MAJIRA YA KANISA LA FILADELFIA

0
6K

(1) MLENGWA WA KANISA


UFUNUO 3:7

“Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika…………”


Kwa hiyo Hapa mlengwa wa kanisa ni KANISA LA FILADEFIA


● MAZINGIRA YA MJI WA FILADEFIA


Mji huu wa Filadefia likuwa maili zipatazo 30 kusini mashariki mwa mji wa Sardi. Mji huu ulijulikana kwa wingi wa zabibu ambazo zilistawi kwa wingi sana katika eneo hilo na hivyo zilitumika kutengenezea Mvinyo (Pombe) wa aina nyingi.


Kwahiyo sifa mojawapo kubwa ya Mji wa Filadefia ilikuwa ni utengenezaji wa Mvinyo ambao ulitokana na Zabibu na hivyo hivyo walikuwepo walevi wengi waliokuwa wanalewa kwa mvinyo katika mji huo wa Filadefia. Sasa likumbuke hilo kuhusiana na kuelewa kwa mvinyo katika mji wa Filadefia na jinsi liatakavyokuja kuhusika katikaunabii kama tutakavyoweza kuona huko baadae


Lakini kumbuka tu kwamba mji huu wa filadefia ulikuwa unasifika kwa zabibu kwa wingi na hivyo kulikuwa na mvinyo wa namna nyingi mbalimbali na walikuwepo walevi wengi sana katika mitaa ya filadefia




(2) WASIFU WA YESU KRISTO


UFUNUO3:7

“……………ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye”

● YEYE ALIYE MTAKATIFU

Hapa kwa kanisa la Filadefia Yesu Kristo anazungumza kama YEYE ALIYE MTAKATIFU ingawa kwenye Makanisa mengineyo hakujitambulisha kwa sifa hiyo. Kama tutakavyoweza kuona kwa undani Zaidi katika majira ya unabii inayohusiana na Kanisa la Filadefia ambayo kimsingi ni majira kuanzia mwaka 1750-1905

Tulijifunza mapema kuwa yale makanisa saba(7) yaliyokuwepo nyakati hizo lakini katika unabii Kuanzia wakati Yesu Kristo anamaliza huduma yake duniani mpaka wakati wa Kunyakuliwa kwa kwa Kanisa, Majira yote hayo yamegawanywa katika sehemu 7 au majira 7 na yale yaliyokuwa yanazungumzwa katika makanisa hayo7 yalikuwa yanawakilisha yale ambayo yangekuja kutokea katika majira hayo 7 tofauti

Kwahiyo Majira ya Filadefia katika unabii ndio kuanzia mwaka 1750-1905. Majira tuliyo nayo sasa nimajira ya Laodikia ambayo ni majira ya mwisho ya saba kabla ya kunyakuliwa kwa kanisa ambayo tutayaangalia baada ya somo hili la majira ya Filadefia

Sasa majira ya Filadefia ndio majira ambayo UTAKATIFU ulirejezwa tena katika kanisa baada ya giza zito sana kupita karne nenda karne rudi. yale ya msingi yaliyokuwa yanafundishwa katika kanisa la kwanza yaliweza kurejezwa Kimsingi UTAKASO ulirejezwa tena katika majira haya, Maana kwa miaka yote iliyopita hakukuwa na kitu cha namna hiyo, Kulikuwa giza sana kama ambavyo tulijifunza lakini majira hayo hatua kubwa sana ilipigwa mpaka kufikia watu kujifunza Utakaso kutokana na mafundisho ya mtu mmoja aliyeitwa JOHN WESLEY ambaye tutamuangalia kwa undani huko mbele tutakapoangalia mambo kwa undani Zaidi kuhusiana na majira haya katika unabii

Ndio maana Hapo yesu anajitambulisha kama Yeye aliye mtakatifu akimaanisha kuwa Kanisa litakuja kuwa katika utakatifu na usafi wa kipekee kama tutakavyoona ilivyokuwa hapo baadae

● YEYE ALIYE WA KWELI

Vile vile Hapa Yesu Kristo anajitambulisha kama Yeye aliye wa kweli akimaanisha kuwa Neno la kweli na ile kweli itazidi kuwa Dhahiri kwa watu wote. Ndivyo ilivyokuwa kwamba Neno la kweli lilianza kufundishwa kwa uzito mkubwa sana katika majira hayo ya kuanzia Mwaka 1750- 1905


Ndio mafundisho yale yote ambayo shetani ameyaficha na giza zito lililokuwa limeificha kweli, Sasa mengi yote yakaibuka kama vile uyoga unavyoweza kuibuka hivyo kila mwaka kulikuwa na mabadiliko ya haraka sana na kasi isiyo kawaida

Tulijifunza kwa Martin Luther alifanya kazi kubwa sana na Mungu akaweza kuwa amemtumia kuweza kulitoa kanisa katika giza kubwa sana la katoliki na lakini tulijifunza kwamba alikwenda kasi kubwakuleta mabadiliko hilo na kubwa kuliko yote kwamba sasa watu walianza kuelezwa kwa unapatikana kwa Imani na si namna ya sacramenti ambazo zilikuwa zinatolewa za namna nyingi mbalimbali za ajabu kama kununua kadi kwa pesa, kutembea juu ya ngazi 28 zilizokuwa zina chupa za kuumiza magoti

Sasa Martin Luther kama tulivyojifunza, bado aliacha mambo mengi sana ambayo hakuweza kuyagusia. Miongoni mwa hayo ilikuwa ni kama UBATIZO WA WATOTO WADOGO ambao uliendelea kuwapo wakati wa Martin Luther kinyume na biblia, na UBATIZO WA MAJI TELE ulirudi katika kipindi hiki cha Filadefia na kweli ikaanza kurudi kama maandiko yasemavyo, Kila jambo likaanza kuletwa Zaidi katika kweli

Ubatizo wa maji tele ukaanza tena katik majira haya ya Filadefia na Utakaso/utakatifu ukaanza kurejeshwa(Uwatakase kwa ile kweli). Kuonyesha mahali kwenye kweli kuna utakaso kwasababu utakatifu ndio kweli yenyewe maana mtu hawezi kumuona Mungu isipokuwa kwa huo utakatifu WAEBRANIA 12:14. Vilevile huu ndio ulikuwa wakati ambapo kulikuwa na UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU ambao ulianza majira haya na watu wakaanza kunena kwa lughampya jambo ambalo lilipotea kwa mika yote tangu wakati wa kanisa la kwanza

● YEYE ALIYE NA UFUNGUO WA DAUDI

Hapa tena Yesu anajitambulisha kama aliye na UFUNGUO WA DAUDI, Yeye mwenye kufungua wala hapana afunguaye naye afunga wala hapana afunguaye

UFUNGUO WA DAUDI-Unazungumzia MIUJIZA KWA JINA LA BWANA

Daudi alitumika sana kama wengi wetu tunavyokumbuka, Kumuendea Goliathi kwa jina la BWANA na kumuua Giliati kinyume na matarajio ya watu wote akawa ameangushwa kwa jiwe dogo tu laini na kaanguka na kichwa chake kikakatwa na wafilisti wakaibika sana. Daudi hakuwa ni mtu ambaye angeweza kupambana na Goliati kwa namna yeyote ile. Daudi kumshinda Goliathi ilikuwa ni MUUJIZA MKUBWA

Kwasababu hiyo ufunguo wa daudi unazungumzia Miujiza, YEYE AKIFUNGUA HAKUNA AWEZAYE KUFUNGA na AKIFUNGA (Kama wakati wa Eliya alivyofunga mvua isinyeshe) HAKUNA AWEZAYE KUFUNGUA. Kwahiyo kufungua na kufunga inazungumzia miujiza, Ufunguo wa daudi unazungumzia miujiza

Kwahiyo Miujiza tena kwa Jina la Bwana, watu kuombewa n akupata miujiza yote haya yalianza kutokea wakati wa majira ya filadefia, maana hayakuwepo miaka yote ya kabla, Wakati wotw Martin Luther haya kuwepomambo haya ya kuombea wagonjwa, bado hayo hayakuja katika ufunua uliokuja kwake, lakini lakuja tu wakati wa majira ya filadefia ambayo ndio majira ya ufunguo wa daudi

Kwahiyo anajitambulisha hapa Yesu kristo kwamba yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, yeye aliye na ufunguo wa daudi ambaye akifunga hapana awezaye kufungua na kifungua hapana awezaye kufunga. Kimsingi anazungumzia miujiza itakayokuja kutokea tena majira haya ya filadefia (1750-1905)

● UHUSIANO WA MVINYO NA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU

Ule mvinyo sasa ambao tumeona habari zake katika mji wa filadefia ulikuwa unaashiria UJAZO WA ROHO MTAKATIFU

WAEFESO5:18

Tena msilewe kwa mvinyo,  ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;

Mvinyo umekuwaq ukihusishwa na Ujazo wa Roho mtakatufu kama kwa wanafunzi wa Yesu katika Matendo sura ya pili walipojazwa Roho mtakatifu watu waliowazunguka waliokuwa hawajui kitu walisema wamelewa kwa mvinyo

Kwanini Ujazo wa Roho Mtakatifu unahusishwa na Kulewa kwa Mvinyo?

