ISA WA QURAN SIO YESU WA BIBLIA

0
5كيلو بايت
Ndugu msomaji,
Zifuatazo ni thibitisho kadhaa zitakazo fundisha kuwa, Isa wa Quran na Yesu wa Biblia ni wawili na tofauti:
 
UTHIBITISHO WA 1
 
MAANA YA JINA ISA Ni jambo la kawaida sana jina au majina kuwa na maana. Mfano majina haya ya kiarabu yana maana hizi: Muhammad, linamaanisha mwenye kushukuriwa, Abdalla ni Mtumwa wa Allah; Abu-Bakar maana yake ni Baba wa bikira; Abu Huraira ni baba wa Mapaka. Aidha majina ya Kiebrania nayo pie yana maana. Malaki ni mtumishi au Mjumbe wa Yehova, Isaya ni Wokovu wa Yehova; Ezekiel inamaanisha Mungu hutia nguvu, Daniel – Mungu ni hakimu wangu.
 
JINA LA ISA MAANA YAKE NINI?Katika Qurani yenye jumla ya juzuu 30; Surah 114; aya 6236; maneno yenye kutamkia 76,440; herufi 322,373; jina Isa linatamkwa lisa au Aysi limetajwa mara 25. Isa pia ameitwa masihi mara 93. Lakini tunaposoma Qurani iliofarsiriwa/tafsiriwa na Imam Baidawi Vol 1 Ukurasa 160 ameeleza kuwa Isa jina la Kiarabu maana yake ni Wekundu unaozidiana na weupe. Hii ndio maana ya Jina la Isa wa Quran. Je, Yesu wa Biblia maana yake nini?
 
JINA LA YESU MAANA YAKE NINI?JINA Yesu linatokana na lugha ya Kiebrania ‘Yehoshua’ katika lugha ya Kigiriki wanasema ‘lesous’ inatamka ‘Yesous’ yaani Yesu. Katika lugha ya Kiarabu wanasema ‘Yasu’, kwa kiingereza ni “Jesus” maana yake ‘Bwana anaokoa au Bwana ni Mwokozi’ Isaya 43:6, 10-11.
Katika Biblia ambayo ina jumla ya Sura 1189; aya 31,102; vitabu 66 – Agano la kale vitabu 39 na agano Jipya vitabu 27; Neno Mwokozi kwa Kiingereza wanasema ‘Saviour’ limetajwa mara 55. Ikumbukwe kwamba katika agano jiypa jina Yesu au Yehoshua (kwa Kiebrania) limetajwa mara 1275 katika aya zipatazo 1226.
 
Zingatia pia kuwa agano jipya lina jumla ya aya 7930 na sura 260 hivyo hapa tunaona jina Yesu maana yake ni Mwokozi na jina Isa ni wekundu uliozidiana na weupe. Kwa kuwa maana ya haya majina tofauti bila shaka Isa sio Bwana Yesu.
 
Leo tumejifunza kwa kifupi tu kuwa, Jina la ISA lenye maana ya Wekundu unao zidiana na weupe ni TOFAUTI KABISA NA Jina la Yesu lenye maana ya MWOKOZI katika Biblia. Zaidi ya hapo, tafsir ya Jina la Yesu kwa Kiarabu ni Yasu na sio Isa kama ambavyo Waislam wanadai katika vitabu vyao.
 
UTHIBITISHO WA 2
Je, kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni sawa na Isa?
Taarifa za Malaika kabla ya kuzaliwa kwao, kadiri ya Qurani na Biblia.
Jibrili alivyomtokea Mama wa Isa == Gabrieli alivyomtokea mama wa Yesu:
WAISLAM-JIBRIL Alienda kwa Mariamu aliyekuwa Msikitini Qurani 19:16-17
WAKRISTO-GABRIEL Alienda kwa Mariamu aliyekuwa nyumbani kwake - Lk 1:26-28
WAISLAM-Mariamu Mama wa Isa haijulikani aliishi kijiji kipi wala mji gani wala hata nchi haijulikani. Isitoshe Quran inasema kuwa Jibril ndiye aliyemletea utume Muhammad asiwapelekee Mayahudi (hana kosa) Sura 2:97
WAKRISTO-Lakini Mariamu Mama yake Yesu alitokewa na Malaika Gabriel akiwa katika kijiji cha Nazareti mji wa Galilaya nchi ya Israeli (Lk 1:26) Mariamu Mama wa Yesu ni Myahudi.
WAISLAM-Jibrili hakutoa salamu kwa Mariamu mama wa Isa ila alijimithilisha kwa umbo la binadamu aliye kamili - Sura 19-17
WAKRISTO-Malaika Gabrieli alimsalimia Mariamu Mama wa Yesu – Luka 1:28
WAISLAM-Jibril alimwambia Mariamu kwamba mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe mwana mtakatifu - Sura 19-19
WAKRISTO-Lakini malaika Gabrieli alimwambia mama wa Yesu kuwa utachukua mimba – Luka1: 31
WAISLAM-Jibrili alisema kwa Mariamu kuwa ili tumfanye mtoto muujiza kwa wanadamu – Sura 19: 21. Isitoshe Jibrili hakutaja jina la mwana kwa Mariamu. Bali alisema ili nikupe mwana mtakatifu.
WAKRISTO-Malaika Gabrieli alisema kwa Mariamu mama ya Yesu kuwa mtoto jina lake utamwita Yesu (Luka 1:31; 2:21) Gabrieli hakusema kuwa atampa mwana Mariamu. Bali alisema, Roho mtakatifu atakujilia juu yako, yaani motto atazaliwa kwa uwezo wa Mungu.
 
