ETI ALLAH AMEKUBALI KUTOA USHAIDI KWA VIUMBE VYAKE?

0
5K

Je, nani atakuwa Hakimu wakati Allah anatoa Ushaidi?

NDUGU WASOMAJI, Hivi Allah anaweza kuwa shaidi wakati yeye ndie anadai kuwa alitoa Utume kwa Muhammad? Hivi Mungu anaweza kwenda kutoa Ushaidi kwa viumbe vyake? Nani atakuwa Hakimu wa hiyo Kesi?

Katika hii aya hapa chini, mhukumiwa ni Allah aliyedai katoa Utume kwa Muhammad, kivipi na tokea lini Mhukumiwa akawa shaidi katika Kesi yake ya jinai?

Quran 4:72 Surat Annisa inasema "wema uliokufikia unatoka kwa Mwenyenzi Mungu na baya lililokufikia linatoka nafsini mwako nasi tumekupeleka kwa watu kuwa Mtume na Mwenyenzi Mungu ni shahid wa kutosha wala hapaitajiwa shaid mwingine ila yeye"

Allah anadai kuwa yeye ndie aliye mpa Utume Muhammad na hapo hapo ALLAH anajihami kuwa mkibisha na au kuwa na shaka na utume wa Muhammad basi yeye ni Shaidi yake. Hivi, MFANO: Rais akimpa Mtu uwaziri, umesha wai sikia Rais anajihami kwa kusema kama wakikukataa mimi nitakuwa Shaidi yako? Kwani Allah ana mshindani mpaka atoe maneno ya kujihami? Je, Allah ni Mungu? Mbona anakubali kuchukia nafasi ya chini ya kuwa Shaidi kwa viumbe vyake? Au kuna Mungu mwingine ambaye ni zaidi ya Allah ndio maana Allah anajihami kwa kusema yeye atakuwa shaidi wa Muhammad?

Ndugu zanguni, tukisoma Biblia, hakuna hata sehemue moja na au aya yeyote ile inayo sema kuwa Yehovah alijihami kwa Mitume wake kuwa, kama wakikataliwa basi Yehovah atakuwa shaidi yao. Allah anadai kuwa yeye ni shaidi lakini ameshindwa kutuambia wapi hiyo kesi itakuwa na nani ni Hakimu!

Binadamu/Sisi labda ndio tunaweza kuwa Mashaidi wa Neno la Mungu lakini si Mungu mwenye Mamlaka yote awe shaid katika viumbe vyake na neno lake. Mungu huwa halizimishi mambo kama Allah wa Uislam. Yesu anasema kuwa yeye Ndie Mwanzo na Mwisho, Alfa na Omega. Hakuna zaidi yake, lakini Allah amekiri kuwa yeye anaweza kuwa shaidi pale mambo yanapokuwa magumu. Hakika Allah hana Mamlaka yeyote yake, ndio maana yeye ni shaidi na sio Mungu mwenye Mamlaka. Sijui nani atakuwa Hakimu wakati Allah amesimama kutoa Ushaidi?

Cerca
Categorie
Leggi tutto
1 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 1 Chronicles 9
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-03-20 04:47:53 0 5K
1 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 1 Chronicles 28
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 25 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-03-20 05:23:17 0 6K
OTHERS
KWANINI WAISLAM WALITENGENEZA INJILI YA UWONGO YA BARNABAS?
SEHEMU YA 1 Mwalimu Chaka SWALI: Kwa nini Wakristo Hamuitambui Injili ya Barnaba?lililoulizwa...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-25 11:10:27 0 6K
SPIRITUAL EDUCATION
MACHO YA TAI AWINDAE MAWINDO YAKE
Macho ya Tai AWINDAE mawindo yake  Kila mmoja wetu tunapaswa kuwa na macho ya kuona...
By Martin Laizer 2023-09-22 09:29:34 2 18K
1 KINGS
Verse by verse explanation of 1 Kings 12
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 33 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 13:41:13 0 6K