JE NANI ALAUMIWE ZAIDI KATI YA ADAMU NA HAWA?

GOSPEL PREACHER
Moderator
Kayıt: 2021-08-24 06:51:00
2021-10-05 18:25:35

KARIBU SANA KATIKA MDAHALO WETU:

UTANGULIZI: Biblia inatufundisha kuwa Mungu ni mwema (Zaburi 106:1) tena huwa anatuwazia mawazo mema na ya amani tena ni mawazo ya kutupatia tumaini siku zetu za mwisho(Yeremia 29:11). Ndio maana lengo lake hasa la uumbaji lilikuwa ni kutengeneza koloni lingine la mbinguni (Dunia), na katika koloni hili amuweke mwanadamu awe kiongozi (Gavana) wa koloni hili. Ukisoma mwanzo 1:1-31) utaona kuwa Mungu aliandaa mazingira bora sana ili huyu mwanadamu aishi maisha mazuri na ya furaha tena ya kifalme (akiwa mtawala). Mwanzo 5:1-2 na Mwanzo 1:27, inaonyesha wazi kuwa hapo Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke katika siku moja (i.e. tukio hili lilifanyika katika ulimwengu wa roho), tena akawabariki na akawaita jina lao Adamu, ndio sijakosea ndugu, Mungu aliwaita wote Adamu. Hivyo mbele za Mungu roho ya mwanaume na ya mwanamke zina thamani sawa, maana wote hawa ni jina lao ni Adamu.

Lakini ukisoma katika Mwanzo 2:7 utaona kuwa, aliyetangulizwa katika ulimwengu huu wa mwili alikuwa ni mwanamume, ambapo Mungu alichukua udongo akaufinyanga na kumtengeneza mwanaume huyu kisha akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, na mwanaume yule akawa nafsi hai.  Baadaye Mungu akampa maagizo mwanaume huyu kuwa anaweza kula matunda yote ya miti katika bustani ya Edeni kasoro tu matunda ya mti ujuzi wa mema na mabaya asiyale, kwa maana siku atakayokula atakufa (Mwanzo 2:16). Pia tunaona katika Mwanzo 2:18-25, kuwa baadaye tunaona Adamu alikuwa mpweke sana kiasi kwamba Mungu akaona kuwa sio vema mwanaume yule aendelee kubaki peke yake, hivyo Mungu akampatia Adamu usingizi na akautoa ubavu mmoja wa Adamu akamtengeneza mwanamke na akamleta kwa Adamu. Adamu alifurahi sana kumpata mwanamke huyu na upweke wake ukaisha.

Mwisho katika Mwanzo 3:1-24, tunaona Nyoka akimdanga mwanamke (Hawa), naye akamuasi Mungu kwa kuamua kuyala matunda yale waliyokatazwa na Mungu kuwa wasiyale, tena akachukua baadhi ya matunda yale akampelekea mumewe (Adamu) naye akayala. Baadaye Mungu alipowaweka kwenye baraza ili wajibu mashtaka yao, hakuna hata mmoja aliyekubali kosa wala kutubu, bali wote wawili walikana makosa yao huku wakitupa lawama kwa wengine (i.e. Mfano Adamu alitupa lawama zake kwa mkewe, huku Hawa akitupa lawama zake kwa Nyoka). Mungu alichukia sana, na ndipo akawapa wale wazazi wetu (Adamu na Hawa). adhabu nyingi zifuatazo:

  1. Wote watakufa
  2. Uadui kati ya mwanadamu na Nyoka
  3. Mwanaume atakula kwa jasho
  4. Mwanamke atazaa kwa uchungu
  5. Mwanamke atatawaliwa na mumewe

Baadae Mungu akawafukuza Adamu na Hawa watoke bustanini Edeni, na akaweka malaika wawili ili kuilinda bustani ya Edeni. Huu ndio ukawa mwanzo wa mwanadamu kuishi maisha magumu, mabaya, yaliyojaa dhiki, laana, magonjwa na matatizo ya kila namna, yaani matatizo yale yanayoonekana na hata matatizo yale yasiyoonekana.

SWALI: Kwa ugumu huu wa maisha, nani alaumiwe zaidi kati ya Adamu na Hawa?

