KWANINI WAISLAM WALITENGENEZA INJILI YA UWONGO YA BARNABAS?
Сообщение 2021-12-25 11:10:27
0
5Кб
SEHEMU YA 1
Mwalimu Chaka
SWALI: Kwa nini Wakristo Hamuitambui Injili ya Barnaba?
lililoulizwa na: Abdullah Mbwana, Mombasa.
lililoulizwa na: Abdullah Mbwana, Mombasa.
Imetibitishwa kwamba kitabu kinachojulikana kama Injili ya Barnaba hakina uhusiano wowote na Ukristo. Ni ushahidi bandia kuhusu Injili takatifu na jaribio la kuwakilisha kwa ubaya dini ya Kikristo.
Kitabu hiki kinachohusishwa na Barnaba kilitafsiriwa katika lugha ya Kiarabu na Dr Khalil Sa'adah, kutoka nakala ya Kiingereza katika mwaka 1907.
Injili hii ilikataliwa kabisa na Wakristo kwa sababu ilikuwa ya kubuni na ya uongo.
Wale ambao waliikubali walikuwa baadhi ya madhehebu ya Waislamu. Walifanya hivyo kwa sababu rahisi sana; kwamba sehemu kubwa ya Injili hii inaunga mkono madai kwamba Kristo hakusulubiwa, lakini sura yake aliwekewa Yuda Iskarioti ambaye alisulubiwa badala yake Yesu. Lakini pia ndani ya Injili inaonekana Yesu eti akitabiri Ujio wa Nabii Muhammad huku akimtaja kwa jina
Maoni ya Wanachuoni
Wasomi ambao wamesoma kwa makini suala hili na kuchambua kitabu hiki, kwa kauli moja wamekubaliana kwamba hiki kitabu, ambacho kwa uongo kimehusishwa na Barnaba, hakikuwahi kuwepo kabla ya karne ya 15. Hii ni karibu miaka 1500 baada ya kifo cha Barnaba halisi. Kama kingeli kuwa kinapatikana kabla ya kipindi hicho, basi Wasomi wa Kiislamu kama Al-Tabari, Al-Baindhawi, na Ibn Kathir wasingelikuwa wamehitilafiana katika maoni yao juu ya mwisho wa Kristo, wala kuhusu utambulisho wa mtu ambaye ndiye aliyesulubiwa badala ya Yesu.
Kama tukirejea nakala za zamani ya Biblia Takatifu za nyuma kipindi cha kabla ya Uislamu na ambayo Qur'an inashuhudia juu ya ukweli wake, hatuoni Injili inayojulikana wala kuhusishwa na Barnaba. Wala haikutajwa katika meza ya yaliyomo, iliyoandaliwa na mababa wa Kanisa, ya vitabu ambavyo vinajumlisha Biblia Takatifu.
Utafiti wa Historia unaonyesha kwamba muswada wa awali wa Injili hii bandia alionekana kwa mara ya kwanza katika mwaka wa1709, katika milki ya Craemer, mshauri wa Mfalme wa Prussia. Kisha kikachukuliwa kutoka kwake na kuwekwa katika Maktaba Vienna katika mwaka wa 1738. Wasomi wote ambao walichunguza muswada huu wamebainisha kuwa kava yake ilikuwa katika mtindo wa mashariki ya kati na kwamba yalikuwemo maelezo mafupi katika Kiarabu. Kutokana na uchunguzi wa karatasi na wino uliotumika, inaonekana kwamba Injili hii imeandikwa katika karne ya 15 au 16.
Msomi wa Kiingereza, Dk Sale, anasema alipata nakala ya kitabu hiki katika lugha ya Kihispania iliyoandikwa na Mustafa al-'Arandi wa Aragon (Hispania), ambaye alidai yeye alikuwa ameitafsiri kutoka kwa nakala ya Kiitaliano.
Utangulizi wa nakala hii anasema kuwa mtawa mmoja aitwaye Marino, ambaye alikuwa karibu na Papa Sixtus V, alitembelea maktaba ya Papa siku moja katika 1585, na kukuta barua ya Mtakatifu Irenaeus akimkosoa Mtume Paulo kwa kutumia hoja zake kutoka kwa Injili ya Barnaba. Baada ya hapo Marino huku akiwa na hamu ya kupata hii Injili. Siku moja alikutana na Papa Sixtus V katika maktaba ya kipapa, na walipokuwa wakizungumza, Papa akalala usingizi. Mtawa huyu akaitumia nafasi hiyo, akakitafuta kitabu, akakipata na kukificha katika mavazi yake. Akisubiri mpaka Papa alipoamka na kisha kuondoka, huku kachukua kitabu hicho pamoja naye.
