda miujiza kupitia watu, vitu na hata wanayama ili kuwadanganya watu na miujiza yao ya uongo (Ufunuo 16:14).


Hakika, kazi za mapepo zikidhibitiwa vilivyo, kazi zote za adui/ shetani zitakuwa zimeshindwa na maangamizi yote ya kipepo hayatapata nafasi tena. Amen.


SEHEMU YA PILI
Somo: Mapepo ni nini?
Lengo Kuu:Uhusiano Baina ya Mtu na mapepo

Lengo Mahsusi: Kujua namna ya kuzishinda roho za kipepo na kazi zake.

Uhusiano Baina ya Mtu na mapepo.

Bwana Yesu asifiwe sana,
Ndugu zangu wapendwa, karibu katika mwendelezo wa somo letu. Katika sehemu iliyotangulia, tulijifunza dhana ya pepo, asili na mkuu wa mapepo. Pia, tuligusia kwa ufupi juu ya utiifu wao juu ya Mungu na hatua ya kuchukua ili kukabiliana na uhalifu unaoendelezwa na mapepo kupitia maombi, toba na kulishika neno la Bwana.
Ndugu mpendwa, katika sehemu hii, tutachunguza Uhusiano uliopo baina ya mtu/binadamu na mapepo.
Tunaposema uhusiano katika muktadha huu, tunamaanaisha, vitu vinavyoweza kumkutanisha mwanadamu na pepo/ roho wabaya.
Yafuatayo ni baadhi ya maeneo yanayoweza kuwakutanisha binadamu na mapepo:-
(a) Sadaka- mwanadamu katika kukamilisha ibada zake, huweza kujikuta anatoa sadaka kwa mapepo. Tukio hili huweza kudumisha uhusiano baina yake na pepo. Zoezi hili, linafahamika sana kama tambiko, amabapo zawadi za wanyama, pombe, mazao mbali mbali na pesa pia hutolewa kwaajili ya masuala ya kiibada.
Sambamba na hili, wakuu wa ibada hizi, hujihusisha na shughuli za uaguzi, uganga, utabili na kubashiri,ramuli n.k.
Kwakufanya ibada hizi,mwanadamu hujifungamanisha na mapepo/ roho wachafu na kuongozwa nao.
Mara nyingine, watu hufanya ibada hizi wakidhani wanamwabudu Mungu na sadaka hizi wanamtolea Mungu, kumbe siyo kweli (Kumbukumbu la Torati 32:17).

Ndugu zangu, ibada hizi ni machukizo kwa Mungu na hapendezwi nazo. Mungu huchukia ibada hizi, yeye hafurahii ibada za namna hii kwakuwa ni ibada za mashetani.(1Wakorintho 10:20-30)

(b) Dhambi na Upagani- huu ni mlango mkuu wakuwanganisha watu na mapepo. Watu wengine hudhania kuwa wapagani hawatahukumiwa, ndugu yangu hukumu ipo tuu, ili mradi tu wewe ni binadamu, lazima hukumu ipo. Kujitenga na Mungu kwa kutenda dhambi adhabu yake ni hukumu, na hata mpagani atahukumiwa kwa dhamili yake. (1Timotheo4:1&2). Ndugu mpendwa, kubali leo umpokee Yesu, awe Bwana mwokozi wako, uwe huru.

(c) Kutii mafundisho ya uongo- mafundisho ya uongo ni yote yanayoenda kinyume na mwongozo wa Mungu. Kwa kuyatii, basi ni dhambi, na hukumu ya dhambi ni mauti. Kutolifata neno la Mungu kama lilivyo ni kufuata mafundisho ya uongo. Ndugu, tambua ya kuwa neno liko wazi na limefunuliwa kwa wote, hakuna atakayesema hakujua. Kila kona leo, kuna dini nyingi amabazo nyingine, hazifundishi kweli ya Mungu kama ilivyo, jiepushe na kujitenga na roho hizo, (1Timotheo 4:3-5).

