CHAKULA CHA YESU KRISTO

0
7K

Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA

SOMO:  CHAKULA CHA YESU KRISTO

L

eo tena, tunazidi kusonga mbele katika kujifunza Kitabu cha YOHANA katika Biblia zetu.  Leo, tunajifunza YOHANA 4:27-45.  Pamoja na mafundisho mengine tutakayojifunza katika mistari hii, tutajifunza pia juu ya “CHAKULA CHA YESU KRISTO“.  Tutayagawa mafundisho yote tunayoyapata katika mistari hii, katika vipengele vinane:-

(1)UHUSIANO WA WANAUME NA WANAWAKE KATIKA WOKOVU (Mst. 27);

(2)WAJIBU WA KUUACHA MTUNGI (Mst. 28-30);

(3)CHAKULA CHA YESU KRISTO (Mst. 31-35);

(4)MSHAHARA WA KUMTUMIKIA MUNGU (Mst. 37-38);

(5)MMOJA HUPANDA AKAVUNA MWINGINE (Mst. 37-38);

(6)NENO LA MWANAMKE (Mst. 39);

(7)WALIMSIHI AKAE KWAO (Mst. 40-42);

(8)NABII HAPATI HESHIMA KATIKA NCHI YAKE (Mst. 43-45).

 

(1)      UHUSIANO WA WANAUME NA WANAWAKE KATIKA WOKOVU (Mst. 27)

Yesu Kristo, aliangalia sana uhusiano wake na wanawake kwamba hauleti dosari yoyote katika usafi wake na ushuhuda wa wokovu wa Injili yake.  Alipokuwa akisema na mwanamke Msamaria pale kisimani, wanafunzi wake walistaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke.  Siyo kwamba Yesu alikuwa hasemi na wanawake kabisa, la hasha!  Alisema nao (LUKA 10:41; 23:28-31; 8:47-48; YOHANA 20:16-17).  Katika tukio la kisimani, wanafunzi wake walishangaa kumwona Yesu akiwa na mwanamke yule Msamaria peke yao.  Hawakuwahi kuona hivyo kabla.  Lakini hata hapa, utaona kwamba ilikuwa ni hadharani – kisimani, mahali ambapo watu wanaingia na kutoka na kuyasikia yote waziwazi.  Ndiyo maana “hakuna aliyesema, Mbona unasema naye?“  Wakati wote, katika lolote, Yesu Kristo alikuwa mwangalifu katika lolote alilolifanya na wanawake.  Aliangalia kwa makini na kuhakikisha kwamba hakuna yeyote atakayesema “Wokovu ni uongo au Injili anayohubiri siyo ya kweli“.  Mtume Paulo vivyo hivyo, alipokuwa anakwenda nyumbani kwa mwanamke Lidia, hakuwa peke yake, alikuwa na wenzake Timotheo na Sila.  Katika timu walifanya kazi miongoni mwa wanawake.  Maneno “Tukaenda“, “Tukaketi“, “Tukasema“, “Akatusihi“, “Ingieni“, yanaonyesha kwamba walikuwa wengi (MATENDO 15:40-41, 16:1-2, 13-15).  Katika utendaji wake wa kazi, pale Paulo Mtume alipokuwa peke yake, alimchukua Akila na Prisila mkewe, wakaenda kutenda kazi na kuwa huru kuingia katika nyumba yoyote au kusema na yeyote.  Mtume Paulo, hakwenda na mwanamke Prisila katika Injili bila kuwa na mumewe.  Sisi nasi hatuwezi kufanya hivyo.  Hakuna kielelezo chochote cha wokovu wetu tunaohubiri, ikiwa mwanaume atakuwa anatembea barabarani au kuzunguka huko na huko, na mwanamke ambaye siye mke wake, kwa kisingizio cha kuitenda kazi ya Bwana (MATENDO 18:1-4).  Baada ya kuokolewa, tunapaswa kuhakikisha SIKU ZOTE kwamba tunakuwa na dhamiri isiyo na hatia.  SIYO MBELE ZA MUNGU TU, ILA NA MBELE ZA WANADAMU, ili mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia yaani WOKOVU (MATENDO 24:16; 2 WAKORINTHO 8:20-21).  Watu ambao hawajaokoka wakimwona mwanaume aliyeokoka anatembea barabarani huku na huko na mwanamke ambaye siye mke wake au wako chumbani peke yao kwa visingizio vya kujifunza Biblia na kuomba; watasema wanafanya uasherati, hata kama siyo kweli.  Tayari hiyo ni hatia.  Uasherati haupaswi kutajwa kwetu kamwe hata kwa kudhaniwa (WAEFESO 5:3).  Mataifa wakiona wokovu siyo kweli kutokana na uhusiano wetu na wanawake, tendo hilo ni kuwawekea vikwazo vya kuwazauia kuingia mbinguni, wakati sisi wenyewe hatuingii (MATHAYO 23:13; LUKA 11:52; ISAYA 57:14; WALAWI 19:14; 1 YOHANA 2:10).  Kutembeleana kwa “kaka“ na “dada“ katika wokovu kwa visingizio vya kutembeleana katika ugonjwa n.k; vinaweza kuleta zinaa katika wokovu (2 SAMWELI 13:6-15).  Mwanaume atamshika mwanamke asiye mke wake mkono tu, katika salamu; siyo mabega, nywele au sehemu yoyote nyingine.  Wanawake watawafuatilia wanawake na vivyo hivyo wanaume.  Hakuna “boyfriend“ au “girlfriend“ katika wokovu.  Hata wachumba ni mwiko kutembeleana na kupikiana vyumbani mpaka baada ya ndoa.  Hata kuja kanisani mwanaume hapaswi kuzungumza na mwanamke mambo yasiyopasa kwa mfano “Binti mbona nyinyi wanawake mnatukataa wanaume kila tunapowachagua muwe wake zetu?“  Huo ni uasherati.