MASHARTI

  1.  Huu ni mdahalo (Debate), hivyo ni lazima uchague upande mmoja wa kuutetea, aidha upande unaosema kuwa Adamu ndiye anayepaswa kulaumiwa zaidi (TIMU EVA) au upande unaosema kuwa Hawa/Eva ndiye anayepaswa kulaumiwa zaidi (TIMU ADAMU). Na kila utakapochangia ni lazima uanze kutukumbusha Timu yako.
  2. Sio lazima uwe mwanaume ndio uwe timu Adamu, unaweza ukawa mwanamke na ukawa timu Adamu. Pia sio lazima uwe mwanamke ndio uwe timu Hawa, unaweza ukawa mwanaume na ukawa timu Hawa.

KARIBU SANA TUANZE MJADALA WETU.

PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-07 19:11:22

TIMU EVA HAPA: Bwana asifiwe! Mada hii nimeipenda mno, Kwan mtazamo wangu, ninaona kuwa makosa yote yaani 100% ni ya Adamu maana yeye ndiye alikuwa meneja/gavana wa bustani ile. Ndio Mungu alipofika Edeni wala hakuanza kumuita Eva, bali alimuita Adamu. 

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-07 19:23:55

Amani ya KRISTO YESU NAWATAKIA SANA WATUMISHI WA BWANA.

naitwa tabitha Prosper nimeipenda sana mada kwakweli na nimefurah sana kupata nafasi ya kushiriki

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-07 19:28:56

TIMU ADAMU HAPA  mwanamke ndio mwenye makosa kwann ashindwe kutii mafundisho yangu Kama aliyetolewa ktk ubavu wangu

Justine Johnson
Member
Kayıt: 2021-08-27 06:35:50
2021-10-07 19:52:06

Naungana na mada nikiwa TIMU ADAMU: Makosa ni ya mwanamke, kwa kuwa

  1. Hakusikiliza maagizo ya mumewe kuwa asiliye Yale matunda
  2. Alisikia maneno ya Shetani na akayatekeleza bila kwenda kuyahakikisha kwa mumewe ili ajue Kama ni ya kweli 
PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-07 20:04:50

TIMU EVA nimerudi Tena: Nimependa majibu ya tabitha na ya Justine, lakini naona wamesahau kuwa jeshi la polisi kwa ajili ya kudhibiti wale wasiofuata sheria. Hivyo lilikuwa ni jukumu la Adamu kuunda mfumo ambao ungeweza kumdhibiti mkewe na kumfanya afuate maagizo ya Mungu.

Na huu ndio ushauri wangu kwa wanaume wenzangu, tunapaswa kutengeneza mfumo wa kipolisi ndani ya familia zetu.

MUHIMU: MFUMO HUU WA KIPOLISI UWE ULIOJAA UPENDO NA MAOMBI, ninawahakikishia kuwa wake pamoja na watoto wote watafuata tu sheria za Mungu ambazo tunazowafundisha.

Nitarudi Tena.

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-07 20:21:40

TIMU ADAMU NIMELUDI TENAAA

AMAN YA KRISTO IKUTUNZE.

AHSANTE MR PROSPER Kwa majibu mazuriii yaliyojaa hekima sana,lakin haifuti Kama makosa ya mwanamke ndio yake.

Alivyoelezwa na kudanganywa na shetani kwann hakwenda kwanza kumshirikisha mtawala wake?

Nakuomba unijibu kwanza hili Mtumishi wa BWANA

GOSPEL PREACHER
Moderator
Kayıt: 2021-08-24 06:51:00
2021-10-08 13:16:33

Aiseee naona mdahalo unazidi kunoga, kwa kuwa mimi ndio mtoa mada hivyo si upande wa kuchagua, ila nachombeza tu. Nimevutiwa sana maoni ya tabitha kwa kweli Mungu akubariki sana, Ila nakukumbusha tu mtumishi kuwa kipindi hicho Mungu alikuwa bado hajasema kuwa Adamu amtawalawe mkewe.

Au chombezo langu limewasaidia TIMU EVA?

PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-08 18:02:47

TIMU EVA HAPA: Nimependa pia swali zuri la tabitha, ameendelea kumlaumu Eva kwa kukokumshirikisha mumewe Adamu. Ingawa Biblia haionyesha wazi lakini naamini kabisa huenda Adamu hakuwa na mahusiano ya karibu na ya kirafiki kwa mkewe. Yaani ni miongoni mwa wale wanaume ambao wanaogopwa na wake badala ya kuheshiwa. Sasa unafikiri mke atakuwaje muwazi mbele zake?

