SOMA KITABU HIKI: ZIJUE SIRI KUBWA ZA SHETANI, ILI UWEZE KUMSHINDA
Posted 2021-11-19 05:59:01
0
7K

TOLEO LA 16
ISBN 978 9987 9717-7-0
UTANGULIZI
Nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI ambaye ndiye mwana wa pekee na sasa yupo mbinguni kwa BABA yake anasubiri tena kuja katika unyakuo akiwa angani awanyakue wale wote ambao wamemkubali, wakaokoka, wakabatizwa ubatizo wa maji mengi yanayotembea na watakaokuwa wanaishi maisha matakatifu peke yake.
Jina langu mimi naitwa Hebron Wilson Kisamo, kabla ya kuwa mtumishi wa MUNGU, mimi kazi yangu ni Professional Driver Guide kazi ambayo niliifanya katika nchi ya Tanzaniakatika mbuga za wanyama katika miji na milima mikubwa yote ya Tanzaniapamoja na Zanzibar. Ilipofika August 2009 nilikuwa nyumbani mchana nilikuwa ninaomba ni siku ya jumapili mchana, ghafla akaja Malaika Mkuu wa MUNGU anayeitwa Mikaeli nikiwa katika maombi, akaniambia Hebronusiogope, katika maombi uliyoyafanya leo na rekodi ya makanisa yote, wewe umefanya kazi kubwa hata kuliko watumishi wote kwa kile ulichokifanya katika ulimwengu wa roho katika ulimwengu wote, niliogopa hiki ni nini? Akanieleza mengine ambayo hayo ni yangu peke yake kisha akaniambia tumekuja watatu nipo na YESU na pia Malaika Gabriel, akanishika mkono, akaja YESU sasa akanikumbatia, na wakati huo kwa ule ukuu wa YESU nilikuwa ninaogopa, na yeye akanieleza yale aliyoniambia ambayo ni yangu, akaondoka, akaja Malaika Gabriel. Yeye akasema na mimi kwa muda mrefu, akaniambia Hebron wewe ni mtumishi wa MUNGU na utakuwa na huduma yako peke yako ambayo utasimamia wewe peke yako na itafika wakati huduma utaianza ukiwa unafanya kazi na itakuwa ni mahali fulani hapa hapa Arusha. Akaniambia MUNGU akubariki sana, haya narudi mbinguni. Niliendelea na kazi zangu lakini maneno hayakutoka katika ufahamu wangu na kila nilipokuwa nataka kuwaeleza watumishi mdomo wangu ulikuwa bubu.
Ilipofika 2010 March, hali ikajirudia YESU akaanza kusema na mimi hata nikiwa na wageni katika gari, na hata nikiwa peke yangu iwe natembea kwa miguu au ninaendesha gari na mara nyingine hata nikiwa Game Drive porini, lakini hakuna mtu yeyote aliyejua, akanieleza mengi sana hata katika habari za wanyama aliowaumba MUNGU ambao wanyama wote hao ni wa BABA yake. Nilikuwa naagalia simba, nyumbu, punda milia na wanyama wengine tukiangalia na YESU na yeye pia anawapenda wanyama na uumbaji wa MUNGU na anachukia sana uumbaji alioumba MUNGU unapoharibiwa na akaniambia Ole wao wanaoharibu uumbaji wa MUNGU yaani kazi ya mikono ya MUNGU. Na wakati mwingine nilikula na yeye chakula nilichokuwa ninakula mimi na akinipa mifano ya maisha aliyoishi hapa ulimwenguni akiwa na wanafunzi wake. Akaniambia nimekula na wewe chakula hiki unachokula kama vile nilivyokula na wanafunzi wangu kipindi kile, wewe ni rafiki yangu na ni mwanangu.
Ilipofika 14/6/2010 siku hii akanitamkia rasmi wewe ni mtumishi wa MUNGU na umeandaliwa kwa ajili ya kanisa la mwisho ili kuwapeleka watu mbinguni. Ndani yako nitaishi mimi, ataishi MUNGU, ataishi ROHO MTAKATIFU. Nitakufundisha kuongoza wewe nipe mwili wako tu. Nikamuambia sawa BABA nipo tayari, kanisa uliite YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, usiogope lolote, adui yako ni adui wa MUNGU. Anayepigana na wewe ajijue anapigana na MUNGU na hakuna chochote kitakacho kudhuru au kukuweza siku zote za maisha yako kuanzia siku hiyo. Akaniambia Hebron utachukiwa sana kwa sababu umenikubali mimi na kwenda na mimi, ila wewe furahi na upige makofi. Na wivu utainuka kutoka kwa watumishi wengi zaidi sababu ya huduma niliyokupa, ila uonavyo hayo uelewe ni shetani yupo ndani yao.
98% wamenisaliti imebakia 2% katika ulimwengu wote ndio watumishi wa kweli na hawa 2% wamekandamizwa na shetani kupitia hawa hawa watumishi, wamekuwa freemason, wachawi, wanyang’anyi, wanatoa makafara, wameifanya nyumba ya MUNGU kuwa ni sehemu ya biashara, michango, kubadilisha neno la MUNGU na kuwalisha watoto wa MUNGU maneno ya uongo, mfano ubatizo wa kikombe, kuabudu sanamu, kuwazinisha na waumini na matendo mengi ya ufisadi. Akaniambia sasa hivi mimi siyo BABA yao wao wanaye babayao ambaye ndie shetani, midomoni mwao wanalitaja jina langu ila ndani ya mioyo yao ni wanafiki, wauwaji wa roho za watoto wa MUNGU. Ila kwa wewe nalijenga kanisa ambalo malango ya kuzimu halitaliweza, kamavile nilivyolijenga kwa Petro. Petro wa leo ndio wewe.
Sikumuelewa YESU ila siku zilivyoendelea aliendelea kunifundisha nikamuelewa na mpaka nikaanza kuifanya kazi yake. Ila hapa nitaelezea nilivyoenda kuzimu kuipiga, nilienda na wazee 24 na Malaika Mikael, baadaye nikawa naenda na YESU akanionyesha mahali pa kupiga na kulipua kuzimu na mpaka nilivyomkamata Joka Kuu 5.11.2012 baadaye nikawa naenda peke yangu kama ilivyo sasa, nikifanya kazi ya kuubomoa ufalme wa shetani na hata ilipofika 2.6.2014 nilimkamata mwanadamu ambaye alikuwa yupo katika nafasi ya tatu katika ufalme wa shetani 1) Joka Kuu, 2) Lusifa, 3) Maxwell; na sasa yupo katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, sasa anaitwa Isaya, yeye alikuwa ndie mtunza siri, zote za shetani na alikuwa anayo mafaili yote ya ulimwengu huu na siri zote za shetani. Ila sasa mafaili hayapo tena kuzimu yapo yamehifadhiwa na serikali ya mbinguni. Hivyo nitawaelezea siri za kuzimu ili mfunguke, sababu shetani ni mpumbavu sana na nia yake ni kutaka hata wewe uangamie ili uchomwe pamoja naye kuzimu
Na sasa ndipo ule unabii wa kanisa la mwisho unatimia na milango ya kuzimu haitaliweza zaidi soma katika blogwww.prophethebron.blogspot.com na website www.prophethebron.org na YouTube yangu utayakuta mambo mengi na utakuwa huru. Ni maneno ya habari njema ili ulimwengu upone na watu wamrejee YESU sababu kweli yupo ila 98% ni yesu wa maboksi (wa uongo ndiye aliyemiliki 98%).
SHUKURANI
Nawashukuru watoto wangu wa kiroho wote niliowazaa kiroho pamoja na watumishi wangu walio katika kanisa langu, wameniombea, na wengine wote wenye mapenzi mema na mimi na kwa YESU WA NAZARETI.
Asante.
MTUME NA NABII HEBRON WILSON KISAMO
KIONGOZI NA MWANZILISHI WA HUDUMA
KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY.
P.O.BOX 74
ARUSHA, TANZANIA.
EAST AFRICA.
