Ni nani anayetawala dunia kati ya Mungu na shetani?

0
5K
Swali linaendelea….Na kama ni Mungu anayetawala kwa nini kuna matukio ya kutisha kama ajali mbaya za magari,ndege,mafuriko kama ya Japan kama Mungu ndiye anayetawala kwanini hayazuii anaacha yanaua watu??? Na ukisoma Mathayo 4:1 na kuendelea, shetani anamwambia Yesu dunia ni Mali yake, nataka kufahamu pia je! Kuna tofauti gani kati ya dunia na ulimwengu nisaidie?
 
JIBU: Dunia yote ni ya Mungu ukisoma;
Zaburi 24:1 ” Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. 2 Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. “
Na pia Bwana Yesu Kristo baada ya kufufuka kwake aliwaambia wanafunzi wake maneno haya; 
Mathayo 28:18″Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. “
Kwahiyo kwa maandiko hayo tunaona kabisa kuwa dunia yote inamilikiwa na Mungu na wala sio shetani, lakini kumbuka pia”dunia sio ulimwengu”. Huu ulimwengu ndio mali ya shetani na ndio yeye anayeumiliki na kitakachokuja kuteketezwa sio dunia bali ni ulimwengu huu mbovu wa shetani ambao ni milki yake aliyojijengea..

Tofauti kati ya dunia na ulimwengu ni hii;

  • Dunia ni vitu vyote vya asili na vya kijeografia unavyoviona kama vile mabara, bahari, miti, milima, hewa, ardhi, mito,mabonde, visiwa,anga, n.k.
  • Na Ulimwengu ni ustaarabu uliobuniwa na aidha Mungu au shetani ili kuifanya dunia iwe na mantiki, paonekane kama ni mahali pa kuishi. mfano. elimu, burudani, miziki, utawala, uchumi, mahakama,Milki, fahari, uchukuzi, mawasiliano, n.k. Haya yote ni mambo yaliyobuniwa kuipa dunia muonekano unaoleta maana. Na ndio maana kwenye Mathayo 4 shetani alimwambia Bwana Yesu nitakupa ULIMWENGU na fahari yake ukianguka kunisujudia.
Kwahiyo dunia itadumu siku zote, lakini ustaarabu uliowekwa na shetani (yaani ulimwengu )utaangamizwa utabaki tu ule uliowekwa na Mungu, na hata hivyo 99% ya ustarabu uliopo duniani leo hii unakaliwa na shetani na ndio maana siku ya Bwana itaharibu ustaarabu wote wa shetani na kuleta ustaarabu mpya wa Kristo hapa duniani huo ndio utakaodumu milele na utakaokuwa ni ule utawala wa miaka 1000 Ufunuo 19 & 20.
 
Na sababu ya Mungu kuruhusu mambo mabaya kutokea kama ajali, vimbunga, mafuriko ni kwasababu ya mambo maovu ya huu ulimwengu yaliyopo kama umwagaji damu, rushwa, uasherati, ulevi, uaribifu wa mazingira, ushoga, vita, n.k. mambo kama haya ardhi haiwezi ikavumilia, yanaiharibu dunia na kupelekea gadhabu ya Mungu kumwagwa juu ya nchi.
 
Tujitahidi tujiepushe na mambo ya ulimwengu huu yanayopita..Tuyatazame yaliyo juu.
 
Kumbuka hizi ni siku za mwisho na Kristo yupo mlangoni kurudi. Kizazi tunachoishi kina dalili za kushuhudia mwisho wa dunia. Chunguza wokovu wako na ujiweke sawa.
 
Mungu akubariki.
Search
Categories
Read More
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 9
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 35 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:33:51 0 6K
NDOA KIBIBLIA
SHAMBA LA MTU MVIVU, ASIYE NA AKLI: MAHUSIANO YA NDOA (NA UCHUMBA)
MAHUSIANO: SHAMBA LA MTU MVIVU, ASIYE NA AKLI(Uvivu na Kukosa Akili Kichocheo Cha...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-07 23:23:24 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
IPONYE NAFSI YAKO, EPUKA MANABII WA UONGO
Muhubiri/ Mtumishi yeyote aliyerudi nyuma na kusahau kusudi lake tayari anageuka kuwa nabii wa...
By GOSPEL PREACHER 2023-06-17 23:43:15 0 8K
MAHUSIANO KIBIBLIA
SEHEMU YA 3: MISINGI YA KIIMANI KATIKA MAHUSIANO YA UCHUMBA HADI NDOA
Bwana asifiwe!! Unaweza kusoma SEHEMU YA 1, SEHEMU YA 2, SEHEMU YA 4 au SEHEMU YA 5 ya somo hili,...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-06 11:43:23 0 5K
MAHUSIANO KIBIBLIA
HIZI NI TABIA HATARISHI KWA MWANAMKE KATIKA MAHUSIANO: UCHUMBA HADI NDOA
KWELI KUU: Tabia ni msingi na kielelezo cha mahusiano bora ya aina yoyote na hasa yale ya uchumba...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-07 23:18:56 0 10K