(d) Kuyafuga- hii ni hali ya kukaa nayo. Njia hii, hutumiwa aidha kwa woga au kwa kuyapenda. Ndugu, hakuana urafiki kati ya pepo na mwanadamu. Daima lengo la pepo ni kuharibu na kuua. Kuna watu wanafuga mapepo, wengine wanayatumia kiganga, wanapagawa mapepo n.k. hili hufanaya roho hizi zifanye masikani ndani ya mtu, ndani ya uzao wake, mali, shamba na ahata mifugo (Mathayo 8:30-32).

Ndugu mpendwa, Kwa kuyapa nafasi mapepo kuwepo katika familia yako, hutoa mwanya wa kuitesa familia kizazi hata kizazi. La msingi hapa ni kuziamuru hizi roho ziondoke katika familia yako. Omba kwa vita na kukemea, ujitenge, uitenge familia yako, uzao wako, mali zako, shamba, biashara, mifugo na kila kitu, kiwe huru. Kikabidhi mikononi mwa Mungu awe Bwana na Mlinzi wako na kila kitu chako.

Sehemu ya TATU

 Somo: MAPEPO

Mada ndogo: “Mtu anawezaje kupata mapepo”
Lengo kuu: kuzijua mbinu zamapepo na kujilinda nazo

Lengo mahsusi: kudumu katika maombi ya vita kuzipinga roho za kipepo.
Ksms tulivyokwisha kuona kuwa pepo ni roho wachafu wasio na mwili wala umbo wenye uwezo wa kuingia ndani ya kiumbe hai na kuchukua umbo na sura ya kiumbe huyo,pamoja na namna mwanadamu anavyoweza kujikuta katika uhusiano na pepo kupitia ibada9 za sanamu, sadaka, kuyafuga n.k. hapa tutaendelea kujifunza juu ya habari hizi ambazo kila mtu ni vema akizijua.
Wakati mwingine, mtu huweza kujikuta katika hali ya kuvamiwa bila yeye kujua. Ndugu yangu mpendwa, kuvamiwa na pepo si mpaka uugue au ujisikie kuwa dhaifu, pepo huweza kuharibu vitu vyako pole pole, mtu aliyevamiwa na pepo, anaweza kumvuruga awe na hasira tu, asifanikiwe katika shughuli zake tofauti kama vile biashara,masomo, kazi ya ajira, ufugaji,kilimo n.k.
Mtu aliyefungwa kwa namna hii, huambiwa kuwa nyota yake imechukuliwa, na hapa ndipo waganaga wa kienyeji na waaguzi husema kuwa umetupiwa mikosi au mizimu imekasirika na kupaswa kutaaswa kwa kuogeshwa dawa,kuchanjwa au kunyweshwa; hatua hii ni hatari sana, kwa humfanya mwanadamu aingie mikataba mingine na mapepo, na hii huwa ni njia ya moja kwa moja, baada ya kipindi fulani, ile hali ya zamani hujirudia na kulazimika kwenda kwa mganga tena ili kukupatia dawa kali zaidi, bila kujiujua unakuwa unafanya mikataba migumu zaidi na kuzidi kuangamia; utakuta mtu anapewa miiko mikubwa mikubwa ambayo haitekelezeki na mwisho wake mtu huyu anakuwa mtumwa na miiko ya kipepo na anapoivunja basi humwangamiza kabisa.
