NDOA AU BILA NDOA, LIPI BORA ZAIDI KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU?

GOSPEL PREACHER
Moderator
Lid geworden: 2021-08-24 06:51:00
2021-09-01 18:01:59

KARIBU SANA KATIKA MDAHALO WETU:

UTANGULIZI: Katika kitabu cha Mithali 18:22, Biblia inasema kuwa, “Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana. Hivyo mke ni kitu chema kutoka kwa MUNGU”. Lakini pia ukisoma Biblia kwa kina utaona kuwa hata Ruthu naye alipopata mume bora na tajiri aliyeitwa Boazi ndipo historia ya maisha yake ikawa nzuri, maana alitoka kuwa masikini akawa tajiri, tena mpaka akapata nafasi ya kuingia katika ukoo wa Yesu Kristo (Ruth 4:9-22 na Mathayo 1:1-17). HIVYO NI WAZI KUWA BIBLIA INARUHUSU KUOA NA KUOLEWA.

Pamoja na hayo, katika kitabu cha 1 Wakorintho 7:7-8 tunaona mtume Paulo, kwa uongozi wa Roho Mtakatifu akisema kuwa, 7 ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi. 8Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo”. HIVYO PIA NI WAZI KUWA BIBLIA INARUHUSU PIA KUTOKUOA AU KUTOKUOLEWA.

MADA YETU NI HII:

Ingawa ni kweli kuwa inawezekana kabisa kumtumikia Mungu ukiwa kwenye ndoa au hata ukiwa hauna ndoa, lakini je, kwa mtazamo wako unaona kuwa wapi ni rahisi zaidi na penye uhuru wa kumtumikia Mungu kwa nguvu zote ili uweze kupata taji ing’aayo mbinguni, je, ni ukiwa kwenye ndoa (yaani ukiwa umeoa au umeolewa) ama ukiwa hauna ndoa (yaani ukiwa hujaoa au kuolewa)?

ANGALIZO:

(1). Huu ni mdahalo (Debate), hivyo ni lazima uchague upande mmoja wa kuutetea, aidha upande wa ndoa (TIMU SULEMANI) au upande wa kutokuwa na ndoa (TIMU PAULO). Na kila utakapochangia ni lazima uanze kutukumbusha Timu yako.

  1. Ukiwa Timu Sulemani: utakuwa unatetea kuwa, ukiwa ndani ya ndoa (yaani ukiwa umeoa au kuolewa), ndio rahisi zaidi kumtumikia Mungu tena kwa uhuru kiasi cha kupata taji ing’aayo.
  2. Ukiwa Timu Paulo: utakuwa unatetea kuwa, ukiwa hauna ndoa (yaani ukiwa haujaoa au kuolewa), ndio rahisi zaidi kumtumikia Mungu tena kwa uhuru kiasi cha kupata taji ing’aayo.

(2). Haijalishi hali yako ya sasa ya ndoa, upo huru kuchagua upande wowote ule upendao, kwa mfano:

  1. Sio lazima uwe ndani ya ndoa ndio uwe Timu Sulemani, unaweza ukawa bado haujaoa au hujaolewa lakini ukaamua kutetea Timu Sulemani.
  2. Pia sio lazima uwe hauna ndoa ndio uwe Timu Paulo, unaweza ukawa umeoa au umeolewa lakini ukaamua kutetea Timu Paulo.

(3). Mjadala huu ni kwa ajili ya kupanua tu uelewa wa neno la MUNGU.

  1. Hivyo hata ukiwa Timu Sulemani haimaanishi kuwa unalo wazo la kuja kuingia katika ndoa hapo baadae, hii ni hiari ya mtu kadri Roho wa Bwana anavyomjalia.
  2. Pia hata ukiwa timu Paulo haimaanishi kuwa unalo wazo la kutokuingia katika ndoa, hii ni hiari ya mtu kadri Roho wa Bwana anavyomjalia.

KARIBU SANA TUANZE MJADALA WETU.

PROSPER HABONA
Moderator
Lid geworden: 2021-08-18 21:09:17
2021-09-01 18:25:26

Bwana Yesu asifiwe! Nianze kwa kusema kuwa MIMI TIMU PAULO: Ila duuuh! nikiri kuwa mada ni tamu kwelikweli. Unajua ukiwa ndani ya ndoa utakuwa na majukumu ya kufanya kwa mumeo au mkeo, hivyo ni lazima utenge muda na fedha kwa ajili ya kutimiza majukumu hayo. Lakini ukiwa Timu Paulo, basi wewe utakuwa huru kutumia muda wako wote na fedha zako kwa ajili ya BWANA. HIVYO NASAPOTI USHAURI WA PAULO KUWA BORA TUWE KAMA YEYE.