EMAIL: maombi@prophethebron.org
WEBSITE: www.prophethebron.org
BLOG: www.prophethebron.blogspot.com
NAMBA ZA SIMU: +255 759 610 820
+255 764 042 149
+255 763 567 402
+255 759 253 593
YALIYOMO
- Utangulizi.
- Shukurani.
- Kuzimu ilivyo.
- Benki ya Kuzimu.
- Mavazi ya Kuzimu.
- Nchi 15 za Kuzimu.
- Mto wa Maji ya Kuzimu.
- Silaha tisa kubwa za shetani.
- Nini maana ya Christmas Tree?
- Nini maana ya Father Christmas?
- Siri za Kuzimu.
- Mawigi (weave) ni nywele za siri za Majini.
- Nguo zote za mitumba zina Mizimu.
- Adamu wa pili ni nani?
- Madawa ya Nywele yaliyotokea Kuzimu.
- Sifa za Nabii wa Mwisho.
- Brian Deacon siyo YESU.
- Sala Ya Toba.
JINSI KUZIMU ILIVYO
Kuzimu ni nini? Kuzimu ni mahali ambapo ni makao ya shetani na Joka kuu pamoja na malaika zake na mapepo na majini. Kuzimu ipo chini ya ardhi ya 900. Kuzimu kuna miji kama hapa ulimwenguni palivyo ila tofauti yake kuzimu pamejengwa kwa mpangilio, kuna magorofa ambayo hapa duniani hamna, kuna viwanda vya magari, nguo, vyakula, silaha na vinginevyo vingi. Katika dunia hii siyo kila mahali kwa chini ni kuzimu, mfano hapa Tanzania katika ardhi yake hata utoboe mpaka mwisho hautafika kuzimu, sababu kuzimu haipo full kama vile huku duniani palivyo, ila nitaelezea kwa ramani ya kuzimu ilivyo kwa chini ukitoboa ardhi utatokea au wanatokea katika ardhi ya China, Russian Federation, Australian Federation, United Kingdom, Lagos, U.S.A, Madagascar, Sudan, Syria, Ethiopia, Angola, Egypt na Libya. Katika utawala wa Joka Kuu alikuwa anao wakuu watatu; wa kwanza Joka Kuu huyu ndiye mungu wao na ndie kiongozi wa miungu yote ya uongo. Pili Lusifa, yeye ndiye mwana wake wa pekee, na tatu ni Maxwell yeye alikuwa ndiye roho mtakatifu wa kuzimu ambaye ndiye roho mchafu wa shetani. Ila sasa nimemtoa kuzimu anaitwa Isaya, ameokoka.
Joka kuu yeye alikuwa anao mji wake unaoitwa Freeman Village ila kwa sasa nimeshaulipua kwa kutimiza kazi ya BABA yangu wa mbinguni alionituma. Yeye aliishi umbali wa ardhi ya milioni mia tatu (300,000,000) kutoka katika ardhi ya dunia.
Lusifa yeye anaishi umbali wa ardhi 299,500,000 kutoka katika ardhi ya dunia.
Maxwell (ambaye ndiye Isaya) yeye aliishi ardhi ya 299,000,000.
Hao wengine wote huko kuzimu wapo mbali katika ardhi ya 100,000. Ukiangalia hapa utaona jinsi Joka Kuu alivyoitengeneza Serikali yake na kujitenga nao mbali, hao wengine wote.
Ofisi ya kuzimu head office ambayo sasa imeshachomwa haipo ilikuwa inaitwa (JLM)- Joka Kuu, Lusifa, Maxwell Office, hapo ndipo palipokuwa na mafaili ya serikali ya shetani ili kuwaangamiza watu.
NOTE:
Katika ofisi hii wachawi wote ndipo walikuwa wanaenda kuchukua nguvu na hata watumishi wanaotumia nguvu za giza na freemason, sasa ulimwengu utapumua sababu ya YESU WA NAZARETI kuubomoa ngome zao na wataaibika huo ndio ukweli, hapo ndipo wanapochukulia pesa na pesa za kuzimu wanatumia dola kabisa.
Kuzimu ni pabaya ajabu chakula chao ni nyama za watu ambao wamekufa huku ulimwenguni na sahani zao ni mafuvu ya vichwa vya watu.
Katika hii ofisi kubwa ilikuwa inavitengo vya kila aina mfano cha makanisa na kiongozi wake ni jini linaitwa Amakuta, wanabadilisha biblia halafu wanawaletea wanadamu elimu tofauti iingizwe kanisani na inapoingizwa tu tayari hilo kanisa linakuwa ni la kuzimu na YESU haonekani hapo. Mfano kanisa lenye ubatizo wa kikombe tayari muelewe limekuwa la kuzimu haijalishi jina la YESU linatajwa. Jiulize ubatizo wa kikombe upo katika biblia unayoisoma? Jibu, haupo au ubarikio wa watu wazima, au kuabudu sanamu, au watumishi kuvaa kofia kanisani, hawa wote asili yao ni biblia ya kuzimu na wanadamu wengi wanapokea mapokeo bila kujua wanamtumikia shetani na mbinguni hawataenda bali ni kuzimu. Hiyo tayari ni njia ya kuzimu.
Kanisa linaloruhusu ndoa za jinsia moja hilo usidanganyike silo la mbinguni, lipo kuwapeleka watu kuzimu katika kanisa nililoliona pamoja na biblia yao, YESU alisema watakuja makristo wengi na watatumia jina lake kuwateka wengi na ndivyo ilivyo. Ashukuriwe YESU aliyenionyesha hayo na niwaeleze siri hizi mpate kupona, ni mambo yaliyofichika yasingejulikana ni mpaka YESU kwa neema yake. Na zaidi wewe mkristo kama unaabudu katika kanisa linalofanya hayo niliyoyaandika chukua biblia yako mfuate pastor muulize mbona ubatizo huu haupo katika biblia akueleze, hana jibu. Ila wewe uelewe ameingiziwa biblia ya shetani na ndio sababu anabatiza ubatizo wa shetani, funguka uelewe hapo hapapeleki mtu mbinguni bali ni mahali pa kuwapotezea watu muda wasimjue YESU wa kweli na akija asiwapate. Amenituma niwaeleze ukweli, watu wote wa mataifa yote, hata unaposoma kitabu hiki maneno haya usione ni ya Hebron, hapana, ndivyo ninavyoelezwa na YESU mwenyewe na wewe uyapokee ili upone, na shetani hapendi mjue siri hii kabisa ila endelea kusoma, yapo mambo mengi katika kurasa zifuatazo.
BENKI YA KUZIMU (JLM BANK)
Benki hii kirefu chake ni Joka Kuu, Lusifa, Maxwell benki. Ndiyo benki ambayo ilikuwa inawapa watu pesa huku ulimwenguni pamoja na freemason ila nimeichoma na mtaona baadhi ya nchi zilizokuwa zikipata pesa kutoka kwenye benki hii, mtaona uchumi ukishuka, au mabenki yakififia na pia matajiri waliokuwa katika mtandao wa freemason wataporomoka. Ni wakati sasa ya watu wanaomtegemea MUNGU kutajirika na kumiliki. MUNGU anachukia sana na kazi hii ataifanya yeye mtakapoyaona hayo msishangae. Benki hii ina wanachama wengi sana waliopo duniani, wakiwemo manabii, wachungaji, wainjilisti, mitume, waalimu, wachezaji mpira maarufu, wasanii maarufu, idadi kubwa wanachukua pesa huko na ni watenda kazi wa shetani (Black Money). Wana pesa ambazo ukiwakagua kimahesabu utaona ni pesa zisizojulikana zimetoka wapi asili yake.
