MWANAUME: SIO MKE WAKO NI WEWE

0
6كيلو بايت

Mchungaji wangu Emmanuel Nhyama Manwele ambaye ni mwalimu wangu wa kwanza wa ndoa na maswala yahusuyo ndoa, alinifundisha akasema,

"Mke ni kama kinanda, ukikipiga vizuri kitakupa muziki mzuri, lakini usipokipiga vizuri hakitakuletea muziki mzuri ila mbaya. Mtu ambaye hakufundishwa kupiga kinanda hawezi kupiga kinanda hicho katika mpangilio sahihi wa ala za muziki kikaleta maana ya wimbo, hata kama mtu huyo anajua wimbo huo, kama hujui namna ya kupiga 'cords' au 'keys' kwenye kinanda, atatengeneza kelele masikioni mwake na masikioni mwa watu." alimaliza.

Kwa kuwa mimi ni mwana muziki nilimuelewa sana hii falsafa, na leo nataka niizungumzie kwani imenisaidia sana maishani mwangu katika ndoa yangu.

Mikono iliyofundishwa vema na kuzoeshwa vema kupiga kinanda ndio inayoweza kupiga vizuri kinanda na kukifanya kitoe sauti ya wimbo unaosikika vizuri masikioni mwa mpigaji na mwa wanaomsikiliza. Mikono hii ina uwezo wa kufanya hivyo kwa sababu inafundishwa na kuongozwa na akili inayofahamu vema muziki, lakini pia yenye ufahamu wa kutosha juu ya wimbo unaopigwa. Kama akili haijui, mikono haiwezi kupiga, na mikono ikishindwa kupiga kinanda itapigapiga tu na kuleta kelele.

Mke wako ni kama kinanda, ndani yake Mungu ameweka hazina ya kila mlio mzuri unaogusa moyo wako, inategemea na wewe tu. Kama unajua kupiga na unajua akilini mwako wimbo wa kupiga na namna ya kupiga, basi utapata ukitakacho kitakachoburudisha nafsi yako. Lakini kama katika akili yako hauna ufahamu wowote kuhusu mkeo, na mikono yako hujaifundisha na kuizoeza kumuhudumia mkeo ili alete mlio uutakao, badala ya jambo zuri utasababisha kelele kwa sababu utapiga-piga tu hovyo hovyo bila utaratibu.

UNAMJUA MKEO?
Usipomjua mkeo kila ulitendalo kwake litaleta kelele, kwa sababu hujui namna ya Kumfanya akutolee kile ukipendacho. Mkeo ana kila kitu chema ukitakacho, inategemea tu na wewe na wala sio mke wako. Kama ilivyo kwa kinanda usipokipiga hata kama unajua kukipiga hakiwezi kutoa mlio wowote. Mpaka umekipikipiga ndipo kitatoa mlio.

Mbaya zaidi ni pale ambapo hujui kukipiga na unacho na unatakiwa kukipiga. Mume, usipomjua mkeo, huwezi kumfanya atoe sauti nzuri (to sound good), atatoa makelele au hatatoa kabisa iwapo mikono yako haitamgusa.

Wimbo wowote uupendao, upo ndani ya kinanda, inategemea tu na wewe kama unaujua wimbo na ala zake za muziki na mikono yako inauwezo na uzoefu wa kupiga hicho kinanda. Vivyo hivyo, mkeo ana kila kitu chema unachotaka, ukipendacho, inategemea na akili yako ina ufahamu kiasi gani kumuhusu, lakini pia mikono yako kama ina uwezo na uzoefu wa kufanya unachokijua.

HUDUMA KWA MKEO.
Ukitaka mkeo akupe ukitakacho na ukipendacho muhudumie kwanza, mchukulie vile alivyo. Ukijua nini anahitaji, ukampa kile anachohitaji, utapata kile unachohitaji. Usipompa anachohitaji, hutapata unachohitaji. Ukimpiga-piga tu bila kujua nini unafanya, utasababisha kelele masikio mwako.