Mtu akiwa amejazwa Roho mtakatifu anakuwa na tabia ambazo zinakuwa ndizo hizo zinafanywa kulinganishwa kwa ujazo wa Roho mtakatifu na kuelewa kwa mvinyo

Kwa kawaida utaweza kuona watu wakiwa wanakunywa pombe watakueleza kwamba wakishakuwa wamekunywa pombe wanakuwa HAWANA AIBU(AIBU INAONDOKA). Kwahiyo unaweza kufanya mambo Fulani Fulani ambayo wasingeweza kufanya kama wasingekuwa wamelewa kwa pombe. Pombe inampa mtu ujasiri ambao asingekuwa nao vinginevyo, Wanaweza kuzungumza na mtu macho makavu, wakamuangalia kwa ujasiri, akizungumza neon lolote ambalo asingeweza kuzungumza nae bila pombe

Mlevi wa pombe anaweza kupita katika msitu wenyewe wanyama wakali akiimba kwa namna asingeweza kufanya bila pombe hiyo. Hivyo pombe utaona inaongeza ujasiri watu hawa, Ujasiri wa kuzungumza maneno ambayo asingeweza kuzungumza kabla

Sasa Sifa/Tabia hiyo kwa upande wa pombe inakuwa ni Negative(Inatokana na matendo mabaya) inakuwa ni tabia isiyo halisi, Sasa tabia halisi ambayo iko katika usafi na utakatifu inapatikana katika Ujazo wa Roho mtakatifu

Mtu akiwa amejazwa Roho mtakatifu Aibu uondoka, Anaweza kuzungumza kwa ujasiri, Anaweza kushuhudia, Anaweza kuhubiri kwa ujasiri, Anaweza kuzungumza maneno asingeweza kuyazungumza bila kujazwa Roho mtakatifu. Petro aliweza kuwa ujasiri hata kuweza kuwahubiri watu 3000 wakaokoka baada tu alipopokea nguvu ya Roho mtakatifu au Ujazo wa Roho mtakatifu

Kwahiyo ujazo wa Roho mtakatifu ulikuja kutokea wakati wa majira ya Filadefia, watu wakaanza kulihubiri Neno kwa ujasiri bila uoga kila mahali kwa dalili na nguvu za Roho mtakatifu kwa nmna isiyo ya kawaida kwa ishara na maajabu ya kushangaza hata uhamsho usio wa kawaida ukaanza kutokea kila mahali

Kwasababu hiyo Bwana Yesu anajitambulisha kama yeye aliye Mtakatifu, Yeye aliye wa kweli, Yeye mwenye Ufunguo wa Daudi, Akifunga hakuna awezaye awezaye kufungua na akifungua hakuna awezaye kufunga. Kwahiyo kulikuwa na kufunguliwa kwa injili kwa namna ambayo haijawai kutokea kabisa huko na ilikuwa ni kilele kabisa cha mabadiliko yaliyotokea miaka mingi tangu nyakati zile za karne za mwanzoni ambazo tumekuwa tukiangalia katika unabii hatua kwa hatua katika majira yote yaliyopita


(3) SIFA NJEMA ZA KANISA

UFUNUO 3:8

Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu

Hawa Filadefia waliokuwepo nyakati hizo walilitunza neno la Bwana pamoja na kuzungukwa na makanisa mengi ambayo yamechuliwa na Mafundisho ya Yezebeli, yamechukuliwa na mafundisho ya wanikolai na makanisa kama sardi ambalo lilikuwa linaonekana hai kumbe lilikuwa n amatatizo makubwa, walikuwepo na watu wanafki. Hapa Filadefia walilitunza Neno la Bwana Yesu na kulishika Neno lake kama lilivyo na hawakulikana jina la Bwana Yesu

Mahali hapa tunajifunza kwamba tunaweza sisi nasi kama kanisa tukawa kama kanisa la Filadefia kwamba wamezungukwa na makanisa mengi sana yaliyokuwa mbali na neon yamechukuliwa na mafundisho ya wanikolai na Mafundisho ya Yezebeli lakini bado wakawa wanalishika Neno la Kristo kama lilivyo, bado hawakulikana jina lake katikati ya giza kuzunguka sehemu nyingine bado wao Filadefia waliendelea kulishika Neno la Mungu kama lilivyo na Yesu anasema TAZAMA NIMEKUPA MALANGO ULIOFUNGULIWA MBELE YAKO

Kwahiyo hapa kimsingi Sifa njema za kanisa la Filadefia lilikuwa kwamba WALILISHIKA NENO KAMA LILIVYO, Tangu nyakati zile za zamani lilivyokuwa likifundishwa nyakati zile za Mitume mwanzoni kabisa mpaka wakati wa Yohana huu ambapo anapeleka waraka kule bado hawa walikuwa wanalishika Neno kama lilivyo na kulitendea kazi walikuwa hawajaweza kuchuja Neno lolote

(4) KALIPIO

Kristo Yesu alipendezwa sana na kanisa hili, ndio maana unaweza kuona kuwa hakuna kalipio lolote lile alilowapatia kanisa hili.

Tukikaa katika Neno la Kristo kama lilivyo kama ambavyo lilifundikwa wakatiwa Kristo yesu wakati wa Mitume hatutaweza kukalipiwa. Yesu Kristo hawezi kusema NINA NENO JUU YAKO. Ina maana Yesu kristo ni kweli, Tukikaa katika kweli tukikaa katika Neno la Kristo kama lilivyo Yesu Kristo atapendezwa sana nasi. Na kaka zangu dada zangu hatuna budi kutafuta kumpendeza Mungu Yesu Kristo aliye kweli kuliko kutaka kuwapendeza wanadamu


Na tukiwa tumekaaa katika Neno la Mungu kama lilivyo ndipo tunapoweza kumpendeza Mungu upeo na hatutapata kalipio, Hatutaambiwa NINA NENO JUU YAKO kama walivyokalipiwa makanisa haya mengine tuliyoangalia habari zake ambayo wenyewe walikengeuka na kuiacha kweli. Tukitaka kumpendeza Roho mtakatifu hata atembee nasi na Kristo Yesu akae pamoja nasi(Kumbuka amesema atakuwa pamoja nasi hata ukamilifu wa Dahari) Laini anakuwaje pamoja nasi hata ukamilifu wa Dahari?Sasa hilo linatuleta katika Kutafakari Sehemu ya Tano(Maelekezo Kuhusu Jinsi ya kufanya)

 

(5) MAELEKEZO KUHUSU JINSI YA KUFANYA

{UFUNUO 3:11}

Naja upesi.  Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako

Ø SHIKA SANA ULICHO NACHO(SHIKA SANA NENO SIO SHIKA SANA DINI)

SHIKA SANA ULICHO NACHO-Maneno yanayozungumzwa hapa wengine kwa faida zao binafsi na upotofu wamekuwa wakifundisha watu kwamba SHIKA SANA DINI ULIYO NAYO, MTU ASIKUDAGANYE ambayo umerithi tangu wazazi wako, umeiirithi tangu kwa babu zako

Maandiko hapahayazungumzi tushike dini tulizo nazo ambazo zinatuongoza katika upotofu. Martin Luther hakushika sana katoliki, Alipokuta kuna makosa chungu mzima ambayo aliyaweka kwenye ubao, alizungumza juu ya ukengeufu wa katoliki waziwazi na hakushika sana dini ya katoliki lakini alizingatia Neno linasema nini?. Na hapa Yesu Kristo hatuambii tushike dini! Hapana! Dini zitakuja na kupita lakini Neno la Mungu linadumu hata milele. Na tunachotakiwa kushika ni NENOLA MUNGU

Pale ambapo tutakuwa tumekwenda katika dini nyingine, hatutakuwa tumekwenda kwa kupenda dini hiyo lakini kama tunatoka dini moja kwenda dini nyingine basi msingi uwe ni kwamba kuhamia sehemu nyingine tumeshapata uhakika kwamba kule wanalishika Neno, Kule wanaongozwa na Neno, Hapo ndio tunakuwa tunampendeza Mungu

Yesu Kristo anasema SHIKA SANA ULICHO NACHO alimaanisha SHIKA SANA NENO, Utaona hilo katika mstari wa 10 uliotangulia wa UFUNUO 3:10 ndio utatupa ufunguo wa kujua maneno haya SHIKA SANA ULICHO NACHO Ulimaanisha nini?

