Yesu Kristo anayo amri na mamlaka ya kusamehe dhambi

0
5K

Kuna jambo lililowahi kutokea hadi likawashangaza watu; hebu fatilia kisa hiki. Biblia Takatifu inasema kwamba:

“Wakaja watu wakimleta mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. Na walipokuwa hawawezi kumkaribia (Yesu) kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Na baadhi ya waandishi waliokuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao,

Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?

Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?

 

Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi – Akamwambia yule mwenye kupooza,

Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.

Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe.” (Marko 2:3-12)

 

Kwa Wayahudi uponyaji haukuwa kitu kigeni kwao kwani hata manabii enzi za Agano la Kale nao walitumia nguvu za Mungu kuponya wagonjwa; lakini, jambo lililoonekana geni kwa Wayahudi ni kusikia Yesu amesema “...Umesamehewa dhambi zako...” (Marko 2:5) Kauli hiyo ya Yesu iliwafanya waone kwamba Yesu AMEKUFURU kwa maana mwenye mamlaka ya kusamehe dhambi ni Mungu pekee. Watu hao walidhani Yesu amekufuru kwa sababu hawakujua kuwa Yesu ni Mungu ingawa alikuwa ameuvaa mwili wa kibinadamu kama sisi.

 

Ukimpokea Yesu; anakusamehe dhambi zako zote. Haijalishi umetenda dhambi nyingi kiasi gani; haijalishi hali uliyonayo hivi sasa. Fahamu kwamba Yesu anakupenda. Neno la Mungu linasema kwamba:

 

“...asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji...” (Isaya 1:18)

Yesu ni Mungu, endapo ukimpokea atakusamehe dhambi zote ulizozitenda. Yesu anakupenda sana. Hebu leo mpe Yesu maisha yako ayatawale; Yesu ataiondoa kiu hiyo ya kutenda dhambi ikufanyayo ushindwe kujizuia kuwaka tamaa mbaya za mwili wako; Yesu atakupatia ulinzi ambao utazuia pepo wachafu wasiingilie maisha yako; Yesu atakubariki na kufungua tumbo lako lililokosa mtoto kwa muda mrefu wote huo unaotaabika hata sasa; Yesu atawarejesha kwako watoto wako ambao wamekataa kukutii hata wametoweka kwako; Yesu atakupatia uzima na kuyaondoa magonjwa yote hayo yanayokutesa hata sasa; Yesu atakubariki na kukupatia uzima wa milele.

 

Kwa kweli nashindwa kuuelezea kwa ufasaha zaidi upendo wa Yesu juu yako kwa maana wewe ni wathamani kubwa sana mbele za Mungu. Mimi nachoweza kukwambia ni kwamba: Yesu anakupenda tena hataki upotee. Mpe Yesu maisha yako sasa ili ufurahie uzuri wa pendo Lake.

Site içinde arama yapın
Kategoriler
Read More
SPIRITUAL EDUCATION
What Is The Purpose Of Life?
Everybody has wondered at one time or another why they exist. What is my purpose in life? Is...
By GOSPEL PREACHER 2023-09-29 09:50:42 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
JIPANGE KABLA YA NDOA!
Bwana Yesu asifiwe… Kwa ufupi; Moja ya tatizo kubwa linalowasumbua  vijana ni...
By GOSPEL PREACHER 2022-03-30 05:16:16 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?
*Je! sisi ni wafalme na makuhani kwa namna gani?*   Na: Martin Laizer   SWALI:...
By Martin Laizer 2024-10-15 09:31:27 5 3K
Injili Ya Yesu Kristo
Biblia inakataza kuapa kabisa, lakini kwanini watu wanaapa mahakamani na katika vifungo vya ndoa?
SWALI: Biblia inakataza kuapa kabisa, lakini kwanini watu wanaapa mahakamani na katika vifungo...
By GOSPEL PREACHER 2022-03-23 18:27:17 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
JINSI YA KUENENDA KWA ROHO.
Wagalatia 5:16 “Basi, nasema enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe tamaa za...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 13:00:32 0 6K