Je! Bikira Maria Ni MALKIA WA MBINGUNI?

0
6KB

JIBU: Neno Malkia wa mbinguni limeonekana mara mbili katika biblia

Sehemu ya kwanza ni katika Yeremia 7:18-20

18 Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi. 19 Je! Watu hawa wanikasirisha mimi? Asema Bwana; hawajikasirishi nafsi zao, na kuzitia haya nyuso zao wenyewe? 20 Kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya miti ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi; nayo itateketea, isizimike.

Na pia ukisoma sehemu nyingine katika kitabu cha Yeremia utamwona akitajwa tena..  

Yeremia 44:17-23 ” Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya. 18 Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba MALKIA WA MBINGUNI, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa. 19 Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimfanyizia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mamiminiko, waume zetu wasipokuwapo? 20 Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake, yaani, watu wote waliompa jibu lile, akisema, 21 Uvumba mliofukiza katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ninyi, na baba zenu, wafalme wenu, na wakuu wenu, na watu wa nchi, je! Bwana hakuwakumbuka watu hao? Je! Jambo hili halikuingia moyoni mwake? 22 Hata Bwana asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo. 23 Kwa sababu mmefukiza uvumba, na kwa sababu mmetenda dhambi juu ya Bwana, wala hamkuitii sauti ya Bwana, wala hamkwenda katika torati yake, wala katika amri zake, wala katika shuhuda yake; ndiyo maana mabaya haya yamewapata kama ilivyo leo. ”

Tunaona habari hizo zote mbili zinaelezea juu ya miungu ya kipagani iliyowasababishia Israeli kuingia matatizoni kwa kwenda kuifukizia uvumba, na kumbuka haina uhusiano wowote na ukristo, kwahiyo mbinguni Mungu anapoishi hakuna malkia, biblia inamtaja MFALME TU!, Naye ni mmoja na si mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO, MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA yeye peke yake.

Hivyo Mariamu sio malkia wa mbinguni, alikuwa ni mwanamke kama wanawake wengine waliokuwa wanamcha Mungu na kupewa neema ya kipekee ya kumzaa Bwana wetu Yesu, lakini hilo halina uhusiano wowote na yeye kuwa malkia, desturi za kuabudu miungu wake ni za kipagani na zilikuwepo tangu zamani AShtorethi/Semiramisi/Artemi mungu mke alikuwa anaabudiwa zamani zile na ndiye aliyekuwa anajulikana kama malkia wa mbinguni.   Kanisa katoliki ndilo lililobeba tamaduni hizi za kipagani kumwabudu Mariamu na kuwa kama kipatanishi kati yetu na Mungu ambayo ni machukizo makubwa mbele za Mungu.   Kwahiyo mkristo yoyote hapaswi kujihusisha na ibada potofu zinazotaja kuabudu miungu “wake”. Ni YESU KRISTO pekee ndiye anayestahili kuabudiwa.  

Ubarikiwe sana.

Pesquisar
Categorias
Leia mais
2 SAMUEL
Verse by verse explanation of 2 Samuel 5
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 33 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-02-05 09:23:36 0 5KB
STANDARD 3
STANDARD 3
List of all subjects for the standard 3 class
Por PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:19:35 0 5KB
Religion
EPUKA MAVAZI YA KIKAHABA
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
Por GOSPEL PREACHER 2022-01-08 10:23:04 0 15KB
OTHERS
UTHIBITISHO 12 KUWA ALLAH SIO MUNGU
  Leo nitawapa Sababu 12 kwanini allah sio mungu. 1. ALLAH NI MUNGU ASIYE NA JINA...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:12:48 0 5KB
NEHEMIAH
Verse by verse explanation of Nehemiah 4
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-04-02 12:16:07 0 5KB