Mpendwa, dawa iko kwa Yesu, jislaimishe leo uwe huru. Yeye pekee ndiye anayeweza kukuweka huru, ndiye anayeweza kuisafisha nyota yako, ndiye anayeweza kukuinua, njoo kwake leo, usikubali kudanganywa,Yesu ndiye yote ndani ya yote. Haleluya.
Zifuatazo ni njia kuu tano za mtu kupatwa na mapepo;-
(a) Kuabudu miungu- hizi ni ibada zinazofanywa katika madabahu ya shetani. Ibada juu ya mizimu, wafu, kuyaomba mali majini,kutaka ushirika na shetani ili kufanikiwa na ibada zote za namna hii. Kwa kufanya ibada hizi, hujitenga na MUNGU hivo kuwa na ushirika na shetani (1Wakorintho 10:20-22)
(b) Kwa matendo maovu ya mwili- mtu aliyetawaliwa na nguvu za mwili/ hisia, hawezi kuwa na ushirikana MUNGU kwa kuwa, mwili siku zote hupambana na roho. Mtu aliyetawaliwa na matdndo ya wili (Wagalatia 5:19-21) hawezi kumpendeza MUNGU kwa kuwe yeye huongozwa na tamaa za mwili wake wala hayuko tayali kuongozwa na ROHO wa Mungu. Hii ni pamoja na uzinzi,uchawi,ulevi,ulafi na ibada zote za sanamu.
NB; Matendo ya mwili- ni matendo maovu yote yaliyo kinyume na sheria ya MUNGU, ambayo watu ambao hawajakombolewa, hutawaliwa nayo kama dhambi ya asili. Ni lazima kuitubu ili uwe salama. Kumbuka, watu waliozoea kufanya dhambi, huweza kupagawa na pepo (Yohana 5:14)
(c) Kwa kuzifuata DINI za Uongo- hizi ni dini za kiudanganyifu, imani zisizoieleza kweli ya MUNGU. Imani zilizokinyume na wokovu kamili kupitia YESU KRISTO. Ni muhimu kujiepusha na imani/dini hizi ili uwe salama. Dini zakiudanganyifu zipo nyingi na zimekwishashika hatamu (Ufunuo12:9, 1Wathesalonike 3:5). Ni vema kuitafuta iliyo imani ya kweli na kuifuata, usiseme mimi nimekulia katika dini fulani, hivyo hii ndiyo dini yangu, hapana, dini haitakupeleka popote, kikubwa ni wokovu kamili ili ufike mbinguni.
(d) Kutokusamehe- hii ni hali ya kutokuachilia, hali ya kulipiza kisasi. Mpendwa, mtu wa kisasi, hawezi kuurithi ufalme wa Mungu, kwa maana mtu ambaye hayuko tayali, hatasamehewa pia dhambi zake. Mtu aliyefungwa na roho ya kutokusamehe, adui humpandikizia watesaji (Mathayo 18:34&35) hizi ni roho za kumkumbusha maovu yote aliyotendewa ili ahisi uchungu rohoni mwake, ashindwe kusamehe.
(e) Mtu asiye na neno- kukaa bila kusoma neno la Mungu na maombi pia, humpelekea mtu kuwa mtupu, hivyo kufanyika masikani ya adui/ibilisi au makao ya pepo (Mathayo 12:44).

