JE NANI ALAUMIWE ZAIDI KATI YA ADAMU NA HAWA?

GOSPEL PREACHER
Moderador
Entrou: 2021-08-24 06:51:00
2021-10-05 18:25:35

KARIBU SANA KATIKA MDAHALO WETU:

UTANGULIZI: Biblia inatufundisha kuwa Mungu ni mwema (Zaburi 106:1) tena huwa anatuwazia mawazo mema na ya amani tena ni mawazo ya kutupatia tumaini siku zetu za mwisho(Yeremia 29:11). Ndio maana lengo lake hasa la uumbaji lilikuwa ni kutengeneza koloni lingine la mbinguni (Dunia), na katika koloni hili amuweke mwanadamu awe kiongozi (Gavana) wa koloni hili. Ukisoma mwanzo 1:1-31) utaona kuwa Mungu aliandaa mazingira bora sana ili huyu mwanadamu aishi maisha mazuri na ya furaha tena ya kifalme (akiwa mtawala). Mwanzo 5:1-2 na Mwanzo 1:27, inaonyesha wazi kuwa hapo Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke katika siku moja (i.e. tukio hili lilifanyika katika ulimwengu wa roho), tena akawabariki na akawaita jina lao Adamu, ndio sijakosea ndugu, Mungu aliwaita wote Adamu. Hivyo mbele za Mungu roho ya mwanaume na ya mwanamke zina thamani sawa, maana wote hawa ni jina lao ni Adamu.

Lakini ukisoma katika Mwanzo 2:7 utaona kuwa, aliyetangulizwa katika ulimwengu huu wa mwili alikuwa ni mwanamume, ambapo Mungu alichukua udongo akaufinyanga na kumtengeneza mwanaume huyu kisha akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, na mwanaume yule akawa nafsi hai.  Baadaye Mungu akampa maagizo mwanaume huyu kuwa anaweza kula matunda yote ya miti katika bustani ya Edeni kasoro tu matunda ya mti ujuzi wa mema na mabaya asiyale, kwa maana siku atakayokula atakufa (Mwanzo 2:16). Pia tunaona katika Mwanzo 2:18-25, kuwa baadaye tunaona Adamu alikuwa mpweke sana kiasi kwamba Mungu akaona kuwa sio vema mwanaume yule aendelee kubaki peke yake, hivyo Mungu akampatia Adamu usingizi na akautoa ubavu mmoja wa Adamu akamtengeneza mwanamke na akamleta kwa Adamu. Adamu alifurahi sana kumpata mwanamke huyu na upweke wake ukaisha.

Mwisho katika Mwanzo 3:1-24, tunaona Nyoka akimdanga mwanamke (Hawa), naye akamuasi Mungu kwa kuamua kuyala matunda yale waliyokatazwa na Mungu kuwa wasiyale, tena akachukua baadhi ya matunda yale akampelekea mumewe (Adamu) naye akayala. Baadaye Mungu alipowaweka kwenye baraza ili wajibu mashtaka yao, hakuna hata mmoja aliyekubali kosa wala kutubu, bali wote wawili walikana makosa yao huku wakitupa lawama kwa wengine (i.e. Mfano Adamu alitupa lawama zake kwa mkewe, huku Hawa akitupa lawama zake kwa Nyoka). Mungu alichukia sana, na ndipo akawapa wale wazazi wetu (Adamu na Hawa). adhabu nyingi zifuatazo:

  1. Wote watakufa
  2. Uadui kati ya mwanadamu na Nyoka
  3. Mwanaume atakula kwa jasho
  4. Mwanamke atazaa kwa uchungu
  5. Mwanamke atatawaliwa na mumewe

Baadae Mungu akawafukuza Adamu na Hawa watoke bustanini Edeni, na akaweka malaika wawili ili kuilinda bustani ya Edeni. Huu ndio ukawa mwanzo wa mwanadamu kuishi maisha magumu, mabaya, yaliyojaa dhiki, laana, magonjwa na matatizo ya kila namna, yaani matatizo yale yanayoonekana na hata matatizo yale yasiyoonekana.

