MWANAMKE NA MWANAUME NA MAHUSIANO: TOFAUTI YA KIMAUMBILE

0
5K

Sote tunajua kabisa ya kwamba kuna tofauti ya kimaumbile kati ya mwanaume na mwanamke, na tofauti hizi zipo kwa makusudi maalumu, na kikubwa zaidi ni kwamba, tofauti hizi ndizo zinawafanya mwanamke na mwanaume wahusiane, tofauti zao kimaumbile ni kwa ajili ya kufaana na si kwa ajili ya kutofautiana.

Mwanamke na mwanaume wametofautiana kimaumbile (ya nje kwanza) si ili watofautiane bali ili wafaane kimahusiano, kila mmoja amfae mwenzake.

Kabla sijaendelea mbele zaidi, naomba niweke jambo moja sawa hapa ili tuelewane vizuri. Biblia inasema kwa kinywa cha Mtume Paulo kuwa, Mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanaume na si mwanaume kwa ajili ya mwanamke Kwa sababu mwanaume alitangulia kwanza (kimwili) kuumbwa na baadae mwanamke lakini katika roho wote waliumbwa kwa wakati mmoja, hakuna aliyemtangulia mwenzake (Mwanzo 5:1-2).

Sasa hii ina maana gani, Maana yake ni kwamba, mwanamke aliumbwa ili aje kuwa msaidizi wa mwanaume na si chombo cha sitarehe au burudani cha kumfurahisha mwanaume, la sivyo mwanamke na yeye asingeliumbiwa uhitaji wa kimwili kutoka kwa mumewe. Maadamu mwanamke naye ameumbiwa uhitaji wa kimwili ambao utatimizwa na mumewe tu, na vivyo hivyo mwanaume naye ameumbiwa uhitaji wa kimwili ambao utatimizwa na mke wake tu, basi mwanamke sio chombo cha sitarehe cha mwanaume. Kama mwanaume anavyomuhitaji mwanamke kimwili ndivyo mwanamke anavyomuhitaji mwanaume kimwili, kila mmoja aliumbwa tofauti na mwenzake huku akiwekewa uhitaji katika mwili wake ili kutoka na tofauti hizo waweza kufaana na kila mmoja kuutimiza uhitaji wa mwenzake. Kwa hiyo hakuna mburudishaji na mburudishwaji, wote ni waburudishaji na waburudishwaji, kila mmoja kwa mwenzake.

Baada ya kusema hayo, naomba sasa tuangalie tofauti hizo. Tutaanza kwa kuwaangalia wanaume wameumbwaje kimwili katika maumbile ya nje.

MWANAUME NA MAUMBILE YAKE

Mwanaume kimaumbile ameumbwa kuwa mtoaji kwa sababu kusudi la kuumbwa kwake ni kuwa baba (Maana yake chanzo au mtoaji), kwa hiyo hata maumbile yake ya nje yanaaksi kusudi la lake la kuumbwa kwake.

Kwa hiyo hata kimaumbile mwanaume ni mtoaji, na kwa sababu hiyo maumbile yake yameumbwa ili kumwezesha kutoa vitu katika chanzo chake. Na moja ya kitu cha kimwili ambacho mwanaume hutoa ni mbegu (sperm) ili kusababisha uzazi, na kwa sababu hiyo maumbile yake yametengenezwa maalumu kwa ajili ya kutoa.

Ukiwa umebaki uchi kabisa, ulishawahi kujiuliza kwa nini uliumbwa hivyo, na hasa unapojiangalia hapo chini? Kwa nini Mungu alikuwekea uume, na pamoja na uume alikuwekea korodani? Au Unadhani ni mtindo tu wa kiuumbaji? Lakini ili mambo yaende vizuri na kusiwe na mkwamo wowote Mungu akamwekea mwanaume tamaa ya mwili ili awe mwanzilishi wa mambo ya kimwili kwa sababu yeye ni chanzo. Hili la tamaa nitalizungumzia siku nyingine kwa sababu linatumiwa vibaya na shetani naye analitumia sana kuharibu.