Jambo la kujiuliza ni hili kwa nini Adamu amuache mkewe peke yake? Siku zote ni jukumu la mume kujaza nafasi yote ndani ya moyo wa mwanamke, na Kama mwanaume hatafanya hivi, basi Shetani ataijaza nafasi hiyo. Na hili likitokea basi ndoa itakuwa chungu sana au itavunjika kabisa.

PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-08 18:21:13

TIMU EVA NIMERUDI TENA: Kwa kuwa Yesu Kristo alifundisha kwa mifano, basi ngoja nami nifundishe kwa mfano.

Kwenye Kijiji kimoja kulikuwa na mti mdogo wa matunda, lakini siku moja watu walikuta majani ya mti ule yamenyauka, kwa kuwa ukame ulikiandama Kijiji kile. Mwisho mti ule ulikauka kabisa. Swali: je tuyalaumu majani kuwa ndio yana makosa au tuilaumu mizizi?

Naamini jibu unalo, hivyo basi kitendo cha Eva kula matunda Yale ni matokeo tu na wala sio chanzo chenyewe cha tatizo. Yaani ni sawa na majani kukauka. Tatizo hasa ni Adamu, yeye kukauka kwake na kupelekea ashindwe kupeleka virutubisho vya kiroho na vya kihisia kwa mkewe, ndiko kulikopelea mkewe kukauka na kumfanya awe rahisi kutekwa na Shetani.

Wanaume tunapaswa kusimama katika nafasi zetu vizuri. Tukiyumba basi nyumba zetu zitayumba pia.

MBARIKIWE SANA, NITARUDI TENA.

Dorcas Juma
Member
Kayıt: 2021-08-19 20:33:08
2021-10-08 18:21:45

Bwana Yesu apewe sifa, Mimi ni team EVA, maada hii nimeipenda Sana na itasaidia kupanua uelewa wangu. Hapo naona ambaye anatakiwa kulaumiwa zaidi ni ADAMU kwanini nasema alaumiwe ADAMU?.? Alaumiwe kwa sababu adamu ndo aliyefanya agano na Mungu, kwahiyo adamu angeendelea kumuonya vizuri mkewe, so mim naona mwenye makosa ni ADAMU.

John Kennedy
Member
Kayıt: 2021-08-27 06:11:22
2021-10-08 18:29:43

BWANA YESU ASIFIWE! TIMU ADAMU HAPA: Kwanza namshukuru Mungu kwa mada nzuri ya leo.

Mtumishi wa Mungu Prosper ubarikiwe kwa maoni mazuri, ila sikubaliani na wewe kwa Jambo hili kuwa Adamu hakumfundisha mkewe vizuri. Ukweli ni kwamba Adamu alijitahidi sana lakini tatizo kuna wanawake ni wabishi, majeuri na hawataki kabisa kusikiliza waume zao. Huenda wameirithi tabia hii kwa mama yetu Eva.

Kwanza ukisoma Mwanzo 3 yote utaona kuwa Eva akimueleza Shetani kuwa wamekatazwa kula matunda ya mti wa ujuzi na mema na mabaya. Swali je Eva alifundishwa Jambo hili na Mungu au na Adamu? Bila shaka alifundishwa na Adamu.

Hivyo Adamu alitimiza wajibu wake lakini Eva ndiye mwenye makosa kwa kufanya ujeuri kwenda kinyume na MAFUNDISHO ya mumewe.

Au mlihitaji Adamu amlazimishe kwa nguvu mkewe Eva ili afuate aliyomfundisha?

John Kennedy
Member
Kayıt: 2021-08-27 06:11:22
2021-10-08 18:33:43

Naomba Timu Eva, hasa mtumishi Prosper na wenzako mnijibu hili?

PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-08 18:47:21

TIMU EVA HAPA: Asante kwa swali zuri mtumishi John, umeuliza kuwa je tulihitaji Adamu atumie nguvu ili kumfanya mkewe afuate sheria aliyomfundisha? Jibu la swali lako ni jepesi sana nalo ni NDIO.

