JIFUNZE MAANA YA MAJINA YA MUNGU (YEHOVA)

0
7Кб

Mungu ni mmoja tu, lakini katika umoja wake amekuwa akijifunua katika majina mengi, kulingana na  uweza wake alionao, au majira Fulani yaliyopita, au matukio ya namna tofauti tofauti  yaliyotokea. Ni sawa, ni raisi Fulani aitwe JOHN, lakini huyo huyo anaweza akaitwa baba sehemu fulani, akaitwa mjomba sehemu nyingine, mhandisi kwa watu fulani, amiri jeshi mkuu eneo Fulani, babu sehemu nyingine n.k.

Unaona utaona vyeo vyote hivyo vimekuja aidha kulingana na wakati, au matukio, au nafasi aliyopo au ujuzi alionao n.k. Na vivyo hivyo Mungu wetu , alijifunua katika  majina mengi, ambayo leo hii tutayatazama kwa ufupi.

  1. ADONAI: Mungu Mwenye enzi yote, kimbilio imara Mwa 15:2‐8, Kut 6:2‐3
  2. ELOHIMU: Mungu mwenye uweza, muumbaji  wa milele, mwenye nguvu (Mwanzo 1: 1, 17:7, Yeremia 31:33)
  3. EL-ELOHE-ISREAL: Mungu wa Israel, Mwanzoh 33:20
  4. EL-OHEEKA: Bwana Mungu Wako Kut 20:2 , 5, 7
  5. EL-ELYONI:  Mungu Aliye juu zaidi ‐Mwa14:18, Dan 4:34
  6. YEHOVA  EL- GIBBOR: Mungu Mwenye Nguvu ( Isaya 9:6-9)
  7. YEHOVA EL-OHEENU: Bwana Mungu Wetu (Zaburi 99:5,8,9
  8. YEHOVA EL – SHADAI: Mungu Ututoshelezaye/ Mungu Mtoshelezi (Mwanzo 17:1) 
  9. YEHOVA HOSEENU: Bwana Aliyetuumba Zaburi 95:6
  10. YEHOVA-MEKADISHKEMU: Bwana atutakasaye (Kutoka 31:13)
  11. YEHOVA-NISI: Mungu ni Bendera yetu (Berani ya vita) (Kutoka 15:26).
  12. YEHOVA OLAMU: Mungu wa milele Zaburi 90:1-3
  13. YEHOVA-RAFA: Mungu-Atuponyaye. (Kutoka 15:26).
  14. YEHOVA-ROHI: Bwana ndiye mchungaji wangu (Zab 23)
  15. YEHOVAH SABAOTHI: Bwana wa Majeshi (1 Samweli 1:3)
  16. YEHOVA SHAMA: Bwana Yupo Hapa (Ezekiel 48:35).
  17. YEHOVA SHALOM: Bwana ni Amani Yangu (Waamuzi 6:24)
  18. YEHOVA TSIDKEMU: Bwana ni Haki Yetu (Yeremia 23:6)
  19. YEHOVA-YIRE: Mungu atupaye (Mwanzo 22:14)..
  20. YE-SHUA (YESU): Mungu utuokoaye.(Mathayo 1:21)

Jina Hili la YESU ndio jina tulilonalo mpaka sasa. Kwa kupitia hili ndio tunapata wokovu, kwa jina hili ndio tunamshinda adui, kwa jina hili ndilo tunapata Baraka, na kwa jina hili ndio tunaishi.

Lakini biblia inatuonyesha pia jina hili sio la kudumu, Upo wakati Kristo atakuja na jina jipya,(Ufunuo 19:12 ) jina hilo wakati huo litakuwa sio la Ukombozi tena, sio la kurehemu tena, bali litakuwa ni jina la kifalme. Na ndio maana wakati huu ambao angali bado neema ipo, usiruhusu, ikupite ikiwa wewe ni bado mwenye dhambi, Leo hii Kristo bado yupo kama kuhani mkuu akitupatanisha sisi na Mungu, ikiwa na maana kuwa mlango wa rehema bado upo wazi kwa kila mtu atakayetaka kuuingia, Lakini hautakuwa wazi sikuzote. Kwani dalili za kurudi kwa Yesu mara ya pili zimeshatimia zote, tunachongojea ni unyakuo tu.

Поиск
Категории
Больше
MASWALI & MAJIBU
Ubatizo Wa Moto Ni Upi?
JIBU: Ni kweli Yohana alibatiza kwa maji na alisema Bwana YESU atakapokuja atatubatiza kwa...
От GOSPEL PREACHER 2022-06-13 09:44:22 0 7Кб
Injili Ya Yesu Kristo
YESU KRISTO AMEKUPA UTAJIRI
Watu wengu wanafikiri kuwa, Mungu aliwaumba ili wawe watu wa kawaida tu, la hasha, Mungu...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:27:06 0 6Кб
Другое
THE ROCKFELLER FAMILY
This is the Rockefeller family. it is one of the wealthiest families in America, and their...
От GOSPEL PREACHER 2021-12-22 00:53:20 0 6Кб
Injili Ya Yesu Kristo
JIANDAE KUFA KIFO KIZURI.
‘Maadam unaishi, lazima utakufa pia, hata kama hupendi kufa, kifo ni sehemu ya maisha na...
От GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:46:10 0 6Кб
Injili Ya Yesu Kristo
SOMA KITABU HIKI: ZIJUE SIRI KUBWA ZA SHETANI, ILI UWEZE KUMSHINDA
TOLEO LA 16 ISBN 978 9987 9717-7-0 UTANGULIZI Nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la...
От GOSPEL PREACHER 2021-11-19 05:59:01 0 7Кб