Kama nilivyowaelezea tokea YESU aniite nikamtumikie lengo ni kuwakomboa watu wa mataifa yote wamrudie yeye na kuwatoa katika mateso ya shetani na kuubomoa ufalme wake kama ilivyo sasa na mpaka ule mwisho wake. Hapa ulimwenguni siyo jambo geni mnasikia watu wamekuwa freemason iwe katika kila sekta ili wapewe pesa na shetani, ni wengi mmesikia kuwa kuna watu wanapesa nyingi hata ukifikiria asili ya pesa zake hautajua alipatia wapi na ndio matajiri wengi katika ulimwengu wote hao walikuwa wanachukua pesa katika benki ya shetani ilivyokuwaga kuzimu ila sasa benki hiyo imechomwa na YESU WA NAZARETI haipo tena na wala watu waliokuwa wanategemea pesa za freemason mtaona wakiporomoka, filisika katika dunia yote, myaonapo hayo ujue ujumbe aliyokuletea Nabii Hebron wa Tanzania umetimia, hawatapata pesa tena sababu benki ya kuzimu nimeichoma moto pamoja na wafanyakazi wake wote huko kuzimu.
Benki hiyo ya kuzimu ilikuwa inaitwa (JLM BANK) kirefu chake ni majina matatu ya shareholders (Joka kuu, Lusifa, Maxwell Bank) benki hii ilikuwa inatengeneza pesa aina ya dola tu na cha ajabu hata huku duniani zikiwekwa katika machine ya kukagua pesa zinaonekana ni original kamahizi hizi zinazotumika duniani. Pesa hizi ndio walizokuwa wakipewa watumishi waliojiingiza katika mtandao wa freemason, wasanii, viongozi mbali mbali, wafanya biashara na baadhi ya vyama vya siasa katika nchi mbali mbali (pesa chafu). Nitaelezea katika kanisa ili watu wapone wasidanganyike sababu kupitia hizi pesa, kupitia watumishi wanaompenda shetani walijiingiza na kuliingiza kanisa kiasi cha 98% ikatekwa na shetani na YESU akabakia na 2% ya watu, 98% ikawa ni idadi ya joka kuu. Ndugu msomaji pesa hizi zilikuwa zinaletwa kimwili kutoka kuzimu kupitia malango ya nchi ambazo nimezitaja katika makala ya Nabii Hebron isemayo Je unajua kuzimu ipo wapi katika ramani ya dunia? Na cha ajabu hata hizo serikali za nchi hazihusiki na kupokea hizo pesa wala kujua. Ilikuwa ni jambo la siri, na cha ajabu mtaona baadhi ya makanisa yanaibuka na utajiri ambao unaleta maswali ghafla ghafla, waliokuwa wanapewa pesa ili waje waieneze injili ya shetani kwa spidi ili YESU akose watu, na utaona ukichunguza sababu wengi mnayajua haya ila leo ni siku ya kuhakikishiwa jibu lako ulilosubiri muda mrefu hadi leo YESU WA NAZARETI anakufichulia. Na kupitia pesa hizo za shetani hapa ulimwenguni yamejengwa makanisa mengi sana kupitia pesa za shetani na watu wakaona ni pesa kutoka kwa MUNGU kumbe ni shetani. Nanukuu maneno ya YESU alivyonieleza hata kabla ya kuiivunja hii benki, akaniambia Hebron mtumishi wangu wanadamu wanafikiri mimi nipo katika hayo magorofa, vinanda, mimi sipo hapo kabisa na sitendi mimi, hayo ni majengo ya shetani, mimi nilibakia nikishangaa ila sasa namuelewa, kumbe pesa ni za shetani. Je nikuulize swali, je shetani akijenga nyumba yake YESU ataweza kuja kukaa katika hekalu la shetani? Jibu, haji, hii ni sababu ya pesa za freemason na unapoabudu katika kanisa la jinsi hilona wewe muumini tayari umetekwa na shetani, leo ufunguke utoke huko.
Kanisa lenye benki- benki hiyo asili ya mwanzilishi wa huduma hiyo uelewe ukweli, huyo amepewa mtaji na shetani na kazi anayoifanya ni kueneza ufalme wa shetani, na kupitia benki hizo kila anayeweka pesa hapo ananyang’anywa nyota, uthamani wa pesa zake zinapelekwa kwa joka kuu na matokeo yake matatizo na kufilisika hakukuachii na mwisho wa kifo chako unabakia kuzimu, sababu pale tu unapopeleka pesa yako katika benki za kanisa nafsi yako inatekwa unakuwa umeshakufa kiroho ila mwili unabakia gogo. Siri anakuwa anajua kiongozi mkuu wa huduma hiyo hayo ni maagano ya kutoka kwa shetani afanye biashara. Wakati YESU WA NAZARETI alisema usisumbukie chochote, fanya kazi yangu, sasa pima maneno hayo.
Yatakayotokea na yameshaanza kuanzia sasa, mtaona muelekeo unapotoa na kufilisika na mengineyo atafanya MUNGU peke yake sababu ya hasira aliyotesewa watoto wake na baadhi ya wachawi na watumishi kuwateka watoto wa MUNGU, ndivyo ilivyo na hakutabadilika.
Pesa hizi za kuzimu zinatumika katika nchi mbali mbali kuvuruga amani iliyoletwa na MUNGU, kazi kubwa ni VITA.
NOTE:
Hivi umeshajiulizaga huko wanakotoaga misaada ya kuwaletea pesa makanisani na miradi je wao hawana shida na hizo pesa? Hivyo ndivyo ilivyotumika kuliingiza kanisa kwenye freemason na kupitia watumishi ambao wanatekwa na shetani. Na kuanzia kutumia jina la YESU kuzini roho za wana wa MUNGU pasipo kujua na kupenda.
MAVAZI YA KUZIMU
A) WANAWAKE
- Mavazi haya ya kuzimu ambayo wanawake wanayovaa hapa ulimwenguni pasipokujua na wengine wakijua kabisa ni ya shetani ambayo yanabuniwa na Yezebeli ili kila anayevaa tayari amemfungia mwanamke baraka zake na pia kuyateka maisha yake na kumfungia asiende mbinguni, sababu katika mwili wake yeye anakuwa ni kahaba kiroho mpaka kimwili haijalishi kimwili yeye hatendi mambo ya ukahaba, ila kutokana na hilo vazi alilolivaa basi tayari anakuwa amevaa ukahaba na mapepo huishi juu yake bila kikwazo chochote.
- Mavazi haya asili yake ni kuzimu na mengine yamebadilishwa kwa kuandikwa kinyume mfano MAX wa kuzimu ikaandikwa WAX, huyu MAX yeye ndiye aliyekuwa namba tatu katika ufalme wa shetani na unapovaa kitu kilichoandikwa kwa jina lake tayari na wewe unamsujudu mzimu wa MAX na kuporwa baraka za maisha yako. Sasa wakawapiga watu upofu wakavipa vitu majina WAX- (MAX), pia NIDA nayo asili yake ni kuzimu.
- Yapo mavazi ya mwanamke ya kuonyesha tumbo wazi.
- Nguo za kuonyesha matiti na kuonyesha mgongo.
- Chupi za bikini.
- Chupi za kike zenye zip na zenye mifuko ya kuwekea pesa.
- Chupi zilizochorwa moyo au zimeandikwa katika nguo za ndani za kike mfano; girlfriend, boyfriend, na maneno mengi tu ya ajabu, karibu, furahi, nakupenda mpenzi.
- Nguo za transparent.
- Stocking zote unapovaa unakuwa unavaa miguu ya majini.
- Vimini, katika ulimwengu wa roho wewe ni kahaba maarufu.
- Nguo zote zenye magamba au picha mfano wa nyoka, mamba, na nyingine zenye madoa doakama ya chui.
- Viatu vyote virefu- unapovivaa tayari unakuwa unaitwa twiga wa kuzimu na madhara yake maisha yako yanaibiwa ni kwa kupitia mlango huo.
- Pochi za mikononi pamoja na mabegi yote yenye scales au magamba au viatu mfano kamamagamba, ukiona tu utajua unapovitumia unakuwa umebeba nyoka na roho za shetani zinakumiliki. Inakuwa ni pamoja na mikanda yeyote yenye mfano wa picha za magamba.
- Nguo zenye mipasuko mbele, mfano katika skirt unapoivaa ina maana umewafungulia mapepo wa uzinzi waingie katika mwili wako na kwa njia hiyo ni lazima wataingia tu sababu wanao mlango.