Hata hivyo, mtu yeyote asomayee maandiko ya St Irenaeus utapata hakuna kumbukumbu ya Injili ya Barnaba na hakuna upinzani wa aina yoyote kutoka kwake dhidi ya Mtume Paulo.
Kuna, hata hivyo, ukweli ambao kila mtu anaweza kujua. Imeandikwa katika Matendo ya Mitume kwamba Barnaba alikuwa Rafiki wa Paulo wa karibu wakati akihubiri Habari Njema katika Yerusalemu, Antiokia, Ikonio, Listra na Derbe. Barnaba pia walihubiri Habari Njema katika kundi moja na mpwa wake Yohana Marko katika kisiwa cha Kipro. Hii inaonyesha kwamba Barnaba alikuwa Muumini katika Injili ya Msalaba ambayo Paulo, Marko na Mitume wengine walikuwa wanahubiri, na ambayo inaweza kwa muhtasari kuwa sentensi moja fupi: Kristo alikufa msalabani kama upatanisho kwa ajili ya dhambi za ulimwengu na kufufuka tena siku ya tatu kwa ajili ya haki ya kila mtu aliye amwaminiye.
Kwa kuwa Injili ya Barnaba inakanusha ukweli huu wa msingi, ni wazi kuwa kitabu hiki ni uzushi tu wa kupotosha kwa hila za ujanja.
Baadhi ya Wasomi wamedhai kuwa mwandishi wa Injili ya Barnaba ni Marino aliyekuwa mtawa, baada ya kusilimu na kubadilisha jina kuwa Mustafa Al-'Arandi. Wengine wana maoni tofauti na wemeamini kwamba nakala ya Kiitaliano sio toleo asili ya kitabu hiki lakini ilikuwa imetafsiriwa kutoka asili ya Kiarabu. Mtu yeyote mwenye kusoma Injili hii ya uzushi ya Barnaba anaweza kuona kwamba Mwandishi ana maarifa mbalimbali ya Qur'an na kwamba mengi ya maandiko ni karibu sana na tafsiri halisi ya aya za Qur'an. . Fuatilia sehemu ya pili ninapoanza kuchambua Injili hii .
SEHEMU YA 2
Mwalimu Chaka
KUHITILAFIANA NA INJILI TAKATIFU
Kuna ushahidi mwingi kwamba Mwandishi wa Injili ya Barnaba alikuwa hana uhusiano wowote na Mitume wa Kristo, au wanafunzi wake ambao waliandika vitabu vyao wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Kuna ushahidi mwingi kwamba Mwandishi wa Injili ya Barnaba alikuwa hana uhusiano wowote na Mitume wa Kristo, au wanafunzi wake ambao waliandika vitabu vyao wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
1.Ushahidi wa kwanza ni kutokufahamu kwa mwandishi JIOGRAFIA ya Palestina ambayo ndiyo nchi na kitovu cha masimulizi ya kidini. Anasema, “Yesu akaenda kando ya ziwa Galilaya na akapanda mashua kusafiri hadi Nazareti, mji wake mwenyewe. Kukawa na dhoruba kubwa na mashua ilikuwa karibu kuzama” (Sura ya 20:1-2). Ni vizuri kujua kwamba Nazareti iko juu ya mlima wa Galilaya, wala sio mji wa pwani, kama mwandishi anavyosema.
2. Mahali pengine anasema, “Kumbuka kwamba Mungu aliamua kuharibu Ninawi kwa sababu hapakuwa na mmoja katika mji huo ambaye alikuwa mcha Mungu. Yeye (Yona) alijaribu kutoroka Tarso, kwa kuwa na hofu ya watu, lakini Mungu akamtupa baharini na samaki akammeza na kumtupa nje karibu Ninawi” (BARNABA Sura 63:4-7). Ni jambo lanalojulikana kwamba mji wa Ninawi ulikuwa mji mkuu wa Dola ya Waashuri na alikuwa umejengwa kando ya ufuo wa mashariki wa Mto Hidekeli, kwenye kijito kinachojulikana kwa jina la al-Khisr. Kwa hiyo, haupo katika eneo la bahari ya Mediterranean kama ilivyoelezwa na mwandishi huyu.
3. Mwandishi alikuwa hana ufahamu juu ya historia ya maisha ya Yesu Kristo. Katika sura ya tatu ya Injili hii ya kughushi, imeandikwa, “Yesu alipozaliwa, Pilato alikuwa Gavana wakati wa uongozi wa Rabi Anania na Kayafa .” ( Sura 3:2).
Hii si kweli kwa sababu Pilato alikuwa liwali kutoka mwaka wa AD 26-36. Anania alikuwa Rabbi mkuu kutoka AD 6, na Kayafa kutoka AD. 8-36.