ABELY PATRICK
Member
Lid geworden: 2021-08-21 20:34:28
2021-09-01 19:09:21

Bwana Yesu asifiwe, naungana na mdahalo huu nikiwa kama Team Suleman, nasapoti kuwa ni vizuri sisi tuliookoka kuoa ili kujitenga na mambo mbalimbali kama; tamaa za mwili. kupoteza muda kufanya kazi za nyumbani Na Kukosa Hata Wa Kukufariji Unapochoka Kwa Huduma Za Kimungu, lakini pia agizo la MUNGU alilosema ZAENI MKAIJAZE DUNIA Tutakuwa Hatujalitii, Kwa Ushauri Wangu Ni Vyema Tuoe, Wapendwa Mbarikiwe.

ABELY PATRICK
Member
Lid geworden: 2021-08-21 20:34:28
2021-09-01 19:12:20

PIA, RUTHU 3:1-5
Kisha Naomi Akamwambia Mkwewe, Je! Mwanangu, Si Vizuri Nikutafutie Raha, Ili Upate Mema? Endelea Usome Pote, Utajifunza Kwamba Naomi Aligundua Ili Mkwewe Ruthu Apate Raha Na Mema Katika Maisha Yake Ni Heri Atumie Mbinu Mbadala Ya Kumuozesha Kwa Boazi Pasipo Hata Boazi Kujua, Lakini Sisi Leo Tunajidai Kusema Tusioe Daah Kweli Et Jaman? Maandiko Yanasema Katika #Isaya 4:1 Itafikia Wakati wanawake Saba Watataka Kuolewa Na Mwanaume Mmoja Sasa Subirini Wakati Huo Ufike Nyie Kaeni Na Team Paulo Yenu

John Kennedy
Member
Lid geworden: 2021-08-27 06:11:22
2021-09-01 19:25:16

Wacha weee, kweli Mtumishi Abely ametoa point za ukweli, kutoka moyoni niseme kuwa mada nimeikubali mno, ila mimi ni TIMU PAULO, lakini ngoja nipange point zang vizur, ili nimjibu mtumish Abely kwa kutumia maandiko.

PROSPER HABONA
Moderator
Lid geworden: 2021-08-18 21:09:17
2021-09-01 19:40:20

TIMU PAULO HAPA NIMERUDI TENA: Nashukuru sana mtumishi Abely kwa point nzuri zilizoambatana na maandiko matakatifu. Lakini bado hoja zako hazijitoshelezi sana kuniamisha kutoka TIMU PAULO kuja TIMU SULEMANI, hebu ngoja kwanza nianze kuchambua point zako vizuri.

  1. Mnaoa ili mjitenge na tamaa za kimwili: Hii ni sahihi ingawa sio sahihi zaidi, maana inawezekana kabisa kujitenga na tamaa za kimwili hata kama haujaoa, mfano hai ni Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye hakuoa lakini hakuwahi kuzini wala kuhisiwa anafanya uasherati. Lakini pia wapo wengi tu walioa au kuolewa, lakini bado tamaa za mwili zinawasumbua.
  2. Mnaoa au kuolewa ili kupata wa kukufariji: Faraja hii unaweza usipate kama mke au mume huyo atakuwa pasua kichwa, kumbuka Mithali 21:19 inasema kuwa Afadhali kuishi jangwani, kuliko kukaa na mwanamke mgomvi na msumbufu.
  3. Mnaoa au kuolewa kwa kuwa ni agizo la Mungu: Ni kweli kabisa hili ni agizo la Mungu, lakini pia hata kuwa kama Paulo nalo pia ni agizo la Mungu. Swali ni je, lipi ni muhimu zaidi katika kumtumikia Mungu? Mimi nasema bora uwe kama Paulo, ila kama umeshaoa, basi endelea kubaki timu Sulemani.

NITARUDI TENA BAADAE.

Dorcas Juma
Member
Lid geworden: 2021-08-19 20:33:08
2021-09-01 19:51:08

Bwana Yesu asifiwe, ninawasalimu katika jina la Yesu. Mimi kama Timu Sulemani nitajibu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Katika mdahalo huu napenda kuwasihi wapendwa wenzangu kuwa katika utumishi wa Mungu, inapaswa kuoa au kuolewa, kwa sababu hii usaidia kuepukana na tamaa za mwili.

Leo tunaona watumishi wengi sana wanaanguka katika dhambi kwa sababu ya tamaa za mwili, hivyo basi inatakiwa kuoa au kuolewa ili kuepukana na hizo tamaa. HUO NDIO USHAURI WANGU KWA WATUMISHI.

PROSPER HABONA
Moderator
Lid geworden: 2021-08-18 21:09:17
2021-09-01 20:00:15

Naona Timu Sulemani mmepata mwanachama mwingine DORCAS, kwa kweli amejaribu kutetea kwa point ya tamaa za mwili, nashauri arudie jibu langu la msingi kwa Abeli kuwa unaweza kuzishinda tamaa mwili hata kama hujaoa au kuolewa kama vile Yesu alivyozishinda, pia unaweza ukawa kwenye ndoa na bado tamaa hizi zikawa zinakuendesha mpaka kupelekea wengi kutoka nje ya ndoa zao.

