HISTORIA FUPI YA IBADA YA KISHETANI YA ROZARI.

0
6K

UTANGULIZI

Katika Biblia hakuna mahali popote pale panapofundisha kuwa tusali rozali, na hata Yesu Kristo mwenyewe pamoja na mitume wake hawakuwahi kabisa kufundisha kuhusu rozali. Je, fundisho hili la kishetani lilitoka wapi? TAFADHALI FUATILIA HISTORIA HII, ILI UIEPUKE IBADA HII YA KISHETANI, KAMA KWELI UNATAKA KWENDA MBINGUNI.

Katika Kalenda ya Kanisa Katoliki, huwa mwezi wa tano na mwezi wa kumi ni miezi ambayo imewekwa kwa ajili ya Bikira Maria na Mama Kanisa. Hivyo hiyo miezi huwa inasaliwa rozari. Wengi waweza kujiuliza kuwa ni kwa nini ifanyike miezi hiyo? Yafuatayo ni majibu, mwezi wa tano umewekwa kwa heshima ya Bikira Maria kutokana na nini kilitokea katika historia hapo nyuma. Mnamo Karne ya 16 mwezi watano kwa miaka yote ulikuwa ni mwezi ambao sikukuu nyingi za kiserikali ndo zilikuwa zikifanyika. Kanisa kwa kutambua hilo nalo likahidhinisha pia mwezi wa tano uwe ni mwezi wa Rozari, na kwa makusudi zaidi Kanisa lililenga kuwa sherehe hizo ziendane na taratibu za wakristu, ni kwa msingi huo sherehe hizo ziliendana na mwezi wa rozari na kutokea hapo ikahidhinishwa kuwa mwezi wa tano wa mwaka ni mwezi wa Bikira Maria. Pia mwezi wa kumi (October) pia ni mwezi wa Bikira Maria na pia ni mwezi wa Kusali Rozari kutokana na historia ya hapo nyuma pia, na ilikuwa kwamba baada ya ushindi wakristo walioupata katika vita baina yao na yule aliyeitwa Lepanto mnamo 7 October, 1571, Papa wa wakati ule Papa Pius V aliufanya huo ushindi kuwa ulitokana na maombezi ya Bikira Maria, na alisema kuwa rozari ni silaha kubwa hata kuliko silaha kubwa za kivita. Ni Kwa msingi huu tunaona kuanzia hapo mwezi wa kumi ukawa mwezi uliotengwa na Mama Kanisa kwa Bikira Maria, na pia ukaitwa mwezi wa Rozari.

Historia yenyewe

Ni kwamba sala ya Rozari inasemekana kuanzishwa na Mt. Dominico aliyezaliwa mnamo mwaka 1170 na kufariki mwaka 1221 na hiyo sala Mt. Dominico aliipata kwa njia ya ufunuo ambapo Bikira Maria alimtokea na kumwamuru awe anasali rozari. Bikira Maria alimwamuru mtakatifu Dominico kusali rozari kwa kipindi hicho iwe kama silaha yake ili kupambana na uzushi uliokuwa umeibuka ukipingana na mafundisho ya Kanisa, na huo uzushi uliitwa ‘ Albigensia’ hili ni kundi lilokuwa na imani kuwa Duniani kuna nguvu nguvu mbili zenye uwiano sawa lakini hupingana na kupigana moja baada ya nyingine, nazo nguvu hizo ni Mungu na Shetani. Hivyo hawa waliamini kabisa kuwa Mungu na Shetani wana nguvu sawa ( Dualistic ) waliamini pia kuwa dunia hii imejaa uovu kwa kuwa iliumbwa na mwovu. Ni kwa msingi huu Kanisa liliamua kupambana na hawa wazushi ambao pia walionekana kupotosha mafundisho ya Kanisa. Ndipo tunaona Bikira Maria anamtokea Mtakatifu Dominico na kumwambia asali rozari ili kupambana na mafundisho hayo ya kizushi. Ni Papa Pio V ambaye mnamo mwaka 1569 alihidhinisha rasmi kusali rozari kwa kanisa nzima na kuhidhinisha rozari iwe jinsi tunavyoiona sasa. Katika zile zama za kati, watawa wamonaki walizoea kusali zaburi 150, na kwa upande wa waumini walei ambao kwa kipindi hicho hawakujua kusoma zaburi iliwabidi wasali sala ya Baba yetu mara 150 baadala ya zaburi 150 na hizo baba yetu walizisali kwa kuhesabu punje 150 zilizokuwa zimefungwa kwenye kamba ndefu ambayo kwa lugha ya kitaalamu iliitwa “ Corona” au kwa Kiingereza “ Crown” kadiri ibada kwa Bikira Maria ilivyoendelea kushamiri mnamo Karne ya 12, sala kwa Bikira Maria ilianzishwa na hivyo kuanza kusali salamu maria 150 baadala ya baba yetu 150.

