Je! Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni ipi?

0
6K

SWALI : Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni ipi?

JIBU: Tukisoma;

Mathayo 12:25-32 ” Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo. 25 Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama. 26 Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje? 27 Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu. 28 Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. 29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake. 30 Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya. 31 Kwa sababu hiyo nawaambia, KILA DHAMBI, NA KILA NENO LA KUFURU, watasamehewa wanadamu, ILA KWA KUMKUFURU ROHO HAWATASAMEHEWA. 32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao. “

Tunavyosoma mistari hiyo tunaona kabisa wale Mafarisayo walikuwa wanajua Bwana Yesu ni kweli alikuwa anatoa pepo, na kutenda mambo yote kwa uweza wa Roho wa Mungu, lakini wao kwa ajili ya wivu, na kwa tamaa zao wenyewe,ili tu wawavutie watu kwao, wakakusudia kwa makusudi kabisa, wawageuze watu mioyo ili watu wasimuamini Bwana Yesu,wawaamini wao, na ndipo wakaanza kutoa maneno ya makufuru wanawaambia watu kuwa BWANA anatoa pepo kwa uwezo wa belzebuli mkuu wa Pepo angali ndani ya mioyo yao walikuwa wanajua kabisa anachofanya ni kwa uweza wa Roho wa Mungu.

Ukweli wa jambo hilo unajidhihirisha kwa Nikodemo ambaye naye alikuwa ni mmoja wa wale mafarisayo alipomwendea Yesu usiku na kumwambia

Yohana 3:1-2″Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, RABI, “TWAJUA” YA KUWA U MWALIMU, UMETOKA KWA MUNGU; KWA MAANA HAKUNA MTU AWEZAYE KUZIFANYA ISHARA HIZI UZIFANYAZO WEWE, ISIPOKUWA MUNGU YU PAMOJA NAYE. “

kwahiyo unaona walikuwa wanajua kabisa lakini kwa ajili ya wivu wakaanza kuzusha maneno ya uongo juu ya kazi ya Roho wa Mungu, sasa huko ndiko kumkufuru Roho Mtakatifu. hivyo basi Bwana Yesu alitoa angalizo tunapozitazama kazi za Mungu, pale mtu mwenye Roho wa Mungu anatenda kazi za Mungu kweli huku tunajua ni Mungu ndiye anayefanya kazi ndani yake, na kuanza kusema yule ni mchawi, au anatumia uchawi, au mshirikina, au tapeli, au mwizi, ili tu watu wasiziamini kazi za Mungu au vinginevyo, au unaanza kuzusha propaganda za uongo juu yake, pengine kwa kusudi la kumkomoa! hapo ndugu utakuwa unajimaliza mwenyewe. (Ni kweli si watumishi wote ni wa Mungu,hao ni sawa kuufunua uovu wao). Lakini Hapa tunamzungumzia yule unayemfahamu kabisa ni mtumishi wa BWANA,..wewe hujui umewakosesha wangapi, ambao kwa kupitia yeye, watu wengi wangeokolewa? kufanya hivyo ni hatari sana tuwe makini.

Hivyo hii dhambi unawahusu wale wanaozipinga kazi za Mungu kwa makusudi kabisa (Mfano wa mafarisayo). Hao kwao hakuna msamaha, hawawezi tena kutubu hata iweje wanachongojea ni ziwa la moto.

Lakini shetani naye anapenda kulitumia hili neno kuwafunga watu wajione kuwa wamemkufuru Roho Mtakatifu na kwamba dhambi zao hazisameheki hata wafanyeje,
Hii inakuja sana sana kwa watu waliowachanga ki-imani, kuna shuhuda nyingi za watu waliofungwa na shetani kwa namna hiyo wakidhani kuwa dhambi zao hazisameheki, kuna watu wamekata tamaa wanajiona kwa wingi wa dhambi zao, Mungu hawezi kuwasemehe tena, pengine wameua, wametoa mimba sana, n.k, Sasa jambo la namna hii likija katika mawazo yako likatae linatoka kwa yule mwovu kukufanya wewe ujione kuwa Mungu hawezi kukusamehe umemkufuru, hivyo usijisumbue kutubu kwasababu Mungu hatakusikiliza.

Kumbuka kama tulivyosema Dhambi hii inakaa kwa wale watu ambao ndani yao mioyo ya toba imekufa, au hofu ya Mungu haipo tena kwao, watu waliojikinai, wanaompinga Mungu katika fikra zao japo kuwa walimjua Mungu na uweza wake wote, wanazipotosha kazi za Mungu kwa makusudi kwa faida zao wenyewe,ili wawavute watu kwao, au wawe washirika wao na sio kwa Mungu. Hivyo basi kitendo tu cha wewe kuwa na hii hofu ya kumwogopa Mungu ujue Roho wa Mungu anatenda kazi ndani yako na hayo mawazo ya kwamba umemkufuru Roho Mtakatifu yapinge huyo ni adui ndio moja ya njia zake hizo ili usiufikie wokovu na anapenda kuwatesa watu wengi katika andiko hili.

Ubarikiwe sana.

Căutare
Categorii
Citeste mai mult
Religion
HOW TO BECOME A CHRISTIAN?
This question is very important, and not all human beings know its answer. But it is very simple...
By GOSPEL PREACHER 2021-08-25 10:01:32 0 5K
1 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 1 Chronicles 21
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-03-20 05:08:28 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
JINSI YA KUENENDA KWA ROHO.
Wagalatia 5:16 “Basi, nasema enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe tamaa za...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 13:00:32 0 5K
OTHERS
Husband and wife
1 "Love your wife as Christ loved the Church." (Ephesians 5:25) Risk your life to help or save...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:54:43 0 5K
ISAIAH
ISAIAH 19
Isaiah Chapter 19 Verses 1-10: The burden of Egypt is a message of both judgment and hope for...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-28 03:41:35 0 7K