KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA.

0
5K

Kwa ufupi..

Bwana Yesu asifiwe…

`` Kwa kuwa,kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka” Warumi 10:13

Ukihitaji kuokoka huna budi kilihitaji Jina la Bwana. Nabii Yoeli anasema,mtu yeyote atakayeliitia Jina la Bwana “ataponywa” Kumbe huna budi kushuka kwa Bwana kwa habari ya uponyaji na kuokoka kwako.

Tunaposema “ kuliitia Jina la Bwana” tunamaana ya kuomba kwa Jina Bwana Yesu kwenye kila eneo. Ingawa Bwana Mungu ajua shida zako, lakini bado unalo jukumu la kuomba ndipo utendewe sawa sawa na hitaji lako. Inawezakana ukawa kweli umeokoka, lakini bado hata hivyo unahitaji kuomba ili usaidiwe. 

Leo nataka tujifunze kwa Petro yeye aliyekuwa mtume wa Bwana,na kupitia andiko hili tunaweza kujifunza kitu hapa ;

Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.  Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoeMara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?” Mathayo 14:28-31

Tunaweza kujifunza mengi kutoka katika maandiko hayo hapo juu. Lakini nataka kujifunza neno moja tu,nalo ni “kuomba katika Jina la Bwana, wakati wa kuzama kwako” Petro anatufundisha njia nzuri ya kuokoka kutoka katika hali mbaya ya kuzama maji. Yeye Petro hakuwa na msaada mwingine isipokuwa ni kumuomba Bwana kwa kupiga yowe! Laiti kama Petro asingeliomba yamkini angelizama ndani ya yale maji.

Kumbuka Petro alikuwa na uzoefu mkubwa wa mambo ya baharini na uvuvi. Lakini safari hii uzoefu wake haukumsaidia isipokuwa ni Bwana tu ndiye aliyemsaidia asife maji, na huku ndiko kuokoka na kupona mauti. Leo inawezekana wewe nawe ukawa na uzoefu mwingi juu ya elimu fulani, lakini nataka nikuambie ukikamatwa kwenye kona mbaya, uzoefu wako kamwe hautakusaidia bali atakayekusaidia ni Bwana Yesu tu.

Petro hakuona tashwishwi kuliitia Jina la Bwana akihitaji msaada. Hata kwako,usione shida kuomba tena kuenda kuombewa na mchungaji aliye karibu nawe kusudi tatizo ulilokuwa nalo ni kama kuzama kwenye maji mengi. Wapo watumishi ambao wanagugumia na magonjwa yao,na shida zao wakiwa wameshikilia taratibu za kidini,na dini zao zimewakinga wakatae kuombewa.! nakushauri ikiwa unahitaji kuombewa fungua moyo wako na nenda kaombewe, Bwana naye atakuponya tu,uwe na imani hiyo ndugu yangu.

Buscar
Categorías
Read More
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 34
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-21 08:57:48 0 5K
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 33
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 33 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-23 05:34:22 0 6K
OTHERS
YESU ATABIRI KUHUSU MTUME WA UONGO AMBAYE NI MUHAMMAD
Tahadhari ya Bwana Yesu: Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani alituonya kuhusu kuwatambua manabii na...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 23:04:26 0 5K
1 KINGS
Verse by verse explanation of 1 Kings 21
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 16:01:03 0 5K
REVELATION
UFUNUO 19
Karibu tujifunze biblia na huu ni mwendelezo wa kitabu cha Ufunuo leo tukiwa katika ule mlango wa...
By GOSPEL PREACHER 2021-10-30 12:21:07 6 6K