SABABU 10 KWANINI USIZINI.
Postado 2026-01-15 11:29:42
0
133
1. Uzinzi ni dhambi pekee inayotajwa kama "UBAYA MKUBWA".
Haimaanishi kwamba dhambi nyingine zote ni nzuri. Zote ni dhambi na hazina mbingu. Lakini madhara ya dhambi ya uzinzi huwezi kuyafananisha na madhara ya dhambi nyingine. Madhara ya uzinzi ni zaidi ya madhara ya dhambi nyingine. Katika Biblia nzima kuna dhambi moja inayotajwa kama "Ubaya mkubwa" nayo ni dhambi ya uzinzi. Kuzini ni kumtenda Mungu ubaya mkubwa. Mwanzo 39:9 [9]Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?.
2. Uzinzi una laana mbaya.
Baada ya kuzini utapata magonjwa yasiyoeleweka na yasiyoisha. Magonjwa hayo hayatakuwa matokeo ya uzinzi mfano ugonjwa wa kaswende, ugonjwa wa kisonono n.k. Bali utapata magonjwa ya ajabu kama laana. Uzinzi una laana. Alalaye na mtu asiye mume wake au mke wake, yaani analala na yeyote bila ndoa,mtu huyo ni mzinzi, Amelaaniwa, Anatembea na laana. Kumbukumbu la Torati 27:20,22-23 [20] Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina. [22] Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina.
3. Hautaurithi uzima wa milele.
1 Wakorintho 6:9 [9] Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti. Uzinzi ni kitu kinyonge sana kisicho na upenyo wa kuingia mbinguni. Na si tu kitu kinyonge bali pia kuzini ni kufanya uovu. Hakuna wafanya uovu wanaoandikwa majina yao kwenye kitabu cha mwanakondoo cha uzima wa milele. Ufunuo wa Yohana 21:27 [27] Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo. Wazinzi wote hukumu yao ya mwisho ni katika ziwa liwakalo moto milele na milele.
4. Uzinzi hupunguza siku za kuishi.
Warumi 6:23 [23] Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. Dhambi na mauti ni marafiki walioshibana na wanafuatana popote. Dhambi na mauti ni marafiki ambao hawajawahi kutengana. Mbinu yao ya ushindi ni kwamba dhambi atangulie mbele kisha mauti afuatie nyuma. Popote unapomuona dhambi ujue rafiki yake mauti yupo nyuma yake/ hayupo mbali naye. Unapozini unajipunguzia siku za kuishi.Hii ni kwa sababu uzinzi mmoja umebeba zaidi ya miaka mitano ya kuishi. Unapozini mara moja tayari miaka yako mitano ya kuishi imefutwa. Ukizini mara ya pili miaka mingine zaidi ya mitano inafutwa. Kwa kadri unavyozini ndivyo miaka yako ya kuishi inavyopungua. Na siku moja usiyoidhania utakapokwenda kuzini ndio itakuwa siku ya kifo chako maana miaka yako ya kuishi yote ulishaimaliza kwenye uzinzi. Mabinti wanaozini
5. Uzinzi ni upandaji. Kila kupanda kuna kuvuna.
Wagalatia 6:7-8 [7] Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. [8] Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Utavuna ulichopanda na sio ulipopanda.Katika mwili wako ukipanda matendo ya dhambi, utavuna uharibifu. Kila pando la uzinzi lina mavuno yake. Baadhi ya mavuno hayo ni pamoja na;Laana, Magonjwa ya ngono, Mimba isiyotarajiwa, Kuharibu hatima, Fedheha na aibu,Kukataliwa,Mzazi bila mipango, Kuzorota uchumi.
6. Uzinzi ni kifungo cha nafsi.
1 Wakorintho 6: 16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Uzinzi sio tu kupata raha. Ni kifungo cha nafsi. Wakati unazini na mtu asiye mume/mke wako hapo mnafanya dhambi. Na atendaye dhambi ni wa ibilisi. Hivyo kile kitendo cha ninyi kuzini, kule kuzimu kunaandika kuwa ninyi ni wa ibilisi na mmefanya agano (Bila ninyi kujua). Na lile agano linatiwa muhuri. Tangu hapo mnaanza kujulikana katika ulimwengu wa giza kuwa mmeungana.Sasa piga picha unazini na watu kumi. Kila unapozini maana yake unafanya agano kwenye ulimwengu wa roho bila wewe kujua. Nafsi yako na huyo mzinzi mwenzako zinasomeka zimeungana(mwili mmoja). Kupitia kuingiliana kimwili kuna agano mnalifanya kuzimu na mnalisaini bila ninyi kujua. Na lile agano linaanza kuishi tangu siku hiyo. Na kwa sababu ya hayo maagano, hutokaa uje kuoa au kuolewa wewe. Na ikitokea umeolewa/Umeoa basi utaolewa kimakosa sana. utaolewa na mtu asiye sahihi, na utaona huko ndani kusivyokalika, kiufupi hiyo ndoa itakuwa jehanamu ndogo iliyopo duniani. Kwanini hautaweza kuoa/olewa? Kwa sababu nafsi yako na ya huyo unayezini naye zinasomeka zimeungana (united) na zimetiwa saini kwahio huwezi kuingia agano la ndoa wakati kuzimu kuna agano linaishi dhidi yako. Na hata ukishaachana na huyo uliyezini naye na ukamblock, jua kule kuzimu lile agano linaendelea kuishi na mnaendelea kusomeka united. Agano halifutwi kwa kublockiana bali linafutwa kwa kulivunjwa kwa maombi.