4. Katika sura ya 142 imeandikwa kwamba “Masihi hatakuja kutoka ukoo wa Daudi lakini kutokana na kizazi cha Ishmaeli, na kwamba ahadi ilitolewa kwa Ishmaili, na sio kwa Isaka” (Sura 124:14). Hii ni kosa kubwa kwa sababu mtu yeyote mwenye kusoma ukoo wa Kristo katika Injili ya kweli ataona kwamba, kulingana na mwili, Yeye alishuka kutoka kwa ukoo au nyumba ya Daudi, na kabila la Yuda.
5. Mwandishi amejumlisha hadithi ambazo hazikuwa na msingi katika dini ya Kikristo. Zifuatazo ni mifano ya hadithi hizo.
a) “Wakati Mungu alisema na wafuasi wa Shetani, “Tubuni na kukiri kwamba mimi ni Muumba wenu, ‘wakamwambia, ‘Sisi tumegeuka na kuacha kukuabudu wewe kwa sababu Wewe ni mdhalimu, lakini Shetani ni mwenye haki kwa wasiokuwa na hatia na yeye ni Bwana wetu.” Basi, Shetani, alipokuwa anaondoka, akatema mate kwenye lundo dogo la udongo na Gabriel akaondoa mate yale na baadhi ya vumbi, matokeo yake akaja mtu kuwa na kitovu katika tumbo lake.” (Sura ya 35:25-27).
b). Yesu akajibu, akisema, 'Hakika mimi nalimuhurumia Shetani wakati nilipojua kuhusu kuanguka kwake na ninawahurumia watu ambao anawajaribu ili wafanye dhambi. Kwa hivyo Mimi nalifunga na kuomba kwa Mungu wetu ambaye alisema na mimi kwa kupitia Malaika wake Gabriel akisema, ‘Unataka nini, ewe Yesu, na nini haja yako?’ Mimi nikajibu, `Bwana, Wewe unajua ubaya gani Shetani imesababisha na kwamba yeye, ambaye ni uumbaji wako, anawaharibu wengi kwa njia ya majaribu yake. Kuwa na huruma, Ee Bwana.' Mungu alimjibu, Yesu. ‘tazama, mimi nitamsamehe ila aseme tu, ‘Bwana, Mungu wangu, nimekosa, nihurumie’ Na mimi nitamsamehe na kumrejesha katika hali yake ya awali.” Yesu akasema, "Niliposikia hii Nilifurahi nikiamini kwamba mimi nimefanikiwa kuleta maridhiano. kwa hiyo nilimwita Shetani, naye alipokuja Shetani aliniuliza, ‘Je nikufanyie nini yenu ewe Yesu?' Mimi nikamjibu, `Wewe utafanya hivyo kwa ajili yako mwenyewe, kwa sababu mimi sihitaji huduma yako, lakini nimekuita na ni kwa faida yako.' Shetani akajibu, `Kama hutaki huduma yangu, Sitaki yako pia, kwa maana mimi ni mbora kuliko wewe. Wewe hustahili kunihudumia mimi. Wewe umetotokama na na udongo lakini mimi ni nimetokamana na Roho.” ( Surah 51:4-20).
Hakuna mtu anayeweza kuamini kwamba hadithi hii ya kishirikina ni kutoka katika Injili ya uongozi wa Mungu. Awali ya yote, Mungu hakufurahishwa na Shetani alipoanguka na akamuondoa kutoka kwa uwepo wake. Sio sambamba na utakatifu wa Mungu kufanya mazungumzo ya maridhiano na Shetani. Pili, tangu mwanzo, Kristo aliingia katika vita visivyokoma na shetani. Biblia inasema, ‘mtu atendaye dhambi ni wa Ibilisi, maana Ibilisi ametenda dhambi tangu mwanzo. Mwana wa Mungu alidhihirishwa kwa sababu hii, ili azivunje kazi za Ibilisi (1 Yohana 3:8). Tatu, katika mapambano yake pamoja na Kristo, Shetani hakuwahi na hajawai jitokeza kusema kwamba alikuwa bora kuliko Kristo. Kinyume chake, katika mkutano huko Kapernaumu alipoamrishwa kumwaja mtu, aliyekuwa amepagawa alilia kwa sauti kubwa akasema, Acha! Tuna nini nawe Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Najua wewe u nani Mtakatifu wa Mungu! (Luka 4:34).
Ni vyema kukumbuka kwamba hoja hii ya Shetani kwa mujibu wa Injili ya Barnaba ni kinyume pia na Qur’ani ambayo anasema Shetani kaubwa kwa Moto (Qu 7:12) na Isa ambaye Waislamu wanadai ndiye Yesu ni Neno atakaye kwa Mungu na pia ni Roho wa Mungu. (Tazama Qur’ani 66:12, 4:171)
SEHEMU YA 3
Mwalimu Chaka
Leo napenda tuangalie baadhi ya mafundisho na upindaji wa maandiko ya Mungu kama tunaona katika Injili hii ya Barnaba.
