UTATU UNATHIBITISHWA KWA KUTUMIA HESABU/HISABATI

0
5K
Kumekuwa na madai na hoja nyingi sana kuhusu hili swala la UTATU. Wengine wanasema kuwa ukijumlisha 1+1+1 unapata 3 na sio MOJA kama ambavyo Wanao amini Utatu wanavyosema.
 
Tatizo kubwa sio KUJUMLISHA bali unajumlsiha kwa kutumia KANUNI ZIPI AU IPI YA HISABATI. Leo katika Max Shimba Ministries tutawajibu watu wote hili swali la HESABU YA 1+1+1 =1?
 
Je, inawezekana au haiwezekani?
 
HESABU/HISABATI ZINA KANUNI ZAKE NA LAZIMA TUZIFUATE, KWA BAHATI NZURI, hapa Kwenye Huduma yetu ya Max Shimba Ministries tunazifahamu sana KANUNI ZA HISABATI.
 
Kuhusu swala la UTATU, Linahusisha NAMBA TATU na hivyo sheria yake lazima iwe ya "TERNARY ADDITION" na sio "BASE TEN ADDITION" kama wengi wenu mnao tumia hiyo hesabu bila ya hata kufahamu kuwa addition yenu MNATUMIA SHERIA YA "BASE TEN" .
 
SASA NINI MAANA YA TERNARY ADDITION:
1. Ternary namba inatumia BASE 3, tofauti na BASE 10 ambayo mkihesabu na kufikia namba 9, unarudi kwenye 1 na kuongeza "SIFURI" = 10. SASA, katika Ternary addition, unapo hesabu namba mwisho wako ni NAMBA MBILI na inayo fuata ni 10, kama kwenye "BINARY ADDITION" namba yako ya mwisho ni MOJA http://www.allaboutcircuits.com/…/d…/chpt-2/binary-addition/ .
 
Ninafahamu wengi wenu labda hamjawai soma Hesabu za juu na mnaweza pata walakini, lakini ingia hapa na ujifunze mwenyewe Ternary addition
http://homepage.cs.uiowa.edu/~jones/ternary/arith.shtml
 
SASA TUANZE KUTHIBITISHA UTATU WA MUNGU KWA KUTUMIA HESABU
MSINGI WA TERNARY ADDITION UNATUMIKA:
 
A. (1 + 1 + 1) Ternary = 10 Ternary
UNAONA JAWABU LAKO NI Ternary (10)
 
SASA namba zetu tumesha zipunguza na kufikia Tenary 10. Ikiwa na maana kuwa, MSINGI UNAO FUATA NI KUZIJUMLIZA HIZO NAMBA " DIGITS MBILI ZA MOJA NA SIFURI KWA KUTUMIA msingi ule ule wa Ternary addition.
 
B. (1 + 0) Ternary = 1 Ternary.
 
SASA TUMESHA PATA JIBU LETU KUWA UTATU UNATHIBITISHIKA KWA KUTUMIA HISABATI, na leo nimewajibu wale wote ambao HESABU SIO SOMO LAO KUWA UTATU UNAJIBIKA HATA KWA KUTUMIA HISABATI.
 
SASA NENDA KAMUULIZE MKUFUNZI WAKO WA HISABABI YAFUATAYO:
A. Ternary ya (1 + 1 + 1 ) = ?
B. Ternary ya ( 1 + 2) = ?
 
UKISHA PEWA JIBU MUULIZE TENA HUYO MKUFUNZI WAKO
C. Ternary ya (1 + 0 ) = ?
 
HAKIKA MUNGU NDIE MWANZILISHI WA HISABABTI na hakuna asilo liweza.
Mungu awabariki sana, na leo UMESHA JIBIWA KUWA UTATU UNATHIBITISHIKA HATA KWENYE HISABATI.
 
KURIDHIKA NA YALE TULIYOFUNULIWA .
 
A. BABA anaitwa MUNGU ( 1 WAKORINTHO 8:6 ).
 
B. MWANA ( YESU ) anaitwa MUNGU ( ISAYA 9:6; YOHANA 20:26-29 ).
 
C. ROHO MTAKATIFU anaitwa MUNGU ( MATENDO 5:3-4 )
 
Katika Isaya 48:16 na 61:1, Mwana azungumza huku akihusisha Baba na Roho Mtakatifu. Fananisha Isaya 61:1 na Luka 4:14-19 kuona Mwana akizungumza. Mathayo 3:16-17 inaelezea ubatizo wa Yesu. Anayeonekana hapa ni Mungu Roho mtakatifu akimshukia Mungu Mwanahuku Mungu Baba akitangaza furaha yake katika Mwana. Mathayo 28:19 na wakorintho wa pili 13:14 ni mifano ya nafsi tatu katika Mungu mmoja.
 
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
Zoeken
Categorieën
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
UTHIBITISHO 10 KUWA YESU NI MUNGU
“Wahubiri wa injili” wa Kiislamu huwa wanapinga kuwa Yesu ni Mungu na unapowakatalia...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:09:17 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
JINSI YA KUENENDA KWA ROHO.
Wagalatia 5:16 “Basi, nasema enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe tamaa za...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 13:00:32 0 6K
SPIRITUAL EDUCATION
Lebo DHAMBI YAKO INAKUFUATA NYUMA 1TIMO 5:24 MWANZO 4:7.
Lebo DHAMBI YAKO INAKUFUATA NYUMA 1TIMO 5:24 MWANZO 4:7. 
By Martin Laizer 2024-03-06 08:37:24 0 4K
SPIRITUAL EDUCATION
613 LAWS OF JEHOVAH GOD
KUSOMA KWA KISWAHILI, BONYEZA HAPA THE 613 MITZVOT  Contextual material for the...
By PROSPER HABONA 2023-04-17 06:10:30 0 10K
OTHERS
Debit Voucher, Credit Voucher, and Transfer Voucher
Voucher is the supporting documents that accountants use as the summary to record into the...
By PROSHABO ACCOUNTING 2022-03-29 20:47:16 0 9K