Ni vema kudumu katika sala na kuomba na kusoma neno ili usiwe mtu, bali Roho wa Mungu afanye makaondani yako. Mtu wa Mungu kamwe si mtupu, huongozwa na kujazwa kwa Roho wa Mungu siku zote.
Ndugu yangu mpendwa, jitahidi sana kuweka utaratibu wa kuwa na muda wa kwenda mbele za Mungu kwa sala na maombi kila siku. Hii itakusaidia kuwa karibu na Mungu zaidi. Kumbuka, unavyomkaribia Mungu, ndivyo unavyozidi kuwa mbali zaidi na shetani.(Yakobo 4:8).

SEHEMU YA NNE

 Somo:MAPEPO

Mada Ndogo: Dalili 10 za mtu mwenye mapepo.
Lengo kuu: kuyajua mapepo na kazi zake.
Lengo Mahsusi: Kila mtu kuweza kumpinga pepo na kazi zake zote kwa 


Jina la Yesu.
Bwana Yesu asifiwe sana,
Ndugu mpendwa, katika sehemu tatu zilizotangulia,tumejifunza maana,asili/ chanzo cha ,mapepo. Natumai umebarikiwa sana. Haleluya! Ndugu mpendwa, napenda kukukarisha katika mwendelezo wa mafundisho yetu juu ya mapepo,ambapo kwasasa tutaangalia kwa kina tabia/dalili za mtu aliyevamiwa na mapepo.
Ni muhimu sana kujua hili. Tabibu mzuri, ni yule anaetibu ugonjwa anaoufahamu, hivyo ni muhimu sana,kujifunza habari hizi,ili kuweza kukabiliana na kila hali kwa usahihi wake.
Pamoja na dalili nyingine ambazo sitazitaja; kwapamoja tuzichunguze hizi zifuatazo:-
(a) Kuwa na nguvu nyingi. Kwa hali isiyo ya kawaida,mgonjwa aliyedhoofu na pengine kulala kwa muda mrefu akiwa hajiwezi, huweza kuwa na nguvu nyingi sana na za ajabu. (Luka 8:28,Marko 5:3&4,Luka 8:29,Matendo 9:15&16). Mtu huyu, huweza kuwa mkali sana,mgomvi na wakati mwingine huweza kuwa na uvutano kama umeme/shoti. Hujiamini sana,na hukasirika zaidi anapowaona wanamaombi.
(b) Kujaa ujasili na kujiamini kupita kiasi. Mtu aliyevamiwa na pepo wachafu,hujiamini na kujiona shujaa; tukio hili hulenga kumchosha mwili,kuwaumiza wanaomuuguza na yeye mwenyewe. Anaweza kujiangusha bila sababu,kujiuma meno,kutafuna baadhi ya sehemu zake za mwili,kujipiga,kujiuma meno,kujikatakata n.k. (Mathayo 17:15,Marko 5:5). Pia,mapepom hutumia njia hii ili watu wamwogope washindwe namna ya kumsaidia mtu wa namna hii kwa kuhofia usalama wao, na kubaki kumwonea huruma tu.
(c) Huonesha maumivu hata anapojiumiza mwenyewe ila haachi kujiumiza. Hili hutokana na kuwa yeye hajitawali,bali hutawaliwa na kuongozwa na pepo wabaya. Huumizwa sana ndani kwa ndani,ila hulazimika kuendelea kufanya kile kitu kinachomuumiza. Mfano, kujikatakata,kujiangusha, kurukaruka n.k. (Marko9:20-22).
(d) Kutokwa povu mdomoni na kuzilai. Mtu aliye na mapepo,anakawaida ya kupoteza fahamu. Aghalabu, hutokwa povu mdomoni anapokuwa hajitambui (Marko9:20). Tukio hili,huwa ni lakumfanyia mazoezi mtu huyu katika maandalizi ya kumuua. Humhamisha kimazingara na kuanza kumchezea, wakati wingine mtu huweza kufa mara moja. Kifo cha namna hii,huwa si kifo halisi,bali huwa amahamishwa kimazingara/uchawi.
(e) Kunena/kuongea kupitia kinywa cha mgonjwa. Mapepo huweza kujitokeza na kunena hadharani,huku yakitoa amri au maelekezo juu ya mahitaji yao. Mengine hudai yanataka damu,yametumwa damu na baadhi ya mambo. (Mathayo 8:29-31,Marko5:5). Kitendo hiki cha kuilaghai,hupelekea uchonganishi,uhasama miongoni mwa jamii na hata maamuzi mabaya. Ndugu mpendwa,usimsikilize pepo,siku zote yeye ni mharibifu tu,hawezi kusema ukweli, na usifuate maelekezo yake,daima msikilize MUNGU.
(f) Wanaweza kutumika kama walimu makanisani kwa mafunuo,ndoto au maono. Hizi roho zinaweza kuleta mafunuo yanayolenga kuwaaminisha maumini kuwa ni mafunuo ya ki Mungu,ili kutaka kuwateka waumini na kuyaamini. Unapaswa kuwa makini sana katika hili. Kumbuka hata Sauli, alitoa unabii kipindi anateswa na roho wabaya.(1Timotheo4:1-5). Jiepushe kuyasikilza maneno yanayonenwa na mtu aliyepagawa na mapepo.