{UFUNUO 3:10}

“Kwa kuwa UMELISHIKA NENOLA SUBIRA YANGU……………….. ”

Umeona inasema Kwakuwa umelishika Neno basi SHIKA SANA ULICHO NACHO. Hapa maelekezo ya kufanyani SHIKA SANA NENO, SI SHIKA SANA DINI! HAPANA!!!. Mungu hapendezwi na sisi kushika sana dini ambayo inatupa kukengeuka na kuiacha kweli. Neno la Mungu ndio kweli hiyo maanake kwa lolote lile tunalolifanya katika ibada zetu katika kumuabudu Mungu lazima tuliangalie katika maisha yetu yote kwaujumla wake, Lazima tuliangalie JE HILI LINALOFANYIKA LINAFANYIKA SAWA SAWA NA NENO? Kama halifanyiki sawa sawa na Neno hatunabudi kulitupilia mbali na kushika Neno

Na Martin Luther aliangalia mambo mengi yaliyokuwa yanafanyika nyakati za katoliki, hizo za giza, akagundua mambo chungu mzima aliyoorodhesha mambo 95 katika ubao wa kanisa la MT PETRO yaliyokuwa hayaendi sawa sawa na Neno. Na sisi nasi lazimawakati wote tuangalie hili au lile linaendana sawa sawa na Neno la Mungu ?Tunashika sana Neno sio Dini

Ø WAJIBU WA KUACHA DINI ZETU ZA ZAMANI ZA WAZAZI

Lazima tuelewe vizuri na tusiogope kuacha dini zetu kabisa, pale ambapo tunaona dini zetu zina mafundisho yaliyo kinyume na Neno, Sasa tujue tupo katika ukengeufu, Tujue tupo katika upotofu. Kwasababu Mungu anataka sana tushike sana Neno si dini.

Na Paulo Mtume anajieleza waziwazi jinsi alivyoacha dini yake!Yeye alikuwa Farisayo mwana wa Farisayo na anasema alishika kwa uzito mkubwa dini yake hiyo lakini alipopata Ufunuo wa kipekee kutoka kwa Bwana Yesu hakutaka shauri na wanadamu bali aliachana na madhehebu hayo aliyokuwa Miaka nenda na Miaka rudi

{WAGALATIA 1:13-16}

Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu.  Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;

Paulo Mtume zamani katika dini ya kiyahudi, Lakini hakufanya shauri na watu wenye mwili na damu bali aliacha dini ya kiyahudi baada ya kugundua yale yaliyokuwa yakifundishwa humo yamekuwa potofu, Wamekuwa wakimkana Bwana Yesu kuwa si masihi. Hivyo akaiacha dini ya kiyahudi na kajiunga na WATU WA NJIA ILE, Alijiunga na Dhehebu ambalo linatajwa lilikuwa linanenwa vibaya kila mahali ambalo ni kanisa la kwanza ndilolilikuwa linanenwa vibaya kila mahali lakini ndio lilikuwa dhehebu jipya la Paulo Mtume MATENDO 28:16 -22

Dhehebu jipya la Paulo Mtume ndio lilikuwa linanenwa vibaya kila mahali na ndilokanisa la kwanza (Watu wa njia ile). Kwahiyo aliacha dini yake na akajiunga na dini mpya kwasababu alikuwa anataka kukaa katika kweli ya Neno la Mungu

Kwahiyo Kaka zangu na Dada zangu mtu anapokwambia mbona umeiacha dini ya Baba yako au mama yako, Wewe umeacha dini yako, uwaeleze watu hawa kuwa Paulo mtume aliacha dini ya kiyahudi akaingia dini Nyingine ili kuifuata kweli na paulo Katia 1WAKORINTHO 11:1 anasema MNIFUATE MIMI KAMANINAVYOMFUATA KRISTO !Halleluyah

Kwa maana nyingine tunafundishwa kuachana na dini ambazo haziko sawa na kweli ya Neno na kwenda katika dini ambazo ziko katika jitihada za kukaa katika kweli ya Neno. Na tusishikirie tu dini za wazazi, Martin Luther hakufanya hivyo wala Paulo mtume hakufanya hivyo, kila mmoja alikuwa na lengo la kukaa katika kweli ili ampendeze Mungu

{EZEKIEL20:18-19}

Kisha nikawaambia watoto wao jangwani, Msiende katika amri za baba zenu, wala msizishike hukumu zao, wala msijitie unajisi kwa vinyago vyao. Mimi ni Bwana, Mungu wenu; endeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda;

Mungu anasema msiende katika njia za baba zenu bali muende katika njia ya Neno. Kwahiyo Mungu wetu ndio maana anasema Shika sana Ulicho nacho, Shika sana Neno maana ndio kitu cha thaman. Kaka zangu na dada zangu siku ile tutakapotoka katika ulimwengu huu, Hutaulizwa ULIKUWA DINI GANI? Hapa kitakachoangaliwa JE ULIKAA KATIKA KWELI? ULIKAA KATIKAUSAFI NA UTAKATIFU? ULIFUATA MAONGOZI YA KWELI?

Ø HATUTAHUKUMIWA SAWA NA SHERIA ZA MAONGOZI YA MAKANISA YETU BALI INJILI YA PAULO MTUME

Katika siku ile ya hukumu mbele ya kiti cha Enzi cha Hukumu atakachokikalia Bwana Yesu atayapima matendo yetu Sawa sawa na Injili aliyohubiri Paulo mtume

{WARUMI 2:16}

“Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu”

Maandiko hayasemi tutahukumiwa sawasawa na sharia za kanisa Katoliki, Hapana! Halisemi tutahukumiwa sawa na Sheria za KiLutherani, Anglikana au Moroviani bali sawa sawa na injili ya Paulo Mtume kwa Kristo Yesu

Lazima tuishi na kujipima, Je tunaishi sawa sawa na kweli iliyohubiriwa na Paulo Mtume?Je tunaishi sawasawa na kweli au la?Kama tunaishi sawasawa na maongozi yanayotokana na kidhehebu tumepotea, siku ile tutahukumiwa kuwa wakosaji. Tutaaibika kama hatutayaangalia kuyatii maagizo yote ya Mungu {ZABURI 119 :6, 9}.

Tafuta kukaa kwenye kweli usiangaike kwamba umeshika hili na lile lakini hili jingine haujashika, Hapo hautasalimika hata kidogo. Sasa hivi unaposoma ujumbe una nafasi ya kuelewa kweli ya kila Neno tunalojifunza katika biblia kama tulivyokwishaelekezana tangu mwanzo wa mfululizo huu, Sasa unatakiwa kushika maagizo ya Bwana yote, Sio moja au mawili eti unasema na mimi nimeokoka lakini Ubatizo wa maji tele Hapana!Utaaibika siku ya mwisho maana andiko linasema katika ZABURI 119:6 kuwa ndipo mimi sitaibika nikiyaangalia maagizo yake yote. Zaburi 119:9 ili tupate kumpendeza Mungu Hatunabudi kutii na kulifuata Neno la Mungu

Ni kweli hatutaibika tukilifuata Neno la Mungu sio tukifuata maongozi ya kidini au maongozi ya kimadhehebu yetu tuliyorithi kwa wazazi wetu! Hapana Ndio maana Yesu anasema SHIKA SANA ULICHONACHO Sio shika sana maongozi ya dini yako au dhehebu lako

Ø TAHADHARI YA UCHAGUZI WA KANISA TUNALOPASWA KUSALI

Lazima tuwe makini sana na madhehebu hayakwa umakini usikae katika kanisa ilimradi tu unakaa katika kanisa unalokaa au unaloshiriki linaweza kukupa mwelekeo wa kwenda motoni au mwelekeo wa kwenda mbinguni sio kitu cha mchaezo

Unaweza kuwa umekaa kwenye kanisa la Sardi ambalo lina jina la kuwa hai kumbe limekufa, Pia unaweza ukawaunashiriki kwenye kanisa la Thiatra ambalo limechukuliwa na mafundisho ya Yezebeli, Mafundisho ya wanikolai, Unaweza ukawa unasali na kushiriki kwenye kanisa la Efeso ambalo limeuacha Upendo wake wa kwanza !Kumbe si swala la kushiriki kanisa ilimradi liko karibu, Hapana!Kanisa la Sardi lipo karibu tu eti basi niwepo hapo!Kanisala Thiatra lipo karibu basi niwepo hapo! Hapana.

Tafuta wakati wote kuwepo katika kanisa kama kanisa la Filadefia mahali ambapo utakaa katika Neno la kweli, Mahali ambapo utaongozwa katika kutokulikana Jina la Bwana Yesu. Utaongozwa katika Neno hata kama kanisa la Filadefia lipo mbali kiasi gani? Maana linaweza kuwepo moja katikati ya makanisa yote 7 ambalo limekaa katika kweli, Linaweza likawa moja au mawili.

