Je umeshapata Zawadi ya Uzima wa milele?

0
6K
Bibilia inaonyesha njia ya wazi ya uzimani.Mwanzo ni sharti tutambue yakwamba tumetenda dhambi kinyume chake Mungu: “Kwasababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Sote tumefanya mambo ambayo hayampendezi Mungu,ambayo yanafanya tustahili adhabu.Kwa kuwa dhambi zetu ziko kinyume kabisa na Mungu aliye uzima wa milele,basi ni adhabu ya milele pekee itoshayo. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti,bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).
 
Hata hivyo Yesu Kristo asiyekuwa na dhambi (1 Petro 2:23), mwana wa Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (Yohana 1:1,14) na akafa ili kutulipia adhabu. “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi,kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu,tulipokuwa tungali wenye dhambi” (Warumi 5:8). Yesu Kristo alikufa msalabani (Yohana 19:31-42), kwa kuchukua adhabu ambayo sisi tulistahili (2Wakorintho 5:21). Siku tatu baadaye akafufuka katika wafu (1Wakorintho 15:1-4), kudhihirisha ushindi juu ya dhambi na mauti. “kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu” (1Petro 1:3).
 
Kwa imani ni sharti tuungame dhambi zetu na tumrejee Kristo kwa ajili ya wokovu (Matendo 3:19). Tukiweka imani yetu kwake, kwa kuamini kifo chake msalabani kama malipo ya dhambi zetu,tutasamehewa na kuahidiwa uzima wa milele mbinguni. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). “Kwa sababu,ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Warumi 10:9). Imani pekee katika kazi aliyo ikamilisha Kristo pale msalabani ndiyo njia ya kweli ya pekee ya uzimani! “Kwa maana nimeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zetu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yoyote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9).
 
Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako,tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka ya kwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haitakuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo peke yake ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumuelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu,najua yakwamba nimetenda dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Nina ziacha dhambi zangu na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu /ya ajabu na kwa msamaha - karama ya uzima wa milele! Amina!”
Zoeken
Categorieën
Read More
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 16
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 28 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-21 04:52:01 0 6K
LEVITICUS
Verse by verse explanation of Leviticus 19
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 95 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 10:22:54 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
SABABU TANO KWANINI WAKRISTO WANAABUDU JUMAPILI
Ndugu msomaji, Katika kijarida hiki kifupi, nitakuwekea sababu tano (5) kwanini Wakristo...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:12:13 0 7K
MAHUSIANO KIBIBLIA
HATARI ZA KUWA NA MAHUSIANO YASIYO SAHIHI
UTANGULIZIMahusiano yasiyo sahihi ni mahusiano ya namna gani? Haya ni mahusiano kwanza kabisa...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-07 23:45:47 0 8K
Injili Ya Yesu Kristo
KWA NAMNA GANI MTU ANAWEZA KUMZIMISHA ROHO MTAKATIFU?
Roho Mtakatifu ni Mungu, mwenye nguvu zote, maarifa yote, anayepatikana kila mahali. Yeye pia...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:55:47 2 6K