Salamu Maria 150 hapo baadaye zilikuja kugawanywa katika makundi/ mafungu na Mtawa mdominica aliyeitwa Henry Kalkar ( 1328-1408), ambapo kila tendo la rozari lilikuwa na mafungu 50 ya salamu Maria ambapo pia kila fungu liligusia maisha ya Bikira Maria na Yesu katika historia ya wokovu wetu. Zaidi ya hapo, mtawa mwingine wa mdominican aliyeitwa Alanus de Rupe aliendelea kugawanya hiyo historia ya matendo ya wokovu wetu katika matendo ya furaha,uchungu, na utukufu kama tunavyoyaona sasa. (NB Matendo ya mwanga hayo ni ya majuzi siyo ya wakati ule). Na nikuanzia hapo Bikira Maria amepewa nafasi kubwa katika shirika la watawa wa Dominican. Hivyo utamaduni wa kusali rozari umeendelea karne hata karne, mfano Papa Leo XIII (1878-1903) aliweka msisitizo mkubwa juu ya ibada ya rozari kwa Bikira Maria. Kuanzia September 1, 1883 Baba Mtakatifu Leo XIII aliandika jumla ya barua za kichungaji 11 zote zikiwa zinaweka mkazo juu ya rozari. 

Najua umedanganywa kuwa eti kusali rozali ni sala inayotokana na maandiko matakatifu( Biblia), na kuwa eti mafumbo ya rozari yote yanapatikana katika agano jipya ambapo ndo tunaona matendo ya Bikira Maria na Yesu Kristo katika wokovu wetu, na eti kuwa rozali inakukumbusha uchungu aliopata Bikira Maria Katika maisha yake hasa ule utabiri wa Simeoni kwa Bikira Maria juu ya mateso na kifo cha mwanae Yesu, Matendo saba ya furaha kwa Maria ambapo yaananza na kupashwa habari kwa Bikira Maria na Malaika wa Bwana, kupalizwa mbinguni, na matendo ya huruma ya Bikira Maria kwa wale ambao wanaendelea kuteseka hapa duniani. Swali ni moja tu, umewahi kupewa ushahidi wa hili katika Biblia?

AHADI 15 ZA UONGO ZA KUSALI ROZARI

Watu wamefundishwa uongo kuwa Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari kila siku. Eti kuwa ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche. Huu ni uongo wa dhahiri, kwani wewe umeshawahi kusoma kwenye Biblia na ukaona mwenyewe jambo hili? Usiamini chochote kile ambacho hakiendani na mafundisho ya Biblia. Ahadi hizo za uongo ni kama ifuatavyo