Tumeona ni Kanisa la Filadefia halikupata kalipio na kanisa la Smirna pekee yao hayakupata makalipio. Yanaweza kuwa ni mawili katika 7. Hivyo tafuta wakati wote mahali ambapo watakaa kwenye Neno, Hawatakuwa ni watu wanaoikana Imani kwa namna moja au nyingine

Na usichukuliwe na kukaa mahali ambapo wapo mawaziri au Rais wanasali hapo eti na wewe ndio unasali hapo! Hatutafuti mahali ambapo Rais anasali au mahali pa heshima lakini tunatafuta Neno si heshima au majengo mazuri! Shika sana Neno, kaamahali ambapo Neno liko! Tafuta Kanisa la Filadefia

Usikae tu Mahali ambapo Neno haliko!!Tunamshukuru Mungu yapo makanisa machache bado Dar na Tanzania ambayo yana mfano wa kanisa la Filadefia! Haya ni Lulu ya kujivunia ambayo hata kama makanisa yote yatachuja viwango vya utakatifu yenyewe bado yatalishika Neno kama lilivyo na ndiomana shetani anapiga kelele anasema MSIENDE HUKO!!Utaona litakuwa ni kanisa linalonenwa vibaya kila mahali kwasababu shetani anaijua Kweli inayofundishwa kwenye makanisa ya aina ya Filadefia.

Ndio maana hata wakati wa Paulo mtume shetani alipiga kelele akisema watu hawa ni watu wanaohubiri njia ya wokovu! Shetani anajua njia ya wokovu kuliko hata unavyofikiri! Shetani anatakatukae kwenye makanisa ambayo yana majina ya kuwa hai kumbe yamekufa!!Oooh tutafute Lulu kwa gharama zozozte tusitafute heshima kwa wanadamu, Tutafute mahali ambapo tutajinza Neno kama hivi na kujiona kila siku umepungukiwa bado hujafika kwenye kimo cha Utimilifu wa Kristo!

Lakini nyakati tulizo nazo walipoaanza kusikia wimbi la wokovu na watu wanabadilishwa na kutoka kwenye madhehebu yenye mafundisho manyonge na kuitafuta kweli ilipo, wametokea watu ambao wanazunguka huku na huku siku za katikati kutafuta Neno lakini siku za jumapili bado wanaendelea kushika madhehebu yao na dini zao na ndio hawa ambao nao unawasikia eti wameokoka katikati ya sanamu, Wanaanzisha vifelloeship vidogo vidogo vya wanaojiita wameokoka ndani ya kanisa ambalo Msingi wake haliamini hata wokovu huona bado wanashilia mapokeo mengi tu ya kidini

Na wengine wanazunguka huku na huku kutafuta maombezi badala ya Neno kama wana kwenda Cliniki au hospitali lakini wakishamaliza kuombewa na kuhudumiwa wanazirudia sanamu na dini zao na kushika mafundisho yale ya kidini bila badiliko lolote. Na wengine wanazunguka kujifunza kwenye makanisa ya Neno alafu wanarudi na masomo yale kufundisha kwenye fellowship zao

Ø KUBADILIKA KWA MAJIRAYA KUFUNGULIWA MLANGO WA MADHEHEBU YA KWELI

Unajua yapo mambo mengine hayawezi kufundishwa LUTHERANI!Ukipiga kelele ya Ubatizo wa Maji Tele huko Lutherani, Unapoteza Muda wako!Utatengwa !Kwahiyo usigombane na watu, hama Nenda kweye makanisa yanayohubiri Kweli ya Neno

Ukisimama katoliki ukaanza kuyapigiza masanamu yao, Ukaanza kupigiza ibada zao za kufukiza mamoshi ya Uvumba! Utakosana na watu, unaweza kukung’utwa hata makofi kwasababu misingi ile imeshikwa miaka Nenda rudi! Mungu amejaribu kushughulika nao, haikuwezekana mpaka Martin Luther akatoka katikati yao! Wewe unaanza kitu gani sasa hivi?

Haya ni majira ya unabii mengine ambayo Mungu ameshatutoa kule katika kusukumana na Katoliki, katika kushughulika nao, Mungu amekwisha kututoa kule, Kwasababu Mungu alikwishashughulika nao kwa miaka nenda miaka rudi, Akaachana nao! Akainua kitu kingine na hiki alikitabiri tangu miaka mingi! Sasa hivi hatuanzii hapo kwasabu kule tulikwishatoka. Sasa hivi tupo katika majira mengine ya mwisho tunamngojea Bwana Yesu

Na mambo haya MLANGO UMEKWISHAFUNGULIWA tayari amekuja akiwa na Ufunguo wa Kufungua,  AMEKWISHAFUNGUA MLANGO! Yakaja makanisa Mengine tena ambayo yanasimama katika kweli!!UNANG’ANG’ANA NA KATOLIKI YA NINI WEWEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!?????????

Amekuja kama yeye aliye na UFUNGUO WA DAUD kuliangusha Ligoliati hilo chini, KATOLIKI na amekuja kusema TAZAMA MIMI NITAFUNGUA na NIKIFUNGUA HAKUNA AWEZAYE KUFUNGA. Katoliki haikutaka makanisa haya mengine yapo, haikutaka uamsho wala chochote cha kupinga Katoliki lakini Yesu akasema Nitafunguana na Hakuna wa kufungua! CAMMON!!!

Mungu akafungua tangu wakati wa Martin Luther akamalizia hiyo kazi kama tulivyojifunza hatua kwa hatua kulikuwa hakuna hiki hapana pale lakini ghafla kuanza kutokea hiki hapa na pale na ndipo yalikuja majira ya Filadefia ambayo akawa amefungua, Sasa mambo mengi ambayo hayakuwepo sasa ameyafungua na ameyaweka wazi yapo katika madhehebu mengine! LAKINI NASHANGANGA UNANG’ANG’ANIA NINI KUBAKI KATOLIKI? Eti wewe utasimama ulipindue likatoliki, ulibadilishe? Unapoteza muda wako ndugu yangu!

Hujui hata majira yanavyokwenda na kubadilika!!huu sio wakati wa kuangalia habari hizo tena !Hiyo kazi Mungu alikwishaipitia, Sasa hivi unapokuwa moja kwa moja umeokolewa unajua moja kwamba hapa katoliki ni pakuachana napo kabisa! Mahali ambapo HAKUNA UBATIZOWA MAJI TELE, Mara moja unakimbia unafuata kweli kwenye Kanisa la aina la Filadefia katika JINA LA YESU!!!

Katika Neno hili ninakwambia kweli, sikwepeshi hapa!Ina maana Yesu anasema Tulishike Neno, sasa unawezaje kusema umeokoka, unakwenda mbinguni bado uko kwenye sanamu?Nani amekudanganya wokovu wa namna hiyo?Wokovu na masanamu umeona wapi?Huu ni upagani moja kwa moja

Wengine wanaenda kwenye Baadhi ya makanisa yanayohubiri Kweli bila kupindisha wala kuangalia uso wala sura ya mtu, Mahali ambapo kuna Misingi yake kwenye kanisa hilo ndio maana wapo hivyo wanalipokea Neno hilo wanalofundishwa kwa furaha ila wako watu wengine wanachukua mafundisho kwenye kanisa hilo ambayo wamejifunza labda MALIPIZO JUU YA NDOA ambapo inaelezwa kuwa ni MUME MMOJA, MKE MMOJA MPAKA KIFO KIWATENGANISHE wanachukua masomo hapa kama kwenye hizo Makala alafu wanaenda kufundisha makanisani yao huko!Kule unakoenda kufundisha unaenda kukung’utwa !ukienda kufundisha juu mme mmoja, mke mmoja mpaka kifo kiwatenganishe kule watakwambia usituletee mafundisho hayo hapa

Sasa Mungu amekwishafungua mlango, ingia kwenye mlango uliokwishafunguliwa wewe!!Acha kuchukua vitu hapa unavipeleka kule! HUWEZI KUJENGA MSINGI JUU YA MSINGI MWINGINE ULIOKWISHA KUWEKWA ! Ni lazima kuwepo na Msingi wa Neno, Msingi wa kweli uwepo tangu mapema !wawepo watu tangu juu kule ambao wamemaanisha kukaa katika kweli kama Neno lilivyo! Kama hakuna kitu kama hicho, utaangaika, utapoteza muda wako!Utakosana na watu na kuvurugana na watu na utaonekana mpuuzi kumbe una kitu cha kweli!Na ndivyo ilivyokuwa kwa Martin Luther alitoka katikati yao, na tena na tena ilikuwa hivyo Mungu anainua hawa, anainua yule kwa lengo lakuwarudisha watu kwenye kweli ya kanisa la kwanza

Lazima tuwe na macho ya kuangaliana kuona hapa ndio kwenye kweli hii na hii ndio kweli? Tunaona haya na yale yanayofanyika hapo, Je yanaendana sawa sawa na Neno? Tukiona wapo sawa na Neno hapo tunang’ang’ania, Tujue tumepata Lulu ndipo Yesu anasema SHIKA SANA ULICHO NACHO