Pia ni kweli watumishi wa Mungu wengi wanaanguka katika tamaa hizi kiasi cha huduma zao kuyumba, lakini ninakuhakikishia kuwa migogoro ya ndoa katika nyumba za watumishi hawa ndio chanzo kikubwa cha kuyumba kwa huduma za watumishi wengi zaidi.

Kwa kuwa nakufahamu hivyo najua kuwa wewe ni muimbaji na kwa sasa bado haujaolewa, sasa pata picha umeolewa halafu mumeo hataki tena uendelee kuwa muimbaji, yaani kila unapoimba yeye anakuvunja moyo tu huku akisema kuwa usimpigie makelele, pia hakuruhusu tena uende kwayani n.k; unafikiri huduma yako itakuaje? Nimeshuhudia wengi wanaume kwa wanawake ambao huduma zao zilikufa kabisa pale walioa au walipoolewa.

HIVYO NINAKUKARIBISHA SANA TIMU PAULO, KWA KUWA NAFASI BADO UNAYO.

ABELY PATRICK
Member
Lid geworden: 2021-08-21 20:34:28
2021-09-01 20:23:48

TIMU SULEMANI NIMERUDI TENA

Asante mtumishi Prosper, ila napenda utambuwe kuwa Paulo Anajua Fika Kwamba, Mungu Anasema Kwenye #Mwanzo 2:18 kuwa, Si Vema Mtu Huyo (adamu) Awe Peke Yake.

SASA HEBU NAOMBA TIMU PAULO MNIJIBU: KAMA ADAMU NA EVA WANGEKUWA TIMU PAULO (yaani wasioe wala kuolewa), SISI LEO TUNGEPATIKANAJE? Na je hata huyo Paulo mwenyewe angezaliwa na nani?

Ni wazi kuwa kama wangekuwa timu Paulo, basi

  1. Mimi Na Wewe Tusingalikuwepo
  2. Hata Paulo Mwenyewe Asingepatikana,

Tukumbuke Kila Alichokiumba Mungu Alikuwa Anaona Ya Kuwa Ni Chema' Je! Kwanini Mwanaume Kukaa Bila Mwanamke Aliona Si Vyema? Mwanadamu Ana Machaguo Mawili Kufanya Kile Anachopenda Pasipo Mungu Kumzuia, Hivyo Paulo Alijachagua Kutushauri/ Kutushawishi Sisi Team Suleman Tuwe Kama Yeye Hapo Sintoweza.

Kwanza Tujue Ya Kuwa Si Kila Ushauri Wa Kimungu Unapaswa Kuutoa Kwa Watu Ambao Hawajakomaa Katika Wokovu (Wagalatia 3:1), Baada Ya Kuona Ushauri Wake Watu Wa Galatia Walikuwa Wameanza Kuupokea Vibaya Ilibidi Kuwafokea Mana Ninaamini Wengine Hawakutaka Kuoa Na Badala Yake Wakawa Wazinzi, Ndipo Paulo Akajitetea Katika Wagalatia 5:7-8, Akatuelewesha Kwamba "kushawishi Kwake (paulo) Hakukutokana Na Alietuita(Mungu). Wapendwa Team Paulo Niwashauri Tena Kama Huna Roho Kama Ya Mtume Paulo Fanya UOE.

PROSPER HABONA
Moderator
Lid geworden: 2021-08-18 21:09:17
2021-09-01 20:37:42

TIMU PAULO HAPA,

Napenda kumjibu Abely kuhusiana na Ruthu, tatizo umeanzia mwishoni mwa historia yake, jaribu kuanza kuisoma historia ya huyu Ruthu tangu mwanzo. Ukifanya hivyo utagundua kuwa kabla ya Boazi, huyu Ruthu alikuwa ameolewa na mtoto wa Naomi. HUENDA Mume huyu wa kwanza wa Ruthu alikuwa ni pasua kichwa tu (ASIYEJALI FAMILIA), maana mpaka anakufa hakuwa ameacha mtoto wala mali yoyote kwa Ruthu, yaani alimuacha Ruthu kwenye umaskini wa kutisha, ndipo Ruthu alipoona hata cha kupoteza ni bora tu amfuate mkwewe Naomi.

SASA UNAFIKIRI KATIKA LINDI LA UMASIKINI HUU WA KUTISHA, ILIKUWA RAHISI KWELI KWA RUTHU KUMTUMIKIA MUNGU KWA UHURU?