  1. Yeyote yule atakayesali kwa imani rozari hii takatifu atapokea neema kuu zenye nguvu
  2. Naahidi ulinzi wa kipekee na neema za kipekee kwa yule atakayesali rozari hii
  3. Rozari itakuwa silaha kubwa dhidi ya nguvu za kuzimu, itaharibu maovu, itapunguza dhambi na kushinda kutofautiana
  4. Itafanya fadhila kukua, kazi nzuri kuongezeka, itapatia roho huruma tele toka kwa MUNGU, itaondoa hamu ya wanadamu kupenda mambo ya dunia na majivuno yake na kufanya wapende zaidi mambo ya mbinguni. Ooh, ni kwa namna gani roho hizo zitajifurahisha na kubarikiwa kwa namna hii.
  5. Roho zitakazojikabidhi kwangu kwa njia ya kusali rozari, kamwe hazitapotea.
  6. Yeyote atakayesali rozari kwa uaminifu huku akiyatafakari matendo makuu  ya rozari, kamwe hatashindwa na ubaya. MUNGU hatamwadhibu katika hukumu yake, hatapotea katika kifo asichopangiwa na atabaki katika neema za MUNGU na kustahili kupata uzima wa milele.
  7. Yeyote atakayekuwa mwaminifu katika kusali rozari, kamwe hatakufa bila ya kupokea Sakramenti takatifu za Kanisa.
  8. Wote watakaokuwa waaminifu katika kusali rozari watadumu katika mwanga wa MUNGU katika maisha yao na saa yao ya kufa na kupata neema zake tele; katika saa yao ya kufa watashiriki fadhila za watakatifu waliopo peponi
  9. Nitawatoa toharani wale wote waliokuwa waaminifu katika kusali rozari
  10. Watoto wangu waaminifu katika kusali rozari watapata fadhila kuu ya utukufu Mbinguni.
  11. Utapata yale yote unayoniomba kwa kusali rozari
  12. Wote wale wanaoeneza rozari hii takatifu nitawasaidia katika mahitaji yao
  13. Nimepata toka kwa mwanangu Mtukufu kuwa mawakili wote wa rozari watapata waombezi toka baraza lote kuu la Mbinguni wakati wa maisha yao na wakati wa saa yao ya kufa.
  14. Wote wanaosali rozari hii takatifu ni wanangu, na kaka na dada wa mwanangu wa pekee YESU KRISTO
  15. Ibada kwa rozari ni ishara kuu ya kuelekea ukombozi

 

SALA YA KISHETANI YA KUSALI ROZARI NA KUMWABUDU MARIA

*rozari - Sala zake na namna ya kuisali*

UTANGULIZI

Ifuatayo ni mada fupi kuhusu namna ya kusali rozari ya Bikira Maria, pamoja na sala kuu zinazosaliwa wakati wa sala hii ya rozari.

Wakati wa kusali unaweza kuongeza sala nyingine zifaazo kadri ya nafasi.

 rozari husaliwa na wakristu kutafakari maisha ya Yesu na Maria yaani Fumbo la Ukombozi, hasa kipindi cha mwezi Mei na Oktoba.

Inahimizwa kuisali kama familia kila siku.

Tusali rozari tupate amani, wakosefu waongoke na wasiomjua Yesu Kristu wamjue na kuokoka.




MAELEZO YA JUMLA

Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba (gusisha msalaba huo kwenye paji la uso, kifuani, bega la kushoto na kwa kutumia msalaba wa rozari huku ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.


Taja kwa ufupi nia za Rozari hii.

Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano,

“Tusali kuombea amani katika nchi yetu na ulimwenguni kote"

au tutolee rozari hii kuwaombea wagonjwa wetu:

 au :tuwaombee wote walioomba tuwaombee" nk. Hiyo ni mifano tu.

 Au unaweza kutoa mambi kuendana na tendo lililotangazwa kwenye kumi husika la tendo la rozari,

au namna nyingine itakayofaa.

Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.

 maneno yafuatayo hutumika

“Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, ……

 Mungu Mwana utuongezee matumaini,

Salamu Maria, ……

Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu kwa mapendo yako,

Salamu Maria, …..”


MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)

Tendo la kwanza ; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu.
Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu .

Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.


Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu.
Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara


Tendo la nne ; Yesu anatolewa hekaluni.
Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo .

Tendo la tano ; Maria anamkuta Yesu hekaluni.
Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.




MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)

Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.


Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.


Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.


