NA UZIMA WA MILELE NDIO HUU, WAKUJUE WEWE ULIYE MUNGU WA PEKEE, WA KWELI NA YESU KRISTO ULIYE MTUMA

0
5K
Ndugu wasomaji,
Leo nitaielezea aya ya Yohana 17: 3 ambayo Waislam wamekuwa wakiitumia mara nyingi sana kudai kuwa eti, Yesu amekana kuwa yeye ni Mungu. Waislam kwa kupitia mihadhara ya kidini na kwa kutumia vijarida mbali mbali wanatishia Umma wa Wakristo kuwa, Yesu ameukana Uungu. Je, hayo madai ya Waislam ni kweli? Je, hiyo aya ina la zaidi la kujifunza?
 
Ili uielewe Biblia vizuri, nilazima usome aya kadhaa ili upate kuelewa nini hasa Mungu anasema kupitia Neno lake. Hivyo basi, nimeweka aya ya 4 na ya 5 ili kufafanua nini hasa Yesu alikuwa anasema katika Yohana 17.
 
Ngoja niziweke aya zote hapa:
Yohana 17: 3 Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue Wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.4 Nimekutukuza Wewe duniani kwa kuitimizaile kazi uliyonipa niifanye. 5 Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako.
 
Yesu katika aya ya 5 [Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako] ==> YESU anasema kuwa
1. Yeye aliishi kabla ya Ulimwengu kuwepo! Hapo panaanza kukupa mwanga halisi, wa nini Yesu alikuwa anasema na Yesu ni nani. Imani zote zinakiri kuwa aliye kuwepo kabla ya vitu vyote ni Mungu. Lakini katika aya ya 5, Yesu nae anadai kuwepo kabla ya uumbaji.
2. Yesu anaendelea kusema katika aya hiyo hiyo kuwa, yeye alikuwa na adhama ya Mungu -"UTUKUFU". Yesu anamwambia Mungu Baba kuwa, AMTUKUZE YESU KWA UTUKUFU ALIOKUWA NAO KABLA YA ULIMWENGU HAUJAKUWAKO. Sasa, kama Yesu, sio Mungu na alikuwa Binadamu wa kawaida, kwanini basi amwambie BABA YAKE AMTUKUZE? Yesu anatumia mamlaka gani hayo kudai Utukufu ambao sio wake bali ni wa Mungu pekee?
3. Kama Yesu sio Mungu. Je, alipo dai atukuzwe na Mungu Baba, huoni kuwa alikuwa anakufuru? Lakini Hatusomi kuwa YESU aliwai tenda dhambi yeyote ile. Hata dini ya Waislam, inakiri kuwa, Katika Binadamu wote ambao waliishi Duniani, ni Yesu pekee aliweza kuishi bila ya kuetnda dhambi na kuwa na dhambi.
 
Ndugu wasomaji, madai ya Waislam kuwa Yohana 17:3 INAPINGA UUNGU WA YESU ni Batili kabisa, maana, leo tumejifunza katika Yohana hiyo hiyo kuwa Yesu aliishi kabla ya Ulimwengu kuwepo na Yesu anautukufu wa Mungu.
 
Aya ya 5 NUKUU: Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako.
HOJA:
 
1. Yesu anadai kuwa aliishi kabla ya ulimwengu kuumbwa.
2. Yesu anadai kuwa anautukufu kama wa Baba yake.

SASA BASI:
1. Yesu ni nani mpaka adai utukufu kama wa Mungu tena kutoka kwa Mungu Baba?
2. Yesu ni nani mpaka aseme kuwa aliishi hata kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, tena namwambia Mungu Baba?
 
Ndugu zanguni,
Mada imekamilika na kujibu maswali ya Waislam kuwa Yesu aliukana uungu wake katika aya 3 ya Yohana 17.
 
Nawakaribisha wote Kwa Yesu Kristo aliye hai. Yeye ndie njia kweli na uziama. Njooni kwake ili mpate maisha ya milele na yenye uzima tele.
Zoeken
Categorieën
Read More
MASWALI & MAJIBU
Je! Inawezekana mtu akawa anafanya miujiza na bado asinyakuliwe?
SWALI: Naomba kuelewa kwanini mtu atoe pepo, aombee wagonjwa wapone, asikie sauti ya Mungu...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-12 23:16:05 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
The Holy Spirit In The Life Of Christ
In Luke 1:35 the angel Gabriel announces to Mary, “The Holy Spirit will come upon...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 06:33:40 0 6K
OTHERS
NANI ALIYE TOLEWA KAFARA, ISHMAEL AU ISAKA?
Kwenye Mwanzo 22:1-18, je inawezekana kuwa mvulana ambaye Abraham alikaribia kumtoa kafara awe ni...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:41:15 0 5K
NDOA KIBIBLIA
SHAMBA LA MTU MVIVU, ASIYE NA AKLI: MAHUSIANO YA NDOA (NA UCHUMBA)
MAHUSIANO: SHAMBA LA MTU MVIVU, ASIYE NA AKLI(Uvivu na Kukosa Akili Kichocheo Cha...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-07 23:23:24 0 5K
BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
test
Jeremiah Chapter 48 Verses 1-47: The Moabites were descendants of Lot who lived east of the...
By PROSHABO NETWORK 2021-12-31 18:31:29 0 8K