NB: mapepo yanaweza kuongea habari juu ya Yesu, ila tu,hayawezi kuongea habari sahihi juu yake.(Matendo 16:16&17,Marko1:24). Usikubali kuyasikiliza wala usiyahoji,yanadanganya tu, kumbuka,hata Yesu aliyakemea yaondoke tu,hata yalipotaka kuongea jambo lolote,yeye aliyaamuru yaondoke (Marko1:34)
(g) Humwamuru mtu kujitenga. Humtenga mtu na watu wengine. Humpeleka maeneo yasiyoyakawaida. Mfano misituni,vichakani,mtoni,kwenye maziwa na bahari,makaburini nk(Luka8:27). Lengo ni kutaka huyu huyu mtu aendelee kuogopwa, lakini pia kumtenga na maeneo ambayo ibada na MUNGU wa kweli hutajwa. Kumkimbuzia maeneo yaligubikwa na ibada za kipepo ili kuweka mikataba zaidi na kuendelea kumfunga.
(h) Kufanya mambo ya ajabu na aibu. Humwondolea utu wake na sitaha. Huishiwa ustaarabu, ndiyo maana anaweza kutembea uchi,kujiasaidia hadharani,kula vyakula vichafu, kufanya mambo yasiyofaa kwa furaha na kwa uhuru wote. Hii ni kwasababu, anakuwa ametengwa na jamii (Luka 8:27) hivyo huwa si sehemu ya mila na utamaduni wa jamii hiyo.
(i) Kuteswa kwa magonjwa ya mwili. Pepo akishamaliza kuingia, mtu huweza kumtesa kwa magonjwa ya kawaida kabisa ili kupumbaza wanaomuuguza mtu,wasijue chanzo cha tatizo.pia hutafutia kisababu cha kumuua.
Mfano wa baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na mapepo ni:-
Ububu (Marko 9:17)
Uziwi na ububu (Marko 9:25)
Upofu na Ububu (Mathayo 12:22)
Kupooza/ uwete (Matendo 8:7)
Kifafa (Marko 1:26,9:20, Luka 9:36) n.k. hufunga masikio kwa uziwi na kinywa kwa ububu ili kutomfanya mtu aweze kujieleza au kukili imani ya wokovu,hii ni kinga kwa mapepo ili kuendelea kumuweka chini ya himaya yao.
(j) Kuabudu miungu/ sanamu.(Walawi17:7,Torati 32:17,Ufunuo 9:20). Wakati mwingine,mtu alifungwa na mapepo, huweza kufundishwa ibada za sanamu na kuanza kuzifanya. Wengine husema, anamizimu ya kiganga (Walawi 20”27), na kujenga uhusiano na mizimu (1Samweli 15:23) kitendo kinachoplekea kuwa mchawi (Isaya 47:9-13,Matendo 19:18&19).

Ndugu yangu mpendwa, habari hizi ni nzito sana,na unapaswa kuzijua ili kujiepushwa nazo wewe na uzao wako na kizazi chako chote.

Swali la kujiuliza ni je, kufukuza pepo ndiyo uponyaji, au kuna uponyaji bila ya kufukuza pepo?
Kama tulivyoona, mapepo husababisha magonjwa, hivyo ili mgonjwa apone sharti pepo atoke.afukuzwe. kuna watu wanajidai eti wanatuliza mapepo, hakuna jambo kama hilo, kikubwa ni kumkemea pepo kwa Jina la Yesu, aondoke akae Roho Mtakatifu.
Mungu aendelee kukubariki na kukufunulia zaidi.

SEHEMU YA TANO
Somo:MAPEPO
Mada Ndogo: Njia 8 za kuyashinda mapepo.
 

Bwana Yesu asifiwe sana,
Ndugu mpendwa, katika sehemu Nne zilizotangulia,tumejifunza maana,asili/ chanzo cha mapepo na dalili kuu za mtu alievamiwa na mapepo. Natumai umebarikiwa sana. Haleluya! Ndugu mpendwa, napenda kukukaribisha katika mwendelezo wa mafundisho yetu juu ya mapepo,ambapo kwasasa tutaangalia kwa kina mbinu/njia za kumshinda pepo.