Ndugu yangu Abely, ninakuombea Mungu akuepushe na hili, lakini jaribu kuwauliza wale waliopata wake au waume pasua kichwa kama mwanandoa huyu wa awali wa Ruthu ndipo utakapotamani kurudisha muda nyuma ili uwe Timu Paulo, lakini tayari Biblia itakufunga, na ukimwacha mkeo itahesabika kuwa ni dhambi kwako. Matokeo yake ndio wengi hujikuta wakiombeana mmoja atangulie, ili anayebaki arudi Timu Paulo bila kuhesabiwa dhambi.

SASA TABU YOTE YA NINI, HAMIA LEO TIMU PAULO INGALI MUDA UNGALIPO.

PROSPER HABONA
Moderator
Lid geworden: 2021-08-18 21:09:17
2021-09-01 20:56:28

NAONA TIMU PAULO tumetumia muda mwingi kujibu hoja za timu Sulemani, sasa ngoja nichokoze mada kidogo. Ukisoma ile 1 Wakorintho 11:1 Biblia inasema kuwa, Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo. Maneno haya aliyaongea mtume Paulo kuwa tuige mfano wake jinsi anavyomfuata Kristo. 

Sasa najua Yesu Kristo anayo mambo mengi sana ambayo Paulo aliyafuata mfano UTAKATIFU, IMANI, UPENDO n.k; lakini pia usisahau kuwa Bwana wetu Yesu Kristo hakuoa, na Paulo naye akafuata na hili pia, hivyo naye hakuoa. Ndio maana hata nyakati hizi za leo, SISI TIMU PAULO tumeamua kumfuata Paulo kama yeye alivyomfuata Yesu. 

JAMANI TIMU SULEMANI, NI KWELI NINYI HAMTAKI KABISA KUMFUATA YESU KWA JAMBO HILI?

Dorcas Juma
Member
Lid geworden: 2021-08-19 20:33:08
2021-09-01 21:09:38

TEAM SULEIMANI  nimerudi tena, Ni kweli tunaona ni watumishi wengi Sana waliooa au kuolewa wanaanguka katika dhambi, hii inatokea pale watu hawa wanaijua kweli lakini wanaamua kupingana nayo. Tukiangalia katika hivi vitabu viwili WARUMI 1:18 na WAEBRANIA 10:26. Utayakuta ha yo.               

Mimi Dorcas mtumishi wa MUNGU ambaye MUNGU  amenichagua katika huduma ya uimbaji, Ni kweli changamoto katika ndoa zipo nyingi Sana na wengi wao huduma zao hufa pale wanapoolewa. Kama Mimi mtumishi wa MUNGU bado sijaolewa na nipo katika stage ya kuolewa, Hata Biblia inasema  ukiomba kwa jina langu nami nitawapa, so Mimi Kama Mimi nitamuomba MUNGU anipe mume bora na si bora mume na huyo mume awe na hofu ya MUNGU na anaye mjua MUNGU.

PROSPER HABONA
Moderator
Lid geworden: 2021-08-18 21:09:17
2021-09-01 21:14:34

OK DORCAS, basi endelea kuomba kweli tena ikiwezekana umshinde Baba yetu wa Imani Ibrahimu ambaye pamoja na kuwa baba wa imani lakini bado changamoto za ndoa zilimshinda, kiasi cha kuzaa na binti yake wa kazi HAJIRI.

Ila pia kuhusu swali la Abeli kuwa kama Adamu na Eva wangekuwa timu Paulo, sisi tungepatikana vipi? Kwa kweli ni swali zuri, sana na linajibika. Timu Paulo bado tunaandaa maandiko yakutosha ili kulijibu.

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-02 01:09:23

BWANA YESU ASIFIWE WATUMISHI,hawali ya yote tumshukuru Muumba mbingu na nchi anayetukutanisha na kutupatia uwezo wa kujadili kwa utukufu wa KRISTO YESU nimeungana na mtumishi uwezo ktk kuungana nanyi kujadili mdahalo huu ulio na nguvu ya ROHO MTAKATIFU,kwa upande wetu sisi Ni 

TIMU SULEMAN

Point Ni sahihi ila kabla hatujaendelea tuulize Kwanza je,mtume Paulo hakuoa?

 

 

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-02 01:15:48

na mambo yote yatendeke kwa uzuri na utaratibu SULEMANI anatambulika alioa tena zaidi ya mmoja,tunawaomba tu TIMU PAULO mtueleze kuhusu yeye hakuwa na familia,tukijibiwa tutaendelea kwasababu tunaitaji kufaham kwanza Hilo.

