Mungu Alikuwa Anaongea Na Nani Aliposema Na “Tumfanye Mtu Kwa Mfano Wetu”,(Mwanzo 1:26)?

0
5K

Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi

JIBU: Mara nyingi Mungu alikuwa anatumia neno “sisi” kama wingi kuashiria kuwa hakufanya mambo yote peke yake, bali alikuwa na wengine aliowashirikisha mawazo yake, Kumbuka kuumba aliumba yeye peke yake lakini mawazo yake ya kufanya baadhi ya mambo aliwashirikisha wengine, hivyo hapo aliposema na tumfanye mtu kwa mfano wetu alikuwa anaongea na malaika zake, na hakuwa anazungumza na nafsi ya tatu katika uungu wake,kama wengi tunavyodhani Mungu ni mmoja tu na hana nafsi tatu, neno “TUMFANYE” halimaanishi ni watatu tu! bali linaweza likamaanisha wawili, au watano, au mia au milioni n.k.

Hivyo tukisema Mungu ana nafsi tatu kwa kuusimamia mstari huu sio kweli, pale Bwana alikuwa anazungumza na malaika zake ambao walikuwa wameshaumbwa kabla yetu sisi, Tunaona pia jambo hili linajirudia sehemu nyingine nyingi katika biblia Bwana akizungumza na malaika zake, Ukisoma

Mwanzo 3:22″Bwana Mungu akasema basi huyu mtu amekuwa kama MMOJA WETU, kwa kujua mema na mabaya”…,

pia,

Mwanzo 11:6 “Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.”

Unaona hapo sehemu zote hizi mbili Bwana alionekana akijadiliana na malaika zake. Mungu huwa anatenda kazi na malaika zake. Tukisoma pia

Isaya 6:8 Kisha nikasikia sauti ya Bwana ikisema, nimtume nani? naye ni nani atakayekwenda KWA AJILI YETU? Ndipo niliposema mimi hapa nitume mimi. Naye akaniambia enenda ukawaambie watu hawa fulizeni kusikia lakini msifahamu; fulizeni kutazama lakini msione…”

Unaona tena hapo Bwana alimuuliza nabii Isaya ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu (yaani Mungu na jeshi lake la mbinguni)?. Kwahiyo Mungu kujadiliana na malaika zake sio jambo jipya tunaweza tukaliona pia kwenye ile habari ya mfalme Ahabu na nabii Mikaya ukisoma

2 nyakati 18:15-22” utaona jinsi Bwana alivyokuwa anashauriana na malaika zake juu ya hatma ya mfalme Ahabu.

Kwahiyo pale katika mwanzo 1:26 aliposema Na tumfanye mtu kwa mfano wetu Mungu alikuwa hazungumzi na YESU wala Roho Mtakatifu bali na malaika zake waliokuwepo kabla yetu sisi. (Lakini kumbuka sio kwamba malaika ndio waliokuwa wanaumba, hapana Mungu peke yake ndiye aliyekuwa muumbaji.)

Ubarikiwe sana.

Zoeken
Categorieën
Read More
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 30
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 55 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-23 05:25:46 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
Ukijibu Kabla Haujasikia, Ni Upumbavu Na Aibu Kwako.
Maelezo ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia,  Ni upumbavu na aibu kwake. Hekima...
By GOSPEL PREACHER 2023-09-22 19:28:42 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
YAFAHAMU MAFUNDISHO YA UONGO
(basi roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani wakiyasikiliza...
By GOSPEL PREACHER 2021-12-22 01:41:05 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
Yesu ni nani?
Yesu wa Nazareti ni nani kwako? Maisha yako hapa duniani na ya milele yanaguswa na jibu lako kwa...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 05:27:05 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
If there is a God, why is there evil?
Agnostics ask: If God is all-powerful and all loving, then why does He permit evil and suffering...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 06:16:47 0 5K