Ndugu yangu mpendwa, kanisa la leo, liko katika mapambano makubwa sana. Upinzani mkubwa unatoka kwa ibilisi alie shetani, mwenye sifa kuu ya uharibifu.

Hatahivyo, Mungu ameliweka kanisa kwa wakati huu wa mashambulizi kwaajili ya kuukomboa ulimwengu. Amelifanya kanisa kama asikari wa mwamvuli ambaye hushushwa katikati ya eneo ambalo bado liko mikononi mwa adui, ila ikikusudiwa kupambana na hata kushinda. Kwa mantiki hiyo, si hoja tena juu ya kushinda kwa kanisa, bali daima linashinda na litaendelea kushinda.

Katika mwendelezo wa somo letu, leo tutaziangalia njia/uwezo wa kuyashinda mapepo.

Kwanza; Yesu alitoa mamlaka kwa kanisa juu ya mapepo (Marko 16:17). Uweza huu wa ajabu, Mungu ameutoa kwa watu wote wanaomwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wao (Yohana 17:20-23). Ujue, watu wengine wanateseka kwa kuwa hawajui, yule aliye ndani yao. Biblia inasema, aliyeko ndani ya aliyeokoka ni mkubwa mno, maana yake ni kuwa, anayashinda mapepo. Usikubali kuteswa na mapepo, kemea kwa jina la Yesu, lililo jina kuu kupita majina Yote, nawe utakuwa huru.

Pili; Mapepo huamriwa kwa jina la Yesu tu (Marko 16:17). Jina maagano na ahadi ni jina la Yesu tu. Usitumie jina lingine lolote lililo nje ya jina la Yesu. Ni jina la Yesu pekee huweza kuponya,kuokoa na kuhuisha, hata mapepo yanajua hivyo. Kutumia majina mengine ni sawa na kukosea anwani wakati wa kutuma barua, ni kweli barua itaenda ila usitegemee kupokea majibu uliyotarajia kwa kuwa barua haitaenda kwa mlengwa.

Tatu; Yafukuize kwa kutumia mamlaka uliyonayo kama ilivyoelezwa katika hoja ya kwanza. Usiyabembeleze. Tumia amri. Watu wengine hutumia majadiliano, huyafanyia sherehe, huyafukizia uvumba,udi na hata kuyachezea muziki wa asili. Ndugu yangu, waswahili wanasema” ukifanya urafiki na mkia wa fisi,utakufirisi” usikubali kukaa meza moja na mapepo, shetani habembelezwi, yatimue kwa mamlaka ya Jina la Yesu (Mathayo 12:28,Luka 11:20).

Nne; Usiyaruhusu kujieleza. Mpiganaji mzuri, hamuulizi adui ametoka wapi, yeye hushambulia hata kikosi kizimahukimaliza, kwa kuwa ni jasili na anajiamani, hababaishwi. Usikubalia kuhojiana na pepo, pepo ni waongo, watakudanganya kwa kutoa habari za uongo ili kulibomoa kanisa (mwili wa kristo) ili kuwatenganisha. Wataibua uadui kati yenu. We yaaamuru yaondoke, hata Yesu mwenyewe aliyaamuru tu yakaondoka (Luka 4:41,Marko 1:34).

Tano; Kwa kufunga na kuomba (Marko 9:29). Ndugu yangu mpendwa, kila mara, adui hushinwa kwa sala na kusoma neno. Jaama mamlaka ya mbinguni ili kumshinda ibilisi. Mtu asiye na maombi ni sawa na bunduki isiyo na risasi, na mtu asiyeomba anafanana na mlinzi anaetegea kazi yake, hutoa mwanya kwa mwizi kuvamia na kupora. Usikubali kuwa mlango wa ulegevu, daima jitahidi kuwekeza neno kwa wingi ili ujipatie maarifa zaidi.