Acha kusikiliza maneno ya kipuuzi ya wazazi ETI NITAKULAANI! Utalaani nini? Huyu mtu anafuata kweli, anamfuata Mungu, Sasa utamlaani katika MUNGU yupi? Maana Yesu anasema Baba hakuniacha kwasababu siku zote nafanya yale yampendezayo!!! Sasa huyu analenga kusogea zaidi katika kumpendeza Mungu na wewe unasema utamlaani? Utamlaani vipi? Mamlaka hiyo ya kumlaani unaitoa wapi na kwa Mungu yupi? Unamlaanije mtu ambaye Bwana hakumlaani? Huu ni Uupuuzi wa ibilisi MITHALI 26:2

 

(6) AHADI

Ø TAZAMA NIMEKUPA MLANGO ULIOFUNGULIWA MBELE YAKO AMBAO HAPANA AWEZAYE KUUFUNGA

{UFUNUO 3:8}

Nayajua matendo yako.  Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga,  kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu


Kaka zangu dada zangu nataka niwaeleze jambo moja kwamba Kristo Yesu anatafuta Mhubiri ambaye atasimama kwenye kweli ili ampe sapoti yote ndio maana anasema Nitampa mlango uliofunguliwa. Lakini wapo watu wengine Utaona wanakimbilia vitu, wao wanatafuta vitu, wanatafuta maspika, wanatafuta microphone, wanatafuta majengo, wanatafuta Pesa!Hivi vitu ni vidogo vya kipuuzi, si vitu vya kuweka kipaumbele bali tunachotakiwa ni kutafuta ile sapoti ya Bwana Yesu katika huduma zetu


Yesu Kristo anasema Enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi na kuwabatiza na kuwafundisha kushika yote nilitowaaamuru MATHAYO 28:19. Tukiwafundisha kuyashika yote, sio moja moja, sio nusu nusu bali tukiwafundisha kuyashika yote aliyotuamuru katika Neno, Yesu anasema ATAKUWA PAMOJA NASI HATA UKAMILIFU WA DAHARI


UKAMILIFU WA DAHARI maana yake ni Majira mpaka majira haya ya kikomo, Majira ya mataifa wakati wa kunyakuliwa kwa kanisa !. Sasa ndio anasema atakuwa pamoja nasi mpaka Ukamilifu wa Dahari

Na hapa anasema TAZAMA NIMEKUPA MLANGO ULIOFUNGULIWA MBELE YAKO, AMBAO HAPANA AWEZAYE KUUFUNGA,  yaani kama tukikaa kwenye kweli hii ndio ahadi ya Yesu Kristo!. Kama tunasimama kwenye kweli, tunafundishwa kweli, tunaongoza watu katika kweli, Yesu anakuwa pamoja Nasi kwa namna isiyo ya kwaida! Anasema ametufungulia mlango!


Watu ambao wana ujasiri wa kuhubiri kweli si wengi, si wote! Watu ambao watasimama katika kweli kwa gharama yeyote, si wengi, si wote! Kristo Yesu akimpata mtu mmoja anayeweza kusimama kwenye kweli, Hii ndio ahadi yake anamfungulia mlango mbele yake ambao hakuna awezaye kuufunga


Ndio maana yapo makanisa yanayosimama kwenye kweli yapo miaka nenda miaka rudi, Pamoja wachungaji wengine waliokinyume na huduma hiyo ya kweli wamepiga kelele madhabahu zote mjini, kila kona katika nchi! Kuwa msiende huko! Kanisa hili au huduma hii ifutwe! Lakini yote hayo hayawezi maana ameshasema Hakuna awezaye kuufunga!Maanake kadinali hawezi kuufunga!Rais hawezi kuufunga wala hakuna yeyote awezaye kuufunga!


Kama tunakaa kwenye kweli Kanisa hilo linakuwa ni LULU maana anasema anafdungua mlango mbele yetu wala hakuna awezaye kuufunga!Msajili wa mambo ya ndani hawezi kulifuata kanisa au huduma ambayo linakaa na kusimama kwenye kweli!Neno la Mungu limeshasema kwamba Nimefungua mlango mbele yako wala hakuna awezaye kuufunga!Hiyo ni FULL STOP !! AMINI NA KWELI!


Katika vizazi na vizazi vinaweza kupata fikiria Tangu wakati ule wa Yohana mtume wa Kanisa la kwanza, miaka iliyofuata mbele yake karibu miaka elfu na kitu kama miaka 1500kulikuwa hakuna kweli hii tunayoizungumza kulikuwa ni giza zito la kutisha!Utaweza kuona hivi vitu vinakuwa nadra kupatikana!Usifikiri ni rahisi rahisi tu kuvipata mahali ambapo wanasiamama kwenye kweli yote bila kuchukuliwa na Uvuguvugu wa makanisa unaoyazunguka


Sio Rahisi kumpata mtu mmoja kama Martin Luther, Martin Luther mmoja unaweza kumpata baada ya miaka mingi sana sana kwasababu gharama zake ni kubwa! Kwahiyo kinapotokea kitu cha namna hii kinakuwa ni lulu!na ndio maana Kristo Yesu anasema Ninafungua mlango kweli kweli hakuna awezaye kufungua


Usipoteze muda wako kushindana na kweli! Usipoteze muda wako na mahali ambapokweli inahubiriwa na kufundishwa utakuwa kama unajiumiza mwenyewe kwa kugonga ukuta!Huwezi kushindana na kweli!Kweli ni kitu ambacho ni Lulu, Ni kitu ambacho Mungu anataka watu wote wakae kwenye kweli ndio maana Roho mtakatifu anawaongoza watu na kuwatia kwenye kweli!Nani wewe mwanadamu kinyangarakata unaweza kwenda kinyume na kweli? Hakuna utakuwa tu Unapoteza muda wako, fanya mambo mengine, ni bora ukauze nyanya sokoni! Maana aliyefungua ni Yesu mwenye UFUNGUO WA DAUDI hivyo acha kabisa kushindana na mwenye Ufunguo wa daudi


Ndugu zangu tukae kwenye kweli! Kuna mashinikizo chungu mzima, kila kona kila mahali, ilina sisis kanisa letu(Kanisa lolote linalosimama kwenye kweli) tupunguze viwango!Tukipunguza viwango tu vya Neno, huyu mwenye Ufunguo wa Daudi anaondoka na ahadi hii inakuwa haifanyi kazi tena kwetu na inaamia kwingine


Sasa ndio maana tunatakiwa tuwe makini, mtu yeyote akitaka kuleta mdomo mdomo, kutufanya tupunguze viwango hivi, tunapaswa kumtimua haraka! Mtu yeyote akija akisema hapa tumezidisha viwango vya utakatifu! TOKA NENDA ZAKO KWINGINE KWENYE DHEHEBU JINGINE!!

Ukimsikia mtu anapiga kelele na kuhoji upuuzi eti oooh mbona madhehebu mengine yanafanya hivi na vile !TOKA NENDA KWAO! Hapa Hapa kwenye Kanisa letu tumedhamiria kukaa kwenye kweli bila kuangalia wengine wanafanya nini!TOKA NENDA HUKO KWAO!USITULETEE MAMBO YA MADHEHEBU MENGINE HAPA. Sisikama kanisa hatupo kuongozwa kama madhehebu mengine yanavyojiongoza yanavyotaka kwa uhuru wao bali sisi tunaongozwa na kweli ya Neno la Mungu


Ujue Mchungaji wako ikiwa anahubiri kweli, anahitaji watu wa kumsapoti, anatafuta watu vichaa kama yeye wakusimama kwenye kweli kwa gharama yeyote na kuishindania!Tukikaa namna hiyo Bwana Yesu atatufungulia mlango mkubwa !Wwako watu wengine ambao hawaelezwi !Wakisia tu kanisa linafutwa!Tayari ameshaondoka !Anavizia vizia akiona halijafutwa anakuja amekaa tena !Kwasababu hawajui maandiko hawa!


Ndugu zangu lazima tujue ikiwa Hapo ulipo wanahubiri na kufundisha kweli yote, Unatakiwa ujivunie kweli iliyopo hapo na ujue Bwana amewashushia Neema kwamba TAZAMA NIMEKUPA MLANGO AMBAO UMEFUNGULIWA MBELE YAKO HAPANA AWEZAYE KUUFUNGA Kwakuwa una nguvu kidogo nawe umelitunza Neno tangu wala hakulikana jina langu


Ø TAZAMA NAKUPA WALIO WA SINAGOGI LA SHETANI

{UFUNUO 3:9}

“Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda. ”

Hapa inasema WALE WASEMAO NI WAYAHUDI KUMBE SIO inazungumziwa Wale wanaosema wameokoka kumbe sio ni wanafki Hivyo Yesu anasema Kama tunakaa kwenye kweli si tu atatufungulia mlango bali hao wengine wote walio sinagogi la ibilisi nitakupa wewe!!


