Yesu ni Mungu

0
5K

Je, Yesu Kristo ni Mungu?
Hebu tuanzie kutafiti ukweli wa hili swali, Je Yesu ni Mungu, kabla ya kuja kwake mara ya kwanza. Je, manabii walimwita nani na/au walitabiri nini juu ya ujio wake.

 

Yesu akasema, Amini, Amini nawaambia, kabla ya Abrahamu kuweko mimi nilikuwa.” Tena kwa ajili ya hayo wayahudi wakashika mawe ili wampige nayo Yesu (Yohana 8:59). Je, wayahudi wangetaka kumpiga mawe yesu kama haingekuwa ya kuwa alisikika akikufuru kwa kusema yeye ni Mungu?

 

YESU KABLA YA KUZALIWA ALITABIRIWA NA MANABII KUWA NI MUNGU: 
King James Bible Isaiah Chapter 9 Verse 6
For unto us a child is born, unto us a son is given: and the government shall be upon his shoulder: and his name shall be called Wonderful, Counsellor, The mighty God, The everlasting Father, The Prince of Peace.
Hii aya hapo juu inakiri kuwa hata kabla ya kuja kwake Mitume na Manabii walitabiri kuwa Yesu ni Mungu. 

 

YESU NI NENO, NENO ALIKUWA MUNGU:

Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe. Kwa hivyo Yesu ni Mungu!


YESU ALIITWA MUNGU NA WAFUASI WAKE:
King James Bible John 20:28
And Thomas answered and said unto Jesus, My Lord and my God.
Hii aya inatuhakikishia kutoka wafuasi wake kuwa Yesu ni Mungu. Yesu hakupinga alipo itwa Mungu.

 

Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). Yesu hamsahihishi kwa kuyasema haya. Tito 2:13 inatuhimiza kusuburi kurudi kwa Mungu wetu na mwokozi – Yesu kristo (Pia tazama petro wa pili 1:1). Waebrania 1:8, Baba asema juu ya Yesu, “Lakini juu ya mwana asema haya, “Na Kiti chako cha enzi, wewe Mungu, Kitadumu milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.”


MWENYEZI MUNGU ALIMWITA YESU MUNGU:
King James Bible Hebrew 1 Verse 8, 9
8. But unto the Son [he saith], Thy throne, O God, [is] for ever and ever: a sceptre of righteousness [is] the sceptre of thy kingdom. 

  1. Thou hast loved righteousness, and hated iniquity; therefore God, [even] thy God, hath anointed thee with the oil of gladness above thy fellows.

Hata Mungu Baba alimwita mwanae Yesu Kristo Mungu. Hii aya hapo juu imethibitisha kuwa Yesu ni Mungu. 


YESU MWENYEWE ALIJIITA MUNGU:
King James Bible Matthew 4 Verse 7
Jesus said unto him, It is written again, Thou shalt not tempt the Lord thy God.
Katika hii aya Yesu Kristo anakiri kuwa yeye ni Mungu.

YESU ALIISHI KABLA YA KUUMBWA KWA DUNIA:

King James Bible John 17 Verse 5

And now, O Father, glorify thou me with thine own self with the glory which I had with thee before the world was.

 

 

Hii aya inatuhakikishia kuwa Yesu aliishi kabla ya kuumbwa dunia. Hayo maneno ni Yesu anasema kwa Baba yake.

 


Hivyo basi leo nimeamua kuweka ushaidi yakinifu kuwa Yesu Kristo ni Mungu.

Katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu Mungu tu(ufunuo wa Yohana 19: 10). Mra nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.

 

Sababu muhimu ya kwamba Yesu sharti awe Mungu ni kwamba kama si Mungu, kufa kwake hakungetoshea kufidia dhambi za ulimwengu wote (Yohana wa kwanza 2:2). Mungu pekee ndiye angeweza kulipia adhabu kama hiyo. Mungu pekee ndiye angeweza kufidia dhambi za ulimwengu wote w (Wakorintho wa pili 5: 21), afe na afufuke kuthibitisha ushindi juu ya dhambi na mauti.


Mungu awabariki sana.
By Max Shimba, A Friend of God

Buscar
Categorías
Read More
1 KINGS
Verse by verse explanation of 1 Kings 21
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 16:01:03 0 5K
OTHERS
ALLAH NA UISLAM NI DINI YA WAFU
Ndugu msomaji, Ukisoma Biblia takatifu ambayo ndio NENO la Mungu, inasema: Mungu ni Mungu wa...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-25 11:45:06 0 7K
Injili Ya Yesu Kristo
Msiba katika bonde la kukata maneno!
Yoeli 3:12-14 “Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafau; maana...
By GOSPEL PREACHER 2022-04-01 08:31:44 0 5K
ESTHER
Verse by verse explanation of Esther 4
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 25 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 12:49:39 0 5K
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 11
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 37 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 14:34:59 0 5K