- Eyeliner- unapopaka katika jicho lako unakuwa unajiwekea alama na wewe ni mfuasi wa shetani, pia napenda uelewe kuwa na shetani na yeye huwa anajipaka eyeliner (wanja) katika jicho lake la kulia ila yeye hulizungushia mchoro wa duara, na unapojipaka wanja basi unakuwa wewe ni mali yake yamkini hata haujui na unampenda MUNGU.
- Kukata nyusi- unapokata hizo nywele unakuwa unayakata maisha yako na ndio sababu maisha ni magumu kwa wanawake wengi hiyo ni sababu moja wapo.
- Kuvaa shanga za kiunoni- kila unapovaa shanga katika kiuno chako unakuwa umejifungia majini, hata ukijifungia cheni ya gold au silver, uelewe tayari unayo majini katika mwili wako na madhara yake wanandoa wanakuwa wazinzi, faraka, ndoto za zinaa, mikosi na balaa, vitu hivyo havifai katika jina la YESU. Unapovivaa unakuwa unaliharibu hekalu la MUNGU kwa kufunga ndoa na mapepo katika kiuno chako, au kwa lugha nyingine hizo shanga ni pete za majini na unapovaa unajifungisha ndoa na wao katika ulimwengu wa roho.
- Nguo za kubana na kuonyesha maumbile yako yalivyo, jinsi ulivyoumbwa mfano hili siyo jambo jipya. Embu tembea katika maeneo mbali mbali utaona wanawake wamevaa suruali zinazoonyesha figure zao, sasa ujiulize wanamuonyesha nani? Jibu, wanawaletea wanaume maroho ya ushawishi ya uzinzi hivyo wanapovaa mavazi hayo tayari wao ni makahaba. Mavazi haya yameletwa ulimwenguni ili uzinzi ustawi na kuwateka wanaume katika majaribu, ili amri za MUNGU zivunjwe na kila anayevaa hivyo uelewe kwanza ni machukizo mbele za MUNGU na pia unatumikishwa katika upande wa shetani eidha kwa kujua au kutokujua. Sasa ufunguke, uyasitiri maungo yako au mwili, ili upone roho yako.
- Kuvaa mavazi ya kiume.
- Kuvaa hereni kubwa kuliko sikio- unakuwa unavaa hereni ya mama wa makahaba. Hereni salama ni ile ambayo ni ndogo ambayo inakuwa sawa na kasehemu cha kuwekea tundu la sikio, hizo kubwa kama bangili hizo ni za mama wa makahaba.
- Kila rangi unayoipaka katika kucha yako uelewe ni dhambi na unayafunika maisha yako usije ukafanikiwa, na pia yanaibiwa na yanapelekwa kuzimu unapewa wewe ya mapepo ambayo ni shida tupu, hata kupaka hyena kujichora mwili, matatoo yote ni dhambi. Unapojichora tattoo, unajiwekea alama wewe ni freemason, ni wa kuzimu siku zote.
- Kila product yenye neno ultra, iwe katika kitu chochote, kinatoka kuzimu kuja kuiba vitu vya wanadamu na kuwaharibu.
- Unapoweka rollers kichwani, unakuwa umejiwekea funza wa kuzimu katika akili zako. Na akili zako na ufahamu kuibiwa na hao funza wa kuzimu na matokeo yake mtu unakuwa haujielewi elewi na akili zinadumaa.
- Kutairiwa wanawake hiyo ni dhambi MUNGU hajamruhusu mwanamke atairiwe. Mwanamke anapotairiwa kile kiungo kilichokatwa kinapelekwa kuzimu na kumuibia mwanamke uthamani wa uke wake na uzao wake na kuharibu ndoa na kufanya mwanamke achanike wakati wa kuzaa na kijiwekea alama wewe ni wa mapepo.
- Pedicure- unaposugua miguu salooni unakuwa unayaondoa maisha yako na unamkufuru MUNGU yeye aliyekuumba na kukuwekea utayari wako katika miguu.
B) WANAUME
- Mavazi ya wanaume ambayo asili yake ni kutoka kuzimu katika viwanda vya kuzimu yapo mengi sana ila nitaelezea kwa kiasi fulani ili mpate picha na mpone.
- Mavazi yote yenye nembo za ajabu, mfano T-shirt inapicha ya mti wa bangi au sigara.
- Nguo yenye picha ufunguo- ina maana ule ufunguo umeivaa hiyo nguo ufunguo huo umekufungia usiende mbinguni na ufanikiwe kumkufuru mwenyezi MUNGU, na hata katika cheni, ukikuta kamaufunguo uelewe ni hatari tupu, hata cheni yenye msalaba ina maana uelewe unapovaa unakuwa wewe umelaaniwa na maisha yako yanasulubiwa katika ulimwengu wa roho. Pia uelewe hakuna msalaba mtakatifu kabisa hata ule aliouliwa nao YESU siyo msalaba mtakatifu ni msalaba wa laana na ndio sababu damu yake ilipomwagika pale msalabani ikatuondolea laana, sasa shetani akabuni njia nyingine na kuwapiga upofu watu waone msalaba ni kitu kizuri na kumbe siyo. Unajihukumu mwenyewe, hata kuzikwa na msalaba ni makosa. Nikuulize swali unapozikwa je unaenda kuhukumiwa na wewe? Au je msalaba ni alama ya mkristo? Jibu siyo. Watumishi wanawapotosha watu kwa kumuamini shetani na kumfanya YESU akose watu wa kwenda mbinguni. Jiulize swali kina Ibrahim, Isaka na Yakobo katika makaburi yaoipo misalaba? Jibu hakuna. Na kamasisi tu uzao wa Ibrahim, kwa nini tusiige mfano wa Baba yetu Ibrahim? Na zaidi je YESU yeye alizikwa na msalaba? Jibu hapana, je YESU si ndiye kweli na alionyesha njia ili tuifuate. Sasa swali, kama alionyesha njia, tuanze katika maisha yake je uliletwa msalaba? Jibu hapana. Sasa hii misalaba madhara yake unapokufa ukawekewa katika kaburi inakufanya wewe uliyekufa usulubishwe katika ulimwengu wa roho, na wote waliozikwa na misalaba wanateseka katika ulimwengu wa roho na shetani anamnyanyulia MUNGU si unaona msalaba wanataka wenyewe niwasulubishe na MUNGU ni MUNGU wa haki analiangalia neno lake, kataa kuzikwa na msalaba iga YESU alivyozikwa, iga mazishi ya Ibrahim, Isaka na Yakobo, pamoja na mitume na manabii wa MUNGU wa kweli waliopita ambao kwa heshima MUNGU amewaita wazee 24. Kataa huo uchafu watu wanapotezwa, amenituma YESU niwaeleze ukweli utakaye sikia utapona, utakaye kaza shingo damu yake haitamlilia MUNGU katika mikono yake.
- Boxer- hizi ni chupi za nyani wa kuzimu unapozivaa unaibiwa na mapepo uthamani wa nguvu zako za kiume na pia unaolewa na majini katika ulimwengu wa roho unakuwa wewe ni shoga. Na mlango ni hii boxer.
- Nguo zote zenye zipu kifuani tu, unapokuwa na nguo ya aina hiyo kila unapofungua zip unakuwa unayachana maisha yako katika moyo wako na unapofungua zipu hiyo unakuwa unayafungua usifanikiwe.
- Kila kitu chenye neno ultra kinatoka kuzimu.
- Mikanda yenye bastola au bunduki- unakuwa umevaa jini bedui katika maisha yako na makata hivyo wanayaharibu. Mikanda yote yenye sura za watu katika bacol au nembo yeyote ile uelewe umeivaa kuzimu na kuzimu inajiunganisha na wewe kupitia katika kitovu chako kwa njia ya bacol ya mkanda.
- Kusuka rasta- unakuwa umevaa pepo kichaa na mara nyingi huja kutokea katika mwili mtu anakuwa kichaa, na pia unakuwa na mambo ya freemason pasipokujua na wengine wanajua.
- Kuvaa suruali mlegezo- hiyo ni dalili wewe ni shoga katika ulimwengu wa roho na unapovaa hivyo unayaita majini yaliyokuoa katika ulimwengu wa roho yeye yazini na wewe.
