KUZIMU Ni Mahali Pa Namna Gani, Je! Huko Wanaishi Watu Wakifa Na Kwenda Kupata Mateso Au Ni Vinginevyo?

0
6K

JIBU: Kuzimu ipo, na ni sehemu iliyo halisi kabisa biblia inaelezea katika (Luka 16:19-31)… Mtu anapokufa katika dhambi (yaani haujaoshwa dhambi zake kwa damu ya YESU KRISTO)..mtu anaenda moja kwa moja kuzimu/jehanum, huko kuna mateso mengi sana, mtu huyo atakaa huko akingojea ufufuo wa wafu, ambao utakuja baada ya ule utawala wa YESU KRISTO wa miaka 1000 kuisha ambapo wafu wote watafufuliwa na kuhukumiwa mbele ya kile kiti cheupe cha Hukumu..  

Ufunuo 20:12 “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.  

Ukisoma pia Yohana 5:28 BWANA YESU aliyasema maneno hayo..

“Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”  

Unaona wale wanaotenda mabaya wote watafufuliwa kwa ufufuo wa hukumu, hivyo baada ya kuhukumiwa kulingana na matendo yao ndipo watakapotupwa kwenye lile ZIWA LA MOTO atakapokuwepo shetani na malaika zake, lenye mateso mengi kuliko jehanum. ni kama tu vile mtu anapokamatwa na hatia anawekwa kwanza mahabusu kwa muda fulani akisubiria kupandishwa mahakamani, sasa akishahukumiwa mahakamani kulingana na makosa yake ndipo anapopelekwa magereza kutumikia makosa yake. na ndivyo itakavyokuwa kwa waovu wote walioikataa neema ya msalaba wa Bwana YESU KRISTO watakapokufa sasa hivi wataenda kuzimu kwenye vifungo na mateso, wakingojea hukumu ya mwanakondoo kisha baadaye watatupwa kwenye lile ziwa la moto.

Lakini wanaokufa sasa katika haki, wanapelekwa mahali panapoitwa “Paradiso” . Paradiso ni mahali panapofanana na mbinguni,lakini sio mbinguni, ni mahali pa raha, wanawekwa humo kwa muda fulani wakingojea ufufuo wa wenye haki, atakapokuja Bwana mawinguni, watafufuliwa na kuvaa miili ya utukufu na kuungana na watakatifu walio hai na kwa pamoja kwenda na Bwana mbinguni kwenye karamu ya mwana kondoo.   Paradiso kwa jina lingine ni Peponi.

1 Wathesalonike 4: 15 “Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.”  

Hivyo ndugu fahamu kuwa kuzimu ipo. Ni sehemu halisi kabisa.

Ubarikiwe sana.  


Search
Categories
Read More
SPIRITUAL EDUCATION
The Holy Spirit Dwells Within
I want to speak to you this month on the Holy Spirit. Today it will be "The Holy Spirit Dwells...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 18:34:26 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
HAZINA YA MTU
PALIPO NA HAZINA YA MTU NDIPO NA MOYO WAKE UTAKAPOKUWA 
By Martin Laizer 2023-09-25 06:09:55 0 12K
OTHERS
NIFANYE NINI ILI KUSHINDA TAMAA ZA MWILI?
JE, NINAWEZA KUISHINDA DHAMBI? Sasa je, tunaweza kweli kuishi humu duniani bila dhambi?  ...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:18:48 0 5K
JUDGES
Verse by verse explanation of Judges 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 40 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 10:42:33 0 5K
Religion
KUMTUMAINI MUNGU
HEKIMA NI KUMTUMAINI MUNGU TU: Huu ndio ukweli hata Kama wapo watakaopinga, lakini ukweli...
By tabitha Prosper 2021-08-31 06:48:51 0 6K