Utabiri wa Ujio wa Muhammad katika Injili ya Barnaba.
Utabiri wa Ujio wa Muhammad katika Injili ya Barnaba.
Katika Biblia tunasoma jinsi Yohana Mbatizaji alitangaza ujio wa Bwana Yesu:
"Sasa huu ulikuwa ni ushahidi wa Yohana, Wayahudi wa Yerusalemu walipowatuma makuhani Walawi, na kumwuliza yeye ni nani. naye alikiri, wala hakukana, alikiri kwamba "Mimi siye Kristo." Nao wakamwuliza, " Ni nani basi? U Eliya wewe?" Akasema, "Mimi siye." "Je, wewe u Nabii yule? "Yeye akawajibu, "La" Basi wakamwambia, "Wewe u nani? ili tuwapelekee jibu wale waliotutuma?, Wanenaje juu ya nafsi yako?" Yohana alijibu kwa maneno ya nabii Isaya, "Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Nyoosheni njia ya Bwana.’”
"... siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, "Tazama Mwana-kondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu!" (Yohana 1:19-29)
Katika Injili ya Barnaba tunaona kisa hiki kimebadilishwa na kumfanya Yesu kutabiri kuja kwa Muhammad, kama Qur'an inasema Isa alifanya (Qur'an 7:157, 61:6).
"Waliona wengi ambao walikuwa wanafuata Yesu, kwa ajili hiyo wakuu wa makuhani wakafanya shauri wao kwa wao ili wamtege Yesu kwa maneno yake. Kwa hiyo wao waliwatuwama Walawi, na baadhi ya walimu wa Sheria kumwuliza, wakisema: "Wewe ni nani" Yesu alikiri, alisema ukweli: ". Mimi sio Masihi" Wakasema: "Je, wewe ni Eliya au Yeremia, au mmojawapo wa manabii wa kale?" Yesu akajibu: "Hapana" Nao wakamwambia, "Wewe ni nani Sema, ili tupate kutoa ushuhuda kwa wale waliotutuma?." Kisha Yesu akasema: "Mimi ni sauti ya mtu apitaye kwa njia yote za Yudea, kwa kilio akisema: “Tayarisheni njia ya Mjumbe wa Bwana, kama ilivyoandikwa katika Isaya." (Sura. 42)
"Ndipo kuhani: akamuuliza "Ataitwaje Masihi atakapokuja ... " Yesu akamjibu, "jina la Masihi ni la kupendeza ... Muhammad, ndilo jina lake lenye kheri" (Surah. 97).
Hapa mwandishi wa Injili ya Barnaba anadai Masihi atakeyekuja ni la kupendeza, yaani Muhammad jina lenye kheri" !!! eti Muhammad ndiye Masihi!!!! ili tutalichambua mbeleni
JE YESU NI MWANA WA MUNGU ?
Katika Biblia jina ‘Mwana wa Mungu’ ni jina lililopewa kwa taifa la Israeli (Kutoka 4:21-23) na pia kwa wafalme wake wote (2 Samweli 7:11-14, Zaburi 2).Kwa mujibu wa Biblia Yesu ni mwana pekee atokaye kwa Baba aliyejaa Neema na kweli. Maandiko yapo mengi kuhusiana na hili. Wanafunzi walikiri ili pia.
"Basi Yesu akaenda pande za Kaisarea Filipi, aliwauliza wanafunzi wake akasema, "Watu unena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? " Wakasema, "Wengine wanasema kuwa u Yohana mbatizaji, wengine wanasema wewe ni Eliya,. Na wengine, Yeremia au mmojawapo wa Manabii." Akawauliza. "Na ninyi je, mnasema mimi ni nani?" Simoni Petro akajibu, "Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai." Yesu akamwaambia, "Heri wewe Simoni mwana wa Yona, kwa maana mwili na damu, havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni." (Mathayo 16:13-17)
Kinyume na Biblia, Qur'an inafundisha kuwa Yesu sio Mwana wa Mungu (Qur'an 9:30). Katika Injili ya Barnaba tunaona kwamba Mwandishi wake Anabadilisha kukiri kwa Petro ili kuendanishe na kile Qur'an inasema:
"(Yesu) aliwauliza wanafunzi wake, akisema:"Watu wanasema mimi ni nani" Wakasema: "Baadhi yao wanasema kuwa u Eliya, wengine Yeremia, na wengine mmojawapo wa manabii wa kale." Yesu akajibu, "Ninyi; nanyi mnasema mimi ni nani?" Petro akajibu, "Wewe ndiwe Masihi, Mwana wa Mungu." Kisha Yesu kwa hasira, akamkemea akisema: "Ondoka na utoke mbele yangu" (Injili ya Barnaba Sura. 70)
Katika Sura ya 222, ambayo ndiyo sura ya mwisho ya Injili ya Barnaba tunasoma:
"Baada ya Yesu kuondoka (baada ya kutoka mafichoni kwa njia ya dirisha la nyumba kwenye bustani ya Gethsemane) wanafunzi walitawanyika kwa njia na sehemu mbalimbali za Israeli na kote duniani, na kwa kweli walichukiwa na Shetani, walipata adha na matezo, kwa mazingizio ya uwongo. Ikawa baadhi ya watu waovu., waliondoka na kujifanya kuwa wanafunzi, wakahubiri kwamba Yesu alikufa lakini hakufufuka Wengine wakahubiri kwamba kweli alikufa, lakini akafufuka. Wengine walihubiri na bado wanahubiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, miongoni mwao ni Paulo kudanganywa. ".
