Ni nani anayetawala dunia kati ya Mungu na shetani?

0
5K
Swali linaendelea….Na kama ni Mungu anayetawala kwa nini kuna matukio ya kutisha kama ajali mbaya za magari,ndege,mafuriko kama ya Japan kama Mungu ndiye anayetawala kwanini hayazuii anaacha yanaua watu??? Na ukisoma Mathayo 4:1 na kuendelea, shetani anamwambia Yesu dunia ni Mali yake, nataka kufahamu pia je! Kuna tofauti gani kati ya dunia na ulimwengu nisaidie?
 
JIBU: Dunia yote ni ya Mungu ukisoma;
Zaburi 24:1 ” Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. 2 Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. “
Na pia Bwana Yesu Kristo baada ya kufufuka kwake aliwaambia wanafunzi wake maneno haya; 
Mathayo 28:18″Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. “
Kwahiyo kwa maandiko hayo tunaona kabisa kuwa dunia yote inamilikiwa na Mungu na wala sio shetani, lakini kumbuka pia”dunia sio ulimwengu”. Huu ulimwengu ndio mali ya shetani na ndio yeye anayeumiliki na kitakachokuja kuteketezwa sio dunia bali ni ulimwengu huu mbovu wa shetani ambao ni milki yake aliyojijengea..

Tofauti kati ya dunia na ulimwengu ni hii;

  • Dunia ni vitu vyote vya asili na vya kijeografia unavyoviona kama vile mabara, bahari, miti, milima, hewa, ardhi, mito,mabonde, visiwa,anga, n.k.
  • Na Ulimwengu ni ustaarabu uliobuniwa na aidha Mungu au shetani ili kuifanya dunia iwe na mantiki, paonekane kama ni mahali pa kuishi. mfano. elimu, burudani, miziki, utawala, uchumi, mahakama,Milki, fahari, uchukuzi, mawasiliano, n.k. Haya yote ni mambo yaliyobuniwa kuipa dunia muonekano unaoleta maana. Na ndio maana kwenye Mathayo 4 shetani alimwambia Bwana Yesu nitakupa ULIMWENGU na fahari yake ukianguka kunisujudia.
Kwahiyo dunia itadumu siku zote, lakini ustaarabu uliowekwa na shetani (yaani ulimwengu )utaangamizwa utabaki tu ule uliowekwa na Mungu, na hata hivyo 99% ya ustarabu uliopo duniani leo hii unakaliwa na shetani na ndio maana siku ya Bwana itaharibu ustaarabu wote wa shetani na kuleta ustaarabu mpya wa Kristo hapa duniani huo ndio utakaodumu milele na utakaokuwa ni ule utawala wa miaka 1000 Ufunuo 19 & 20.
 
Na sababu ya Mungu kuruhusu mambo mabaya kutokea kama ajali, vimbunga, mafuriko ni kwasababu ya mambo maovu ya huu ulimwengu yaliyopo kama umwagaji damu, rushwa, uasherati, ulevi, uaribifu wa mazingira, ushoga, vita, n.k. mambo kama haya ardhi haiwezi ikavumilia, yanaiharibu dunia na kupelekea gadhabu ya Mungu kumwagwa juu ya nchi.
 
Tujitahidi tujiepushe na mambo ya ulimwengu huu yanayopita..Tuyatazame yaliyo juu.
 
Kumbuka hizi ni siku za mwisho na Kristo yupo mlangoni kurudi. Kizazi tunachoishi kina dalili za kushuhudia mwisho wa dunia. Chunguza wokovu wako na ujiweke sawa.
 
Mungu akubariki.
Buscar
Categorías
Read More
JOSHUA
Verse by verse explanation of Joshua 17
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 17 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 08:20:25 0 5K
Networking
How to choose the right marketplace business model
To build a sustainable and successful marketplace platform, you need to find a business model...
By Business Academy 2022-09-17 03:32:43 0 6K
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 44
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 24 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-21 09:58:36 0 6K
DANIEL
DANELI 3
Jina la Bwana wetu na Mkuu wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu katika mwendelezo wa kitabu...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-05 23:37:05 0 7K
2 SAMUEL
Verse by verse explanation of 2 Samuel 10
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 25 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 09:37:38 0 5K