ALIYE TABIRIWA KWENYE KUMBUKUMBU YA TORATI NI YESU AU MUHAMMAD?

0
7Кб
Katika Kumbukumbu 18:17-18; 33:1-2, na 34:10-11, ni Muhammad aliyetabiriwa hapa, kama baadhi ya Waislam wanavyodai?
 
Jibu: Kumbukumbu 18:15-18 inasema Mungu atamwinua nabii, kuwa watamsikia, kama Musa kutoka miongoni mwao, miongoni mwa ndugu zao. Je Yesu alikuwa nabii? Je Wayahudi walio wengi walimsikia Yesu? Je Yesu alikuwa mmoja wa Wayahudi? Je Yesu alikuwa Myahudi? Waislam wanapaswa kutokuwa na shida kuafiki kuwa mistari hii inamfaa Yesu kuliko Muhammad. Kama angalizo la kihistoria, kabla ya Nicea Archelaus (262-278 B.K.) pia alizungumzia jinsi ambavyo Kumbukumbu 18:15 isivyoweza kuwa inamwongelea mtu mwingine yoyote yule isipokuwa Yesu Kristo kwenye Disputation with Manes sura ya 43 uk.219.
 
Yafuatayo ni maoni zaidi.
 
a. Kumbukumbu 33:1-2 inasema "Bwana", na Waislam hawamwiti Muhammad Bwana wao. (Waislam wa ‘Alawite na makundi mengine ya Ghulat wanamchukulia Muhammad kuwa Mungu, lakini maoni hayo siyo kawaida kwa Waislam.)
 
b. Kumbukumbu 34:10 kwamba "Wala hakuinuka tena katika Israeli nabii kama Musa." Wasifu huu uliandikwa, huenda na Yoshua, muda mrefu kabla Yesu hajaja.
 
c. Kumbukumbu 34:10 inasema "uso kwa uso", na Muhammad hajawahi kusema kuwa alipata maneno yake moja mwa moja kutoka kwa Mungu, bali kupitia malaika (Sura 2:97). Yesu aliwasiliana moja kwa moja na Mungu Baba kwa mujibu wa Yohana 1:18 na vifungu vingine.
 
d. Mstari unaofuatia, 34:11, unasema kuwa hakuna nabii mwingine yoyote aliyefanya miujiza hiyo mikubwa kama Musa. Muhammad, kama ilivyoandikwa kwenye Kurani (Sura 17:90-93) hakuwahi kufanya miujiza kama hii, isipokuwa kusema Kurani. (Kurani inapingana na jinsi mapokeo ya baadaye ya Hadithi yanavyosema.)
 
e. Kwenye Kurani yenyewe, Sura 29:27 inasema unabii umekuja kupitia Isaka na Yakobo. Kwenye tafsiri ya Yusuf Ali ya Kurani, anasema, "Na tumewapa (Abraham) Isaka na Yakobo, na tumeagiza miongoni mwa wazao wake unabii na ufunuo . . ." Wakati ambapo mabano kwenye jina la Abraham yapo kwenye tafsiri ya Yusuf Ali, neno lote "Abraham" halimo kwenye Kurani ya Kiarabu, na Yusuf Ali aliona haja ya kuongeza neno "Abraham" kwenye maandiko ambayo Waislam wanayaona kuwa ni neno la Mungu.
 
f. Mwisho, Petro, mtume wa Yesu, alisema andiko hili lilitimia kwa Yesu kwenye Matendo 3:22-26. Mtume Petro alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kujua jambo hili.
 
1. Ama, Yesu alifanya makosa ya kumruhusu mtu mwongo kama Petro kuwapotosha watu, kwa kwa karibu miaka 2,000, ambao wamekuwa wakijaribu kumfuata Mungu, na Mungu hakuinua kidole kuwaambia watu ukweli.
 
2. Au, Yesu alijua alichokuwa anafanya wakati alipomchagua Petro, na Mungu hakusahihisha kitu ambacho hakikihitaji masahihisho yoyote yale.
 
3. Vinginevyo, Petro hakusema hivyo, na kitabu cha Matendo ya Mitume kilipotoshwa kabla ya maelezo ya maneno hayo ya kwanza tuliyo nayo toka nje ya Biblia yanayoturejesha kwa Yesu, karibu mwaka 138 B.K.
 
Viongozi wa awali wa kanisa walisema kuwa mstari huu ulimwongelea Yesu. Baadhi yao ni
Justin Martyr 138-165 B.K.
Irenaeus 182-188 B.K.
Tertullian 220-220 B.K.
Origen 225-254 B.K.
Chrysostom 407 B.K.
 
Justin Martyr alizaliwa karibu mwaka 114 B.K., ingawa watu wengine hudhani mwaka 110 B.K. Apology yake ya kwanza iliandikwa kati ya mwaka 138 B.K. na mwaka 165 B.K. wakati wa kifo chake. Ni dhahiri kuwa alitakiwa kusoma unabii huu unaomwongelea Yesu kabla ya kuandika.
 
Muislam anaweza kusema kuwa Justin hakukosea tu bali pia manuscripts zote za Agano Jipya ziliunukuu usemi wa Petro kimakosa.
 
Pia, tafsiri kwenye lugha nyingine zilifanywa mapema sana; tarehe za hapo juu si za tafsiri za kwanza, bali ni tarehe za manuscripts za zamani zaidi ambazo zipo leo hii. Hizi zinaaminika kwa sababu zimepita kwenye mtiririko huru ambao watu wanaweza kuutumia kuthibitisha manuscripts za Kiyunani. Mtiririko wote wa manuscripts hizi, kutoka Afrika kwenda Asia, unaafiki kuwa Petro alisema hivi akimwongelea Yesu.
 
Tazama When Cultists Ask uk.43-44,45-46 na When Critics Ask uk.125-126, uk.131-132, na uk.133 kwa habari zaidi.
 
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Поиск
Категории
Больше
OTHERS
How to Change WordPress Logo in Login Page?
  Updated on Sep 10, 2020  Posted by Editorial Staff  Website...
От Shabea Disony 2022-09-04 21:37:51 0 8Кб
Injili Ya Yesu Kristo
NINI MAANA YA KUUMBWA KWA MFANO WA MUNGU?
Mungu ni Roho. Je wewe ni nani?Katika somo hili la uumbaji wa binadamu, nitajibu hoja na maswali...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:12:32 0 5Кб
Injili Ya Yesu Kristo
UNYENYEKEVU.
Bwana Yesu asifiwe... Kwa ufupi. ” Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni...
От GOSPEL PREACHER 2022-03-30 04:54:56 0 5Кб
Injili Ya Yesu Kristo
KIASI NI NINI KATIKA UKRISTO?
Kiasi kama tafsiri yake  ilivyo ni  kuwa na uwezo wa kudhibiti jambo/tendo lisipitilize...
От GOSPEL PREACHER 2022-05-21 04:15:18 0 5Кб
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 8
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 27 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-01-24 14:28:26 0 5Кб