ROHO MTAKATIFU NI MUNGU

0
5K

Ndugu msomaji,

Watu wengi hawafahamu kuhusu Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu Ni Nani?

Baadhi ya watu wanadhani Roho Mtakatifu ni aina fulani ya nishati, uweza au radi. Lakini wanakosea.

Roho Mtakatifu Ni Mtu, nikimmanisha kuwa sio Mtu kwa maantiki ya Binadamu. 

Na kwa kweli ni ‘mtu’ muhimu sana; ni Nafsi ya Tatu katika Utatu wa Mungu (Mt 28:19) (2Kor 13:13). Yeye ni mtu roho, kama vile wewe ulivyo ila Yeye hafungwi na mwili. Twaweza kumwomba kila siku tukisema, ‘Roho Mtakatifu,  nijaze kwa uweza wako, niongoze, nipe hekima na ujasiri’ kwa sababu ni mtu kweli tunayeweza kuzungumza naye na kujihusisha naye.

Wengine wanasema kuwa ni Nguvu Fulani ya Mungu. Wengine wanasema ni Malaika Jibril. Lakini, Biblia inatumabia nini kuhusu Roho Mtakatifu?

Hebu ungana nami moja kwa moja na tujifunze kwa pamoja kwa kutumia aya za Biblia kuhusu Roho Mtakatifu. Kwa kifupi, ROHO MTAKATIFU ni Mungu. 

Swala la kuwa Roho mtakatifu ni Mungu limo ndani ya aya nyingi za biblia kama vile Matendo 5:3-4. Katika ayah ii Petro anapambana na anania aliyemdanganya Roho mtakatifu na nasisitiza yakuwa “hukumdanya mtu bali Mungu.” Hili ni tangazo la wazi kwamba kumdanganya Roho mtakatifu ni kumdanganya Mungu. Tunaweza pia kujua Roho mtakatifu ni Mungu kwa kuwa ana tajwa na hali sawa na za Mungu. Roho mtakatifu yuko kila mahali katika Zaburi 139:7-8, “nitaenda wapi nijifiche na Roho? ama nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda juu mbinguni, huko uko; nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko,” tena katika wakorintho wa Kwanza 2:10 tunaona hali yakuwepo kila mahali kwa Roho mtakatifu “Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake mtakatifu. Kwa kuwa Roho huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni nani ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani yake? Vivyo hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.”

Tunaweza kujua kweli kwamba Roho mtakatifu ni Mungu kwa kuwa ana akili, hisia na mapenzi yake. Roho mtakatifu hufikiri na hujua (Wakorintho wa kwanza 2:10). Roho mtakatifu anaweza kuugua (Waefeso 4:30). Roho hutuombea (Warumi 8:26-27). Roho mtakatifu hufanya maamuzi kutokana na mapenzi yake mwenyewe (Wakorintho wa kwanza 12:7-11). Roho mtakatifu ni Mungu, sehemu ya tatu ya utatu wa Mungu. Kama Mungu, Roho mtakatifu anaweza kufanya kazi ya msaidizi na mshauri kama vile Yesu kristo aliyevyoahidi kuwa atakuja kufanya (Yohana 14:16,26; 15:26).

Je, Roho Mtakatifu Ni Nafsi Halisi?

Madaktari husema kwamba nafsi halisi ni sharti iwe na akili, hiari, na hisia. Na Roho Mtakatifu tunampima kwa vigezo hivyohivyo vitatu.

Je, Roho Mtakatifu Ana Akili?
Akili ni uwezo wa kujifunza, kuelewa na kufikiri. Ndiyo, ana akili sana! (Rum 8:27) (1Kor 2:10-13).

Je, Roho Mtakatifu Ana Hiari?
Hiari inahusiana na kusudio, uchaguzi, takwa na azimio. Ndiyo, Roho Mtakatifu ana hiari yake mwenyewe na anakubaliana na Baba na Mwana (1Kor 12:11).

Je, Roho Mtakatifu Ana Hisia?
Je, ana hisia na hisia kali? Anapenda na hiyo ndiyo hisia yenye nguvu sana aliyonayo, na kuna hisia kali katika kuugua kwake awapo kwenye maombezi (Rum 15:30; 8:26,27).

Mungu awabariki sana.

Site içinde arama yapın
Kategoriler
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
MAFUNDISHO YA MASHETANI
1 Timotheo 4 : 1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-04 16:00:49 0 5K
MAHUSIANO KIBIBLIA
NIFANYE NINI ILI KUSHINDA TAMAA ZA MWILI?
Septemba mwaka 2011, Mwanafunzi mmoja wa shule ya Sekondari alinitembelea nyumbani kwangu hapa...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:16:15 0 6K
OTHERS
Bible Verses about Honoring Parents
The New Testament binds a great responsibility on children when it says in Ephesians 6, verses...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:58:36 0 7K
Injili Ya Yesu Kristo
MKRISTO NA UCHUMI: CHRISTOPHER MWAKASEGE
Utangulizi SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASIKINI! (Namna ya mkristo kuishi katika hali ngumu ya...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-19 07:19:55 0 12K
JOB
Verse by verse explanation of Job 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 37 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 13:15:14 0 5K