Ndio, Adamu alipaswa kutumia nguvu, na Kama angetumia nguvu zifuatazo basi kamwe Eva asingeangukia kwenye mtego wa Shetani, nguvu hizo ni:

  1. Nguvu ya upendo: Mke asipouona upendo halisi kwa mumewe, mke huyu kamwe hatafuata sheria za mumewe. Hivyo Adamu alipaswa kutumia nguvu ya upendo.
  2. Nguvu ya urafiki: Bila ya mume kuwa rafiki wa mkewe basi mwanamke hatakuwa muwazi kwake. Adamu alipaswa kutumia nguvu kubwa ili kumfanya mkewe awe rafiki yake, na angefanya hivi basi Eva angekimbilia kwa Adamu ili kuthibitisha ukweli wa maneno ya Shetani. Tatizo kipindi hicho kulikuwa na watu wawili Sasa Kama Adamu hakuwa rafiki wa mkewe, unafikiri kwa nini Eva asiwe rafiki wa shetani?
  3. Nguvu ya uongozi: kiongozi anapaswa sio tu kutoa maagizo bali zaidi sana ni kusimamia utekelezaji wa maagizo hayo. Hivyo Adamu alipaswa kutumia nguvu zaidi ya uongozi.
Dorcas Juma
Member
Kayıt: 2021-08-19 20:33:08
2021-10-08 19:10:28

Team Eva mtumishi john nitakijibu Kama ifuatavyo, Adamu sio kwamba anatakiwa kutumia nguvu ili kumuelekeza mkewe hapana Bali napo tunaangalia aliyeweka agano na Mungu ni nani? Mfano dhahiri soma 1wafalme 13:1-34 utaona habari za nabii kijana na nabii Mzee, so adamu asingekula hilo tunda hata wasingejihisi Kama wapo uchuchi ila kwa kuwa hata aliyeweka agano na Mungu na yeye aliamua kula tunda ndo maana yote hayo yalitokea.

Suzan John
Member
Kayıt: 2021-08-27 06:29:27
2021-10-09 14:56:36

Nachangia nikiwa Timu Adamu: Nina swali moja kwa Dorcas, je yule nabii mkubwa ambaye alimpotosha yule nabii mdogo, yeye hakuhesabiwa kosa?

Biblia inasema kuwa, majaribu hayana budi kuja ila ole wake yeye ambaye majaribu huja kwa sababu yake. Yaani ole wake yule ayaletaye. Hivyo mwenye ole kubwa ni yule nabii mkubwa ambaye alileta jaribu kwa yule nabii mdogo. Hivyohivyo pia, mwenye ole kubwa ni kwa EVA ambaye ndiye aliyeleta jaribu kwa ADAMU. 

Nawasilisha.

Suzan John
Member
Kayıt: 2021-08-27 06:29:27
2021-10-09 15:02:24

Nimerudi Tena: ukweli ni kwamba EVA alikosa utii kwa Mungu na kwa mumewe. Pia yeye ndiye alimuudhi Mungu sana, ndio maana wanawake tumepewa adhabu kubwa kuliko wanaume. Ukiacha, kifo, uadui kati yetu na nyoka pamoja na kuzaa kwa uchungu; lakini pia tukaongezewa kutawaliwa na waume zetu.

Lakini wanaume wao wanazo tatu tu yaani: Kifo, uadui kati yao na nyoka pamoja na kula kwa jasho tu.

Hivyo basi aliyepewa adhabu kubwa ndio mwenye makosa zaidi.

Paul Ngemy
Member
Kayıt: 2021-09-15 18:03:22
2021-10-09 15:44:35

Kwa kweli mada ni tamu, nimefikiria sana nimeona TIMU EVA ndiyo inakosha.

Suzan umejitahidi kweli kutoa hoja nzuri, lakini hebu tujiulize pamoja swali: je tusiwalaumu polisi pale uhalifu unapoongezeka kwenye jamii? Bila shaka jibu ni hapana, tunapaswa kuwalaumu Tena sana, maana ni jukumu lao kuzuia na kupambana na uhalifu. 

Kwa mtazamo huo huo ndio tunaomlaumu Adamu maana yeye ndiye aliyepewa sheria pamoja na mamlaka ya kusimamia utekelezaji wake.

  • Sasa kwa nini aliamua kuruhusu uhalifu ule mkubwa utokee kwenye lindo lake?
  • Tena mbaya zaidi, na yeye pia akajiunga na uhalifu ule kwa yeye kuamua kula matunda yale. Kwa nini asilaumiwe?