Tendo la nne ; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.


Tendo la tano ; Yesu anakufa Msalabani.
Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.




MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)


Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.

Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni . Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.

Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu .


Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni.
Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.

Tendo la tano ; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema .




MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)


Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani.
Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.


Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.


Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.


Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.


Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.

SALA ZA rozari

KANUNI YA IMANI

Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, mwumba mbingu na dunia. Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu; aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka katika wafu; akapaa mbinguni; amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, uzima wa milele. Amina.


BABA YETU...

Baba Yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe; ufalme wako ufike, utakalo lifanyike, duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina


SALAMU MARIA...

Salamu Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote. Na Yesu Mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.


ATUKUZWE BABA...

“Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina”;


EE YESU WANGU...

Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi”;


TUWASIFU...

“Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef”.


DAMU YA KRISTU..

Damu ya Kristu, iziopoe roho zinazoteseka toharani, izitie nuru ya uzima wa milele. Amina.

Au;

RAHA YA MILELE..

Raha ya milele uwape ee Bwana, na mwanga wa milele uwaangazie. Wapumzike kwa amani. Amina.





LITANIA YA BIKIRA MARIA

Bwana utuhurumie

Bwana utuhurumie

Kristo utuhurumie

Bwana utuhurumie

Bwana utuhurumie

Kristo utusikie

Kristo utusikilize


Mungu Baba wa Mbinguni,                                        Utuhurumie

Mungu Mwana Mkombozi wa dunia                          Utuhurumie

Mungu Roho Mtakatifu                                              Utuhurumie

Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja                                 Utuhurumie


Maria Mtakatifu                                                          utuombee

Mzazi Mtakatifu wa Mungu                                       utuombee

Bikira Mtakatifu Mkuu wa mabikira                          utuombee

Mama wa Kristo                                                         utuombee

Mama wa neema ya Mungu                                        utuombee


Mama Mtakatifu sana                                                 utuombee

Mama mwenye usafi wa moyo                                   utuombee

Mama mwenye ubikira                                                utuombee

Mama usiye na doa                                                     utuombee

Mama mpendelevu                                                      utuombee

Mama mstajabivu                                                        utuombee

Mama wa Muumba                                                     utuombee

Mama wa Mkombozi                                                  utuombee

Mama wa Kanisa                                                        utuombee

Bikira mwenye utaratibu                                             utuombee

Bikira mwenye heshima                                              utuombee

Bikira mwenye sifa                                                     utuombee

Bikira mwenye uwezo                                                            utuombee

Bikra mweye huruma                                                  utuombee

Bikra mwaminifu                                                        utuombee


Kioo cha haki                                                              utuombee

Kikao cha hekima                                                       utuombee

Sababu ya furaha yetu                                                            utuombee

Chombo cha neema                                                     utuombee

Chombo cha kuheshimiwa                                          utuombee

Chombo bora cha ibada                                              utuombee


Waridi  lenye fumbo                                                   utuombee

Mnara wa Daudi                                                         utuombee

Mnara wa pembe                                                         utuombee

Nyumba ya dhahabu                                                   utuombee

Sanduku la Maagano                                                  utuombee


Mlango wa Mbingu                                                     utuombee

Nyota ya asubuhi                                                        utuombee

Afya ya wagonjwa                                                      utuombee

Kimbilio la wakosefu                                                  utuombee

Mtuliza wenye huzuni                                                 utuombee

Msaada wa waKristo                                                  utuombee


Malkia wa Malaika                                                      utuombee

Malkia wa Mababu                                                     utuombee

Malkia wa Manabii                                                     utuombee

Malkia wa Mitume                                                      utuombee

Malkia wa  Mashahidi                                                 utuombee

Malkia wa Waungama dini                                         utuombee

Malkia wa Mabikira                                                    utuombee

Malkia wa Watakatifu wote                                       utuombee

Malkia uliyepalizwa Mbinguni                                    utuombee

Malkia wa rozari                                          utuombee

Malkia wa amani                                                         utuombee


Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,

Utusamehe ee Bwana.