Mwandishi wa Injili ya Barnaba anafanya juhudi kusahihisha Injili ya kweli iliyotangulia na Paulo. NIngependa kuuliza Ni lini na ni kwa jinsi gani Mwandishi alipata ufahamu kwamba wanafunzi hao walikuwa wametawanyika katika sehemu mbalimbali duniani? Swali hili Naliacha wazi, lakini kwa urahisi tunaweza tuIkalijibu, kwa maana sisi kama Wakristo tunatambua kwamba ni ubunifu mwingine wa bandia .
Fuatilia sehemu ya Nne
SEHEMU YA 4
Mwalimu Chaka
Tunazidi Kuichambua Injili Hii ambayo inajaribu kuhusishwa na Mtume Barnaba.
Leo tuangazie Mwandishi.
MWANDISHI: Muislamu ambaye alikuwa na uelewa kiasi wa Biblia Kuna uhakika kabisa na wa kutosha kutibitisha kwamba mwandishi wa Injili hii bandia ni Muislamu. Mtu yeyote akisoma kwa makini kitabu hiki kinachojulikana kama Injili ya Barnaba atapata kina mguso wa Kiislamu ndani yake.
i) Kwanza, kitabu hiki kina maelezo ya kufanana na Kristo. Katika sura ya 112 inasema: "Jua, ewe Barnaba, ya kwamba mimi ninahofia. Mmoja wa wanafunzi wangu atanisaliti kwa vipande thelathini vya fedha. Zaidi ya hayo, nina uhakika kwamba yule atakayenisaliti atauawa kwa jina langu, kwa sababu Mungu ataniinua juu ya nchi na kubadilisha sura ya huyo atakayenisaliti ili kila mmoja aweze kufikiri yeye kuwa ni mimi. Na wakati akifa kifo kibaya na cha kutisha, nitabaki na aibu hiyo kwa muda mrefu duniani. Lakini wakati Muhammad, mtume mtakatifu wa Mungu, akija, aibu hii itaondolewa kwangu” "(Surah 112:13-17).
Habari hizi ni sanjari na mafundisho ya Kiislamu ya Zama za miaka ya kati
ii) Kifo cha Yesu. Biblia inafundisha kuwa Yesu alisulubiwa na kufa. "Kisha (Pilato) akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Lakini alikuwa kuamuru Yesu apigwe mijeledi, akamtoa ili asulubiwe. ... Walipokuwa wakienda, walikutana na mtu mmoja wa Kirene aitwaye Simoni, wakamshurutisha auchukue msalaba. ... Walipikwisha kumsulubisha, wakagawana mavazi yake kwa kura ... ‘Yesu akalia tena kwa sauti kubwa, akaitoa roho yake". (Mathayo 27:26-50.)
Kinyume na Biblia, Qur'an inafundisha kuwa Isa ambaye anadaiwa kuwa ndiye Yesu hakusulubiwa na wala hakufa msalabani (Qur'an 4:156-157). Tunaona tena jaribio, katika Injili ya Barnaba la Mwandishi akijaribu kubadilisha tukio la kusulubiwa kwa Yesu ili kuendana sambamba na kile Qur'an inasema:
"Mungu alitenda ajabu hata, Yuda akabadilishwa kisura kuwa kama Yesu na hata katika usemi wake pia na askari walichukua Yuda wakamfunga ... Hivyo wale watu wakamwongoza mpaka mlima wa Kalvari, ambapo walitumia kutundika wahalifu,na ndipo wakamsulubisha Yuda "(Sura. 216-217).
Sasa hapa bila shaka ameowanisha usemi ya Qurani kuwa " Bali walibabaishiwa mtu mwingine wakamdhani kuwa Nabii Isa!!!