Yaani ni sawa na polisi kukubali KUPOKEA sehemu ya fedha zilizoibwa, tena kutoka mkononi mwa muhalifu mwenyewe.

Naungana mkono na mtumishi Prosper, kuwa 100% ya makosa ni ya Adamu mwenyewe. Huo ndio ukweli japokuwa mchungu.

 

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-13 05:38:50

 Amani  Kristo Yesu nawatakia watumishi wa Bwana.ndio mmeshaliza time EVA hoja na maswal yenu watumishi

Kwa utambulisho ni timu ADAMU nimeludi tena nimesoma kwa makini sana majibu ya timu Eva.

Lakin nawaomba niwakumbushe jambo unajua hata uwepo wenu mm adamu sikuuona kwangu ila Mungu wa mbinguni ndio aliona ni vyema uje ukawe msaidizi wangu,swali la kujiuliza kabla haukuletwa ktk bustani mbna hakuna kilichokwenda tofauti wala kuyumba wala sheria ya Mungu kuvunjwa,naungana na John Kennedy wanawake ni wajeuri na wabishi haelewi hadi aone,Mtumishi PROSPER  NAKUOMBA UNIJIBU SWALI HILI NI KWELI MM ADAMU SINA UPENDO. KWA EVA?? kama. Ni hivyo kwann kumuita hadi jina na hata kusema ni nyama katika nyama yangu ni mfupa katka mfupa wangu inasaidia nn yote hayo na je haionyeshi utawala wangu kwa Eva au msaidizi hatawaliwi na kuongozwa?? 

Jukum la Nani kuzingatia Sheria Zaid???

Na kwnn kuchuma kabla ya kuja kuniuliza?

Tuashum alisahau Eva maagizo

Lakin nawaomba mnijibu vyema sana kuhusu hili swali

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-13 05:45:02

kwann aliruhusu tamaa kumuingia na kushindwa kuizibiti hata kuruhusu kula ikiwa alishasema Mungu alisema inamaanisha anatambua na kujua? Tufundshane vyema hapo timu Eva popote Mlipo mteteen eva wenu

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-13 05:48:47

Mtumishi Paul nakuomba unifafanulie kivipi niliruhusu?

PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-13 05:51:22

Asante kwa maswali mazuri tabitha kwa hakika nimeyapenda. Unajua nilivyoona kimya nikajua timu Adamu mmeshakubali kushindwa vita. Kumbe bado kuna mwanajeshi mmoja hajakubali eeeh. Basi ngoja nijibu hoja zako ili nawe ukubali kama wenzio.

PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-13 05:58:42

Mtumishi tabitha umeuliza maswali yafuatayo:

Je Adamu alikuwa hampendi Eva? Jibu: alikuwa akimpenda mkewe tena sana. Tatizo ni je upendo huu mke aliujua na kuuona? Kumpenda tu mwanamke haitoshi Kama hautamuonyesha na kuhakikisha kuwa ameona na kujua kuwa anapendwa.

Pia ukauliza: jukumu la nani kuzingatia sheria? Ni jukumu la wote waliopewa sheria, lakini ni jukumu la kiongozi kuhakikisha sheria zinafuatwa.

Kwa nini asijekuuliza? Hili ndilo kosa alilofanya Eva, lakini lilichochewa au lilisababishwa na Adamu. Atamwelezaje mwanaume ambaye Hana uhakika na upendo wake? Atamwelezaje mwanaume ambaye hana uhusiano nae wa kirafiki? Ndio naona ingekuwa vyema kama Eva angemtupia lawama zake mumewe Adamu na sio Shetani, maana Shetani alipewa nafasi na Adamu; INGAWA JAMBO ZURI ZAIDI LILIKUWA NI KUTUBU ILI MUNGU AWASAMEHE.

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-13 06:01:49

ni Kweli kwamba mtumishi paul unasahau kabisaa kwamba mimi siye niliyeruhusu uhalifu kutokea na sikuungana nae,nakuomba nikuulize swali ni jambo baya kumuamini Eva Wang nikiamini hawezi kunifanya nidhurike kwa jambo lolote Kama msaidizi wangu na ulitaka niwe nae kila sehemu kuimalisha uharifu usitokee???

Kwahiyo hata kwako utakuja umlinde na kumfatilia kila sehemu atakayokuwa anakwenda? Utaweza???? 