7. Uzinzi hulitia unajisi hekalu la Mungu
1 Wakorintho 3:16-17 [16] Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? [17] Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi. Mwili wako ni makazi ya Roho Mtakatifu. Mwili wako unapaswa kuwa nyumba ya sala. Kitendo cha kuacha kusali (kumtii Mungu) na badala yake unafanya uzinzi mwilini mwako maana yake umepachika wanyang'anyi. Uzinzi ni unyang'anyi. Marko 11:17 [17] Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi. Mwenye hekalu atakapokuja atakuharibu Ili kukufundisha kwamba mwili wako ni kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya Sofia,Fetty,Kevoo na Hance. 1 Wakorintho 6:13 [13] Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana,
8. Huharibu mfumo wa kitajiri ulio katika nafsi.
Kila mwanadamu amebarikiwa, amewekewa mfumo wa kitajiri na ukuu ndani ya nafsi yake alipokuja kuishi duniani. Amebarikiwa kwa baraka zote za rohoni na mwilini. Waefeso 1:3 [3] Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo. Unapozini unaiuza nafsi yako kwa shetani. Anakuondolea uhalali wa kumiliki na kutawala kwenye uchumi wako. Na ndio maana unakuta ukishika hela inayeyuka mkononi hujui imeenda wapi, hujaifanyia mambo ya maana yenyewe imeisha. Au ukipokea mshahara wako tu yanaanza kujitokeza mambo yanayohitaji fedha na fedha zako zote zinaishia humo huku unakuwa hujafanya kitu cha maana. Kama unazini sahau kuwa na utajiri wa kudumu.
9. Unachafua vazi lako jeupe lililopo mbinguni.
Yesu hakutangulia mbinguni kutuandalia makao tu, bali kutuandalia pia mavazi meupe tutakayoyavaa kama raia wa mbinguni.Kila anayeokoka anaandaliwa vazi mbinguni. Anapotenda dhambi maana yake amechafua vazi lake mbinguni. Akitubu vazi hilo linasafishwa si kwa sabuni ya kleesoft bali kwa damu ya mwanakondoo. Kadri unavyogelea kwenye uzinzi unalifanya vazi lako mbinguni liwe na doa sugu ambapo mwisho wa siku litakosa neema ya utakaso. Na ukiwa na vazi lenye doa mbinguni huingii. Wengi hawalijui hili. Wanazini wanazini kumbe mbinguni wanayatia madoa mavazi yao. Mara paaap leo tunapewa mavazi yetu yaliyoandaliwa mbinguni tunapanga mstari kukaguliwa wenye mavazi safi wananyakuliwa juu, wenye mavazi yenye doa wanaachwa chini. Sijui utatoboa?.
10. Uzinzi unaua hatima kuu ya mtu.
Uzinzi ni mtego wa kuua huduma kubwa za watu,vipawa vikuu vya watu,hatima za ukuu za watu pamoja na karama nyingine. Shetani anafahamu kwa hiyo hatima yako kubwa itampa madhara mengi kwenye ufalme wake wa giza. Kwahio ili akuzuie usifike kwenye hatima yako anahakikisha unatumbukia kwenye uzinzi. Uzinzi ni zimamoto ya hatima ya mtu. "A cat caught eagle" Pastor Chris Oyakhilome Mtu mwenye hatima kubwa ni sawa na tai. Inafikirisha sana kuona tai arukaye juu sana na kwa kasi amekamatwa na paka?, je paka alipaa juu mawinguni akamkamata tai?. Ni dhahiri kwamba tai ndiye aliyeshuka ardhini hadi akakamatwa na paka. Hapa ndipo tunaona kwamba uzinzi huwa haumfati mtu bali mtu ndiye anaufata uzinzi. Na akiisha kuufata anakamatwa hapohapo. Ni aibu wewe tai kukamatwa na paka. Paka akikukamata hakuachi salama anaweza kukusababishia madhara yatakayokufanya uishie kuishi ardhini hadi unakufa. Yaani ule uwezo wako wa kupaa juu unakuwa haupo tena.
#USIZINI_TENA
UBARIKIWE.
Pesquisar
Categorias
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Leia Mais
Je! Mtu Aliyeokoka Anaruhusiwa Kumiliki Lodge Ambayo Ina Bar Ndani Yake?
Swali linaendelea….na kutoa fungu la kumi kwa kupitia hiyo?,kwa mfano mimi nina rafiki...
UTAWALA WA MIAKA 1000
Shalom mtu wa Mungu, karibu tujifunze maandiko matakatifu, kama Biblia inavyosema...
JIFUNZE KUENENDA KWA ROHO ILI USIMHUZUNISHE ROHO MTAKATIFU
Shalom, hakuna namna mwamini anaweza kuishi maisha ya kumpendeza Mungu hapa duniani bila kuenenda...
Verse by verse explanation of Genesis 37
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 58 questions at the...