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-02 01:58:50

TIMU SULEMANI TUNALUD NINAAMBATANA NA MTUMISHI UWEZO KUJADILI.

wakati tunasubiri majibu Kuna Jambo likae vizuri hapo kuhusu ndoa maana yake Ni makubaliano ya watu wawili wenye jinsia ya kiume na ya kike kuamua kwa pamoja kuishi pamoja na pia KUMTUMIKIA MUNGU haiusishi idadi ya watu hyo Ni wewe na nafs yako kuiponya,roho yako kuwa salama.sasa tunapojadili suala hili Cha kwanza kutazama ambayo pia ni point yetu ya 1.KUTIMIZA MPANGO WA MUNGU

mpango wa MUNGU unaonekana ktk uumbaji alipoufanya na maneno mazur kuyaachilia kwa wanadam hao,ukisoma vyema utaelewa,Mungu aliona mbali pale adamu alipokuwa peke yake na kuamua kumtwalia msaidizi wa kuambatana nae,Mungu alikuonea huruma wewe mwanaume kwa upweke ulio nao japo Adam alizungukwa na vitu vyote na hakuwa na uhitaji wakati huo Hadi pale Mungu alipoona mwenyew,Kuna nguvu sana mnapoambatana wawili namzungumzia mwanamke na mwanaume ktk KUMTUMIKIA MUNGU kwa Nia moja kwa moyo ulio Safi kwa Kila mmoja kusimama kwa zamu yake na nafasi yake aliyopewa na Mungu KUMTUMIKIA MUNGU.ni sahihi tunaepuka tamaa za mwili bado haitoshi kwa maana mtu hujaribiwa kwa tamaa yake mwenyew siku zote ukitaman Cha mtu ukikosa uwezo kukipata utawaza kumuibia hata katika ndoa ukitamani nje utakwenda tuu nje na hapo sio kwa mwanamke au mwanaume wanakuwa hawana uelewa Wala macho ya kutazama kuwa wanaemkosea Ni Muumbaji wao Jehovah na kumrudisha Yesu msalabani mara ya pili,ktk KUMTUMIKIA MUNGU Kuna mamb mengi sana tena sana maana huo Ni mjumuisho wa mambo yote yaliyo mapenz ya Mungu kwetu kufanya na kutekeleza hivyo Ni Jambo jema uoe au uolewe Ni mmoja lakin sio zaidi ya hapo Kama alivyofanya SULEMAN kuwa na wanawake wengi

 

 

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-02 02:25:25

TIMU SULEMANI HEWANI TENA TUMELEJEA

WATUMISHI ombi langu hebu tusome vzur maandiko haya 1wakorintho 7:1-20

TIMU SULEMANI tuna ushindi wote kwamba ni Jambo jema zaidi KUMTUMIKIA MUNGU ukiwa umeoa au kuolewa tusipende kuchukua maandiko nusu nusu ya nn kumkosea Mungu kwa kuwaka tamaa ndani kumkosea Mungu ili kuonekana na watu kuwa una uwezo wa KUMTUMIKIA MUNGU hata kama haujaoa au kuolewa ikiwa dunia imejaa dhambi ya uzinz kwa waliooana na uasherati kwa wasio oana hasa vijana.

jambo jema tena sana KUMTUMIKIA MUNGU ukiwa umeoa au kuolewa kwa lengo la kutekeleza maagzo ya kuhubiri WATU WATUBU KWA MAANA UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA kwa aliyekwisha kuamini aishi Kama mgeni au msafiri kwa kuvumilia Hadi mwisho apate kuokoka.

PROSPER HABONA
Moderator
Lid geworden: 2021-08-18 21:09:17
2021-09-02 04:02:03

Ubarikiwe sana tabitha, ngoja nikujibu tu kwa ufupi, JIBU NDIO MTUME PAULO HAKUOA, Kama ambavyo Yesu Kristo naye hakuoa. Me

ILA NIMESOMA POINT ZINGINE ZA TABITHA nimeshindwa kuelewa, maana naona Kama anaanzisha timu ya tatu yaani timu SULEPAU, maana timu Sulemani Yupo na timu Paulo pia yupo.

BAKI TU TIMU SULEMANI, SISI WENZIO TIMU PAULO TUNAMTUMIKIA MUNGU KWA UHURU, kumbuka ukiwa timu Sulemani utahitaji ruhusa ya mumeo ili kwenda baadhi ya maeneo ili ukamtumikie Mungu, na akikataa, hauwezi kwenda. Wakati wanawake timu Paulo wao wanakwenda tu.

PROSPER HABONA
Moderator
Lid geworden: 2021-08-18 21:09:17
2021-09-02 04:34:37

TIMU PAULO HAPA

Timu Sulemani nyote hebu someni vizuri maneno ya YESU katika Mathayo 22:29-30. Mmeona eeh? Sasa napenda mjue kuwa TIMU SULEMANI ni ya muda tu na mwisho wake ni hapahapa duniani ila TIMU PAULO ni ya milele maana ipo mpaka mbinguni. Yaani kila atayekwenda mbinguni atakuwa timu Paulo, KWA KWELI TUMEJIPANGA KUPOKEA WANACHAMA WAPYA MBINGUNI. 