Kama unaweza yanini kumfundisha lengo linakuwa lipi kwako kwa mwanamke tofaut na zimsaidie kushinda anapokuwa yupo mwenyew kushinda vishawishi. 

Unajua hata kwa Mungu wetu aketiye Enzin katupatia Sheria zituongoze na kushinda hila za shetani sasa tukienda nazo tofauti kosa la Mungu au sisi bibi harus wa KRISTO?? 

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-13 06:09:17

yaan Timu Adamu hatutakuja tuishiwe Point kwasababu Adam ni mwanaume ni kichwa cha Kristo utofaut ni kwamba alikula akijua kuwa hata alipotambua mkewe alikula aliamini mkewe hawezi kwenda kinyume na mapenz ya Mungu Kama msaidizi wake

PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-13 06:12:15

Ni kweli Eva aliingiwa na tamaa, hilo hatulipingi, TIMU EVA tunachosema ni hiki, Adamu ndio chanzo cha tamaa hii. Kwa nini asiujaze moyo wa mkewe? Kumbuka moyo wa mwanamke haupaswi kubaki tupu, la sivyo Shetani ataujaza tu. Adamu Kama angeujaza moyo wa mkewe, upendo, urafiki, utii, trust n.k, kwa hakika Eva angelishinda jaribu lile la Shetani kirahisi sana.

TIMU ADAMU, TUMEELEWANA?

PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-13 06:16:44

Sasa naona mtumishi tabitha umeamua kujiunga na TIMU EVA maana hata sisi ndicho tunachomlaumu Adamu, kwa nini ashiriki uhalifu ule? Kwa hili tu alipoteza sifa za kuwa kiongozi. Adamu alipaswa asile matunda Yale, na badala yake yeye Kama kuhani wa familia, alipaswa kuomba msamaha kwa Mungu kwa uovu uliofanywa ndani ya familia yake. Mungu ni wa rehema huenda angeisamehe familia ile.

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-13 06:18:52

Kumbe Kama adamu nilitakiwa kuzisimamia si ndio kumbe hamna tofauti kwa Mungu Wetu wa Mbingun anavyofanya kwetu,hivyo makosa aliyotenda Eva unamaanisha kwamba sikumuweka huru juu ya upendo wangu kwake kwa sehemu Gani mnionyeshe timu Eva

Paul Ngemy
Member
Kayıt: 2021-09-15 18:03:22
2021-10-13 06:26:25

TIMU EVA HAPA: Mtumishi tabitha umeuliza swali zuri, kuwa kivipi Adamu aliruhusu? Siku zote ukishindwa kupanga unakuwa umepanga kushindwa. Kwa hiyo kwa Adamu kushindwa kupanga mpango mzuri wa kiroho na wa kiupendo, basi aliruhusu uangamivu wa Shetani kuathiri familia yake. 

Pia umeuliza kuwa je naweza kumfuatilia mke wangu kote anakokwenda? Jibu ni ndio: nikijenga mfumo mzuri moyoni mwa mke wangu, popote kule ambako atakapokutana na jaribu la Shetani, basi ataisikia sauti yangu ikimsemesha moyoni mwake kuwa, mke wangu ninakupenda, ukifanya uovu huu utaupoteza upendo wangu, na mbaya zaidi itakuwa dhambi mbele za Mungu.

Kengele hii itamfanya ashinde jaribu lolote lile, na bila shaka huu ndio mfumo wa kipolisi anaouzungumzia mtumishi Prosper.

TIMU ADAMU  KARIBUNI KWA MASWALI YA NYONGEZA.

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-13 06:27:01

Hapana mtumwa tabitha ni mwaminifu hadi kufa Mtumishi Prosper nipo timu Adamu tu.nakuomba nikujibu swali lako kwamba inaonekana hakujaza tamaa ktk moyo wa Eva hadi shetani kupata nafasi Mimi ninakataa ni hapana.

nakuomba nikuulize swali unaweza kuujaza moyo wa mwanamke Kwa mambo hayo?

PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-13 06:34:08

Ndio ninaweza mtumishi, kwa kuwa nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu (Wafilipi 4:13).

