Je! Mtu Aliyeokoka Anaruhusiwa Kumiliki Lodge Ambayo Ina Bar Ndani Yake?

0
6K

Swali linaendelea….na kutoa fungu la kumi kwa kupitia hiyo?,kwa mfano mimi nina rafiki yangu anafanya kazi kampuni ya TBL kazi ya kampuni hii ni kutengeneza na kuuza bia kama yalivyo makampuni mengine kama Serengeti nk. Huyu ndugu ni mkristo aliyeokoka na jumapili bila shaka hutoa fungu la kumi na sadaka zingine pia ana cheo kanisani ..je! ni kuna makosa yoyote kufanya hivyo?


JIBU: Kumiliki bar ni dhambi, vilevile kumiliki lodge lenye bar ni dhambi..biblia inasema wazi katika

Kumbukumbu 23:18 “usilete ujira wa kahaba wala mshahara wa mbwa katika nyumba ya Bwana, ni machukizo”

Kumbuka na sio tu kazi ya bar tu, bali hata na kazi nyingine yoyote isiyokuwa halali mfano biashara ya madawa ya kulevya, ufisadi, ulanguzi,uuzaji pombe,wizi, kamari, uuzaji sigara n.k kamwe usijaribu kufanya hivyo ukadhani kuwa Mungu ataziridhia sadaka zako, hata kama unatoa nyingi kiasi gani au kwa moyo kiasi gani, kwa kufanya hivyo utakuwa unajichukulia laana badala ya baraka, ni machukizo mbele za BWANA, kutii ni bora kuliko dhabihu(1 Samweli 15:22) Mungu ni mtakatifu na sio mtaka-vitu.

Kwahiyo unapokwenda mbele zake ni vema kufahamu kuwa yeye ni Mtakatifu na anaihitaji roho yako sana zaidi ya vitu vyako. Kwahiyo kuhusu hiyo kazi anapaswa aache,kwasababu biblia imeturuhusu kiungo chetu kimoja kikitukosesha tuking’oe. kumiliki bar ni dhambi..Hivyo amwombe tu Mungu awe mwaminifu atampa kazi nyingine tena nzuri zaidi ya hiyo.. Mungu Alisema kuwa anajua tunayahitaji hayo yote

Mathayo 6:31 “Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.”

Kwahiyo asiwe na wasiwasi hilo suala la baada ya kuiacha hiyo kazi atakula nini? hilo amwachie Mungu.Hivyo mshauri atafute kazi nyingine inayompa Mungu utukufu.  

Ubarikiwe sana.  

Buscar
Categorías
Read More
OTHERS
Kwa nini imani ya Kikristo ni bora zaidi ya Kiislamu?
1. Utangulizi Kuamini juu ya Mungu Mmoja, ni imani katika Uwepo wa Utendaji wa Mungu mmoja [1]....
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 06:28:18 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
NINI MATARAJIO YA MUNGU KWA VIJANA?
1 Yohana 2:14 “…. Nimewaandikia ninyi,vijana kwa sababu mna nguvu,na neno la Mungu...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 07:29:25 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
Jilindeni na chachu ya Mafarisayo
Luka 12:1 “Wakati huo, makutano walipokutanika elfu elfu, hata wakakanyagana, alianza...
By GOSPEL PREACHER 2022-04-01 08:33:24 0 6K
NDOA KIBIBLIA
MWANAMKE SIMAMA KWENYE NAFASI YAKO ILI UIPONYE NDOA YAKO
Namshukuru Mungu ambaye anazidi kunipa neema ya kuandika na kuandika masomo mbalimbali na pia...
By GOSPEL PREACHER 2021-12-16 12:14:48 0 6K
PRE-UNIT
PRE-UNIT 2
List of all of subjects for pre-unit 2 students
By PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:09:26 0 5K