- Kofia zote ambazo vijana wanasema ni za kileo zote zinatoka kuzimu na kijana anapovaa akili yake huibiwa ndoto zake zote hubakia boksi, na ndio sababu idadi kubwa ya wanaovaa hizo kofia fuatilia utakuta ni wavuta bangi, walaji wa cocaine, wahuni, wameharibika ni sababu ya hizo kofia zenye majina ya ajabu na ya wanamziki na watu ambao tayari ni wanachama wa freemason..
- Nguo za kubana kupitiliza mfano T-shirt, suruali, inakubana unayaonyesha maungo yako jinsi yalivyo.
- Kusuka nywele- unaposuka tayari uelewe wewe tayari ni mke wa jini fulani kuzimu, na unaye mume unayemtumikia katika ulimwengu wa roho japo wanadamu hapa duniani wanakuwa ni wanaume tu ila ni boksi.
- Mashati yenye mipasuko katika sehemu za mifuko, mashati haya watu hawapendi kuyachomekea sababu yana mipasuko, sina haja ya kuelezea sana, yapokama Kaunda suti. Nguo yeyote ya mwanaume yenye mipasuko sehemu za kiunoni hizo zote ni za kuzimu, unapoivaa uchumi wako unapasuka na maisha yako yanakuwa ni ya shida shida tu.
- Nguo zenye sura ya nyoka, mamba, chui, madoa doa, viatu venye magamba au ukiviona vina sura ya magamba haijalishi ya aina gani havifai, ni viatu vya kuzimu.
- Viatu vilivyochorwa tick (Ö) au X ina maana hiyo tick unakubali jina lako liandikwe katika ufalme wa shetani na X ina maana maisha yako yanatiwa X yote.
- Kila kitu chenye jina MAX uelewe asili yake ni kuzimu na kina madhara.
- Viatu vyenye majina ya ajabu na vingi havielezeki hata sitaweza kuviacha kuandika even kwa 30 days, omba ROHO MTAKATIFU akufunulie wakati unahitaji viatu omba atakuongoza na roho ikigoma tu wacha, hiyo ni dalili.
- Kofia zote za duara zisizo na chepeo halafu zina kamba au kinaninginia unapozivaa, unakuwa umeweka kwato ya jini katika maisha yako na nyingine ni kofia za duara ile zimetobolewa mashimo mengi zote hizo ni makwato ya majini na shetani amewaletea wanadamu ili wawe wajinga na wasimjue MUNGU wa kweli siku zote za maisha yao, sasa uamuzi unao wewe utavaa makwato ya majini au utayatupa.
- Mwanaume anapovaa bangili (ringi) hapo unakuwa umejiingiza na kufunga ndoa na shetani, ila utakapoivua tu tayari umevunja ndoa na shetani, ringi hizi watu wengi wanafungulia vinywaji au kutumia kama silaha wakati wa kupigana na zaidi mwanaume hautakiwi kuvaa bangili katika mkono kabisa, unapovaa unafunga ndoa na shetani, na pia hata wengine wanafunga nyuzi katika mikono, hapo tayari umefunga ndoa na shetani na wewe ni mtu wa shetani, sasa amua, ila wengi wanajua kabisa ni masharti waliyopewa kuzimu inawezekana ni raia, mfalme, au mtu wa karibu, utashangaa siku zote ipo katika mkono, watu wanafikiri ni urembo, hapana hilo ni agano la shetani.
- Kutoboa masikio au sikio- iwe ni mtu yeyote yule wapo hata wachungaji wanatoboa masikio na kuvaa hereni- hao wote katika ulimwengu wa roho ni mashoga wala YESU hana ushirikiano nao. YESU hana mashoga. Jiulize hawa wanatokea wapi? Ni mashoga wanaoeneza injili ya yesu wa uongo na kuwapeleka watu kuzimu.
- Shetani aliwateka wengi hata waliookoka katika maeneo mbali mbali ila YESU amenituma niwaeleze ukweli sababu anaona mnavyoteseka na hampati majibu na akaniambia Hebron haya mateso yasingewapata wanadamu ila yamewapata sababu niliowaita wamemgeukia shetani na ndio anakuwa baba yao hivyo wanafanya kazi ya baba yao ambao ni lusifa hata wanangu wanateseka na kuangamia ila nimefurahi sasa sababu upo wewe Hebron, nimekupata wewe uliyenikubali kunitumikia na kuyatenda yale ambayo mimi na BABA yangu mbinguni na ROHO MTAKATIFU ndio tunayoyataka, na pia Hebron nataka uelewe kabla ya wewe kuumbwa MUNGU alishakuandaa na akajua ikifika muda wake atakusimamisha na anajua utaifanya kazi yake sababu anajua yeye aliyokuumba hivyo usiogope lolote. MUNGU alikuficha siku zote kama vile alivofichwa Musa akatunzwa na Farao hakuuwawa, hivyo ndivyo ilivyo kwako na utaifanya kazi yangu vizuri sana na kuzimu haitakuweza milele. Sasa nimefurahi sababu kila akusikilizaye na kubadilika na kutii unayowaeleza atapona sababu ndani yako MUNGU ameweka majibu ya viumbe vyote na kila kitu. Maneno haya kila nikumbukapo nasikia machozi yananitoka kwa ajili ya watumishi walivyomsaliti YESU hata na kugeuka freemason, wachawi, waongo, wanyang’anyi ila usiogope ninajua kinachokuja na watu mtamfurahia YESU WA NAZARETI.
- Haya magauni ya harusi ya kuzimu- kila gauni la harusi lenye kuburuza mkia- ina maana ule mkia unaoburuzwa ni mkia wa lusifa. Lusifa anao mkia ila nilimkata mkia wake. Unapofunga ndoa na gauni la jinsi hiyo ndoa yako unampa lusifa. Na unapovaa gauni la harusi unaonyesha mabega na manyonyo unakuwa unavaa gauni la pepo kuzimu la kufungia harusi zao na wewe unajiunganisha hivyo hivyo na mama wa makahaba. Ukiangalia leo hii watu ndio wanasema ndio fashion. Hii siyo fashion mimi nasema yote ili nisije nikaulizwa na YESU siku ile ya mwisho sikuwaeleza ukweli ili mpone na usijisumbue hata kama jina lake YESU linatajwa haiunganishi hiyo ndoa sababu la hilo vazi mimi pia nilikuwa sijui, ila sasa uelewe ili upone. Wanawake mkatae sasa msiwekewe tena mikia ya shetani ukauburuza.
- Kujipaka rangi ya kucha. Kila rangi inayo maana yake, rangi zote ulimwengu maana za kucha asili yake ni kuzimu. Ukipaka hizo rangi unaharibu maisha yako pasipo wewe kujua na hizo rangi zimechanganywa na rangi za ngozi za watu waliokufa baada ya kuchunwa ngozi zao na mashetani wakala nyama zao. Sasa unapozipaka unakaribisha majini katika maisha yako na uthamani wa mikono unaibiwa, hata pesa hazikai wala kazi zako hazibarikiwi sababu MUNGU hana mahali pa kupitishia baraka katika mikono yako sababu shetani ameshaweka vitu vyake katika mikono yako.
- Kucha za bandia- hizo ni kucha za majini walizozikata kuzimu kama vile na wewe unavyokataga zako, unapozivaa kucha za bandia unakuwa unawapa majini uthamani wa kucha zako ambapo katika kucha zako zipo Baraka wanaziiba zako unabakia na zao na unakuwa tayari umeingia urafiki na majini pasipo kujua japo wengine wanajua na wanayapenda majini.
- Nguo zote ambazo za wanawake zinakuwa na mipasuko zote hizo asili yake unakuwa unajitengenezea mkia wa lusifa na lusifa kuitumia njia hiyo kukupata.
- Nguo ambazo ni short ni fupi zinazoonyesha mapaja na hupendwa sana kuvaliwa na masecretary katika ofisi mbali mbali, sasa hilo vazi kila unapolivaa ina maana unamkubali shetani kabisa ila sasa uelewe haifai.