Hii ndio maana mahali popote kwenye kweli watu watakuwa wanamiminika kutoka Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi wanaletwa na Yesu, maana amesema NAKUPA! Ndio maana hawa wasiokaa kwenye kweli wanabaki wanapiga kelele Mbona watu wanataka kwetu itakuwa Mhubiri Fulani anaiba kondoo zangu! Sio yeye anaiba bali NAPEWA NA YESU! Utawasikia wanalalamika Oooh Mchungaji Fulani anachukua watu wetu tena wale vizito vizito ndio wanaondoka !Na bado wataondoka wengi maana Yesu anasema Nakupa maana Kondoo sio wako ni wa Bwana

Bwana Yesu atawatoa kwako huko kwasababu anataka awalete kwenye kweli, Maana Neno linasema Roho mtakatifu anawaongoza watu na kuwatia kwenye kweli yote, na hiyo ndio kazi ya Roho mtakatifu anawatafuta wale wanaopenda kweli ila wapo kwenye sinagogi la shetani anawatoa huko na anawaongoza na kuwapeleka kwenye kweli yote


Kumbe kama unataka kanisa lako likue Fundisha kweli, Acha bla bla, Acha maneno maneno, Au sio wa kwako atapewa Mtumishi mwingine anayehubiri kweli. Utashangaa unao 10 ila 8 wote wanataka wanakwenda kwa Mtumishi anayehubiri kweli. Kwasabu aliye na vingi atazidishiwa na yule aliye na vichache hata hivyo alivyo navyo atanyang’anywa na kupewa mwenye vingi. Hii ndio kanuni


Kwahiyo ndugu yangu nakupa shauri wewe mhubiri tena ushauri wa bure kwamba unataka kanisa lako liongezeke! Fundisha kweli ya Mungu kama ilivyo bila kuchuja mambo Fulani Fulani unayoyaona ni madogo!Na! Na sio kufundisha kweli bali wewe mwenyewe uiishi kweli sio unafundisha kweli ya utakatifu alafu wewe mwenyewe unaishi maisha ya ajabu ajabu


Kuna watumishi anahubiri kweli ila naishi maisha ya ajabu anapigana na mkewe!Nani atakaa kwenye kanisa hilo? Wewe unamkung’uta mkeo, washirika wanaona tena hadharani, unamwambia “mke wangu si chochote si lolote! Huyu ni shetani mkubwa”. Wewe ukimuita mke o shetani maanake unajiita wewe mwenyewe shetani! Wewe si ndio kichwa? Sasa kama mkeo ni shetani, wewe je ni nani? Maanake kama mkeo ni shetani, wewe ndio kichwa cha shetani!


Kwahiyo wapo hata viongozi wa kanisa wanabondana na kuvurugana na wake zao, washirika unafikiri hawawaoni? Wanalazana nje, wanazungumza maneno ya ovyo na kutukanana!! Washirika wanaangalia tu, Hivyo Ukisimama na kuhubiri au kufundisha wao kuwa neno linasema hivi, Wanakuangalia tu wanakuona mnafki mkubwa! Jihubiri wewe mwenyewe! Jifundishe wewe mwenyewe kwanza


Ukisema “Oooh mke wangu ndio kikwazo, shetani mkubwa huyu” wewe ndio kichwa cha shetani! Kama umeshindwa kumuongoza mkeo, Utaliongozaje kanisa? Wewe muongo mkubwa, kaa utafute uso wa Mungu, akupe hekima ya kumuongoza mkeo kwanza ili mkitoka mnahubiria kweli basi muhubiri sawa sawa na kweli mnayoiishi


Wewe mkeo amevaa makorokoro chungu mzima na mikorogo chungu mzima, alafu unasema unasimamia kweli? Watakusikiliza kweli! Maana hautakosa watu 5 au 6 wa kukusikiliza !lakini wajanja watakaa watapima watakuona ni muongo maana unashindwa hata kumsimamia mkeo!Kwahiyo unaanza kuishia kweli wewe mwenyewe na ni gharama alafu ndipo unafundisha kweli alafu basi walio wa sinagogi la shetani unapewa!


Kwahiyo Kwa kanisa kukua na kuongozeka unaanza kwenye maisha yako, unaanza wewe mwenyewe kukaa kwenye kweli ya usafi na utakatifu wa Yesu alafu hayo mengine ndipo yanapoweza kumfuata na ndipo Yesu anakupa walio sinagogi la shetani


Mungu akisema nitawaleta! Nani awezaye kuzuia? Hata wapige kelele kutaka kukuchafua na kuichafua huduma yako na kuwakataza watu wasije kwako eti kuwa wewe ni nabii wa Uongo, unatumia pepo, nguvu za giza lakini utashangaa watu wanakuja tu kujazana kwako makali kwenye kanisa la kweli ya Neno


Lakini ikiwa unazungumza bla bla, mataputapu huwezi kuwafanya watu kukaa na kuongozeka kwa namna yeyote!Hivyo tunatakiwa kuhubiri kweli na kufundisha kweli ingawa ni gharama lakini tunakubali gharama hizo kama tunataka walio wa sinagogi la shetani tupewe na waletwe kwetu


Kaka zangu dada zangu tusipende maneno ya kubabaisha kinafki! Tunasema Tumeokolewa wakati sio kweli siku ya mwisho Tutaaibika na kufedheheka maana Mungu anatujua atasema sikuwajua ninyi kamwe, ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu. Kwahiyo tunatakiwa kuwa makini sana ili tuweze kuhakikisha, tunakaa katika kweli yote


Ø TAZAMA NITAWAFANYA WAJE KUSUJUDU MBELE YA MIGUU YAKO

{UFUNUO 3:9}

Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo.  Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.


Tukikaa kwenye kweli kuna baraka za ajabu sana !Hawa jamaa wanaopiga kelele juu ya huduma yako ya kweli na kukuchafua na kukupinga, wewe waangalie sana! Ukikaa kwenye kweli, hili neno litakuja kutimia bila shaka!Lazima watakuja kusujudu mbele ya miguu yako kwasababu Mungu amekupenda


Kwasababu hiyo Usibabaike na watu wanaopiga makelele ya fujo fujo chungu mzima kwa ajili yako na huduma yako, wewe wape muda tu, watakuja kusujudu mbele zetu labada sisi wenyewe tupunguze viwango au tuache kweli. Lakini kama tunasimama kwenye kweli, tuendelee kwenye kweli hiyo, hawa Utaona mmoja mmoja anatoka kila mahali, anakuja kusujudu kwasababu Mungu ametupenda!


Kumbe hiki siokitu cha kuacha kumbe kama tutaendelea kushika kweli kumbe watakuja kusujudu?oooh ndugu zangu hiki kitu sio cha kuacha na kuchuja viwango vya neno. Ukikaa kwenye kweli mahali popote unaposali kwenye kweli ilimradi ni kwenye kweli basi hizi ahadi zitatimia

Ø KWAKUWA UMELISHIKA NENO NAMI NITAKULINDA

Kaka zangu dada zangu kama tutakaa kwenye kweli na utakatifu, tunalindwa kwa namna ya ajabu sana. Maana unaweza kukaa miaka mingi mpaka ukasahau kama kuna kuumwa kwasababu Mungu kasema nitakulinda. Si unakumbuka jinsi Martin Luther alivyilinda na Mungu? Alivyokuwa aanatafutwa ili auwawe?Tunakumbuka jinsi Mungu alivyomlinda? Vile vile tunakumbuka jinsi Yohana alivyolindwa hata kwenye kisiwa cha Patmo?Mungu ndivyo alivyosema ukikaa kwenye kweli, Mimi nitakulinda

Ndugu zangu tukikaa kwenye kweli tunakuwa wa thamani kubwa sana na hii ndio kanuni kuwa Ukitaka ulinzi uongezeke, wewe kaa kwenye kweli bila kuchanganya masomo ila tunapokuwa tunachanganya masomo tunakuwa tunajiondolea ulinzi. Wewe kaa kwenye kweli, kaa kwenye usafi, kaa kwenye utakatifu, unawekewa ulinzi wa ajabu sana !Wewe ni mtu wa thamani sana ukikaa kuihubiri na kuifundisha kweli!!

