Je! Inawezekana mtu akawa anafanya miujiza na bado asinyakuliwe?

0
5K

SWALI: Naomba kuelewa kwanini mtu atoe pepo, aombee wagonjwa wapone, asikie sauti ya Mungu Ikimwambia hiki na kile kuhusu watu na yeye mwenyewe kufunua siri za mioyo yao, halafu bado asiende mbinguni au asinyakuliwe? Hili linawezekanikaje?


JIBU: Ni sababu ile ile ya Mungu kumpa mwovu afya, chakula, miaka mingi ya kuishi, mvua, uzao, ujuzi, akili, utashi,n.k. vipawa hivi vyote vinatolewa na Mungu, kwasababu yeye anawanyeshea mvua yake waovu na wema. sasa kwa kupewa baraka zote hizo haimpi uhakika mtu huyo kupata uthibitisho ya kuwa Mungu yupo na yeye,

Kwasababu hivi vitu vyote hata mchawi anapewa kitendo cha kuwa tu mwanadamu tayari vinaambatana na wewe, kuna vitu Mungu akikupa haviondoi hata uwe mbaya kiasi gani kama ilivyo kwa shetani Mungu hakumnyang’anya nguvu zake zote japokuwa ni muasi, lakini sababu ya Mungu kuruhusu hayo yote ni kuonyesha uwepo wake dhahiri ili mtu asiwe na udhuru katika siku ya hukumu kwamba hakuuona utukufu wake…

Siku zote Mungu anabaki katika NENO lake, mtu anayempendeza ni yule anayelishika NENO lake kwa kuishi maisha matakatifu yampendezayo, HILO TU! na ndio maana Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake katika Luka 10:20″

Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni. “

Unaona tunapaswa tufurahie pale majina yetu yanapoandikwa mbinguni na sio pale pepo wanapotutii kwasababu kuna watakao toa pepo, watakaoona maono, watakao ponya wagonjwa, watakaotabiri na bado watakuwepo kuzimu.

Soma mistari ifuatayo;

Kumbukumbu 13:1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. 4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye. 5 Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya Bwana, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako.

Na ndio maana Bwana alimalizia na kusema….

Mathayo 7:21-27 ” Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. 24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; 27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.”

Hivyo usipumbazwe na karama yoyote ile uliyonayo au mtu aliyonayo, Dumu katika Neno la Mungu na utakatifu. Hilo tu.

‘bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni’.

Ubarikiwe.

Site içinde arama yapın
Kategoriler
Read More
REVELATION
UFUNUO 11
Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Ufunuo, biblia inasema “Heri asomaye na wao...
By GOSPEL PREACHER 2021-10-30 11:26:46 0 5K
HOLY BIBLE
What does it mean that Jesus is the Son of God?
Jesus is not God’s Son in the sense of a human father and a son. God did not get married...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 04:23:35 0 5K
MAHUSIANO KIBIBLIA
UMEHESABU GHARAMA?
Mahusiano ya uchumba hadi ndoa yanajengwa. Na kama yanajengwa, basi yana gharama na yanachukua...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-07 23:57:20 0 6K
JOB
Verse by verse explanation of Job 27
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 22 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-03 04:03:51 0 5K
BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
Should Christians desire wealth?
For the Christian, wealth requires extreme caution. While wealth is not evil or bad in and of...
By BIBLICAL FINANCES 2021-12-29 15:23:39 0 6K