IJUE BIBLIA YA SHETANI

0
5K

BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote ambao mmeumbwa na mwenyezi MUNGU na siyo shetani kawaumba. Mnamo mwaka 2010 YESU aliponiita nikamtumikie sababu kanisa limetekwa na shetani 98% katika ulimwengu wote na sasa yeye amebakiza muda mchache arudi kama alivyonieleza YESU yeye peke yake. Ni mambo mengi aliyonieleza ila kwa leo nitaelezea jambo moja ila zaidi ingia katika website yanguwww.prophethebron.org ingia katika link zake utayajua mengi aliyonieleza kwa ajili ya ulimwengu huu  pamoja na wewe pia,  anawapenda watoto wa MUNGU sana ila shetani hawapendi kabisa na anataka mumkosee MUNGU ili mchomwe naye siku ile ya mwisho.

Zipo njia na mipango mingi sana aliyoiandaa shetani na  mimi  simwogopi kabisa pamoja na maajenti wake wala sitakubali watoto wa MUNGU wapotezwe na shetani pamoja na maajenti wake. Moja ya mbinu za shetani nilipoenda kuzimu nikiwa na YESU pamoja na malaika Mikaeli na jeshi la mbinguni nilionyeshwa biblia za shetani ambazo ameziandaa  kwa ajili ya kuja kuvurugia wakristo fahamu zao na kuvutwa  katika upande wa shetani . Biblia hizo zipo mbili moja tayari ipo duniani sasa inatumika na ya pili bado haijafika, biblia hiyo imefananishwa na biblia takatifu ila itaitwa jina la mji fulani na mtu maarufu ambaye yeye ni mtenda dhambi na ni mwanachama wa illuminati na freemason.

Kwanza kabisa nataka uelewe kitabu kitakatifu cha kikristo ni biblia ile ambayo ni kwanza au kwa jina Holy bible, biblia ukisoma katika  kitabu cha Ufunuo wa Yohana 22:18 -19 inasema; namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki mtu yeyote akiyaongeza, MUNGU atamuongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu  hiki, na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya kitabu hiki MUNGU atamuondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. Biblia hizo nilionyeshwa na YESU na nikaziona na majina, kilichoandikwa hata kabla ya kutuma hapa ulimwenguni. Biblia hizi zina vitabu vya agano jipya na la kale ila tofauti utaona haziitwi Holy bible juu ya kitabu hicho au kuiita Biblia tu litaongezewa  jina lingine mwenye akili na afahamu. Fahamu roho wa BWANA anaeleza mataifa yote ili msiangamie. 

Biblia  hizo ziliandaliwa kule kuzimu toka mwaka 1952 ila 2015 ndiyo imefika ulimwenguni na nyingine itakuja ila mtazijua tuu. Lengo la biblia hizo ni kuwateka wakristo na kuvuruga fahamu zao ili huyo aliyeileta hiyo biblia hapa duniani atakapokufa na wote  wanaozitumia watamfuata na yeye alipo ambapo atakwenda kwa shetani, na yeye anajijua kabisa anachokifanya ni nini?  Cha kufikiria jiulize neno linasema atakaye yaongeza maneno ya biblia au kuyapunguza tayari hataenda mbinguni. Sasa tazama hiyo biblia inaitwa kwa jina gani? Tofauti na biblia imeongezwa mengine. Na zaidi hata na mtu atakayeisoma au kuitumia itampoteza na ile siku ya mwisho yale mapigo yatamfuata na yeye kwa sababu alifuata biblia iliyoongezewa au kupunguzwa tofauti na MUNGU alivyoipitisha ile yake.

Jambo lingine jiulize mbona aliyeandika hiyo biblia yeye ni mfuasi wa vyama vya shetani? Na je mbona yeye anajiita yeye ni MUNGU? Je hauoni huyo ni pepo kabisa, MUNGU hafananishwi na chochote wala kitabu chake Biblia  hakiitwi kwa jina la mji wowote, au mtu au nchi. Sasa mwenye kufahamu na afahamu na zaidi jaribu kuangalia biblia zilivyo, utaona hazina picha ya mtu, mnyama, fuvu la kichwa, samaki na vinginevyo. Ni HOLY BIBLE au BIBLIA, BIBLE tu. Hiyo ndiyo katiba aliyotupa wanadamu tuifuate na aliyoipigia muhuri wake, sasa shetani na yeye kaleta katiba yake akiifananisha na biblia, akaweka vitu vyake na kujifanya yeye ni MUNGU, usitumie hizo biblia utakuwa umejiunganisha na huyo aina ya mungu shetani sababu tu ya kutumia biblia yenye jina la mtu au vitu, hiyo inatoka kuzimu. Na zaidi mchunguze hata kibinadamu matendo yake na yeye alivyo je anao uhusiano na YESU utakuta ni muhuni, mfisadi, na mengineyo mengi. Yatakusaidia kupata picha vizuri. YESU anarudi mrejeeni yeye msifuate yesu wa uongo na miungu ikataeni.

Sema, BWANA YESU naomba unisamehe, unikomboe upya  uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, najitenga na biblia zilizoitwa kwa majina ya watu kama nilizisoma au kuzitumia, sitaki maana nimejua ukweli kitabu chako kitakatifu hakibadiliki jina lake wala kuongezewa na hautatoa biblia nyingine tena zaidi ya ile ya kwanza. Hizi nyingine ni za shetani. Naomba unilinde, uniongoze . AMEN

Căutare
Categorii
Citeste mai mult
OTHERS
KWANINI MUHAMMAD ALITAKA KUJINYONGA “COMMIT SUICIDE”?
1. MUHAMMAD ALITAKATA KUJINYONGA2. MUHAMMAD ALIPANDA MLIMANI NA KUJARIBU KUJIRUSHA ILI AFE3....
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:55:32 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
NYOTA KIBIBLIA
Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima   UTANGULIZI: Huu ni mwendelezo wa somo la Nyota na...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 02:29:59 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
UNAUTUMIAJE UPAKO WA MUNGU JUU YAKO?
Mathayo 21:28-32 – Ukisoma andiko hili utaoona habari  baba mmoja aliyekuwa na...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:23:25 0 5K
2 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 2 Chronicles 16
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 25 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 01:36:26 0 5K
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 19
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 73 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-21 05:00:24 0 5K