Wewe mwenyewe Kumbuka kuna watu walikuwepo mahali kwenye kweli, lakini sasa hivi wameacha wapo mitaani, angalia nyuso zao tu! Kama kweli wewe ni shahidi, utakuwa umeangalia na kuchunguza vizuri !Utakuwa umeona Nyuso zao zimechakaa muda mfupi sana !wengi tukikutana nao tunaweza hata kuwasahau maana amechoka amekuwa mzee kwa muda mfupi sana

Chenye thamani ndani ya nyumba yako si ndio unakilinda zaidi?Pesa kwa kuwa ni za thamani kwako, je utaziweka popote tu? Kumbe tukikaa kwenye kweli ndugu zangu tunalindwa ndio maana ni vigumu hata kumjua kijana ni yupi na mzee ni yupi? Watu wana miaka 60 au 70 lakini ukiwaona wapo fit au imara kama chuma kwasababu wako kwenye kweli!!Kwasababu Mungu anasema atakulinda

Ø NITAKULINDA UTOKE KATIKA SAA YA KUHARIBIWA

UFUNUO 3:10 “………mimi nami nitakulinda,  utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi…”

Hapa kwasababu majira ya Filadefia yanatangulia majira ya laodikia ambayo ni majira kabla ya dhiki kubwa, sasa hapa anazungumza kwamba atalindwa atoke katika saa ya kuharibiwa

SAA YA KUHARIBIWA/KUJARIBIWA inayozungumziwa itakayoujiria ulimwengu wote kuwajaribu wakaao juu ya nchi ndio wakati wa dhiki kubwa ambayo hakuna mfano tangu ulimwengu upate kuwako

Hapa ni neno jingine linatufundisha kwamba kanisa ambalo limekaa kwenye kweli katika utakatifu hawatakuwako katika dhiki kubwa lakini hao watakatifu watatolewa/watanyakuliwa kabla ya kipindi hicho cha kujaribiwa ulimwengu wote.

Ø KUNA TAJI YA KUKAA KWENYE KWELI

UFUNUO 3:11 “Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. ”

Kwahiyo tukikaa kwenye kweli yote wakati wa majira yetu ya laodikia yanapokuwa yanafika ukingoni, Yesu Kristo anakuja kulinyakua kanisa lakini wengine wote watabaki kwenye dhiki kubwa ila sisis tutaondolewa wala hatutapambana na dhiki kubwa na ndio maana anasema NAJA UPESI SHIKA SANA ULICHO NACHO ASIJE MTU AKAITWA TAJI YAKO

Kaka zangu dada zangu tukikaa kwenye kweli kuna taji maalum inawasubiria wote ambao walimaanisha kukaa kwenye kweli na utakatifu wote bila kujichanganya na kuangalia wengine wanaowazunguka wanaishije baliwao walishika viwango vyote vya neno kama vilivyo. Hivyo kadiri tunavyokaa kwenye viwango vya usafi tunazidi kung’ara ila tusing’are kwa kujilinganisha wenyewe kwa wenyewe maana biblia inatuita hatuna akili bali tujilinganishe na Bwana Yesu ndipo tutapokea hiyo taji kama tukisimama kwenye kweli dakika hizi za mwisho

Ø ASHINDAYE NITAMFANYA KUWA NI NGUZO

UFUNUO 3:12 “Yeye ashindaye,  nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa…………….. ”

Kama jinsi tunavyofahamu Nguzo ndizo zinatumika kushikilia jingo zima lisianguke ndivyo ilivyo katika kanisa Mungu anasema tukikaa kwenye kweli yake basi atatufanya kuwa ni Nguzo katika kanisa, kama Mungu alivyowafanya PETRO, YAKOBO NA YOHANA kuwa ni NGUZO KWAKANISA LAKWANZA

WAGALATIA 2:9 “tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo,  walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara”

Hawa ni viongozi wa juu wa kanisa lakwanza na wanaitwa ni Nguzo na Yesu aliwaandaa kuwa nguzo alipokuwa anapanda mlima mrefu faraghani akamtwa Petro, Yakobo na Yohana na wengine wote anawaacha ila alikuwa anawaandaa kwa uongozi wa masafa marefu

Sasa watakaokaa kwenye kweli na kuishindania kwa masafa marefu zaidi, hawa nao watakuwa ni nguzo katika hekalu la Mungu mbinguni, ina maana kule juu Utaona wale ambao wamekuwa katika usafi na kung’ara sana watatengwa watakuwa ni nguzo

Ø ASHINDAYE ATALIFAHAMU JINA JIPYA LAYESU NA LA MJI MPYA

UFUNUO 3:12 “….. nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya

Kaka zangu dada zangu Yesu huku duniani tunamfahamu kwa majina mengi tofauti tofauti ambapo baadaye aliitwa YESU. Jina YESU maanake ni MWOKOZI, hilo jina Mwokozi litakuwa halina maana kule mbinguni, kwasababu wakati wa kuokoa utakuwa umekwisha. Neno KRISTO maanake Masihi mpakwa mafuta wa Bwana. Hilo nalo litakuwa limekwisha wakati wake

Kwahiyo YESU KRISTO majina yote hayo yatakwisha wakati ambao unakuja si mrefu atakapokuja Bwana Yesu, hatimaye atakuwa na JINA JIPYA !Na tutalifahamu jina hilo jipya sisi ambao tutakaokuwa miongoni mwa washindao

Mungu atakuwa na jina lake ambalo tutalijua jina lake hilo la mwisho atakalolitumia kule mbinguni! Kama anavyoitwa YEHOVA leo, kule atakuwa na jina jingine litakalokuja, na jina la mji huo mpya Yerusalem mpya litakuwa na jina lake ambayo yote tutayapata kujulishwa sisi tutakao kuwa miongoni mwa washindao. Bwana atusaidie tuwe na sikio tukae kwenye kweli ya Neno lake kwa gharama yeyote ili tuyaone hayo yote yakitimia sasa na hata Milele katika JINA LA YESU!!!

(7)UNABII KUHUSIANA NA MAJIRA YA KANISA

Tulikwishagusia gusia kuhusiana na mabo Fulani Fulani kwamba Kanisa la Filadefia katika unabii linazungumzia majira kuanzia mwaka 1750- 1905. Kama tulivyokwisha kudokeza hapomapema, baada ya Martin Luther aliyemaliza kazi nzuri sasa katika majira ya Sardi ambayo tulijifunza kwa kuangalia maana ya Neno SARDI Kuwa ni wale wanaotoroka

Baada ya Majira ya Sardi ambayo yanazungumzia wale wanaotoroka lakini Martin Luther na watu chungu mzima walitoroka katika kanisa katoliki na kuanza kukaa kwenye kweli iliyokuwa imefunuliwa. Na walioendelea kutoroka wengi sana na kila mmoja kati ya hao waliokuwa wanatoroka, ikawa sasa anafumbuliwa macho na Martin Luther kujaribu kutafuta kile ambacho hapa hakipo na wanataka kiwe hivi!Sasa wengine hata wakaingiza vitu tofauti tofauti

Na hayo yalizaa makanisa mengi sana, kwa huyo Martin luther hatimaye wale wafuasi waliojulikana kama Kanisa la Kiinjili (Evangelical Church) ikaongezwa hiyo LUTHERANI lakini baadae ikaja MOROVIAN nayo ikaibuka kipindi hicho, lakini tofauti ndogo ndogo, ndipo ikaja ANGLICAN(ANGLIKANA) ambayo nayo ilitokana na mambo ya kitawala ! Anglican nayo ikatokeza hapo ndani ya Anglikan vipande viwili HIGH CHURCH na LOW CHURCH. Hii High Church inakuwa bado inafanana fanana na ukatoliki kwa sehemu kubwa, bado masanamu sanamu yapo tena lakini LOW CHURCH tena yenyewe ni tofauti kidogo inasogeleana na Lutheran

Kwahiyo ikawa sasa wanazidi kutoroka, wanazidi kutoroka, wanazidi kutoroka hivyo ina maana baada ya kipindi hichi cha kutoroka kuanza ikawa ndio mwanzo wa kuendelea kutoroka sasa. Kila mmoja akiwa anakaa anautafuta uso wa Mungu ili apate kuona kuna kitu gani ambacho bado kimepungua na huyu anakifanya hicho hivyo yakaanza kutokea mambo mengi, wahubiri wengi ambao si rahisi kutaja mmoja mmoja lakini kulikuwa na mamia kwa mamia waliojitokeza katika kipindi hiki cha Filadefia, Kila mmoja anaibuka na hiki, na huyu mwingine anaibuka na kile na uhamsho ukiambatana nayo na mambo mengi sasa yakaanza kurejeshwa

Ø UFUNUO JUU YA WATU WANAOKUBALIKA KUHESABIKA KATIKA KANISA

Mtu mmoja wapo ambaye alikuwa katika hatua za mwanzo mwanzo wa kipindi hichi cha Filadefia anaitwa JOHNATHAN EDWARD ambaye alikuja kufariki mwaka 1758,  Miaka michache baada ya kipindi hiki au majira haya ya Filadefia kuwa yameanza

Yeye naye alikuwa amejifunza masomo ya Martin Luther na akawa hatimaye umeokolewa, sasa yeye huyu Johnathan Edward akaongeza kitu kingine zaidi ambapo kwa miaka michache kabla ya kufa katika kuhubiri kwake na kufundisha akakaza zaidi kusema, watu wanaotakiwa kutambulika kama washirika katika kanisa, wanatakiwa kuwa ni watu waliookolewa