Mifano hii inaonyesha jinsi Mwandishi wa Injili ya Barnaba kwa utaratibu anavyojaribu kuandikwa upya Injili ya Biblia kwa kuifanya ikukubaliane na Qur'an.
Ni katika matukio adimu ambapo anafanya makosa. Tukiangalia mabadiliko haya tunaweza kuelewa malengo ambayo Mwandishi alikuwa anajaribu kufikia. Alikuwa anarudia kuandika Injili ili sasa iwe imemekubaliana na Qur'an; alikuwa anajaribu kuwashawishi watu kuwa Yesu alifundisha kile ambacho Qur'an inafundisha.
iii) Tatu, kuna madai kwamba Maandiko matakatifu yemeharibiwa. Katika sura ya 12 ananukuu Kristo kama akisema: "Kweli nawaambieni, kwamba kama kweli isingelitokomezwa kutoka Kitabu cha Musa, Mungu asingelimpa Daudi, baba yetu, Kitabu cha Pili yaani Zaburi. Na kama kitabu cha Daudi kisingeli potoshwa Mungu haziniamini kwa injili aliyoikabidhi kwangu, kwa sababu Bwana Mungu wetu habadiliki na Yeye alitamka ujumbe mmoja kwa wanadamu wote ... Wakati mjumbe wa Mungu akakapokuja atasafisha sehemu ya kitabu changu ambayo itakuwa imepotoshwa kwa na waovu” (Sura 124:8-10).
Kauli hii ni kashfa dhidi ya uhalisi wa maandiko yote Matakatifu na haiwezekani kuwa imetoka kwa Kristo, ambaye alisema, “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.” (Mathayo 24:35).
Baadhi ya Waislamu wameniambia kwamba kwa kuwa Injili ya Barnaba ina baadhi ya mafundisho machache kinyume na Qur'an. Basi hii inathibitisha haikuwa imeandikwa na Muislamu kwa kuwa Muislamu asingelifanya aina hii ya makosa.
Hata hivyo, kwa sababu tu mwandishi amefanya makosa madogo na machache kuhusu Uislamu haina maana yeye sio Muislamu. Waandishi wa Kiislamu leo bado ufanya makosa madogo madogo katika maandishi yao. Hii haina maana wao sio Waislamu, ila tu ina maana wao wanajifunza, kama sisi sote pia.
Ni sawa na Mwandishi wa Injili ya Barnaba. Hivyo bado pana uwezekano mkubwa zaidi kwamba Mwandishi wa Injili ya Barnaba alikuwa Muislamu.
Fuatiilia sehemu ya tano ambapo nitajaribu kulinganisha baadhi ya mafundisho ya Injili hii dhiti ya Qurani
SEHEMU YA 5
Mwalimu Chaka
Injili ya Barnaba ni ushuhuda pinzani dhidi ya Qur'an:
Tayari nimekwisha onyesha jinsi Kitambu hiki kilivyo na mafundisho yaliyo kinyume na Biblia Takatifu.. Yafuatayo ni baadhi ya maandiko yaliyomo katika Injili hii ya Uzushi ya Barnaba ambayo, kwa kweli pia, yanakwenda kinyume na kile kilichomo ndani ya Qur'an: Pamoja na hayo Bado Waislamu wengi Maamuma, wanashabikia kitabu hiki japo baadhi ya wasomi kama vile Sheikhy Shabir Ally wamekiri wazi kuwa Injili hii ni uzushi wa miaka ya karne ya kumi na saba. Ebu tutizame baadhi ya Aya za injili hii tukilinganisha na yaliyomo ndani ya Qurani
Tayari nimekwisha onyesha jinsi Kitambu hiki kilivyo na mafundisho yaliyo kinyume na Biblia Takatifu.. Yafuatayo ni baadhi ya maandiko yaliyomo katika Injili hii ya Uzushi ya Barnaba ambayo, kwa kweli pia, yanakwenda kinyume na kile kilichomo ndani ya Qur'an: Pamoja na hayo Bado Waislamu wengi Maamuma, wanashabikia kitabu hiki japo baadhi ya wasomi kama vile Sheikhy Shabir Ally wamekiri wazi kuwa Injili hii ni uzushi wa miaka ya karne ya kumi na saba. Ebu tutizame baadhi ya Aya za injili hii tukilinganisha na yaliyomo ndani ya Qurani
1. Yusufu akaenda kutoka Nazareti, mji wa Galilaya, na mke wake ambaye alikuwa na
mimba ... kuandikishwa kutokana na amri ya Kaisari. Alipo fika Bethlehemu, hakupata nafasi ya kupumzika kwa sababu mji ulikuwa mdogo na wageni walikuwa wengi. Alikwenda nje ya mji mahali ambapo wachungaji hukaa. Wakati Yusufu alikuwa angali huko, siku za Mariamu za kujifungua mwanawe zikatimia. Bikira alikuwa kuzungukwa na mwanga mkali sana, NA ALIJIFUNGUA MTOTO WAKE BILA
UCHUNGU WALA MAUMIVU YOYOTE YA KUZALIWA KWA MTOTO
( Surah 3:5-10).