Kwa hiyo, maumbile ya mwanaume na hasa ya uzazi ni kwa ajili ya kumwezesha kutoa kile kilichomo ndani yake. Na kwa sababu mwanaume ni mwanzilishi hana mvuto wowote wa kimaumbile, hajaumbwa kimwili ili kuvutia kwa sababu yeye ni mwanzilishi wa kila kitu kimahusiano.

MWANAMKE NA MAUMBILE

Kimwili, mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanaume, kama msaidizi, mwanamke aliumbwa ili awe mpokeaji, apokee kutoka kwa mwanaume na kukipa uhai kile alichokipokea kwa mwanaume, kile kilichotolewa na mwanaume.

Ili aweze kuwa mpokeaji mwanamke alitofautishwa na mwanaume kimaumbile. Maumbile yote ya mwanamke yameumbwa kwa madhumuni mawili kama mpokeaji na mtoa uhai kwa kile alichokipokea kutoka kwa mwanaume:

  1. Kupokea viungo vya mwanaume vinavyotumika kutoa mbegu iliyoko ndani yake ili kwa kupokea viungo hivyo aweze kupokea mbegu na kuipa uhai.
  2. Kuipa uhai mbegu aliyoipokea, na ndio maana ana tumbo la uzazi na ana maziwa kwa ajili ya kunyonyeshea kilichotolewa.

Mwanamke ameumbwa kimaumbile na kuwekewa uke na maziwa, lakini pia alifanywa kimaumbile ili awe na mvuto, ili kumvutia mwanaume. Maumbile ya mwanamke kwa sababu yeye ni mpokeaji na si chanzo au mwanzilishi, yamefanywa kwa usitadi ili kumvutia chanzo.

Sasa, basi hawa wawili wameumbwa tofauti kimaumbile ile wafaane kimahusiano na kutoka katika kufaana watimilize kusudi la kuumbwa kwao na kutofautiana kwao kimaumbile. Lakini ili kazi ya Mungu iwe yenye kufurahiwa, katika uhitaji wao huo Mungu aliweka raha ya kimwili inayosikiwa na kila mmoja iwapo kila mtu na hasa wanaume watajitia bidii katika kutimiza uhitaji wa mwenzake wa kimwili.

Niweke tena msisitizo, tofauti ya kimaumbile ina lengo la kutimiza kusudi na kufurahiana, kila mmoja amfurahie mwenzake, na kila mmoja amfae mwenzake, na hapa hakuna mburudishaji na mburudishwaji, na kwa sababu hiyo mwanamke sio chombo cha starehe kwa mwanaume, mwanaume anamuhitaji mwanamke kama ambavyo mwanamke anavyomuhitaji mwanaume. Na ushahidi wa kwanza ni ushahidi wa kimaumbile katika miili yao na uhitaji wa kimwili kwa kila mmoja wao.

Maumbile ya nje ya mwanamke yameumbwa ili kuhamsha hisia (tamaa) za mwili za mwanaume na hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu. Kwa mwanaume anapaswa kuitawala na kuizuia tamaa yake mpaka wakati sahihi, yaani mpaka awe ndani ya ndoa. Nitakapokuwa nazungumzia tamaa nitazungumzia hili kwa undani zaidi.

Mwanaume ni mtoaji na mwanamke ni mpokeaji, naomba hii hoja (point) ikae moyoni mwako kwa sababu nitaizungumzia sana. Tumeanza na kuangalia kimwili ktk maumbile ya watu hawa wawili waliotofautishwa kwa kusudi la wao kufaana katika kuishi kwao pamoja huku wakipeana heshima.

Wewe kama kijana unapaswa kuyaelewa ili kufanya vizuri katika mahusiano yako. Usipomwelewa mwanamke na usipojielewa wewe kama mwanaume utashindwa kuishi na mwanamke na kumpa heshima kama mwanamke.

Site içinde arama yapın
Kategoriler
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU.
BRIAN DEACON ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-19 05:33:52 0 4K
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 17
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 24 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 14:58:31 0 5K
Networking
How to find the best marketplace growth strategies
After you have seeded your marketplace with a stable initial user base, it's time to start...
By Business Academy 2022-09-17 04:03:44 0 9K
NEHEMIAH
Verse by verse explanation of Nehemiah 6
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 12:22:32 0 6K
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 30
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 48 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-21 06:56:28 0 5K