USIDANGANYIKE, MATUMIZI YA VIDEO ZA NGONO KWA WANANDOA NI DHAMBI

0
6K

Shalom wapendwa,

Leo katika kona yetu hii ya Mahusiano, uchumba na Ndoa napenda tuangalie juu ya matumizi ya video za ngono kwa wanandoa, madhara yake na je, ni dhambi au sio dhambi. Nianze kwa kusema kuwa, matumizi ya video hizi za ngono kwa wanadoa ni dhambi mbele za Mungu, huu ni ukweli usiopingika. Unaweza usinielewe, lakini utanielewa hapo baadaye nitakapokuwa nakufafanulia kwa nini ni dhambi kwa nuru ya maandiko matakatifu ya Biblia.

Kwanza kabisa nianze kwa kueleza kwa nini nimeamua kuandika makala hii au fundisho hili. Siku za hivi karibuni watu fulani waliniunga kwenye group la whatsapp la ndoa la watu waliookoka. Waliniomba niwe mmoja kati ya walimu wengi na wachungaji wengi katika group hilo nitakayekuwa nafundisha maswala mbalimbai ya ndoa. Kweli nilikubali, lakini cha kushangaza, baadhi ya wana-group na wengine wao wakiwa ni wachungaji wakaanza kurusha picha na video zinazoonyesha watu wakifanya ngono. Nilishindwa kuvumilia, nikaamua kuuliza. Majibu niliyopewa ni kwamba, hiyo ni moja ya njia ya kujifunza tendo la ndoa ili kuboresha ndoa zetu na kwamba haina shida yoyote. Kweli nilipatwa na mshituko kwa sababu watu wa group hili wameokoka na wanaabudu katika madhehebu mbalimbali ya wokovu. Kuna wachungaji walisimama na kutetea swala hili kuwa si dhambi kabisa kwa wanandoa lakini kwa wale ambao hawajaoa na kuolewa kwao ndio dhambi. Nilipigwa na butwaa. Sitaki nikuambie ni nini kiliendelea.

Mbali na kwenye group hilo, siku moja nilikwenda kwa mmoja wa wazee wa kanisa wa kanisa fulani linaloamini wokovu. Sikumkuta yule mzee, nikaomba niwekewe mkanda wowote nikute naangalia, ndipo wenyeji niliowakuta wakaniambia kuwa naweza kwenda kuweka mwenyewe. Kufupisha hadithi hii, nilikwenda, nikiwa natafuta mkanda wa video wa kuweka macho yangu yaliangukia kwenye mkanda mmoja, nilipouweka nikakuta ni mkanda wa ngono. Lakini pia nimekutana na maswali mengi kuhusiana na swala hili kama ni sawa au sio sawa, na wote wanaouliza ni watu waliookoka, na wengine wao hasa vijana wanaitumia sana tu. Wengine wanaangalie na kuipakua kutoka mitandaoni. Hii ndio sababu nimepata msukumo wa kuandika somo hili ili kuwanasua wengi katika dhambi hii ya tamaa chafu, uwasherati na uzinzi.

KWA NINI KUANGALIA VIDEO AU PICHA ZA NGONO NI DHAMBI HATA KAMA UKIWA UMEOA?

Kinachofanyika katika video hizo ni uzinzi na uasherati
; Watu wanaocheza picha au video hizo ni watu ambao hawajaokoka, pili hawajaoa wala kuolewa, na kwa sababu hiyo kile kinachofanyika ni uzinzi na uasherati. Hakuna dhambi inayotoka kwa Mungu, kwa hiyo moja kwa moja bila shaka yoyote msukumo wa wanaofanya hivyo ni msukumo wa kishetani, na shetani ndiye anayesimamia jambo hili. Na kwa ujanja wake anaamua kulitakasa ili lionekane kuwa sio dhambi kwa hao wanaoangalia ili mradi tu wawe wameokoka. Lakini katika video hizo uchafu mwingi unatendeka kama vile kuingiliana kinyume cha maumbile. Hata hivyo, unaweza kuniuliza kuwa, kwa hiyo mimi ninayeangalia tu na kisha kufanya na mke wangu au mume wangu ninatenda dhambi gani wakati mimi sijafanya.

1Korintho 6:9
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyikewaasherati hawataurith ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti.

Ni vyema ukaelewa kuwa tendo hili linaamsha tamaa za mwili, kwa kadiri unavyoangalia ndivyo unavyotamani, na kwa sababu hiyo unanajisika. Dhambi haiji tu kwa kutenda bali pia kwa kutamani vitu visivyofaa. Napenda kukwambia kuwa ni dhambi kutazama watu wengine hata kama wameokoka wanapokuwa wakishiriki tendo la ndoa.

Hakuna utakatifu wala heshima yoyote katika kuangalia picha au video hizo; Ni vyema ikaeleweka kuwa, Biblia imeagiza kuwa kila mmoja ajue jinsi ya kuuweza mwili wake katika hali ya utakatifu na heshima na si katika tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu (1Wathesalonike 4:4 - 5). Kila unapoangalia video hizi za ngono kitu cha kwanza kinachoibuka hapo ni tamaa mbaya, kwa sababu hao unaowaangalia hawafanyi tendo hilo katika hali ya utakatifu na heshima bali katika tamaa mbaya. Na tamaa hiyo ikiwa na msukumo wa kimapepo nyuma yake. Kwa sababu video hizi zinanajisi moyo wako, basi zinaondoa utakatifu wako.