Ujumbe wa Qur'an unathibitisha kwamba Mariamu alijifungua mwanawe kwa njia ya uchungu wa uzazi-kama mwanamke yoyote yule. Qur’ani inasema,
Ujumbe wa Qur'an unathibitisha kwamba Mariamu alijifungua mwanawe kwa njia ya uchungu wa uzazi-kama mwanamke yoyote yule. Qur’ani inasema,
"Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali. KISHA UCHUNGU WA MTOTO KUZALIWA-AKAMPELEKA KATIKA SHINA LA MTENDE. (akawa anazaa na huku) Anasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya na ningekuwa niliyesahaulika kabisa!" (Surat Maryam 19:22-23). "
Zaidi ya hayo hamna ushahidi wa Qurani wala hadithi unaomtaja Yusufu kama MUME wa Mariamu. Qurani pia haionyesi kamwe kuwa SIKU ZA KUZAA zilitimia; ila tunamwona Ruh mwaminifu ambaye tunaambiwa ni Jibril akijimithilisha kwa umbile la Mwanadamu huku Mariamu yumo upande wa Mashariki mwa Msikiti; anampa taarifa za kupata mimba na wakati huo huo anashika mimba, anaondoka mpaka chini ya mtende anazaa huko na jioni anarejea nyumani na mtoto ambaye mtoto huyu ana uwezo wa kuongea siku hiyo hiyo
QU 19:16. Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki. 17. Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu. 18. (Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamngu.19. (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika.20. Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba?21. (Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.22. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali.23. Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa! 24. Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji!25. Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.26. Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu. 27. Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu! 28. Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba. 29. Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi.30. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai.31. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai.32. Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu.33. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.34. Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.
2. "Jinsi mlivyo wanyonge enyi, Wanadamu, kwa maana Mungu
amekuteuweni, kama Wana na akakupeni paradiso. Lakini
ninyi wanyonge mkaanguka chini kwa ghadhabu ya Mungu,
kwa hadaa ya Shetani, nanyi mkatolewa peponi ".
amekuteuweni, kama Wana na akakupeni paradiso. Lakini
ninyi wanyonge mkaanguka chini kwa ghadhabu ya Mungu,
kwa hadaa ya Shetani, nanyi mkatolewa peponi ".
(Surah 102:18-19).
Qur'an inapinga swala la ubaba wa Mungu na kudhai kuwa jambo ili ni kashfa, inayostahili adhabu katika moto wa Jehanamu. Inatoa onyo kwa wale walio sema: Mwenyezi Mungu amejifanyia mwana (Surat Al-Kahf 18:4-5).
"4. Na kiwaonye wanao nena: Mwenyezi Mungu ana mwana. 5. Wao hawana ujuzi wa jambo hili, wala baba zao. Ni neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu. 5
3.Ndoa: Injili ya Barnaba inafundisha wazo la Biblia kuhusu ndoa, kwamba ndoa inamfunga mwanamme na mwanamke sawasawa kwa pamoja:
"Mwanamme atosheke na mwanamke ambaye Muumba
wake amempa yeye, naye asahau kila mwanamke mwingine
wake amempa yeye, naye asahau kila mwanamke mwingine
( Sura 116:18);
"Basi Mwanamume awe radhi na kutosheka na mkewe
ambaye muumba wake amempa, na asahau kila Mwanamke
mwingine"(Surah. 115).
ambaye muumba wake amempa, na asahau kila Mwanamke
mwingine"(Surah. 115).
Wakati ambapo Qur'an inafundisha mitala na ndoa ya wake wengi ikisema, "Basi oeni mnaowapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne. Na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi oeni mmoja au wawekeni (Masuria) wale ambao mikono yenu ya kuume ya kuume imewamiliki ... "(Surat Al-Nisaa, Wanawake '4:03).
4."Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: ‘Bwana, kuna waumini katika Jahannamu ambao wamekuwepo huku miaka sabini elfu. Iko wapi rehema yako, Ee Bwana? Nakusihi, Bwana, waweke huru kutokana na adhabu hii kali. Kisha Mungu akuamuru Malaika wanne wenye kibali zaidi kwenda Jehanamu na kuleta kila mtu ambaye ni wa dini ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kuwaongozaa hadi peponi.” (Surah 137:1-4).