Advertisements
REPORT THIS AD

(2)      WAJIBU WA KUUACHA MTUNGI (Mst. 28-30)

Tukitaka kumpendeza Mungu, ni lazima tuwe tayari kuiacha mitungi yetu na kwenda kufanya kazi ya Mungu.  Mtungi ni chochote kinachoonekana ni cha muhimu kwetu duniani.  Ni lazima tuache biashara zetu na kwenda Kanisani au kufuatilia watoto wachangas kiroho.  Lolote lile iwe watoto, mume, kazi ya Kaisari n.k; yote hayo ni mitungi.  Tusiruhusu yatuzuie kumtumika Mungu.  Mwanamke huyu alipoacha mtungi wake, aliwaleta wengi kwa Yesu.  Asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wa Yesu (LUKA 14:3).

(3)      CHAKULA CHA YESU KRISTO (Mst. 31-35)

Chakula kwa mwanadamu, ni kitu ambacho tunakitolea muda wetu wote.  Katika kufanya kazi tunatafuta chakula, tunatumia saa nyingi kwa siku katika kula asubuhi, mchana na usiku.  Bila chakula cha mchana, wengine wataona maisha magumu mno.  Chakula cha Yesu Kristo kilikuwa kuyatenda mapenzi ya Mungu yaani kuihubiri Injili ili watu waokoke kama kwa mwanamke huyu Msamaria.  Hicho ndicho kilichokuwa chakula Na. 1, kwa Yesu.  Chakula cha mwili kilifuata baadaye.  Sisi nasi inatupasa kumfuata kwa kutoa maisha yetu yote kuihubiri Injili na kuwasimamisha watoto wachanga katika wokovu (YOHANA 13:15; 1 PETRO 2:21).

 

(4)      MSHAHARA WA KUMTUMIKIA MUNGU (Mst. 36)

Mshahara mkubwa unamsubiri kila mtu anayetoa muda wake mrefu kumtumikia Mungu.  Wengi kwa kutokuelewa, wanafikiri kumtumikia Mungu ni kazi isiyo na faida.  Inaweza ikaonekana hivyo hapa duniani, lakini kama tungepata ufahamu, kila mmoja wetu angetafuta kwa bidii, kumtumikia Mungu, kwa gharama yoyote; ili ajilimbikizie mshahara tele wa milele mbinguni (ISAYA 49:4; 2 NYAKATI 15:7; 1 WAKORINTHO 15:58).

