JINSI YA KUENENDA KWA ROHO.

0
6K

Wagalatia 5:16 “Basi, nasema enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe tamaa za mwili”Hapa tunaona Paulo anawaagiza wagalatia kwamba waenende kwa Roho na lengo kubwa ni ili wasizitimize tama za mwili.

Lengo la waraka huu mfupi ni kukueleza namna unavyoweza kuenenda kwa Roho, na hii ni kwa sababu Yesu  mwenyewe alisema ni heri mimi niondokeili aje mwingine msaidizi huyo Roho wa kweli. Na
kama tunaye Roho mtakatifu ni lazima tujue ni kwa namna gani tutaenenda kwa roho?Neno la Mungu/ Mungu anaposema, enendeni kwa Roho ana maana hii:- 

(a)            Kila unalolizungumza, lizungumze chini ya uongozi wa Roho mtakatifu. Yohana 12:49-50. Yesu mwenyewe hakunena neno lolote kwa shauri lake, bali kila ambalo baba alimwambia kupitia Roho mtakatifu. Hivyo hata wewe
kama unafundisha, unahubiri, unaonya hakikisha unachokisema Roho mtakatifu ndiye amekuruhusu ukiseme. Usiseme kitu cha kwako halafu ukasema Roho mtakatifu amekuongoza.

(b)            Tii uongozi wake .Yohana 16:13 “ lakini atakapokuja huyo Roho wa kweli; atawaongoza awatie kwenye kweli yote…….” Moja ya kazi za Roho mtakatifu ni kutuongoza na kututia kwenye kweli yote. Hivyo kuenenda kwa Roho maana yake ni kutii katika yale anayotuambia maana hata yeye haneni kwa ridhaa yake isipokuwa yale anayoyasikia kutoka kwa Mungu. 

(c)             Jifunze kuyafikiri mambo ya Roho wa Mungu. Warumi 8:5b “
Bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho”Kuenenda kwa roho kunajumuisha kukaa chini na kuanza kutafakari mambo/kazi za Roho mtakatifu. Vile jinsi utendaji wake ulivyo, karama zake, vipawa, tunda la Roho na vile jinsi anavyofanyika msaidizi katika maisha yako.

(d) Kuliishi tunda la Roho.Wagalatia 5:22 “lakini tunda la Roho ni upendo, Furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi………”Sikiliza ukijifunza au kadri unavyoishi maisha yaliyojaa upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi ndivyo unavyokuwa umejiweka kwenye mkao wa kuongozwa na Roho au ndiko kunaitwa kuenenda kwa Roho. 

 (e) Kwa kuyakataa na kuyafisha/vunja matendo ya mwili katika maisha yako. Wagalatia 4:28-31 ule mstari wa 30 unasema” Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa muungwana”Biblia inapozungumzia kumfukuza mjakazi pamoja na mwanawe ina maana ya kuyafukuza, kuyapinga, kuyaondoa, kuyafisha, kuyaharibu matendo ya mwili katika maisha yako ambayo yametajwa katika. Wagalatia 5:19-21 ikiwa ni pamoja na uasherati, ulevi, husuda, uadui, ugomvi, uchafu, ufisadi nk.Naamini baada ya ujumbe huu utaanza kuenenda kwa Roho na kuomba msaada wa Mungu katika maisha yako kwenye eneo hili..

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nawe.

Zoeken
Categorieën
Read More
OLD TESTAMENT
THE BOOK OF EXODUS
Welcome to Proshabo Online Bible Study (POBS). This is the best platform for you to study your...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-28 01:38:46 0 6K
OTHERS
Islam offers HELL and that is all
Allah Promised hell for his followers:  Sura 3:185, "Every soul shall have a taste of...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:08:53 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
MAISHA BAADA YA KUBATIZWA NA ROHO MTAKATIFU.
Mtu anapozaliwa mara ya pili kwa kumkaribisha Bwana Yesu ndani ya maisha yake, huingia katika...
By GOSPEL PREACHER 2023-04-13 13:06:36 0 7K
Networking
11 marketplace metrics you should be tracking to measure your success
Which marketplace metrics should you really track to know your marketplace is successful? One...
By Business Academy 2022-09-17 04:01:13 0 11K
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 17
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-22 17:54:08 0 5K