JIHADHARI USIMKATAE MUNGU KATIKA FAHAMU ZAKO

0
5KB

Shalom, leo nipe muda nikuonyeshe jambo muhimu sana katika safari yetu ya wokovu hapa dunia kupitia kitabu cha Warumi. Warumi 1:28 imeandikwa ‘Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa’. Katika hali ya kawaida tumezoea kusika na kuona watu wakikataa kufuata maelekezo, sera au miongozo fulani kwa maneno na matendo yao na hivyo tunajua upande wao kutokana na mwitikio wao.

Sasa kupitia andiko hili tunaona, kumbe mtu anaweza kumkataa Mungu kwa fahamu zake. Naam, kwa mawazo mtu anaweza kumkataa Mungu na Mungu naye akamuacha mtu huyo. Sasa hii ni hatari kubwa, maana mtu anaweza akafikri Mungu yupo upande wake, kumbe Mungu alishamuacha.

Je, walimkataaje Mungu walimkataaje Mungu katika fahamu zao? – Ndio ni vema kupata jibu la swali hili ili na sisi tusifanye makosa kama yao maana kwa kosa hilo walitengwa kabisa na Mungu, naam aliwaacha. Kitendo cha kuwaacha ina maana hawakuwa na Msaidizi, wakafanya yasiyowapasa, muda wao ukatekwa na maisha yao yakakosa uelekeo wala hayakuwa na matoekeo yaliyokusudiwa, hivyo wakaishia pabaya, naam mahali pa majuto ya milele.

Je, tunajifunza nini: Ujumbe unatuonya na kutusaidia tujue kwamba:

Mojawalikataa wazo la ufalme wa nuru kwa kuruhusu wazo la ufalme wa giza kwenye fahamu zaonaam mioyo yao. Ndio, uasi wao ulianzia kwenye mawazo yao, wakakataa wazo la Mungu kwa kuridhia, wazo la Shetani. Naam wakachagua giza badala ya nuru, uongo badala ya kweli, wakaelekeza mioyo yao kwenye mawazo ya ufalme wa giza.

Ndio, katika yale waliyopitia, walikataa kufikiri kuhusu Mungu, hawakutafuta au kurudi kuona neno la Mungu linasemaje kuhusu mapito yao. Naam, hawakutoa nafasi kwa mawazo ya ufalme wa nuru au elimu ya Mungu kwenye fahamu zao  kuhusiana na mapito yao au mambo yaliyokuwa yanawakabili.

Mbiliwaliipa nafasi elimu ya ufalme wa giza na sio elimu ya Mungu: Watu hawa hawakutaka  kuipa nafasi, kuitunza wala kuifanya endelevu, elimu ya Mungu ndani yao. Je, ni kwa namna gani?, ni kwa sababu walishindwa kuzipinga fikra za yule mwovu zilizojiinua kinyume cha elimu ya Mungu kwao.

Ndio, kwa kuwa hawakuwa na elimu ya ufalme wa nuru, wasingeweza kuzitambua fikra za elimu ya ufalme wa giza na kwa njia hiyo walikuwa wanaiuzuia kweli isipate nafasi, istambulike wala isiwe na nguvu kwenye mioyo na maisha yao. Naam, kwa lugha nyingine walishirikiana na ufalme wa giza, kuendeleza kazi za ufalme huo na sio za ufalme wa nuru (Warumi 1:18).

Tatuwalimdharau Mungu: Maandiko yanatuambia hata pale walipomjua Mungu hawakumtambua kwa kumpa utukufu na kumshukuru Hii ina maana katika yote waliyotenda wakafanikiwa, waliona ni uwezo na nguvu zao na hivyo kujitwali utukufu wa Mungu na kumuonyesha dharau kubwa (Warumi 1:21).  

Nnnewalitoa muda wao kwenye vitu au mambo yasiyofaa na hivyo wakaaingiza katika mioyo yao fikra za uasi dhidi ya Mungu wao.  Naam kwa tendo hilo fikra za uongo (giza) zilizima, zilizuia fikra za kweli (nuru) maana walichagua giza badala ya nuru, uongo badala ya kweli, mauti badala ya uzima na kwa jinsi hiyo wakawa wamebadili kweli ya Mungu kuwa uongo.

2 Wakorintho 11:3 imeandikwa ‘Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenumkauacha unyofu na usafi kwa Kristo’. Kwenye kila wazo la Mungu kuna wazo kinzani toka kwenye Shetani, ni wazo la uasi didi ya sheria za Mungu.

Hatari ni kwamba Shetani anaingiza fikra za uharibifu kwa mtu kwa namna ambayo mtu atafikiri ni fikra za ufalme wa nuru, kama ilivyokuwa kwa Hawa pale bustanini kwa hila. Ndio, anguko la Hawa lilianzia kwenye fahamu zake kwa kutoa nafasi kwenye fikra za ufalme wa giza.

Ndugu zangu, Mungu anaumia sana kuona uumbaji wake unamkataa, naye anauliza mbona mnanikataa? Sasa ikiwa jambo hili liliwagharimu waliotutangulia ni vema tukajifunza kutokana na makosa yao. Kumbuka, lengo la mawazo ya ufalme wa giza ni kutia au kuleta giza kwenye moyo wa mtu ili kuharibu fikira zake na hivyo kumuondoa mtu huyo kwenye kweli ya Mungu.

Ujumbe huu ukutie nuru moyoni mwako ili usiharibiwe na fikra za yule mwovu maana imeandikwa ‘Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake’ (2 Wakorinto 2:11). Nakusihi, jihadhari usije ukamkataa Mungu katika fahamu zako kwani matokeo yake ni mabaya sana. Ndio, kanisa usijisahau ukalala na kumpa Ibilisi nafasi, BWANA yuaja kuwachukua watu wake, tunza mavazi yako, wala usiguse kitu kichafu (asomaye na afahamu).

Utukufu na Heshima vina wewe Yesu, Wastahili BWANA

Rechercher
Catégories
Lire la suite
MASWALI & MAJIBU
Inaruhusiwa Kula Nyama Ya Nguruwe Kwa Mkristo Wa Kweli? Pia Je, Mkristo wa Kweli Anaruhusiwa Kunywa Pombe/kuvuta sigara?
JIBU LA 1: Kwa ufahamu hakuna tatizo lolote kula nyama ya nguruwe au chakula chochote ambacho mtu...
Par GOSPEL PREACHER 2022-06-13 08:59:21 0 6KB
REVELATION
UFUNUO 6
Katika kitabu cha ufunuo sura ya tano, tunaona Mungu akiwa ameketi katika kiti chake cha enzi...
Par GOSPEL PREACHER 2021-10-30 09:45:30 0 5KB
SPIRITUAL EDUCATION
What will happen to those who die without hearing anything of Christ Jesus?
The Holy Bible makes it conspicuous and crystal clear that while there are might be people in the...
Par MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 06:15:50 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
YESU ATAKUPONYA.
Bwana Yesu asifiwe… Kwa ufupi, “Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili...
Par GOSPEL PREACHER 2022-03-30 04:53:31 0 4KB
MAHUSIANO KIBIBLIA
KANUNI YA MUDA KATIKA MAHUSIANO
Muda hupima upendo wangu kwako.Kama kweli nakupenda, nita tumia kiasi kikubwa cha Muda wangu kwa...
Par GOSPEL PREACHER 2021-11-06 15:03:16 0 4KB