- Kuvaa pini katika ulimi, unapotoboa ulimi tayari unampa mama wa makahaba ulimi wako na vitu vyako kisha unabakia na ulimi wake na anakamata fahamu zako na kisha kwa kutumia ulimi huo uliovalisha pini anautumia kunyonya viungo vya siri vya kiume na mwanaume atakayefanyiwa hivyo anakuwa viungo vyake vimemezwa na Yezebeli katika ulimwengu wa roho kupitia mwili wa mwanadamu. Kazi kubwa ni kumeza viungo vya kiume kwa njia ya kuvinyonya na pia hata ukinyonywa ulimi au kiungo chochote na mtu aliyetoboa ulimi, uelewe anatumika kumeza vitu vya watu na ndani yake yupo Yezebeli na ndiyo sababu ametoboa ulimi. Ilikumjua mtu mwenye Yezebeli au Yezebeli anaishi ndani yake angalia ulimi ametoboa na katika ulimwengu wa roho na yeye anakuwa ni mtoto wa Yezebeli na Yezebeli anauhalali sababu anayo alama yake katika ulimi.
- Alama nyingine ya Yezebeli ni inayokufanya kuunganika katika kitovu cha mtu na Yezebeli utaona mtu anatoboa kitovu au anatoboa pembeni ya kitovu, hii ina maana amejiunganisha kupitia kitovu, huyo mwanadamu atakuwa anatabia za kipepo, hata kutembea uchi, mlevi, hafai kuolewa au kuwa mke bora, sababu atakuwa ni kahaba.
- Na wengine wanatoboa (wanawake) wanakitoboa KISIMI wanakivalisha pini, yaani ukiona hivyo uelewe kile kiungo cha kike alicho nacho huyo binti siyo cha bindadamu ni cha pepo, kama alivyo mama wa makahaba na yeye amejitoboa na anavaa pin kubwa ya dhahabu ambayo ina urefu wa 30 cm na unene wa 2 cm. Mmh, haya mambo yanatisha kiasi hata mimi nimeandika huku nilikataa nisione alivyo ila YESU amenitia nguvu ili niwaeleze mjiepushe msifikiri ni vizuri hayo sasa yaelewe, okoka uvitupe hivyo vitu.
- Na alama nyingine ya mtu mwenye Yezebeli anavaa pini katika macho, bangili miguuni hasa bangili moja katika mguu mmoja na kujichora katika mapaja au kuchora moyo na alama ya mshale au kuandika majina ya watu katika mapaja au tumboni, mgongoni au popote katika mwili.
MALAPA MEKUNDU
Malapa yote yenye rangi ya nyekundu siyo salama sababu unapoyavaa unaibiwa maisha yako na shetani. Na katika haya malapa shetani aliweka pepo kivutio na ndio sababu utaona idadi kubwa ya watu wana malapa mekundu, haya yapo hapa ulimwenguni kwa ajili ya kuharibu maisha ya mwanadamu. Unapoyavaa maisha yako yanakuwa ni magumu sababu yale yako uliyopewa na MUNGU yanaibiwa utayari wako katika miguu na kukufanya wewe kubakia na maisha hatari ndio sababu ya hiyo red.
PIPI KIFUA, PIPI KIJITI
Kila unapokula pipi kifua uelewe unakuwa unakula makamasi ya majini na unakula TB, unakula ukimwi na magonjwa ya kifua pamoja na pumu.
Pipi kijiti- kila unapokula pipi kijiti ina maana ile pipi ndio dunia na kile kijiti kilichoichoma hiyo pipi ni wewe unaichoma dunia katika maisha yako usifanikiwe, na maana nyingine ni wewe unajiharibu maisha yako.
VIFAA VYA UJENZI (Baadhi)
- Mabati- yapo mabati yanayotoka katika nchi za America na South Africa ni tofauti na mabati yaliyozoeleka miaka mingi katika nchi mbali mbali. Unapoyatumia katika nyumba yako tayari paa lako umelifunika na shetani na ni vigumu YESU hata Malaika kuja katika nyumba za watoto wa MUNGU sababu ni haya mabati, tayari kuna kitu cha shetani.
- Vipo vitasa vya milango vyenye rangi yeyote ya brown, unapotumia vile vitasa katika nyumba yako vinatumika sasa ndio mlango wa majini kuja kwako na kuingia bila tatizo na kuiba vitu vya watu kwa njia ya kipepo, na hata ukifunga na ufunguo wana kuja na kuvifungua na kuingia kimwili kabisa katika nyumba
- Rangi- zipo rangi zinaanza na herufi S na nyingine herufi C unapopaka ragi hizi katika nyumba yako unakuwa umepaka makamasi ya majini katika nyumba yako, makufuru, balaa mikosi na kukufanya Baraka za MUNGU zisije katika nyumba yako na hata Malaika kuja kwako, hii ni sababu ni uchafu na watu hawajui, asili yake ni kuzimu, hazikomboleki wala hazitakasiki. YESU anawasaidia watu wote ili wapone. Unapoipaka katika nyumba, unapaka chuma ulete na ni mlango wa majini kuja kwako sababu upo na vitu vyao
Vipo vingi ila endelea kusoma vitabu vya Nabii Hebron na kuingia katika blog yawww.prophethebron.blogspot.comutajifunza mengi. Yote aliyowatendea wanadamu huyu mjinga shetani. YESU akanipeleka ninayajua na ninapowaeleza ukweli huu mnapona roho zenu na maisha yenu yatakuwa mazuri sawa sawa na MUNGU alivyopanga. Ila shetani alibuni viwanda ili aharibu maisha ya watu, YESU WA NAZARETI anawapenda sana mrejeeni yeye, wakati wake umefika wa kurudi, usidanganyike tena, katika makanisa mkifundishwa kinyume na biblia hao ni maajenti wa shetani ili kufaulisha kazi zake za kuua roho za wana wa MUNGU.
NCHI 15 ZA KUZIMU.
Nchi hizi ni tofauti na nchi zilizopo hapa ulimwenguni ila katika nchi hizi ambazo viongozi mkuu ni Rais ambaye anaitwa Kaini, huyu ndiye mtoto wa Adamu wa kwanza ambaye ndiye aliye muua Abel (Soma Kitabu cha Mwanzo 4: 6-14) baada ya kifo chake Kaini kufa kimwili, shetani alimpa cheo cha Urais katika hizi nchi 15 na katika hizi nchi 15 wapo Marais na hufanya uchaguzi kila tarehe 25.12 kila mwaka hufanya uchaguzi wa Urais na katika hawa Marais ambao wengine wapo hapa ulimwenguni ni watu maarufu na matajiri, wengine ni waimbaji wa mziki matajiri sana, kumbe ni Marais kuzimu ikiwemo pamoja na baadhi ya makochi maarufu wa timu za mpira katika vilabu maarufu huku ulimwenguni. Mnawaona ni watu wa kawaida kumbe ni Marais katika nchi za shetani huko kuzimu. Lengo za hizi nchi za kuzimu zimechukua utajiri wa nchi za huku ulimwenguni wakapeleka huko na ndio sababu utaona nchi huku ulimwenguni lazima maana na hata baraka zilizopo hazitoshi kumbe hizi nchi 15 za shetani ndizo zilizoiba Baraka za nchi hizo, na katika nchi hizi ili hawa freemason na manabii wa uongo waende kwa Joka Kuu lazima wafike katika nchi hizo, hapo ni mahali pa kupumzikia na wapewe visa ya kwenda au kibali, na pia kulikuwepo na ndege kubwa sana moja ambayo ilitumika kama ya usafiri, ndege hiyo ikaitwa AIR-UWMK- Air Umoja wa Mataifa Kuzimu. Ila sasa nimesha ilipua pamoja na nchi zote sasa hivi hamna mahali pa kwenda ni vita katika ulimwengu wa roho. Haya yote nakufunulia watu wote wa mataifa ili muelewe jinsi shetani alivyo mbaya na manabii wa uongo, muelewe kazi walizokuwa wanazifanya ili kuangamiza roho za wana wa MUNGU. Sasa mtapona, mliokata tamaa na mlio uliwa kiroho, utafufuka. Amenituma YESU niuharibu ufalme wa shetani na ndivyo ilivyo, waliokuwa wanategemea nguvu za gizahawatafanikiwa tena, kila Rais aliyepata cheo hicho kwa shetani lazima alienda katika hizo nchi za kuzimu apewe amri ya kuua watu na kutoa makafara na kupewa pesa za kampeni. Kwa sasa hizi nchi nimezilipua na Malaika Mikaeli hazipo tena.
