WASABATO MTAACHA LINI KUPOTOSHA ULIMWENGU

0
71
 
Shalom wapendwa: Nashukuru kwa WAKRISTO wote wanaoendelea kushirikiana na mimi kutoa elimu SAHIHI ya KIMUNGU na pia niwashukuru WASABATO wastarabu ambao wamekuwa WAKIJIBU kwa hoja za MAANDIKO SI kwa matusi.
 
Hata hivo katika kuendeleea kuhojiana na WASABATO nimegundua mambo mengi sana ikiwemo:
  1. Wasabato wanalazimisha Biblia au Mungu aseme wanavotaka wao , yaani unakuta andiko linasema hvi wao wanaligeuza liseme tafsiri kama Yao..UPOTOSHAJI
  2. Wengi wamekalilishwa vimaandiko vichache hivo hawana Cha kujibu...wanaishia kutukana.
HEBU TWENDE KWENYE MADA
  • HOJA ya kwanza:WASABATO wamekuwa wakiipamba sana sabato kwamba ni mhuri wa Mungu ,inatukumbusha uumbaji na ni siku ya Bwana:
  • WAKRISTO:Kama ni ya MHIMU hivo kwanini Yesu au mitume hawakuisisitiza kushika ? Katika nyaraka za Paulo , Petro au YAKOBO hakuna Mahali wamesisitizwa watu wa mataifa kushika kama wanavofanya WASABATO WA marekani?
  • WASABATO;Hata Yesu kiongozi wetu alishika: Luka 4:16, hivo yatupasa kumfuata
  • WAKRISTO:Yesu alizaliwa kwenye: torati hivo ilimpasa kushika yote Galatia 4:4-5
  • WASABATO:ukisoma mathayo 5:17 Yesu hakuja kutangua torati mpaka yote yatimie
  • WAKRISTO;kama Yesu hakuja kutangua torati mbona nyie hamtahili watoto wenu kwa muda kama alivofanyiwa Yesu ?
  • WASABATO:Sasa hivi tunatohara ya rohoni
  • WAKRISTO:Kama ni hivo hata sisi hatushiki sabato ya siku tunasabato ya rohoni
  • WASABATO:Sabato imekuwepo tangu enzi za Adamu na Eva,yenyenyewe haibadiliki.
  • WAKRISTO:nipe andiko la agizo kwa Adamu kushika sabato au kupumzika SIKU ya sabato
  • WASABATO:mwanzo 2:1-3, kut 20:8-11
  • WAKRISTO ;hapo mbona hakuna sehemu Mungu kaagiza kushika sabato kwa Adamu Bali linaeleza alichokifanya Mungu
  • WASABATO:amesema aliitakass maana yake aliitenga kwa ibada
  • WAKRISTO :kwahiyo katakasa ndo kuamuru kushika sabato kwa Adamu , mbona sasa hamna andiko linaloonyesha Adam KUFANYA ibada siku hiyo?
  • WASABATO:sio Kila kilichofanyika kimeandikwa
  • WAKRISTO:Haya tuseme ni kweli sabato ni MHIMU na sisi wakristo tumekosea nyinyi mko SAHIHI, mbona sasa hatuoni madhihirisho aliyosema Yesu kwenu?? Kama kutoa mapepo , kunena kwa lugha Marko 16:16-18
  • WASABATO:Hata WALOKOLE wanafanya hivo SI kwamba ni Mungu maana Yesu alitabiri manabii wa uongo watakuja na KUFANYA miujiza
  • `WAKRISTO:Kwani wanachofanya WALOKOLE na mnachofanya nyinyi nani anafanya kama walivofanya mitume na kanisa la kwanza? Yaani kuhusu madhihirisho ya Roho mtakatifu
  • WASABATO:mhmhmhm
  • WAKRISTO :Mbona nyie mkazo wenu ni kushika sabato tofauti na fundisho la mitume? Hata kwenye mikutano yenu mnatangaza mambo ya Sabato na vyakula ..Kuna mkutano wowote wa Yesu au mitume wakihubiri hiki mnachofundisha?
  • WASABATO;Watu wamesahau amri za amungu lazima tuwakumbushe..
  • WAKRISTO:mbona mitume hawakuwakumbusha watu wa mataifa ambao hata hawakuijua maana ya sabato ?
  • WASABATO;mitume WALISALI SIKU ya sabato..matendo 15,17,13.
  • WAKRISTO:Lakini Paulo alienda humu kukutana na wayahudi waliokuwa WALISALI sabato , Ili awahubirie kuhusu Yesu ..na wokovu sasa naongelea Paulo alipoenda kwa watu wa mataifa mbona hakuhubiri Suala la Sabato na vyakula kama mnavofanya nyie Bali alihubiri wokovu kama wafanyavo WALOKOLE.
  • WASABATO;mhmhmh
MWISHO
Wapendwa naendelea kusisitiza siko hapa kama content creater au kupoteza muda niko hapa kufundisha kweli. Naomba utafakari viZuri bila panic Anza kuchunguza mambo na mruhusu Roho mtakatifu akufundishe utakuja kubaini kwamba ninachozungunza ndo ukweli matupu.
 
WASABATO tangu enzi za Miller wamekuwa wadanganyifu na wanatumia MAANDIKO ya kukutisha Ili uingie kwenye mfumo.
 
Enzi za Miller waliwatisha watu Yesu anakuja Yesu anakuja watu wakajaa kwenye mfumo mwisho wa siku 1884 hakuna kilichotokea wakaambulia manyoya TU wafuasi wake.
 
Elen G white amekuja na Suala la Sabato na vitisho vingi kwamba wasiosali jumamosi wataenda jehanamu , watu wengi wanaoendelea kujaa kwenye mfumo siku moja watakuja kulia kama wale wa enzi za Miller.
 
Kupitia andiko hili nazani utaendelea kubaini kitu.
 
UONGO USIPOKEMEWA HUWA UNAGEUKA NA KUONEKANA KAMA UKWELI.
Căutare
Categorii
Citeste mai mult
2 KINGS
Verse by verse explanation of 1 Kings 13
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 16:04:51 0 5K
MASWALI & MAJIBU
Naomba Kujua Watakaoenda Mbinguni Je! Ni Wengi Au Wachache?
JIBU: watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?..Ni swali ambalo halikuulizwa tu na...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-13 09:01:02 0 7K
Injili Ya Yesu Kristo
Jesus Saves
Jesus saves from what and from who? Jesus is the most important figure in all of human...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 05:36:34 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
JIHADHARI USIMKATAE MUNGU KATIKA FAHAMU ZAKO
Shalom, leo nipe muda nikuonyeshe jambo muhimu sana katika safari yetu ya wokovu hapa dunia...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 13:02:56 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
UTHIBITISHO WA UTATU WA MUNGU
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:36:40 0 6K