JINSI YA KUMJUA MWENZI WAKO ALIYEKUSUDIWA NA MUNGU

0
6K

Leo napenda tuangalie mambo yatakayokufanya umjue mwenzi wako wa ndoa uliyekusudiwa na Mungu. Wanaume wapo wengi na si kila mwanaume anafaa kuwa mume wako. Wanawake wapo wengi lkn si kila mwanamke anafaa kuwa mke wako. Anayefaa kuwa mume wa mwingine hafai kuwa mume wako, anayefaa kuwa mke wa mwingine hafai kuwa mke wako. Kumbuka, wewe mwanamke hufanani na kila mwanaume, na wala wewe mwanamume hufanani na kila Mwanamke, Mungu anakupa wa kufanana na wewe, tofauti na hapo mwingine unayemtaka anatoka kwa wanadamu au shetani. Na huyo atakutesa kwa sababu hamfanani. Ndege warukao pamoja ni wale wanaofanana. Na kufanana huku ni kule kupatana ktk utu watu wa ndani, ni kufanana kunakupelekea kufaana. Kama hamfanani hamtapatana, na kama hampatani hamtafaana. Ukioa au kuolewa na usiyefanana naye umekwisha.

Sasa tuangalie namna gani unaweza mpata wa kufanana nawe, yaani aliyekusudiwa na Mungu:

1. Mtegemee na umtangulize Mungu kwa kila hatua ktk jambo hili.

Mungu hamtupi kamwe mtu anayemtegemea yeye. Kwa kuwa unamtegemea Mungu, basi, utaomba kwa ajili ya kutaka mwongozo wa Mungu ktk jambo hili. Mungu atakachofanya ni kuuelekeza moyo wako umuelekee mtu aliyekusudia awe mwenzi wako wa ndoa maisha yako yote. Mungu husema nasi kupitia mioyo yetu. Huweka nia na mawazo, au hali ya upendo mioyoni mwetu ktk yale makusudi yake tuliyomuomba. Kwa hiyo ukimtegenea ukamwomba atafanya hivyo.

2. Usiwe na haraka ya maisha {ya ndoa}, kuwa mtulivu na ukubali kusubiri.
Mtu mwenye haraka ya maisha hutapatapa kwa kutaka mafanikio ya haraka, hawezi kusubiri na kwa sababu hiyo ataangukia ktk mtego wa shetani. Maombi yatafanya kazi iwapo hutakuwa na haraka. Mara nyingi wa kwanza kukujibu maombi yako huwa ni shetani ili aharibu mpango na kusudi la Mungu ktk maisha yako. Kama utakuwa na haraka ya ndoa shetani atakupa mume au mke ili aharibu maisha yako. Kwa hiyo ni vyema kuwa muangalifu sana. Kubali kusubiri hata kama unaona umechelewa. Uhakika wa safari sio kuwahi kufika bali ni usalama wa safari. Haraka inaweza kusababisha ajali njiani hatimaye ukafa na usifike mwisho wa safari yako.

3. Tumia Akili yako Vizuri.
Mungu amekataza kuzitegemea akili zetu lkn ameamuru kuzitumia akili zetu kwa jinsi ipasavyo. Kwa hiyo tumia akili yako kufanya hukumu {judgement} ili kupambanua mwema na mbaya. Hata kama unaasilimia 100 kuwa huyo anayetaka au unayemtaka kuwa mwenzi wako anatoka kwa Mungu bado tumia akili yako kabla, wakati, na baada ya kufanya maamuzi.

Chunguza familia yao na ukoo anaotoka, hapa huitaji maombi, unahitaji akili. Chunguza tabia yake, tafuta kujua mahusiano yake na jamii inayomzunguka. Tabia ni muhimu kuliko vitu alivyonavyo, hautaishi naye kwa sababu ya mali, elimu au uzuri alionao, utaishi naye kwa sababu ya tabia njema aliyonayo. Usiwe mvivu wa kufikiri, usiwe mvivu wa kutumia akili yako kupambanua mambo.

4. Upendo wake kwako.

Si kila anayekuja kukuchumbia anakupenda, na wala si kila anayekukubali umuoe anakupenda. Kwa hiyo ni vyema kuhakikisha upendo wake kwake.

Upendo si vitu anavyokupa upendo ni namna yeye anavyojitoa kwako si kwa manufaa na faida yake, bali kwa faida yako. Upendo ni nia yake juu yako, haujajengwa ktk vitu au mali alizonazo mtu, umejengwa ktk utu wa mtu ktk hali yoyote. Muda tu ndio kipimo cha upendo. Pia anayetaka tendo la ndoa kabla ya ndoa hakupendi. Anayekupenda atakulinda.

5. Utayari wake kwako.

Ukiona mtu amekuchumbia halafu hayuko tayari kukuoa huyo si wako, anatafuta kukuharibia. Ukiona umemchumbia mtu halafu hayuko tayari kuolewa na wewe, hakupendi ila kuna kitu anatafuta. Lkn ukichumbiwa au kuchumbia mtu asiyekuwa tayari kuweka bayana mahusiano yenu kwa wazazi wa pande mbili au kwa viongozi wenu wa dini, au walezi wenu jua kabisa umeliwa. Haiwezekani muwe kwenye mahusiano miaka miwili, hata mmoja hakuna anayefahamu tena hata bila sababu za msingi. Ukiona unapozungumzia swala la ndoa na mwenzi wako hajali, anapotezea au kukasirika jua umeliwa.

Site içinde arama yapın
Kategoriler
Read More
NDOA KIBIBLIA
JIFUNZE KUFIKIRI KABLA HUJACHUKUA UAMUZI WA KUOA AU KUOLEWA
Nawasalimu kwa jina la Yesu . Leo katika nyanja hii ya vijana, nimeona ni vema tukashirikishana...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 07:13:49 0 6K
OTHERS
Marriage in Islam and Christianity
Islam: A Muslim man can marry more than one wife. Some suggest that he can have 4 wives at one...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 19:51:12 0 5K
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 44
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 24 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-21 09:58:36 0 6K
REVELATION
UFUNUO 17
Karibu tujifunze kitabu cha Ufunuo leo tukiwa katika mwendelezo wetu wa sura ya 17, Biblia...
By GOSPEL PREACHER 2021-10-30 12:05:54 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
KWA NINI TUMEOKOKA?
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu wote. Karibuni tujifunze Neno la MUNGU la uzima wetu sasa na...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-06 09:38:24 0 5K