Aya hizi zinapingana na Qur'an, ambayo kabisa inakanusha suala la msamaha, kwa watakao kuwa jehenamu, kwa maana inasema: "Kwa Hakika Mwenyezi Mungu amewalaani makafiri na amewaandalia Moto unao waka kweli kweli na watadumu
humo milele daima; hawatapata mlinzi wala msaidizi "(Surat Al-Ahzab 33:64-65).
humo milele daima; hawatapata mlinzi wala msaidizi "(Surat Al-Ahzab 33:64-65).
Lakini pia liko fundisho la Kiislamu kuwa wapo baadhi ya Waumini wa Kiislamu ambao mwanzo wataingia Jehenamu, walipie makosa na dhambi zao kwa muda mle motoni kisha baadaye Allah atawatoa mle eti kwa kuwa walikuwa wanatamka japo shahada
5. Masihi: "Na Yesu alikiri na kusema, 'Amin nawaambieni kwamba mimi sio Masihi.' Nao wakamwuliza, `Je, wewe ni Eliya au Yeremia au mmojawapo wa Manabii wa zamani? ' Yesu akamwambia 'Hapana'. Kisha akamwambia, 'Wewe ni nani ili tupate kuwashuhudia wale waliotutuma? Yesu alisema, 'Mimi ni sauti ya mtu aliaye katika Yudea, Mtayarishieni njia Mtume wa Bwana ". (Surah 42:5-11).
Qur'an inasema:
"Malaika alisema: Ewe Maryamu! Tazama! Mwenyezi Mungu anakubashiria Neno kutoka kwake, ambaye jina lake ni Masihi Isa, mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, ni mmoja wa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu) "
"Malaika alisema: Ewe Maryamu! Tazama! Mwenyezi Mungu anakubashiria Neno kutoka kwake, ambaye jina lake ni Masihi Isa, mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, ni mmoja wa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu) "
(Surat Al Imran 3:45) .
Katika Sura ya 97 ya Injili ya Barnaba, ni wazi kuwa Muhammad ndiye aitwaye Masihi.. Qur'an, kama vile Biblia inampa jina hili Yesu pekee.
Ni jambo la ajabu na la kuchekeza kutambua kwamba katika utangulizi wa Injili wa Barnaba; Yesu ameitwa “KRISTO” na katika Sura ya 42 na 82 "Barnaba" anakana kwamba Yesu ni MASIHIi. Ni mtu asiye na ufahamu wa kiteolojia na mjinga kilugha anayeweza kufanya kosa kama hili; kwa sababu "Christos" ni neno la Kigiriki yaani Kiyunani ambalo kwa Kihebrania ni "Masihi". ndugu wapendwa, Je, kuna, kwa kweli, ushahidi wa uzushi na kughushi dhidi ya Injili na Qur'an zaidi kuliko ushahidi huu? Je, kuna Muislamu ambaye anaamini huu upotoshaji kwamba Masihi ni Muhammad mwana Abdullah (s.a.w) na wala sio Bwana Yesu ?
6. Mbingu:
Qur'an inafundisha kwamba kuna mbingu saba:
“Zinamtukuza zote mbingu saba na vilivyomo ndani yake
“Zinamtukuza zote mbingu saba na vilivyomo ndani yake
(Qur'an Bai Israil, Wana wa Israeli 17:44).
Hata hivyo Injili ya Barnaba inafunza ya kuwa kuna mbingu tisa;
Hata hivyo Injili ya Barnaba inafunza ya kuwa kuna mbingu tisa;
"Kweli nakwambia kwamba mbingu ni tisa, ambazo kati yake kumewekwa sayari, ambazo zina umbali wa safari ya mtu, miaka mia tano moja hadi nyingine."
(Surah. 178).
(Surah. 178).
Поиск
Категории
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS
Больше
HOW RICH WAS KING SOLOMON?
Exactly how rich was King Solomon? How much gold did he possess? Did God make him...
A’isha: Mke wa Muhammad Mwenye Miaka Tisa
Watu wengi wamesema kuwa Muhammad alifanya tendo la ndoa na mke wake mwenye umri mdogo zaidi,...
MAMBO YA KUMSAIDIA KIJANA ALIYEOKOKA AISHI MAISHA YENYE USHUHUDA MZURI
Mtume Paulo katika waraka wake kwa Timotheo anamwambia hivi, ‘Mtu awaye...
MWANAMKE NA MWANAUME NA MAHUSIANO: TOFAUTI YA KIMAUMBILE
Sote tunajua kabisa ya kwamba kuna tofauti ya kimaumbile kati ya mwanaume na mwanamke, na tofauti...
BIOLOGY: FORM 1
List of all topics in Biology for form 1 class: CLICK HERE TO DOWNLOAD.
INTRODUCTION TO BIOLOGY...