Haya sio maneno yangu bali ni maneno ya YESU KRISTO mwenyewe, maana alisema kuwa MBINGUNI kule tutaakaoishi milele, huko, hakuna KUOA Wala KUOLEWA. Hivyo sisi timu Paulo hatutashangazwa na maisha ya mbinguni kwa kuwa tutaendelea kubaki timu Paulo milele.

SASA TUKIFIKA MBINGUNI OLE WAKE MWANAMKE ALIYEKUWA TIMU SULEMANI, AJE KUNIBEMBELEZA ETI NIMUOE, ha ha ha jibu langu litakuwa ni SHINDWAAAAAAAAA.

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-02 04:57:35

TIMU SULEMANI HEWANI TENA

Hapana Timu Paulo mm sipo kwenu kwangu npo huku huku Timu suleman Kama hakuoa nitafatilia vyema kwasababu inatambulika alioa,ahsante kwa majibu mazur ila suala la kuoa na kuolewa Ni muhimu sana,mwanaume ni mtawala ck zote alivyo KRISTO juu ya kanisa,tatizo sio kunipangia wapi pa kwenda Nini Cha kufanya yapi nisifanye kwasababu Hilo Ni jukum lake na happy ndio palipo na ugumu kiasi wa ndoa maana mwanamke kupangiwa mambo Ni mgumu kidogo,lakin hlo halikwamishi kutokuolewa na KUMTUMIKIA MUNGU hata kama ananizuia kwenda ibadani,mikesha na kuimba hata kuudhuria ibadani,kikubwa Cha kutazama maandiko yanasemaje hlo ndilo la kufuata,mfano mwanaume anakuzuia kuja ibadan kuimba maandiko yanasemaje kwamba mwanamke anapaswa kumtii mume wake nitatii kutokufika lakin kwa upande wangu sitakaa kizembe lazima niliitie jina la Bwana ashughulike na mume wangu tena kwa namna kubwa ya ajabu Kama kweli anahitaji nimtumikie kwasababu Kama aliwatetea wana wa Israel kutoka misri kwa farao Tena kwa mapigo ya kutosha,MUNGU HUYO HUYO anaweza kunitoa misr ambapo Ni nyumba niishiyo na farao akiwa amesimama Kama mume wangu na Musa atakuwa Ni mtumishi wa Mungu Kama vile mchungaji,mwalim au kiongoz wa mahari ninapomwabudu Mungu akiwa anamueleza mume wangu aniachilie nimtumikie Bwana wangu,MUNGU NI MWAMINIFU atanijibu na kunitoa kwa ushindi mkuu ambao hata naamini hata mume wangu hakiwa hajaokoka ataokoka tu tena kwa machozi solution Sio kushndana nae mwanaume ikiwa popote Mungu anaitika uliitapo jina lake.hivyo MTUMISHI DORCAS JUMA usijali ktk swali alilokuuliza,yote yanawezekana kwake AAMINIYE HIVYO KUOA NA KUOLEWA NI JAMBO LA LAZIMA

 

 

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-02 05:07:42

Ahahaahahaahaaaahhhhhh!!!!!!!!!!!!!!

TIMU SULEMAN HAPAA

Nakuomba nikujibu MR PROSPER  Ni kweli mbingun hakuna kuoa au kuolewa ila sio kwa mwili huo uliouvaa katika dunia hii mbingun Kuna miili mipya kabisaaa ambapo Kila anaekwenda kumsifu Mungu aliye hai na kumwabudu daima,au nikuulize swali wewe Ni malaika au mwili wa mbingun umeshauvaa tiali??

John Kennedy
Member
Lid geworden: 2021-08-27 06:11:22
2021-09-02 05:17:44

MUUMINI MWAMINIFU WA TIMU PAULO HAPA

Mtumishi Prosper nakupongeza sana kwa kuendelea kujenga hoja nzuri za kuwajibu timu Sulemani, ngoja mimi nijibu kwanza hili swali la mwisho la Abely ili tuisambaratishe kabisa timu Sulemani.

Mtumishi Abely aliuliza kuwa Kama Adamu na Eva wangekuwa timu Paulo, je sisi timu Paulo na hata Paulo mwenyewe tungekuwa wapi?

Ili swali mtumishi Abely ni zuri sana, tatizo tu ameliuza kuanzia katikati ya stori, hebu namwomba arudi mwanzo kabla siku ya sita ya uumbaji haijafika, na akirudi hapo ajiulize je huyu Adamu yeye alizaliwa na nani? Pia na huyu Eva naye alizaliwa na nani? JE TIMU SULEMANI MNAWEZA KUNIJIBU KWANZA KUHUSU WAZAZI KIMWIIL WA ADAMU NA EVA WALIKUWA KINA NANI? Mkijibu hili, ndipo mtakuwa na hoja ya msingi ya kuhofia kuwa timu Paulo  tungeongezekaje na kuwa wengi duniani, bila kuhamia kwenu timu Sulemani.

