FAHAMU KUHUSU JINA LA FARAO

0
5K

Kwa ufupi…

Bwana Yesu asifiwe…

Je unafahamu nini kuhusu jina hili la farao? Basi ngoja nikujuze kidogo kuhusu jina la Farao.

Farao sio jina kama majina mengine bali ni cheo kilichotumika kwa wafalme wa Misri. Hivyo Farao ni cheo cha kifalme wa kimisri, yaani ni sawa na kusema jina linalotumika kumuelezea kiongozi wa juu katika nchi katika nchi zetu leo; tunatumia neno “ raisi”. Kwa hiyo tuna “ raisi fulani, raisi fulani.n.k”Kulikuwa na baadhi ya wafalme waliotawala Misri,wapo kama kumi na mbili au kumi na tatu,wale waliotajwa katika maandiko,ambao hao wote waliitwa kwa jina la Farao.

Miongoni mwa cheo hiki,Wafalme wengine wawili walikuwa na majina yao tofauti na jina hili,Wafalme hao ni Necho and Hophra.
Bali wengine walibakia na cheo hicho cha Farao.Mtililiko ufuatao unatupa picha nzuri ya Farao kama walivyotajwa katika maandiko matakatifu;

  1. FARAO (Mwanzo 12:14-15,)Huu ulikuwa ni wakati wa Abrahamu kama B.C.1920
  2. FARAO(mwingine) Alikuwa ni Farao ambaye akida wake alikuwa ni Potifa Mwanzo 37 :39 39 :1,Matendo 7:10,13. Ilikuwa ni kabla ya Kristo, kamaB. C. 1728. Hata hivyo wengine husema kwamba FARAO huyu ni mtoto wa FARAO Yule wa katika Mwanzo 37:36
  3. FARAO(mwingine) *Huyu ni Farao mwingine aliyeinuka juu ya Misri asiyemfahamu Yusufu Matendo 7 :18,Kutoka 1 :8,Soma tena Waebrania 11 :23,Hata hivyo,kuna FARAO mwingine aliyeinuka katika kipindi cha Musa alipokimbilia Midiani na ndio Farao ambaye alikufa kabla ya Musa kufikisha umri wa miaka themanini aliporudi kutoka Midiani kwenda Misri,Soma Kutoka 2:11-23,Kutoka 4:19,na Matendo 7:23
  4.  FARAO(mwingine)Huyu ni Farao ambapo aliwazuia Waisraeli wasitoke Misri.Soma Kutoka 5:1-14,Kutoka sura ya 31,2Wafalme17 :7,Nehemia 9:10,Zaburi 135:9
    Rumi 9:17; Waebrania 11:27, alitawala kama B. C. 1491.(Kabla ya Kristo)
  5. FARAO(mwingine)Huyu alikuwa ni Farao katika kipindi cha Daudi 1Wafalme 11:18-22; B. C. 1030.
  6.  FARAO(mwingine)
    Huyu alikuwa ni Farao ambaye ni baba mkwe wake Selemani, 1Wafalme 3:1; 7:8; 9:16,24, B. C. 1010.

     

    PAMOJA NA FARAO HAO,WAPO WENGINE KAMA VILE;

  7. SHISHAKI-B. C. 975, 1Wafalme 11:40; 1Wafalme 14:25; 2 Nyakati12:2

  8. ZERAH,-Alikuwa ni mfalme wa Misri na pia alikuwa ni mfalme a Ethiopia katika kipindi cha Asa , B. C. 930;

  9. SO,
    -Huyu alikuwa akiitwa SO hivyo hivyo na ndilo jina lake.Ilikuwa Katika kipindi cha Ahazi, B. C. 730,Soma 2 Wafalme 17:4.
  10. TIRHAKA( Tirhakah,)
    *Huyu alikuwa ni mfalme wa Ethiopia na Misri(KUSHI)Katika muda wa Hezekia B. C. 720, Soma2 Wafalme 19:9; Isaya 37:9.

  11. FARAO-NEKO
    *Alikua ni mfalme wa Misri katika kipindi cha Yosia B. C. 612, Soma 2 Wfalme23:29-30; 2 Nyakati35:20-24, etc.

     

    MWISHO .
    UBARIKIWE.  

Căutare
Categorii
Citeste mai mult
Alte
BOOK OF GENESIS
Book of Genesis Explained Genesis is the book of beginnings. It records the beginning of time,...
By PROSHABO NETWORK 2021-10-02 23:29:25 0 7K
PSALMS
Verse by verse explanation of Psalm 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 34 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-04 17:53:38 0 5K
UCHUMBA KIBIBLIA
HASARA ZA KUFANYA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA.
Andiko la Msingi ni Mithali 5:1-20. Mungu ndiye aliyewaumba mtu mume na mtu mke, akawaweka...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 07:16:45 0 9K
MAHUSIANO KIBIBLIA
MWANAMKE NA NGUVU YA USHAWISHI (UBEMBELEZI)
Mwanamke aliumbwa na nguvu ya ushawishi ndani yake kwa kusudi la kuweza kutimiliza jukumu lake...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-07 23:52:21 0 7K
NDOA KIBIBLIA
NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE
Mithali 14: 1 ‘Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu...
By GOSPEL PREACHER 2021-12-16 12:09:11 0 8K