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-13 06:38:13

yaan timu adamu tupo juu sanaa lazima mkubali makosa ni yenu to, maandiko yananiambia katka mithali maandalio ya moyo ni ya mwanadam lakin jawab linatoka kwa Bwana.mtumishi Prosper na Paul mnachonionyesha ni kwamba nyinyi mnafanya uwekezaji tu suala la kutenda ni la mwanamke kwakuwa yeye amepewa hali ya utendaji ndani yake kwa adam yeye ni mwekezaji sasa mnasemaje adamu hakuweleza ikiwa mwanamke katk kujieleza alisema Mungu alisema tusiyale unamaanisha kwamba uwekezaji wa adamu ulikuwa wa matunda tu waliyokatazwa? 

Suzan John
Member
Kayıt: 2021-08-27 06:29:27
2021-10-13 06:41:52

TIMU ADAMU NIMERUD: Mungu akubariki sana tabitha umetoa hoja nzuri, ingawa timu EVA wanajifanya hawataki kuelewa. Mwanamke mwenzetu Hawa, ndiye wa kulaumiwa. Maana mwanaume ni kichwa ndio lakini mwanamke ndio moyo familia. Ni jukumu la mwanamke kumlinda mumewe kwa maombi, na sio kumshawishi mumewe kufanya uovu Kama Hawa alivyofanya kwa Adamu, Sarah alivyofanya kwa Ibrahimu.

Ukweli mwanume anahitaji neema ya Mungu tu Kama aliyoipata Ayubu, ili kuweza kuushinda ushawishi wa uovu kutoka kwa mkewe. Hivyo Hawa ndiye wa kulaumiwa.

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-13 06:44:20

unayaweza ndio tena yote katika uwekezaji tu na sio utendaji kwa maana hilo lipo ndani ya mwanamke,kosa ktk hayo yote ypo ktk utendaj au uwekezaji??

Timu Eva nawaomba mnijibu kwakweli muache kuficha makosa yenu timu Eva 

PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-13 06:49:52

Ninafurahi ni kwamba mtumishi tabitha ameanza kuelewa na muda si mrefu utabadili timu. Ngoja nikueleze zaidi. Hakuna utendaji bila uwekezaji. Yaani hata Mungu aliwekeza kwanza katika uumbaji ndio akamweka mwanadamu afanye utendaji.

Tunachomlaumu Adamu ni kwamba yeye alifanya tu uwekezaji katika kumfundisha mkewe sheria za Mungu, lakini hakufanya utendaji katika kusimamia na kuhakikisha kuwa sheria za Mungu zinafuatwa.

 

Suzan John
Member
Kayıt: 2021-08-27 06:29:27
2021-10-13 06:56:24

Naona mpaka Sasa timu EVA mnabebwa na pointi moja ya mtumishi Prosper kuwa Adamu alipaswa kutengeneza mfumo wa kipolisi ili kumlinda mkewe. HEBU TIMU EVA NAOMBA MNIJIBU: Ni nchi gani ambayo mifumo ya kipolisi ya nchi hiyo imefanikiwa kuzuia uhalifu kwa 100% ?

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-13 07:01:40

waooooooh mtujibu sasa tuwasahihishe makosa ya Eva wenu

Safiiii ubarikiwe Sana mtumishi susan John 

tabitha Prosper
Member
Kayıt: 2021-08-18 11:17:07
2021-10-13 07:04:28

swali la nyongeza mtuelekeze katka utendaji na uwekezaji kwa adam na Eva timu Eva, tuelewane hapo

PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-13 07:08:12

Naona tabitha amepiga simu kambi ya Timu Adamu ili aletewe msaada, na mtumishi Suzan ametumwa kuokoa jahazi. Ok karibu sana mtumishi Suzan, ngoja nijibu hoja na maswali yako. 

PROSPER HABONA
Moderator
Kayıt: 2021-08-18 21:09:17
2021-10-13 07:13:51

TIMU EVA HAPA: Mtumishi wa Mungu Suzan ameuliza kuwa je serikali ya nchi gani ambayo mfumo wake wa kipolisi umeweza kuzuia uhalifu kwa 100%?

Jibu: kwa kuwa kiwango cha chini cha watu katika serikali ni watu wawili (mtawala na mtawaliwa), basi zipo serikali nyingi sana zilizofanikiwa katika hili, muda hautoshi kuziandika zote. LAKINI MFANO MZURI NI SERIKALI YA NCHI YA FAMILIA YANGU, wala sijivuni bali utukufu namrudishia Mungu.

Suzan John
Member
Kayıt: 2021-08-27 06:29:27
2021-10-13 07:28:26

Duuuuuuh, familia imekuwa nchi tena?