SWALI: Kwa ugumu huu wa maisha, nani alaumiwe zaidi kati ya Adamu na Hawa?

MASHARTI

  1.  Huu ni mdahalo (Debate), hivyo ni lazima uchague upande mmoja wa kuutetea, aidha upande unaosema kuwa Adamu ndiye anayepaswa kulaumiwa zaidi (TIMU EVA) au upande unaosema kuwa Hawa/Eva ndiye anayepaswa kulaumiwa zaidi (TIMU ADAMU). Na kila utakapochangia ni lazima uanze kutukumbusha Timu yako.
  2. Sio lazima uwe mwanaume ndio uwe timu Adamu, unaweza ukawa mwanamke na ukawa timu Adamu. Pia sio lazima uwe mwanamke ndio uwe timu Hawa, unaweza ukawa mwanaume na ukawa timu Hawa.

KARIBU SANA TUANZE MJADALA WETU.

PROSPER HABONA
Moderador
Entrou: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-13 07:36:20

TIMU EVA HAPA: Mtumishi Suzan ameuliza kuwa je, familia inaweza kuwa nchi?  

JIBU: NDIO

Kwa wasomaji wa Biblia wanaelewa hili vizuri kabisa, ngoja tuangalie mifano ifuatayo:

  1. Nchi ya kwanza ilianza na familia moja tu ya Adamu
  2. Baadae Mungu akaua vyote kwa gharika, kisha ikabaki familia ya Nuhu tu, hivyo nchi nzima ilikuwa ni familia ya Nuhu tu.
  3. Nani asiyejua kuwa nchi ya Israel yote ni familia ya Yakobo? Kwa hiyo mtumishi Suzan, familia ndio inayounda nchi na ndio nchi yenyewe. Ndio maana Shetani akitaka kuharibu nchi huwa anaharibu familia na nchi inaharibika.

 

tabitha Prosper
Membro
Entrou: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-15 11:10:39

TIMU ADAMU NIMERUDI TENAA

timu EVA naona mnapambana kweli kutetea makosa yenu aliyoyaamua na kuyafanya eva

tabitha Prosper
Membro
Entrou: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-15 11:14:35

ni hakika na kweli timu Eva kwa Mwl Prosper kutufundisha lakin katika maana yako hyo hyo nakuomba utuelezee ktk upande wa Eva imechangia vipi Sasa ktk familia ya ADAMU ikiwa makosa Ni ya Eva???

Philip Nshekanabo
Membro
Entrou: 2021-09-15 16:12:15
2021-10-17 14:39:42

bwana apew sifa wapendwa Yan apo m naona Eva our mama kwa kweli ndo alaumiwe kwa sabab alimsha mumew Adam tunda na m naswali apa je Adam acnge kula ingekuaje

PROSPER HABONA
Moderador
Entrou: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-17 14:50:42

Timu Eva Nimerudi: Nina swali moja tu kwa Philip, kwa tafsiri rahisi Hawa na shetani ni waalifu na Adamu ndiye aliyepewa mamlaka ya kusimamia sheria (polisi), Sasa je tuwalaumu wahalifu au tuwalaumu polisi?

Philip Nshekanabo
Membro
Entrou: 2021-09-15 16:12:15
2021-10-17 14:57:29

Bwana apew sifa guys uwez zuia mvua isinyeshe Ila unaweza kujuzuia we usinyeshew nazan utakuwa umenielewa kaka

tabitha Prosper
Membro
Entrou: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-18 20:05:13

Sanaaaaaaa,timu EVA hawawez kuzuia mvua kunyesha Kama wakiweza watuambie wangewezaje kwa Eva wao

Philip Nshekanabo
Membro
Entrou: 2021-09-15 16:12:15
2021-10-19 03:49:07

bwana apew sifa wapendwa jamn mdahalo wetu auishi tunapenda tujue nan alaumiwe

tabitha Prosper
Membro
Entrou: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-19 17:56:36

wa kulaumiwa Ni Eva anaepinga atoe sababu isiyopingika na sisi timu Adamu