Waebrania 13:4
Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.

Kwa hiyo, jambo lolote ambalo linanajisi na kuchafua hali ya mtu ya utakatifu haliwezi kuwa njia bora ya wana wa Mungu ya kujifunza jambo jema alilolianzisha Mungu. Hatuwezi kutenda yale aliyotupa Mungu katika usafi kwa kutumia njia chafu zinazochafua usafi wa yale aliyotupa Mungu. Kutumia picha au video za ngono kujifunza au kuamsha hisia zetu ni kuchukua uchafu na kuutia katika usafi, safi haitabaki kuwa safi itakuwa chafu tu. Huwezi kuniambia kuwa wewe mtu wa Mungu unajifunza kutoka kwa waasherati na wazinzi kupitia uasherati wao na uzinzi wao halafu ukabaki katika hali ya utakatifu wako, hicho ni kitu kisichowezekana kabisa, na hakipo katika ufalme wa Mungu.

Hagai 2:12 -13
Mtu akichukua nyama takatifu katika upindo wa nguo yake, naye akagusa kwa upindo wake mkate, au ugali, au divai, au mafuta, au chakula chochote, je kitu hicho kitakuwa kitakatifu? Makuhani wakajibu, wakasema, La.
Ndipo Hagai akasema, Kama mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti, akigusa kimojawapo cha hivi, je! Kitakuwa najisi? Makuhani wakajibu wakasema, Kitakuwa najisi.


Katika kifungu cha maandiko hapo juu, mstari wa 12 unaonyesha kuwa mtu hawezi kufanya kitu najisi kuwa kitakatifu eti kwa sababu amebeba kitakatifu. Hivyo ndivyo ilivyo kwa maisha ya kawaida tunayoishi kila siku. Eti kwa sababu ndani yako umembeba mtakatifu kila kilicho kinajisi utakifanya kitakatifu kwa kukigusa. Kinajisi kitabaki kuwa kinajisi tu hata kama wewe mtakatifu utajaribu kukifanyakuwa kitakatifu kwa utakatifu wako. Huwezi ukaufanya uzinzi na uasherati liwe jambo takatifu la kujifunza kutekeleza tendo la ndoa ambalo kwa asili yake lilifanywa kuwa safi na takatifu, la sivyo unalinajisi na tendo la ndoa lenyewe. Sasa kitakachokuwa kinatokea katika kitanda chako na mkeo au mmeo ni uasherati na si tendo la ndoa takatifu kwa sababu umekwisha najisika wewe na mwenzako.

Lakini katika mstari wa 13 inaonyesha kuwa kilicho kinajisi kikigusa kitakatifu, kitakatifu kinakuwa najisi. Kwa sababu hiyo, picha hizi za ngono kwa watu waliookoka ni vitu najisi, tunapojihusisha navyo tunanajisika na kuwa najisi. Sio kwamba kwa sababu sisi ni watakatifu tutavifanya viwe vitakatifu, maadamu tunavigusa katika maisha yetu kweli vinatunajisi kabisi.

Kwa hiyo ni muhimu tukaelewa kuwa, sio kwa sababu wewe ni mtakatifu utafanya vitu visivyo vitakatifu viwe vitakatifu kwa matumizi yako, bali vilivyo vinajisi vitakunajisi na wewe. Na hivi ndivyo ilivyo kwa picha au video za ngono kwa sisi watakatifu wa Mungu. Picha na video hizi hazijatengenezwa katika hali ya utakatifu, wahusika ni wazinzi na waasherati, lakini pia njia hii si njia iliyokusudiwa anadamu tujifunze tendo hili, na kwa kuwa jambo hili (la hizi video na picha) halijatoka kwa Mungu bali kwa shetani, lina mkakati wa kuharibu utakatifu na usafi wetu kwa Mungu.

Hata hivyo mbali na hayo yote, picha hizi na video hizi zina madhara katika maisha yetu ya kiroho na ya kimwili;

  1. Husababisha upungufu wa nguvu za kiume kwa mwanaume na kupoteza hamu ya kushiri tendo la ndoa kwa mwanamke. Hatari ya mwanamke kupoteza mvuto wake wa kukutana na mwanaume na badala yake kujiridhisha mwenyewe ni mkubwa sana. Pia anaweza kuanza kuwa na njozi za mapenzi ambazo nazo zitachangia kupoteza hamu ya kukutana na mumewe.
  2. Hupelekea pepo la uasherati na uzinzi kuanza kufanyakazi na wahusika wanaojihusisha na picha na video hizo.
  3. Hupelekea wahusika waanze kutamani kufanya kupita mipaka ya tendo la ndoa kwa kuanza kukutana kinyume cha maumbile.
  4. Ni mwanya ambao shetani anautumia kupanda mapando yake katika maisha ya wahusika na watoto wao kwa sababu wanakuwa wamemfungulia nafasi katika eneo hilo.

Mungu akubariki sana.

Zoeken
Categorieën
Read More
OTHERS
SHETANI NA MAJINI MACHAFU YASILIMU NA KUWA WAISLAM
1. Mtume Muhammad akutana na Majini usiku na kuyafundisha Quran.2. Shetani na yeye aingia...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 05:58:59 0 5K
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 11
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-22 11:28:51 0 5K
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Joshua 10
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 49 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 07:40:06 0 5K
JOB
Verse by verse explanation of Job 2
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 24 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 13:28:46 0 5K
2 SAMUEL
Verse by verse explanation of 2 Samuel 13
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 09:44:30 0 5K