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye  dhambi za dunia,

Utusikilize ee Bwana

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,

Utuhurumie.

Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,

Tujaliwe ahadi za Kristo.


Tuombe

Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote;  na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.


SALAMU MALKIA...

Salamu Malkia, Mama mwenye huruma, uzima, tulizo na matumaini yetu, salamu. Tunakusihi hapa ugenini sisi wana wa Eva. Tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika bondeni huku kwenye machozi. Haya basi, Mwombezi wetu, utuangalie kwa macho yako yenye huruma. Na mwisho wa ugeni huu, utuonyeshe Yesu, mzao mbarikiwa wa tumbo lako. Ee mpole, ee mwema, ee mpendelevu, Bikira Maria.


KUMBUKA...

Kumbuka, ee Bikira Maria mwenye rehema, tokea zamani zote haitambulikani kumeachwa mwenye aliyekimbilia ulinzi wako, mwenye aliyetaka msaada wako, mwenye aliyetaka maombezi yako. Nami nimetumaini kwako, nimekimbilia kwako, ee Mama yangu, Bikira asiye na mfano, nimekuja kwako, nasimama mbele yako mimi mwenye dhambi. Mama wa Neno wa Mungu, usiyachukie maneno yangu, uyapokelee, uyasikilize, ukanifanyizie. Amina.


SALA KWA MTAKATIFU YOSEFU

Ee Mt. Yosefu mwenye heri, tunakimbilia kwako katika masumbuko yetu, na kisha omba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda Bikira Mtakatifu Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya kumtunza Mtoto Yesu, twakuomba sana, utuangalie kwa wema sie tuliokuwa fungu lake Yesu Kristu, tukakombolewa kwa damu yake. Tusimamie katika masumbuko yetu kwa enzi na shime yako.

Ee Mlinzi amini wa jamaa takatifu, uwakinge watoto wateule wa Yesu Kristu. Ee Baba uliyetupenda mno tuepushe na kilema chochote cha madanganyo na upotevu. Ee kinga yetu mwezaji, utusimamie huko juu mbinguni ulipo, tunaposhindana na wenye nguvu wakaao gizani. Kama vile siku za kale ukamwopoa Mtoto Yesu katika hatari ya kuuawa, na leo hivi likinge Kanisa Takatifu la Mungu katika mitego ya adui, na katika shida yote; mtunze daima kila mmoja wetu, tufwate mfano wako, ili tupate na msaada wako, kukaa na utakatifu maisha, kufa kifo chema, na kupata mbinguni makao ya raha milele. Amina.


TUNAUKIMBILIA...

Tunaukimbilia, ulinzi wako, Mzazi Mtakatifu wa Mungu. Usitunyime tukikuomba katika shida zetu, utuokoe siku zote kila tuingiapo hatarini, ee Bikira mtukufu na mwenye baraka. Amina.

WOTE WANAOSALI IBADA HII YA KISHETANI, SEHEMU YAO NI KATIKA ZIWA LA MOTO.

Buscar
Categorías
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
YESU ATAKUPONYA.
Bwana Yesu asifiwe… Kwa ufupi, “Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili...
By GOSPEL PREACHER 2022-03-30 04:53:31 0 4K
Injili Ya Yesu Kristo
MWANANGU, YULE MAMA HAKUMALIZA VIZURI SAFARI YAKE
Mwanangu yule mama hakumaliza vizuri safari yake! Hivi ndivyo Mchungaji wangu, alivyoanza...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:39:49 0 5K
OTHERS
Maana Ya Namba 40.
Ndugu msomaji wangu Hivi karibuni nimepokea Maswali kadhaa kutoka kwa watu mbalimbali wakiuliza...
By GOSPEL PREACHER 2022-04-01 15:44:49 0 6K
JOB
Verse by verse explanation of Job 4
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 13:31:42 0 5K
1 KINGS
Verse by verse explanation of 1 Kings 11
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 51 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 13:10:21 0 6K