Sita; Kuwa na Imani thabiti (Mathayo 17:19-20). Maombi pasipo imani, ni sawa na dhihaka. Ni bora ya majaribio, kuliko kudhihaki. Daima, kuwa jasili na umwamini Mungu na neno lake, ndipo litatimia kwako. Mtu asiyeamini, maombi yake hupeperushwa na mawimbi,hivyo hata majibu ya maombi yake hupeperushwa tu,kwakuwa hayana nguvu yoyote ndani yake.

Saba; Kwa Kumwamini Mungu (Marko 6:5&6), ukimwamini utamtegemea kwa kila jambo(Marko 9:23&24). Ukiwa na imani kwake, utakuwa na ujasili. Mwamini Mungu,ili athibitishe ujasili wako.

Nane; Kwa Muujiza. Mungu, ni Mungu wa maajabu, hufanya mambo yaliyojuu ya fahamu za mwanadamu. Hufanya mambo ya kushangaza, kuweza kufanya miujiza mikubwa mno,amabayo hata uwezo wa wasomi,hufikia kikomo. (Matendo 19:11&12), tunaonao nguo za Paulo zikifanya maajabu, ni muujiza wa nguo kutoa pepo. Ni kwa kuwa kuna upako unaokuwa sambamba na wamchao Bwana. Tegemea Miujiza kama uko kwenye uwepo muda wote. Kumbuka, imani wakati mwingine haionekani (Matendo 16:16-19), hivyo miujiza huithibitisha imani.

Swali la kujiuliza ni je, kila mtu anaweza kumtoa pepo?Jibu ni Hapana, si kila atakaye tumia jina la Yesu anaweza kutoa pepo, tena anaweza hata kujikuta yuko kwenye wakati mgumu zaidi kwa kuwa jina la Yesu lina uwezo wa ajabu, hivyo mtu anapaswa kulitumia kama silaha huku akihakikisha amejilinda vizuri mahali alipo (Matendo 16:13-16), mtu asiyejulikana katika ufalme wa Mungu, anapoliita jina la Yesu, huwa kama mtoto anaemlilia mama asiye wake, hata akimuonea huruma vipi, hawezi kuwa mama yake kabisa. Hii ni kwasababu, hawana utambulisho kwa Yesu, japo wanatumia jina lake(Luka 7:22&23).

Ifahamike kuwa, mtu ambaye hajamwamini Yesu,pengine ni mpagani kabisa, akiombewa, pepo hutii amri ya mwombaji na kuondoka, lakini kwa kuwa anayeombewa hajaamini, yule pepo huweza kurudi na kufanya makao tena ndani yake. Ni sawa na mpiganaji vitani anaevamia, na kupamabana na kuondoka bila kuacha walinzi. Adui, anakuwa na uwezo wa kurudi tena na kujimilikisha na hata akaweka ulinzi wake ulio imara zaidi kuliko ule wa awali (Mathayo 12:44&45).

Ndugu mpendwa, naimani unaendelea kubarikiwa kwa mafundisho yetu. Huu ndiyo utakuwa mwisho wa mada yetu. Usikose mada zijazo. Mungu akubariki. 

Suche
Kategorien
Mehr lesen
FORM 5
FORM 5
List of all subjects for the form 5 class ACCOUNTANCY ADVANCED MATHEMATICS AGRICULTURE BASIC...
Von PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:25:36 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
Mtu ambaye amemwamini Yesu lakini akafa bila kubatizwa je! atenda mbinguni?
JIBU: Inategemea kama hapo kabla alishausikia ukweli au la, kwa mfano kama mtu alishaufahamu...
Von GOSPEL PREACHER 2022-03-29 23:47:51 0 4KB
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 46
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 24 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-01-21 10:04:48 0 5KB
LEVITICUS
Verse by verse explanation of Leviticus 16
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 58 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-01-24 10:15:50 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA.
Kwa ufupi.. Bwana Yesu asifiwe… `` Kwa kuwa,kila atakayeliitia Jina la Bwana...
Von GOSPEL PREACHER 2022-03-30 05:01:07 0 5KB