ATHARI ZA MAHUSIANO YA UCHUMBA YA MUDA MREFU KUPITA KIASI (Miaka 2 au zaidi)

0
6Кб

1. Huweza Kufungua Milango ya uasherati kwa Wachumba
Inaweza kupelekea kwenye maisha ya uasherati kati yenu kwasababu mtakuwa mmetumia muda mwingi kuwa pamoja na kujihalalishia uhalali wa kushiriki tendo la ndoa na kujiona tayari mmeshazoenana na kujihisi ni kama mke na mume tayari.

2. Inaweza kupunguza kasi na kiwango chenu katika mambo ya Mungu.
Kukaa sana katika uchumba kupita kiasi kutaweza kushushaa kiwango chenu cha mambo ya kimungu kwasababu mtapeleka nguvu kubwa ya vipaumbele vyenu na muda wenu kwenye mambo ya mahusiano kuliko kupeleka kwa Mungu.

3. Inanyonya kwa kiwango kikubwa sana nguvu za kihisia kati yenu. (It is emotionally demanding).

  • Muda mwingi unakuwa unamuwaza mchumba wako.
  • Huna uhakika huko aliko kama yupo salama?
  • Hakuna wengine walio msogelea na kutaka kukupindua.
  • Kutaka kujua yupo wapi sasa, anafanya nini, nk.
  • Inachukua mawazo yako kwa sehemu kubwa sana na wakati mwingine hata kazi zako hauzifanyi vuzuri.
  • Sasa inapokuwa ni kwa muda mrefu inaweza kukunyonya sana kiwango cha hisia zako.


4. Inaweza kupelekea mawazo yasiyofaa na ya upinzani kutoka kwa ndugu zenu, jamaa na marafiki.

  • Uchumba unapokaa kwa muda mrefu sana kupita kiasi unawafanya wanandugu kuanzisha maneno maneno ambayo yanaweza kuharibu na kila kitu katika mahusiano hayo.
  • Kuna msemo wa kiswahili unasema kuwa "bata ukimchunguza sana huwezi kumla" kama mmekaa katika uchumba kwa muda mrefu sana, inaweza kuwafanya wanandugu kumfuatilia mchumba wako kwa ukaribu kwa muda mrefu na kuanza kugundua vikasoro vidogo vidogo ambavyo hata kama vilikuwa vinaweza kurekebishika wao wanavishikia bando na kusema huwezi kuoana na yule kwasababu ya hivyo vikasoro kasoro,


5. Inaweza kusababisha uchumba kuvunjika kabla ya kuoana.

  • Kukaa katika mahusiano ya uchumba kwa muda mrefu kunaweza kupelekea hata uchumba wenyewe kuvynjika.
  • Kukaa katika uchumba muda mrefu kunaweza kuwafanya hata ile shauku mliyokuwa nayo ya kuoana iweze kwisha kabisa na kuwafanya mjikute mkivunja na uchumba wenyewe.


6. Italeta majeraha makubwa sana baina yenu hasa baada ya uchumba kuvunjika kutakuwa na majuto na maumivu sana kwasababu Zifuatazo:

  • Kupotezeana muda miongoni mwenu.
  • Kupoteza pesa na vitu mbalimabli mlivyopeana wakati wa uchumba (loss of resources).
  • Maumivu ya kumwaga siri zako hata zile za ndani kabisa ambazo usingependa mtu mwingine azijue, sasa unakuwa huna uhakika kama hatamweleza mtu mwingine huko nje.
  • Aibu kwa ndugu, jamaa na marafiki na jamii kwa ujumla na kujiona kuwa wameshindwa (failure to the public image).
  • Hupelekea historia mbaya (bad records) kwa wachumba watakao fuata na hasa kama uchumba ujao hautafanikiwa pia.


7. Kuendesha Uchumba Wa Muda Mrefu Ni Gharama Kubwa.

  • Safari za mara kwa mara kwaajili ya kuonana na mchumba wako.
  • Mitoko "outing" za mara kwa mara pamoja na mchumba wako.
  • Mawasiliano ya kila dakika na mchumba wako.
  • Kutumiana zawadi za mara kwa mara na mchumba wako.
Поиск
Категории
Больше
SPIRITUAL EDUCATION
UPAKO NA UTISHO WA MUNGU – NGUZO YA KUTETEMESHA MATAIFA NA KUVUNJA MAMBO YA KIZAZI CHA ZINAA
Mstari wa kufungua:“Bwana atawatawala mataifa; Bwana atawaponda watawala wa dunia;...
От GOSPEL PREACHER 2026-05-14 13:33:27 1 99
OTHERS
A’isha: Mke wa Muhammad Mwenye Miaka Tisa
Watu wengi wamesema kuwa Muhammad alifanya tendo la ndoa na mke wake mwenye umri mdogo zaidi,...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 05:41:42 0 10Кб
Injili Ya Yesu Kristo
MOTO WA KIGENI
Walawi 10:1-2 “Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake,...
От GOSPEL PREACHER 2023-06-25 01:00:10 2 9Кб
REVELATION
UFUNUO 20
Bwana wetu YESU KRISTO apewe sifa, karibu katika mwendelezo wa kitabu cha ufunuo, leo tukiwa...
От GOSPEL PREACHER 2021-10-30 12:40:40 0 6Кб
Injili Ya Yesu Kristo
FAHAMU KUHUSU JINA LA FARAO
Kwa ufupi… Bwana Yesu asifiwe… Je unafahamu nini kuhusu jina hili la farao? Basi...
От GOSPEL PREACHER 2022-03-30 05:04:49 0 5Кб