NAMNA IMANI INAVYOWEZA KUFANYIKA MSAADA KATIKA MAISHA YAKO.

0
5KB

 Siku zote neno la Mungu linasema katika 2Petro 5:7 kwamba siku zote Mungu anajishughulisha na mambo yetu/mahitaji yetu ya kila siku. Yapo mahitaji mbalimbali ya kiroho, kiuchumi, kindoa, kimahusiano nk. Ambayo tunahitaji kuona tunafanikiwa vema. Katika kujishughulisha na mahitaji yetu, Mungu ametupa imani ili itusaidie kuunganisha/kutengeneza njia kati ya haja tulizonazo na msaada wa Mungu.

Lengo la ujumbe huu mfupi ni kukuelezea tafsiri fupi ya Imani, makundi matatu ya imani na kisha namna hiyo imani inavyoweza kufanyika msaada katika maisha yako. Katika kile kitabu cha Waebrenia 11:1 Biblia inasema, Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Katika hii tafsiri kuna mambo makubwa mawili kama siyo matatu yamezungumziwa kwanza ni kuwa na hakika, na pili ni ya mambo yatarajiwayo; katika haya yatarijiwayo yapo yasiyoonekana
 Makundi ya imani

(a)Imani katika yale ambayo Mungu amekueleza au amekuagiza.


Hili ni kundi la kwanza la Imani; na imani hii inakuja kwa kuamini yale ambayo Mungu anakuagiza kuyafanya. Mfano Ibrahimu alipoambiwa aende nchi ya ugenini. Mwanzo: 12 yote na pia Nuhu alipoagizwa aitengeneza safina.

(b) Imani unayojiumba/unayoiumba ndani yako kutokana na ahadi za Mungu juu yako.


Imani hii inakuja kwa wewe kuwa na ufahamu fulani kuhusu ahadi za Mungu na kwa sababu umezisikia hivyo ndani yako unatengeneza Imani yenye matendo itakayokupa kila kilichobebwa ndani ya ahadi. Eg. Mfano wa mwanamke mwenye kutoka damu. Marko 5

(c)Imani katika ahadi za Mungu .


Imani hii inakuja kwa wewe kuamini tu kile ambacho Mungu amekisema katika Neno lake kama ahadi kwako. Mfano Imani ya sara, kwamba atapata mwana hata katika uzee wake .

Namna Imani inavyofanyika msaada:

Imani yoyote ile siku zote ina matendo yake, na si hivyo tu bali imani hufanya kazi kwa kushirikiana na matendo yake. Chanzo cha Imani yoyote ile ni kusikia, sasa Imani katika Kristo inakuja kwa kusikia habari za kristo, Imani katika Jina la Yesu, Damu ya Yesu, Roho mtakatifu nk. Inakuja kwa kusikia habari za kristo, Imani katika Jina la Yesu, Damu ya Yesu, Roho mtakatifu nk inakuja kwa kusikia habari za jina la yesu, Damu ya Yesu, Roho Mtakatifu nk.

Hivyo kwanza ili uone imani ikikusaidia jifunze kujisemea kile unachokisoma  ili usikie neno la Mungu linalozungumza eneo unalohitaji msaada Mfano, Biashara, ndoa, Huduma nk. Imani inaumbwa kwa wewe kujisemea kile unachoamini.
Hivyo uzao wa Imani ni sawasawa na kile ulichosema (ulichoamini) + matendo yake .

 Ukitenda tendo au matendo kinyume na kile ulichoamini au kusema bali imani hiyo haiwezi kuzaa. Isipozaa basi ujue huenda imani hiyo imepungua au matendo uliyoyatenda ni kinyume na ulichoamini, yaani umekosea kwenye matendo. Una imani nzuri lakini matendo ya hiyo imani hayasaidii kuzaliwa kwa kile ulichokisema.

Naamini sehemu hii ya kwanza kuhusu imani itakusaidia kujua namna imani inavyofanyika msaada katika maisha yako ya kila siku.

Ubarikiwe.

Rechercher
Catégories
Lire la suite
FORM 4
FORM 4
List of all subjects for the form 4 class AGRICULTURE BASIC MATHEMETICS BIOLOGY BOOK-KEEPING...
Par PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:25:06 0 6KB
SPIRITUAL EDUCATION
USIKUBALI USHAWISHI WA DAKIKA 1 WA SHETANI
BWANA ASIFIWE, unaweza kupakua (download) somo hili kwa kubonyeza hapa. Au unaweza ukaendelea...
Par MOCARECI CHURCH 2021-11-06 21:10:13 0 7KB
EZRA
Verse by verse explanation of Ezra 7
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
Par THE HOLY BIBLE 2022-04-02 06:19:12 0 6KB
OTHERS
VLOOKUP function
Use VLOOKUP when you need to find things in a table or a range by row. For example, look up a...
Par PROSPER HABONA 2024-01-01 20:56:17 0 4KB
OTHERS
THERE IS A GOD How the World’s Most Notorious Atheist Changed His Mind
In the parable of the lost sheep, in the Gospel of Luke, Jesus says there shall be more joy in...
Par MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:00:09 0 6KB