MTO WA MAJI YA KUZIMU?
Nampenda YESU WA NAZARETI sana ambaye ananifunulia haya ili niwaeleze mpone na kumvua shetani mavazi yake abakie uchi kama ilivyo sasa mmemjua mambo yake na alivyowafunga na ni adui ya wanadamu ila amenituma YESU kazi yangu niuharibu kabisa ufalme wake na ufalme wa YESU WA NAZARETI usimame katika ulimwengu wote.
Yeremia 1: 9-10.
Nilipoenda kuzimu nikiwa na Malaika Mkuu anayeitwa Mikaeli pamoja na Malaika wengine wapiganaji na YESU akiwepo na serikali yake akinionyesha shetani jinsi alivyowaunganisha wanadamu na kuzimu na kuwaunganisha na vitu vyake pasipo kujua na akijua kuwa kwa kutumia njia hiyo YESU WA NAZARETI hata wapata hawa wanadamu tena. Sasa kama ni mtu mwenye akili ni YESU WA NAZARETI, hakuna kama yeye na yeye ndiye anipaye akili za kuupindua ufalme wa shetani na mengineyo yote.
Nitaelezea kuhusu mto uliopo kuzimu, ni mto mkubwa sana kama vile mto mississipi uliopo Marekani. Mto huo wa kuzimu unaitwa Timberland river, nilishtuka sana kusikia jina hilo la Timberland, akanionyesha ulivyo na kazi zake. Mto huu ndio mto ambao kila mtu anayebatizwa kwa ubatizo wa maji ya kikombe, au ya kisima, au kubatizwa kwa jina la mchungaji hao watu wanakuwa katika huo mto wa shetani na YESU hawapati na katika mto huo ni mto ambao manabii wa uongo huenda kuchukua maji ya kuzimu halafu wanawaambia watu huku duniani ni maji ya baraka, kumbe ni kinyume, ni maji ya mauti na ukimwagiwa lazima uanguke chini unapoanguka chini basi unaunganishwa na kuzimu kupitia ardhi unakuwa tayari wewe ni wa shetani. Na pia kila walipokuwa wanaishiwa nguvu waliokuwa wanaenda katika huo mto wanaoga na kupata nguvu. Ila sasa nimeuharibu hakuna tena huo mto na utaona wakiaibika, wale wote waliomsaliti YESU WA NAZARETI wakamkimbilia shetani, kiburi chao tayari kimeisha. Na pia katika ulimwengu kila unapovaa kitu kimeandikwa Timberland unakuwa wewe mwanadamu tayari ni wa shetani japo wewe hauelewi kimwili, iwe ni chochote cha jina hilo, asili yake ni mto uliopo kuzimu, freemason na manabii wa uongo wanaelewa ninachokisema na wanatamani kufa sababu siri zao YESU anaziweka peupe.
Shetani kavuliwa nguo sasa yupo uchi. Na mimi Hebron siri hizi nazitoa kamavile aniagizavyo BWANA WA MABWANA, MFALME WA WAFALME, ambaye vitu vyote ni yeye kaviumba. Usikie, uamue, upone na umrejee YESU. 98% shetani aliteka kwa njia mbali mbali, ikiwemo na mto wa kuzimu unaitwa Timberland River.
SILAHA 9 KUBWA ZA SHETANI.
Majini haya yapo tisa na chakula chao yanakula chuma, haya majini yapokama roboti, kila jini ana nyota zake. Golo 1 ana nyota 10, Golo wa 2 ana nyota 8, Golo wa 3 ana nyota 6, Golo wa 4 ana nyota 4, Golo wa 5 ana nyota 2, Golo wa 6 ana nyota 1, Golo wa 7 ana nyota 50, Golo wa 8 ana nyota 40, Golo wa 9 ana nyota 100.
Hizi ndizo silaha za mwisho za shetani anazotegemea na kwa sasa serikali ya mbinguni ipo kazini inazibomoa nikiwemo na mimi ambaye niliyetumwa kuangamiza ufalme wa shetani.
Msaidizi wa majeshi ya kuzimu baada ya Max, kumtoa katika kazi ya Joka Kuu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi mkuu. Nilipomteka na kutolewa katika serikali ya jeshi hilo la shetani, alibakia msaidizi wake ambaye ni jini linaloitwa Samora, ila Samora lenyewe nimelifunga pingu lipo katika gereza ambalo limejengwa na Malaika ili kuwafunga hawa mashetani na kuwatesa mpaka ile siku ya Jehanamu ifike uchomwe moto pamoja na baba yao Joka Kuu.
NINI MAANA YA CHRISTMAS TREE?
BWANA YESU ASIFIWE, nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI, ambaye kupitia yeye ndio tunapata siku ya Krismasi ambayo watu husherekea kukumbuka kuzaliwa kwake mwana huyu wa MUNGU aliye hai na aliye maarufu kupitia manabii wote waliopita na maarufu kupita viumbe vyote na ndiye MWANA WA PEKEE wa MUNGU.
Leo nitaelezea maana ya mti wa Krismasi, unayo maana gani na pia nitaelezea kuhusu mti unaoitwa (Christmas Tree) hauna uhusiano na siku aliyozaliwa YESU kabisa bali mti huu unao uhusiano na miungu iliyoitwa Tammuz. Kama nilivyoelezea katika makala ya Nabii Hebron uisome kuhusu Father Christmas (neno) huyo ni mzimu wa mtu aliyeitwa Santa Claus ila usome utaelewa vizuri na wewe utaachana na kuweka midoli katika siku ya Christmas, badala ya kuiita hiyo siku ni ya YESU peke yake, mbinu za shetani kuivuruga hii siku ya Christmas na kuwapiga wanadamu upofu wajijue kama wanamsherekea YESU siku hiyo. Shetani aliwateka wakristo wa enzi hizo ambao ni wana dini wakaamua katika siku hiyo maarufu ambayo ni kukumbuka kuzaliwa kwa YESU WA NAZARETI, na kumtukuza MUNGU aliye hai, shetani akawashika wanadamu fahamu zao katika siku hiyo wakaweka mti na mti ukaitwa mti wa Christmas. Na siri ya mti huu, zamani wapagani waliamini miungu wa mimea na ndio waliamini ndiye mungu wao, sasa wakamuingiza huyo mungu wao wakampamba katika tarehe hiyo ya Christmas ili kuiteka hiyo siku asiabudiwe MUNGU wa kweli na kila anayeweka mti huo wa Krismasi hadi leo ajielewe anaupanda ufalme wa Babeli katika moyo wake na anatekwa katika ulimwengu wa roho anakuwa anampamba mungu Tammuzi au mungu mimea pasipokujua.