Huu ndio Ufunuo uliokuja kupitia kwa huyu Johnathan Edward, Huyu ndiye aliyeweka msisitizo wa Andiko hili kama ifuatavyo

MATENDO 2:47 “wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote.  Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa

Akasisitiza akasema Mtu kama hajaokoka hana sehemu katika kanisa, Kwahiyo watu ambao hawajaokoka hawapaswi kuhesabika kama washirika wa kanisa

Kwahiyo Unaona kila aliyekuwa kuwa anatoroka, huyu anakuja na Ufunuo ambao unazama zaidi katika Neno na kupelekea watu katika kweli zaidi

Ø UFUNUO JUU YA KUANZA KWA MIKUTANO YA INJILI HADHARANI

Sasa akaja mhubiri mwingine ingawa hapa hatutaweza kutaja wote maana wako mamia kwa mamia ambapo kila mmoja alikuwa anakuja na Ufunuo juu ya hili na hili na lile mpaka hivi leo. Mhubiri huyu ni GEORGE WHITEFIELD ambaye ane alikuja kufariki mwaka 1770 ila kabla ya kufariki kwake alifanya kazi kubwa sana

George whitefield katika mambo ambayo yanakumbukwa yeye ndiye alikuwa wa kwanza kufanya mikutano ya kwanza ya hadhara ya injili ambayo leo inajulikana kama CRUSADE

Mikutano ya injili haikufanyika sasa wakati wa Martin Luther kwani yeye Luther alipokuwa labda anatoka anapelekwa mahakamani Fulani watu huko njiani wanakusanyika ndio basi anazungumza nao, alafu anaondoka lakini Rasmi MIKUTANO YA INJILI YA HADHARANI ilianza kipindi hiki cha George Whitefield maana kabla ya hapo walikuwa wanaamini mahubiri yeyote lazima yafanyike ndani ya kanisa kama ni watu kuokoka, kama watu ni kutubu na kumpokea Bwana Yesu ni lazima iwe kanisani lakini sio hadharani

Haikuruhusiwa na ilikuwa ni kitu kigeni mtu kwenda kushuhudia mitaani, au kwenda kuhubiri mitaani au barabarani au masokoni!Hapana hilo halikukubalika. Hivyo George white Field alikuwa wa kwanza kuanza kuhubiri kwenye mikutano ya hadhara.

Ø UFUNUO WA KUHUBIRI BILA MAJOHO

Kama tulivyotangulia kuona kuwa George Whitefield ndiye alikuwa mwanzilishi wa kwanza wa kuhubiri kwenye mikutano ya hadhara, lakini vile vile alikuwa ndiye wa kwanza kuhubiri BILA MAJOHO!. Haya majoho ya kidini dini ambayo yalikuwepo bado katika dini hizo. Hivyo akaanza kutoka kuhubiri na kufundisha akaeleza, jinsi ambavyo Yesu Kristo na mitume walikuwa wanahubiri namna gani?

Alieleza kuwa Yesu na mitume walihubiri hadharani kila mahali kwenye boti, kwenye Pwani ya mto, akawa anaelezea jinsi ambavyo wakina Paulo mtume jinsi hata walivyokuwa gerezani wamevuliwa nguo na kuwa uchi wa mnyama, huku damu zinachuruzika, huyu mmoja anazungumza Bwana zangu, yanipsa kufanya nini nipate kuokoka?Hawakuwa hata na nguo lakini wakawa wanamwambia MWAMINI BWANA YESU, NAWE UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO

Hivyo anawaeleza kuwawakati wote hawa wakina Pulo wanahubiri, Jekulikuwa na majoho gani?au walivaa majoho yeyote?. Akaanza kuzungumza jinsi ambavyo mitume wametoka kwenye ghorofa moja kwa moja baada ya kujazwa Roho mtakatifu, mara petro akaanza kuhubiri, HAWAKUWA NA MAJOHO ilikuwa nje tu anazungumza na watu, haikuwa hata kanisani

Akaanza kurejea katika kweli ya mafundisho mbalimbali jinsi Yesu Kristo alivyokuwa anapita mitaani, anampata Mathayo na kuwaambia akina Petro na Yohana nifuateni, wanaziacha nyavu zao na baba zao!Hivyo akaanza kurejea kuwa huko hawakuwa kanisani. Kwahiyo George whitefield akaanza kutoka kuhubiri masokoni, mitaani na kila mahali tangu asubuhi mpaka jioni, watu wakawa wanashangaa ni kitu cha ajabu, kwasababu Nyakati zote za kikatoliki ilikuwa ni mwiko, haijawai kutokea hivyo na vile vile hata Nyakati za Martin Luther haijawai kutokea Lutherani

Hivyo wakaanza kuona mikutano ya injili inafanyika nje wakati huo. Hivyo George whitefield akahubiri sana habari za wokovu kiasi yeye alikuwa uingereza sehemu mojainaitwa New England ilifikia mahali hata wakatimmoja alifanya mikutano ya injili akawa na mahudhurio ya watu 8000 kila siku mwezi mzima na kuakaanza wimbi kubwa la uamsho sana wakati wa miaka karibu ya kufa kwake 1770 na hatimaye akaanza kuhubiri watu mpaka 2000 kwenye kusanyika moja nje na linakumbukwa sana kusanyika moja lililokuwa na watu 20, 000 ambalo aliwapelekea kushiriki meza ya Bwana hadharani

Lakini kama tulivyozungumza kwamba kila mmoja alikuwa na upungufu fulani kila mmoja anakwenda masafa lakini bado kuna upungufu fulani hapa na pale, Mungu analeta Ufunuo tena. Pamoja na kazi ya ajabu ambayo alikuwa ameifanya huyu George whitefield ya kuanzisha kufanya mikutano ya Injili lakini bado aliapata matatizo akawa anafundisha kitu kilichokuwa kinaitwa ELECTION AND PRE DESTINATION yaani alikuwa anahubiri akisema yaani Mungu katika Mpango wake tangu mwanzo amewachagua watu fulani wa kuokoka na watu wengine wa kwenda motoni!Ndio alikuwa anafundisha hivyo kitu ambacho si kweli kilikuja kupingwa hapo baadae

Kwahiyo Unaona ilikuwa ni kwamba kweli wanatoroka, alipokuwa anatoroka Martin Luther alipata Ufunuo mpaka hapa, alafu anakuja huyu mwingine anapata Ufunuo alafu anaendelea mbele zaidi na mwingine anapata Ufunuo juu ya jingine anaendelea zaidi. Mfano Martin Luther hakupata Ufunuo wowote Kuhusu Ubatizo wa maji tele ila anatokea mwingine anapata Ufunuo juu ya hilo na anaendelea mbele zaidi! Ikawa hivyo

CHIMBUKO LA MAFUNDISHO YA UTAKASO/UTAKATIFU

Sasa baada ya hao wengine kupita akaja JOHN WESLEY ambaye ndiye chimbuko ya fundisho la utakatifu, Ni mtu ambaye

Ø HISTORIA YA JOHN WESLEY NA MAFUNDISHO YAKE

JOHN WESLEY alizaliwa mwaka1703 na kufariki mwaka 1791. John Wesley wakati akiwa na miaka 6 aligundua kwamba Mungu alikuwa na makusudi naye kwa namna ya tofauti

Nyumba ya wazazi wake ilikuwa ni ya ghorofa ambapo siku moja nyumba hiyo ilishika moto na watu wote wakakimbia hadi wazazi wake na wengine wote walikimbia ili kuokoa maisha yao ila wakamsahau kitoto hicho (John Wesley) kwenye jingo hilo linalowaka moto. Ila kitoto hiki kikiwa na miaka 6 kikatenda kusimama kwenye dirisha lililokuwa limefunguliwa wakati moto unaendelea kuwakakila kona unalipuka isipokuwa sehemu hiyo kaliposimama katoto hako ndio moto haukufika lakini chenyewe kakawa kanacheka

Like
1
Căutare
Categorii
Citeste mai mult
SPIRITUAL EDUCATION
SELF DELIVERANCE
NO DEMONS ALLOWED SELF DELIVERANCE PROVERBS 6:5 "...DELIVER THYSELF..." If you want to get...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 19:28:32 0 5K
OTHERS
Je, Muhammad Ametabiriwa Kwenye Biblia?
SEHEMU YA KWANZA Waislamu wanashikilia kwamba Muhammad alitabiriwa kwenye Biblia. Andiko lao kuu...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 09:29:25 0 5K
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 22
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 44 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-22 18:04:42 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
Why did Jesus have to die?
When we ask a question such as this, we must be careful that we are not calling God into...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:39:49 0 5K
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 28
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 28 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-21 06:39:38 0 5K