MAANA HALISI YA IBADA YA KWELI

0
1KB

MAANA HALISI YA IBADA KWA UJUMLA. EBR 10:25

Ibada ni tendo la heshima ya hali ya juu linalotolewa kwa Mungu au kwa kitu kinachoheshimiwa kama mungu. Ni kitendo cha kuonyesha unyenyekevu, utiifu, shukrani, na utukufu kwa moyo wote.

KATIKA MUKTADHA WA IMANI YA KIKRISTO, IBADA INAHUSISHA:

Ibada ni tendo la ndani la Kumuabudu Mungu katika Roho na kweli (Yohana 4:24)na ibada hii ya Roho na kweli hudhihirishwa mwilini kwa njia zifuatazo

- Kusifu na kuimba nyimbo za kiroho.

- Kusujudu, kufunga, kutoa sadaka, na kushiriki sakramenti kama Meza ya Bwana.

- Kujitoa kwa Mungu kwa mwili na roho—maisha yenye utakatifu ni ibada ya kila siku (Warumi 12:1).

-kukusanyika kwa pamoja kama watu wenye nia Moja Ili kumtukuza Mungu na kuyapeleka mahitaji yenu kwa pamoja kama Wana wa baba mmoja na Bwana mmoja katika Kristo Yesu (Ebrania 10:25)

KIBIBLIA, KUNA AINA KUU TATU ZA IBADA:

1. Ibada ya kweli kwa Mungu – inayotokana na Roho Mtakatifu na Neno la Mungu. Yohana 4:23-24, Nehemiah 9:3,Luka 24:50-53.

2. Ibada kwa shetani – kwa njia ya ushirikina au uchawi. Isaya 47:10-14,Warumi 1:25, Yeremia 10:14,2:11,16 :20, Zaburi 115:4-7, Ufunuo 9:20-21.

3. Ibada za wanadamu walizojitungia – ambazo hazina msingi wa maandiko. Mathayo 15:1-9

 Neno "ibada" linatokana na Kiarabu عبادة (ibadah), likiwa na mizizi ya maana ya "utumwa" au "kujitoa kwa unyenyekevu" kwa Mungu.

 Kwasababu hiyo Ibada ni tendo la kiroho linalounganisha Ulimwengu wa mwili na Ulimwengu wa kiroho, Ibada ni unyenyekevu wa moyo juu ya Mungu au kitu chochote unachokipa Heshima ya Hali ya juu Leo hii tunaona wakristo wengi hawafanyi Ibada ya kweli Bali wafanya ibada ya Mwilini Ili waonekane na watu zaidi sana wengi wameheshimu mambo Yao kuliko Mungu na kama tunavyojua ibada ni tendo la Heshima ya Hali ya juu sana juu ya kile unachokiamini hivyo ikiwa kazi yako inaweza kukufanya usimfanyie Mungu ibada basi ni WAZI KUWA wewe unaabudu kazi ya mikono yako na siyo Mungu, Leo hii viambatanishi kama vitambaa,maji,sabuni Keki za upako zimepewa Heshima ya Hali ya juu kuliko Mungu na jina la Yesu.

Hivyo geuka Leo mpe Yessu Maisha yako naye atakujaza Roho Mtakatifu nawe utaabudu katika Roho na kweli naye atakuongoza na kukufundisha Zaburi 32:8

BY. EV. MARTIN LAIZER.

 

Suche
Kategorien
Mehr lesen
MAHUSIANO KIBIBLIA
KANUNI YA MUDA KATIKA MAHUSIANO
Muda hupima upendo wangu kwako.Kama kweli nakupenda, nita tumia kiasi kikubwa cha Muda wangu kwa...
Von GOSPEL PREACHER 2021-11-06 15:03:16 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
ASILI MBILI ZA YESU KRISTO
Tokea Dunia ianze, hapajawai toke Mtu yeyote alieishi kama Yesu Kristo. Yesu ni mtu wa maana sana...
Von MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 06:22:50 0 9KB
SPIRITUAL EDUCATION
ALLAH IS NOT TRIUNE
The final proof that Allah is not Yahweh Elohim of the Holy Bible is that Allah is not a...
Von MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 19:46:05 0 9KB
Injili Ya Yesu Kristo
NAFASI YA MAWAZO KATIKA KUVIPIGA VITA VYA KIROHO
Vita vya kiroho, ni vita ambayo inapigwa katika ulimwengu wa roho, kwa jinsi ya rohoni baina ya...
Von GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:28:21 2 6KB
OTHERS
MUHAMMAD NI MTUME BANDIA
1. Hakutumwa na Mungu2. Alipewa Utume na Mkewe3. Alichezewa na Mashetani tokea utoto wake Leo...
Von MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 05:33:15 0 5KB