Asili ya mti uitwe jina la Christmas tree ilianza Europe, France na Germany, katika biblia hakuna neno mti wa Krismasi, na cha ajabu katika ulimwengu wote watu wanapigwa upofu waliookoka, wapagani, watu wa dini hawaijui siri hii na hata wakiijua hawasemi ukweli wazi wazi ili watu wapone roho zao. Amenituma niwaeleze ukweli peupe peupe. Anayetaka apone atapona, anayekaza shingo majibu atayapata. Huu mti unaoitwa Christmas tree nataka muelewe kwanza haina ushirikaa kabisa na siku hiyo ya kuzaliwa BWANA YESU WA NAZARETI, ila lengo la mti huo ni miungu inayoitwa Tammuz (miungu ya mimea ambayo watu waliamini ile rangi ya kijani ina nguvu katika mimea enzi hizo) hivyo pasipo kumjua MUNGU wa kweli wakaona eti aliyemzaa YESU ndie miungu ya mimea, wakati ukifikiria wewe peke yako utaona mti hauwezi kumzaa mtu, hata kumuuumba, bali mti unatawaliwa na wanadamu kama viumbe vingine. Na pia Christmas tree siyo ishara ya kuzaliwa kwa YESU bali ni ishara ya Ashera au mhimili wa miungu ya Tammuz, na shetani alitumia mbinu kubwa mpaka akauteka ulimwengu na hadi leo watu badala ya kumpokea YESU na kufurahia katika mioyo yao wanatekwa na shetani katika ulimwengu wa roho kila aliye na huo mti iwe nyumbani, kanisani, ofisini, hotelini anakuwa amaemuabudu mungu Tammuz, na siku hiyo unakuwa umejiimarisha kwa mungu Tammuz pasipo kujua. Ila wachawi wanajua na viongozi wa freemason, wanajua na watumishi wa uongo wanajua kabisa, wanafurahia mpigwe upofu mfe roho.
Natumaini mpaka hapo at least umepata picha kiasi Fulani ila zaidi endelea kusoma makala ya Nabii Hebron utajifunza mambo mengi sanaaliyonifundisha YESU na niwafundishe ili mpone. Madhara ya kuita mti au kitu chochote kiitwe ni Krismasi hiyo ni dhambi, na ni kumnyang’anya YESU happy birthday yake na kuipa miungukama vile huu mti badala ya kuitwa mti tu ukaongezwa Christmas hapa ni kumkufuru MUNGU. Kama ulikuwa haujui tubu, usiweke miungu tena nyumbani kwako, hata katika kanisa, na kila mahali wanapoweka mti katika kanisa panakuwa ni mahali pa miungu siku hiyo na MUNGU wa kweli hashiriki katika kambi ya miungu. Je upo tayari kuweka miungu ya Tammuz kwa kuweka mti wa Krismasi? Na kumkana MUNGU aliye BABA yake YESU WA NAZARETI? Ambaye siku yake ya kukumbuka kuzaliwa imeingiliwa na kubadilishwa jina lake pasipo watu kujua. Yeye ni mfalme asiyefananishwa na kiumbe chochote wala kwa jina lolote lile, na ndiyo maana katika ulimwengu huu hakuna mtu anayestahili kuitwa YESU. Sasa muulize swali yeye anayejiita ni YESU, je alizaliwa na Maria? Na je alikufa na kufufuka? Na je yeye ndie atakayekuja kutunyakua katika unyakuo? Na je muulize mbona upo hapa ulimwenguni haujapaaga tokea enzi hizo? Na mbona haupo na wale wanafunzi wako hapa uliwenguni, tuonyeshe Petro na wenzake 11, jibu hana. Huyo ni feki ndani yake ni miungu inayojifananisha na YESU ili awadanganye watu kuwa yeye ndie na kumbe ni uongo.
Nataka muelewe injili ya kweli na siyo ya uongo na ukweli unachanganya, yaani nuru na giza, kitu chochote cha MUNGU halifai kufananishwa au kuitwa kwa jina lake, unapofananisha au ukaita ujue tayari umemkufuru MUNGU. Hata leo wakristo wengi wanamkufuru MUNGU pasipo kujua sababu ya mapokeo ya miungu mfano halisi ni tendo la kuweka mti wa Krismasi kanisani, nyumbani pako, wewe badala ya kumpamba YESU katika roho, sifa na kusujudu, unampamba mti halafu unaviita ndiyo siku kuu ya kuzaliwa YESU WA NAZARETI hapo umepotea kinachotokea katika ulimwengu wa roho unapandiwa roho za huo mti katika moyo wako na mambo ya miungu na ule mwisho unabakia kwenda jehanamu sababu utakuwa umevunja moja ya amri kumi, usivisujudie vitu, mheshimu MUNGU aliye muumba wako, usimfananishe na chochote kile, sasa huu mti haujafananishwa na YESU? Je haujavunja amri ya MUNGU? Tubu leo na uitupilie mbali wala usiweke kanisani wala popote kama kweli wewe hautaki kumkufuru MUNGU.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote naomba unisamehe niliabudu miungu ya mimea bila kujua au kwa kujua narudi kwako MUNGU WA KWELI nisamehe nioshe kwa damu ya mwanao YESU WA NAZARETI, najitenga na miungu yote, sishiriki tena kuita mti uitwe jina lla Christmas wala kuinunua, najitenga na mapokeo ya miti hiyo na maroho yote. Nisaidie nikuabudu wewe katika roho siku ya Christmas na siku zote nikusifu wewe peke yako. Amen.
NINI MAANA YA FATHER CHRISTMAS?
Ndugu msomaji, napenda kuwafundisha watu wote wa ulimwengu huu kuhusu neno FATHER CHRISTMAS ni nini na chanzo chake, maana watu wengi hata mimi nyumbani kwangu wakati wa Krismasi nilinunuaga huyo mdoli anayeitwa Father Christmas pasipo kujua maana yake mpaka YESU WA NAZARETI aliponifunulia siri hii.
Akaniambia Hebron nikuulize swali? Nikasema ndiyo BABA, akaniuliza hivi Krismasi ni sikukuu ya nini? Nikamjibu, ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwako, akasema sawa kabisa. Sasa kwa nini badala ya wanadamu kumkaribisha YESU yaani mimi katika nyumba zao na makanisayao, wanampamba huyo anayeitwa Father Christmas. Nikashtuka. Akaniambia, je? Hebron, mimi ndiye huyo mdoli anayevalishwa nguo nyekundu na madevu? Nikajibu, siyo.
{
"@context": "https://schema.org",
"@type": "BlogPosting",
"headline": "SOMA KITABU HIKI: ZIJUE SIRI KUBWA ZA SHETANI, ILI UWEZE KUMSHINDA",
"description": "<div dir="ltr" style="text-align:justify;"><strong>TOLEO LA 16</strong></div>
<div dir="ltr"...",
"image": "https://proshabo.com/content/uploads/photos/2021/11/proshabo_d9a85d737701771c0c777c53394aa277.png",
"author": {
"@type": "Person",
"name": "GOSPEL PREACHER",
"url": "https://proshabo.com/preacher"
},
"publisher": {
"@type": "Organization",
"name": "PROSHABO",
"url": "https://proshabo.com"
},
"datePublished": "2021-11-19 05:59:01",
"dateModified": "2021-11-19 05:59:01",
"mainEntityOfPage": {
"@type": "WebPage",
"@id": "https://proshabo.com/blogs/604/SOMA-KITABU-HIKI-ZIJUE-SIRI-KUBWA-ZA-SHETANI-ILI-UWEZE"
},
"url": "https://proshabo.com/blogs/604/SOMA-KITABU-HIKI-ZIJUE-SIRI-KUBWA-ZA-SHETANI-ILI-UWEZE",
"articleSection": "Injili Ya Yesu Kristo",
"keywords": "",
"wordCount": "65535",
"commentCount": "",
"interactionStatistic": [{
"@type": "InteractionCounter",
"interactionType": "https://schema.org/CommentAction",
"userInteractionCount": ""
},
{
"@type": "InteractionCounter",
"interactionType": "https://schema.org/ViewAction",
"userInteractionCount": ""
}
]
}
Cerca
Categorie
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Leggi tutto
JINSI LAANA YA ROHO MTAKATIFU INAVYOENDELEA MIONGONI MWA WAHUBIRI WA INJILI PASIPO KUJIJUA.
JINSI LAANA YA ROHO MTAKATIFU INAVYOENDELEA MIONGONI MWA WAHUBIRI WA INJILI PASIPO KUJIJUA.
Verse by verse explanation of Joshua 19
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 33 questions at the...
Verse by verse explanation of Exodus 20
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 53 questions at the...
ETI, YESU ALIPOKUWA AMEKUFA DUNIA ILIKUWA INAENDESHWA NA NANI?
Hili ndilo swali la wafuasi wa Muhammad kwa Wakristo na leo nitalijibu hapa.
Hili ni swali...
Verse by verse explanation of 2 Samuel 6
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 34 questions at the...