Biblia inasema, "Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake" (Mithali 27:18). Ukimtunza mkeo utakula matunda yake, usipomtunza hutakula matunda yake.

Vyovyote vile mkeo alivyo kwako ni matokeo ya wewe ulivyo kwake. Kwa nini? Kwa sababu wakati unamuoa alikuwa vile alivyokuwa na ndio maana ukampenda ukamuoa. Sasa, kama sasa hivi amebadilika na kuwa usivyopenda wewe, sio yeye ni wewe, yeye hana tatizo ila wewe, umeshindwa kum-play vizuri. Kwa hiyo kama kuna wa kubadilika ni wewe na sio yeye.

Muziki unakua, kama muziki unakua na mpigaji anapaswa kukua ili aendane nao, awe na uwezo mkubwa wa kupiga. Lakini kama atabaki pale pale basi muziki utamshinda uwezo. Ili aweze kuumudu muziki ni lazima akue nao, kwa kadiri unavyokuwa ndivyo na yeye akue, ama sivyo atashindwa kuumudu.

Vivyo hivyo kwa mke, yeye pia anakua, na katika kukua kuna mabadiliko yanayochukua nafasi. Kwa hiyo kama mkeo atakua lakini wewe akili zako na ufahamu wako ukabaki pale pale ulikokuwa unamjua wakati unamuoa, mke atakushinda. Utaanza kuona mkeo kuwa ni changamoto kubwa. Na kwa sababu hiyo utashindwa kummudu.

Huwezi kufanya jambo zaidi ya ufahamu wako na akili yako, pale ufahamu wako na akili yako inapoishia ndipo palipo na ukomo wa utendaji wako na ukomo wako wa kumudu jambo. Mkeo akikua na kuongezeka kupita ufahamu na akili yako atakushika tu, na hapa tatizo si yeye, tatizo ni wewe.

Biblia inasema, "Enyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili" sasa mke akikushinda maana yake amekushinda akili. Kama yeye ana shida ambayo ni changamoto kwako, akili na ufahamu wako unatakiwa uwe mkubwa au wa juu kuliko ile shida yake. Shida na changamoto ni sehemu ya mabadiliko yanayotokea wakati wa ukuaji.

Sasa kama wewe unaona mkeo amekwisha kuwa tatizo hicho ni kipimo kuwa mkeo amekua na kuongezeka kupita akili na ufahamu wako, kwa hiyo cha kufanya hapo si yeye kubadilika kwa wewe kumbadilisha, bali ni wewe kubadilika kwa kujinoa zaidi kiakili na kiufahamu ili kukabiliana na tatizo hilo. Tatizo likikushinda maana yake mkeo amekua na kuongezeka kupita akili na ufahamu wako na wewe umeshindwa kukua na kuongezeka kumpita yeye.

Kama mwanzoni alikuwa mtu mzuri, kwa nini sasa awe mtu mbaya? Tatizo si yeye, tatizo ni wewe. Badilika.


NYONGEZA KATIKA KUKAZIA MAARIFA KUKAZIA MAARIFA

Mtoto katika kukua kwake na kuongezeka kwa mwili wake huwa anapitia mabadiliko mengi ambayo ili asiwe katika ugomvi na mwili wake, kichwa chake kinatakiwa nacho kikue na kuongezeka kiakili na kiufahamu ili kukabiliana na changamoto hizo, awe mtoto wa kike au wa kiume.

Kwa mtoto wa kike mabadiliko anayokutana nayo katika ukuaji wake ni kuanza kuona siku zake za hedhi kila mwezi mara tu baada ya kuvunja ungo, kuota nyele kwapani na sehemu zake za siri, kuanza kuwa na tama ya mwili nk.