 

(5)      MMOJA HUPANDA AKAVUNA MWINGINE (Mst. 37-38)

Kabla ya wanafunzi wa Yesu, manabii wengi walikufa kwa ajili ya Neno la Mungu.  Yohana Mbatizaji pia alikatwa kichwa kwa ajili ya Injili na wengi wengine.  Yesu naye ilimpasa kufa kwa misingi hiyohiyo.  Hata baadaye mitume nao walikufa vivyo hivyo, pamoja na wamishonari wengi.    Wote hawa wamepanda, nasi tunavuna hivi leo.  Tunaweza kumhubiri mtu asiokoke.  Tumepanda mbegu kwa kufanya hivyo atakuja kuvuna mwingine.  Yote ni sawa, tuzidi kuitenda kazi (1 WAKORINTHO 3:6-8; MHUBIRI 11:4-6).

(6)      NENO LA MWANAMKE (Mst. 39)

Neno la Mwanamke Msamaria siku ileile aliyokuwa ameokoka, lilileta watu wengi kwa Yesu.  Wanawake hatupaswi kujidharau. Mungu huwatumia wanawake kipekee kuwaleta wengi kwa Yesu, pale tu wanapoondoa kujidharau na kujiamini.  Wako manabii wengi waliokuwa wanawake katika Biblia – Miriamu (KUTOKA 15:20), Hulda (2 WAFALME 22:14), Noadia (NEHEMIA 6:14), Debora (WAAMUZI 4:4), Anna (LUKA 2:36).  Shime tuitende kazi ay Bwana.  Siyo kwa uwezo wetu, bali kwa uwezo wa Mungu tunaitenda kazi (ZEKARIA 4:6; WARUMI 9:16).

(7)      WALIMSIHI AKAE KWAO (Mst. 40-42)

Walipomsihi Yesu akae kwao zaidi, uamsho uliendelea.  Sisi nasi inatupasa kuendelea kumsihi Yesu na Roho Mtakatifu kwa maombi kila siku, ili uamsho uendelee kati yetu, ikiwa wanakaa kwetu.

(8)      NABII HAPATI HESHIMA KATIKA NCHI YAKE (Mst. 43-45)

Yesu Kristo, hakupokelewa vema na kupata heshima, Nazareti, hapo alipolelewa (LUKA 4:16, 22-30; MATHAYO 13:54-55).  Sisi nasi itakuwa hivyo.  Tunaweza tukawashuhudia ndugu zetu wasikubali ushuhuda wetu.  Ikiwa hivyo, tuwaunganishe na wale wasiowajua.

…………………………………………………………………………………………………………………………………..

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “somo” hili, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe..

Pesquisar
Categorias
Leia Mais
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Deuteronomy 30
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 19 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-01-25 07:02:11 0 5K
MASWALI & MAJIBU
Naomba Kujua Watakaoenda Mbinguni Je! Ni Wengi Au Wachache?
JIBU: watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?..Ni swali ambalo halikuulizwa tu na...
Por GOSPEL PREACHER 2022-06-13 09:01:02 0 7K
OTHERS
KORAN HAIKUTEREMSHWA KUTOKA KWA ALLAH
Je, ungependa kuwafahamu waandishi wa Koran? Katika somo letu la leo, tutajifunza kuhusu...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:27:10 0 5K
ESTHER
ESTA SURA YA 8, 9 & 10
Jina la YESU KRISTO BWANA wetu lisifiwe. Karibu kwenye mwendelezo wa kitabu cha Esta, leo...
Por GOSPEL PREACHER 2022-01-20 02:55:34 0 6K
OTHERS
Yesu Kristo hajaumbwa bali alikuwepo tangu milele yote
Ni kweli kabisa kwamba Yesu alikuwepo tangu milele yote kabla ya kuumbwa kitu cho chote kile....
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:58:23 0 4K