John Kennedy
Member
Lid geworden: 2021-08-27 06:11:22
2021-09-02 05:21:24

TIMU PAULO KWA MARA NYINGINE TENA

Wakati timu Sulemani mnaendelea kutafakari hoja yangu, niwaombe tu msisahau kuwa MUNGU anao uwezo wa KUZAA, ndio maana tukiokoka tunakuwa tumezaliwa na MUNGU hivyo tunakuwa watoto wa Mungu, kwa hiyo Mungu anao uwezo kabisa wa kuifanya dunia ijae watu, hata kama sisi sote tutakuwa TIMU PAULO.

MUHIMU:

Timu Sulemani msisahau kuwa, hata mwokozi wa ulimwengu YESU KRISTO tunayemwamini, naye alizaliwa na mwanamke Mariam ambaye mpaka anapata mimba ya YESU ALIKUWA HANA MUME, hivyo alikuwa timu Paulo. Sasa Kama Yesu alizaliwa na binti huyu aliyekuwa timu Paulo, unafikiri Mungu angeshindwaje kutufanya sisi timu Paulo tuendelee kuzaa na kuongezeka bila kuupoteza Upaulo wetu?

NJOONI HUKU MUMTUKIE MUNGU KWA HURU NA KWA NGUVU ZAIDI.

PROSPER HABONA
Moderator
Lid geworden: 2021-08-18 21:09:17
2021-09-02 05:27:24

Aisee kweli John umejibu kwa hekima sana, TIMU PAULO safiiiiiiiiiii, sasa ngoja tusubiri majibu kutoka timu Sulemani, huku timu Paulo tukiandaa mabomu mengine.

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-02 08:48:01

TIMU SULEMAN HEWAN TENA 

haujanishawishi bado mtumishi John katika uumbaji ambao Mungu aliufanya Ni yeye aliye pande zote anasimama kimwili na kiroho kwakuwa Muumbaji wetu hata Sasa japo kwa kuanzia adamu na Eva wanasimama kimwili kwa sisi tuliofuatia mtumishi hivyo katika uumbaji Mungu hajakosea kwa Kila hatua iliyofanyika swali la kujiuliza kwa TIMU PAULO kwann MUNGU kumletea adamu Eva ikiwa uwezo was kuishi mwenyew adamu alikuwa nao??

 

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-02 09:58:25

lakini pia ikae vizur hapo team paulo kwamba MUNGU WETU ALIYE HAI Ni muumbaji ambapo hata Sasa unaendelea ndan ya tumbo la mwanamke alafu mwanamke anakizaa yaan anakitoa nje kilichoumbwa tumbon kwa Mungu ni uumbaji ambao una fomla ya kujizalisha wenyew kwa uendelevu na uhai,Kama alifinyanga udongo na kuwa mwili akapulizia pumzi tukawa nafsi hai tutasemaje adamu wana wazazi wa mwili ikiwa Ni Mungu ndiye muhusika wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-02 10:07:39

na Mariam mama wa Yesu Kristo kwa upande wake sio sahihi kwamba alikuwa Timu Paulo hapo hakiangaliwi kitendo Cha ndoa isipokuwa makubaliano ya mwanamke na mwanaume kuishi pamoja Kama familia na KUMTUMIKIA MUNGU kwa pamoja kwasababu kabla ya uweza wa ROHO MTAKATIFU KUWA JUU YAKE alishakuwa yupo katka makubaliano na mwanaume aitwaye yusuph na Hadi mahar alishamtolea tiali isipokuwa hawakuanza kukaa pamoja kwasababu Kama ilikuwa Ni kwasababu ya kumleta MWANA WA MUNGU DUNIANI kwann aliendelea kuzaa watoto wengine au kuishi na yusuph ikiwa mwanzo alikuwa Timu Paulo??

PROSPER HABONA
Moderator
Lid geworden: 2021-08-18 21:09:17
2021-09-02 13:36:07

TIMU PAULO HAPA

Kwak kweli tabitha una maswali mazuri na yaliyoenda shule. Timu Paulo tumeyaona na tutayajibu kwa hekima kubwa. Haswa kuhusu hili la Mama wa Yesu yaani bikira Mariamu kuwa TIMU PAULO. Hata hivyo kabla ya majibu ya kina hayajaletwa, wewe hujiulizi tu kwa nini huyu dada anaitwa bikira Mariamu, je wadada wa namna hii wapo wangapi ndani ya timu Sulemani?