Kama kichwa chake kitakuwa hakijakua kiakili na kiufahamu, changamoto hizi katika mwili wake zitakuwa ni tatizo kwa sababu atashindwa kuzimudu. Hataweza kunyoa nyele zake za kwapani na sehemu za siri, hawezi kujua majira ya siku zake za hedhi na kwa sababu hiyo hawezi kujitunza, ataona mambo yote haya ni mzigo mzito na nitatizo kwake, na kwa hiyo hatayafurahiya wala kuyapenda.

Mtoto wa kiume naye vivyo hivyo, mwili wake utakutana na mabadiliko ambayo kichwa chake kitatakiwa kikubaliane nayo na kuchukuliana nayo kisha kiyamudu. Mabadiliko hayo ni pamoja na kubalee kunakopelekea yeye kuanza kusikia tama za mwili, nyele kuota makwapani na sehemu zake za siri, kujisikia kuwa amekuwa na anahitaji uhuru katika mambo yote nk. Kama mtoto huyu atakuwa hajakua kiakili na kiufahamu mabadiliko haya yatakuwa ni changamoto ambazo atashindwa kuzimudu na kwa sababu hiyo ataona kama ni tatizo.

Tatizo hapa si mwili, tatizo ni kichwa kimekosa akili na ufahamu. Mume ni kichwa cha mkewe na mke ni mwili wa mumewe, wawili hawa wanapoingia katika ndoa, kwa kadiri siku zinavyosonga ndivyo wanapaswa kukua na kuongezeka kwa pamoja. Lakini iwapo mwili ambao ni mke utakua na kuongezeka na kichwa ambacho ni mume hakitakua na kuongezeka kiakili, basi, kichwa kitashindwa kuumudu mwili pindi utakapokuwa kwenye mabadiliko. Hapa tatizo si mke, tatizo anakuwa mume.

Biblia imesema kuwa, Mume aishi na mkewe kwa akili, kwa nini? Kwa sababu mume ni kichwa na mke ni mwili, kichwa ndicho chenye akili na ufahamu, na ndicho chenye macho, kwa sababu hiyo ndicho kinachotakiwa kiuongoze mwili na kuutunza pasipo kushindwa.

Akili ndizo zinazojua kuwa mwili umechafuka, na ufahamu ndio unaojua kuwa ni nini cha kufanya mwili unapochafuka. Akili ndizo zinazojua kuwa mwili umechoka, au ni dhaifu, au unaumwa, na ufahamu ndio unaojua ni nini cha kufanya ili kuurudisha mwili katika hali yake; na vyote hivi viko kichwani.

Iwapo tutaukuta mwili ni mchafu, tena unanuka, na bado mtu mwenye mwili huo anaushutumu mwili, moja kwa moja tutajua kichwa chake hakina akili za kutosha kumudu changamoto katika mwili wake. Na ndivyo ilivyo katika ndoa, Mume ni kichwa na mke ni mwili, kwa hiyo, mume anapashwa aishi na mkewe kwa akili.

البحث
الأقسام
إقرأ المزيد
OTHERS
MTUME PAULO ANAVYO WANYIMA USINGIZI WAISLAM
Kati ya watu wanaowasumbua sana ndugu zetu Waislamu ni shujaa wa Bwana Yesu, Mtume Paulo. Na hii...
بواسطة MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 05:04:40 0 7كيلو بايت
SPIRITUAL EDUCATION
Empirical Evidence for God
Outline of impeccable Evidences for Theism to non theism.1. Contingency – Why does...
بواسطة MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 02:36:50 0 5كيلو بايت
OLD TESTAMENT
THE BOOK OF EXODUS
Welcome to Proshabo Online Bible Study (POBS). This is the best platform for you to study your...
بواسطة THE HOLY BIBLE 2022-01-28 01:38:46 0 5كيلو بايت
Injili Ya Yesu Kristo
MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU.
BRIAN DEACON ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe...
بواسطة GOSPEL PREACHER 2021-11-19 05:33:52 0 4كيلو بايت
OTHERS
Where is hell? What is the location of hell?
Various theories on the location of hell have been put forward. A traditional view is that hell...
بواسطة MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:19:11 0 5كيلو بايت