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-02 15:12:01

wapo wengi sanaaaaaaaaaa MR PROSPER kwenye timu yetu ya suleman hata huko kwenyewe Timu Paulo wanaokuja kujiunga waliokata tamaa kupata mwenz wake kwa mda mrefu kumsubiri au unakuta kwenye timu suleman yamemshinda kustahimili ndio anaamua kuwa huko akijua Kuna usalama usalama ni kuoa au kuolewa 

 

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-03 23:50:04

tujipongeze TIMU SULEMANI KWA USHINDI MAANA TIMU PAULO POINT WAMEISHIWA MAANA SIO KWA UKIMYA HUU

GOSPEL PREACHER
Moderator
Lid geworden: 2021-08-24 06:51:00
2021-09-04 07:22:48

MTOA MADA HAPA

Mtumishi tabitha unaonekana una kiu ya ushindi eeh!? Ninyi endeleeni tu kuweka point zenu nzitonzito, muda ukifika mimi ndio nitasema nani mshindi, lakini pia, nitawapa nafasi wadau wengine waweze kupiga kura. 

Pia timu Paulo mpo wapi mbona mpo kimya mno?

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-04 23:40:10

timu SULEMANI hapa, ahsante kwa nawe MTOA MADA kuona timu Paulo mpo kimya na ndio maana tumejiona nasi tuna ushind kwasabab ya ukimya wa TIMU PAULO sisi hatuna shaka kama ndio Mimi nasubir kwa hamu tufundishane TIMU SULEMANI ndani ya YESUUU

ABELY PATRICK
Member
Lid geworden: 2021-08-21 20:34:28
2021-09-07 13:02:16

NAPENDA TEAM PAULO WOTE MSOME HAPA HALAFU MUELEWE

1Wakorintho 11:8-12 INASEMA , 8 Maana Mwanaume Hakutoka Katika Mwanamke Bali Mwanamke Katika Mwanaume, 9Wala Mwanaume Hakuumbwa Kwa Ajili Ya Mwanamke, Bali Mwanamke Kwa Ajili Ya Mwaeaume,

MUELEWE HIZI POINT MBILI
11walakini Si Mwanamke Pasipo Mwanaume, Wala Mwanaume Pasipo Mwanamke Katika "Bwana".
# Maana Ya Katika Bwana Ni Kwamba , "kila Anaemtumika Mungu Hapaswi Kuishi Pasipo Mke Au Mume!!
NB, Mungu Ndie Muanzilishi Wa Ndoa Na Si Paulo.


HATA MALAIKA WALIONA MUNGU KAWAPENDELEA WANADAMU KUWAPA MABINTI WAZURI WAOE, MALAIKA WAKAGOMA WAKAJA KUOA

ABELY PATRICK
Member
Lid geworden: 2021-08-21 20:34:28
2021-09-07 13:02:32

Mwanzo 6:2 ,, Hebu Niwaulize IBRAHIMU Na Ubaba Wake Wa Imani Alioa,,
Wewe Na Imani Yako Hiyo Unasema Ni Heri Tusioe Heee Jaman Mnatutaka Nini Nyie,??

tabitha Prosper
Member
Lid geworden: 2021-08-18 11:17:07
2021-09-08 04:36:37

Bwana Yesu Asifiwe sanaaaa!

Am tabitha binti wa Mr Prosper ni timu SULEMANI wakati mnaendelea kututafutia majibu ili kutupatia pia swali letu lingine ni hili SASA KAMA MUNGU ALIONA UWEZO WENU WA KUKAA TIMU PAULO MWANAMKE ALIUMBWA KWA AJIRI YA NINI KATIKA DUNIA HII?

NA KAMA KWA AJIRI YA KUWA MSAIDIZI KWA MWANAUME KWA NAMNA GANI?

NA JE HUO USAIDIZI KWA WANAUME NDIO PASIPO KUMUOA MWANAMKE?

Nasubiri majibu tuendeleeeeee maana timu suleman ni motoo Wala hatuwi wa baridi Wala uvuguvugu ila kwa timu PAULO kwa haraka haraka nawaona mmekuwa wa baridiiiii yaan Kama kanisa la laodekia vile...

Roho Mtakatifu awafunulie tunawaombea Timu PAULO

PROSPER HABONA
Moderator
Lid geworden: 2021-08-18 21:09:17
2021-09-08 05:21:04

TIMU PAULO BADO TUPO.

Tunaandaa makombora mazito tena ya nuclear, ili tusambaratishe point zenu zote. Ingawa ninakiri kuwa ni point nzuri na zilizoenda shule.

Philip Nshekanabo
Member
Lid geworden: 2021-09-15 16:12:15
2021-09-18 17:40:11

ah kweli ukuwa mean ya ndoa unaweza kumpendeza Mungu na wanadamu ambao unawapelekea ilo neno

RICHARD SAMWEL
Member
Lid geworden: 2021-08-19 19:48:33
2021-09-30 17:13:09

Hii ni mada nzuri mno hivyo tunaomba irudiwe