TOFAUTI YA KUZALIWA KWA ISA NA YESUIsa bin Mariam Yesu Kristo
 
WAISLAM-Isa alizaliwa katika shina la Mtemde – 19:23
 
WAKRISTO-Yesu kazaliwa katika hori la kulishia ng’ombe. Luka 2:7
 
WAISLAM-Kuzaliwa kwa Isa haijulikani mimba ya mama yake ilichukua muda gani maana malaika Jibrili alisema nikupe mwana mtakatifu mara akachukua mimba na kuzaa. (19: 22-23)
 
WAKRISTO-Lakini Mariamu Mama wa Yesu siku zake za kuzaa zilitimia. (Luka 2:6-7)
 
WAISLAM-Qurani haionyeshi kama Isa alitabiriwa na manabii kuwa atazaliwa
 
WAKRISTO-Lakini Biblia inatuthibitishia kuwa Manabii walitabiri kuzaliwa kwa Yesu, (Isaya 7: 14; 9:6) utabiri huu ulitolewa na Nabii Isaya miaka 750 kabla ya Yesu kuja kuzaliwa nao ulitimia (Mathayo 1:18-23)
 
WAISLAM-Isa haijulikani alizaliwa katika kijiji gani wala mji, wala nchi aliyozaliwa Qurani haikueleza.
 
WAKRISTO-Biblia inatujulisha kuwa Yesu alizaliwa Bethelehemu ya Uyahudi katika Mji wa Daudi umbali wa maili 5 toka kusini mwa Yerusalemu nchi ya Israeli (Lk 2:8-16). Kuzaliwa kwake mahali hapo pia ni kutimiza unabii uliotolewa na nabii Mika miaka 750-686 kabla ya kristo kuja wakati wa wafalme hawa wakitawala – Jotham, Ahaz na Hezekia wafalme wa Yuda. Yesu mwenyewe alizaliwa kama mwaka wa 4 wakati wa Mfalme Herode.
 
WAISLAM-Isa aliongea na watu akiwa mototo mchanga, na kusema kuwa yeye ni mja wa Mungu amepewa kitabu na amefanywa Nabii (Sura 19:30-33)
 
WAKRISTO-Yesu hakuongea na mtu akiwa mtoto mchanga. Alianza kuwauliza maswali na kutoa majibu akiwa na wazee Hekaluni akiwa na miaka 12. (Luka 2: 42-49)
 
Hivyo tunaona kwamba tuna tofauti nyingi tu kati ya Bwana Yesu na Isa. Swali kwako mfuatiliaji je, Isa bin Maryamu ndiye Bwana Yesu Mwokozi? Tafakari.
 
Mungu awabariki sana na tuendelee kujifunza tofauti za Isa wa Quran na Yesu wa Biblia.
 
UTHIBITISHO WA 3
Je, Yesu ni Mwana wa Mungu?
Je, Isa bin Mariam ni Mwana wa Mungu?

Biblia inasema kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu. Katika hii mada, tuanze kwa kuangali, Je, Biblia inasema nini kuhusu Yesu? Kumbuka kuwa, Biblia ndio ilikuja kwanza kabla ya Quran. Ushahid unonyesha kuwa Biblia ilikuwepo miaka 632 kabla ya Quran kuandikwa na marafiki zake Muhammad.


YESU NI MWANA WA MUNGU

Tunaona hapa Biblia inatuambia YESU KRISTO ni Mwana wa Mungu (YOHANA 20:30-31) hapa Yesu mwenyewe anasema yeye ni Mwana wa Mungu ( MATHAYO 26:59-64; 16:13-17 ) , Neno Mwana linamzungumzia Yesu Mwana siyo kuwa Mungu anazaa la hasha

Yesu anaitwa mwana wa Mungu kwa sababu alizaliwa kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Hata sisi tumezaliwa kwa mara ya pili kwa Roho tunapo mwamini Yesu Kristo hivyo tunahesabika kuwa ni wana wa Mungu.(WAFILIPI 2:14-15,YOHANA 1:12). Kwahiyo Yesu anapoitwa Mwana wa Mungu maana yake ni chapa ya  Mungu (HUIOS) WAEBRANIA 1:1-3. Ndiyo maana hapa Yesu anawaambia wanafunzi wake, mumeniona mimi ; mumemuona Mungu, maana yake ndiyo hiyo (HUIOS) yaani chapa ya Mungu (YOHANA 14:7-9)

Tunaona hapa Yesu alisema Yeye ni Mwana wa Mungu  (YOHANA 9:35-37)
Shetani naye anajua kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu (MARKO 3:11,LUKA 4:41).
Malaika nao wanasema kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu (LUKA 1:30-35)
Mungu mwenyewe anasema kuwa Yesu ni Mwanangu mpendwa (MATHAYO 3:17,MATHAYO 17:5   )


ISA WA QURAN SIO MWANA WA MUNGU

Kama kuna jambo ambalo Allah Mungu anayeabudiwa na waislamu analikataa sana kupitia Qurani basi jambo hilo si lingine bali ni uwana wa Mungu. Allah anasema hivi.
Quani 6:101 Suratul Al-An-am [Wanyama]
Yeye ndiye Mwumba wa mbingu na ardhi. inamkinikanaje awe na mwana, hali hana mke. Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu.
Qurani 9:30 Suratul At-Tawba [Kutubu]
Na mayahudi wanasema “uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu;”na “Wakristo wanasema Masihi ni Mwana wa Mwenyezi Mungu” Haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasina na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao, Mwenyenzi Mungu uwaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa!

Allah anasema katika aya hizo hapo juu kuwa, yeye hana Mwana na kuwa Wakristo na Wayahudi wanamsingizia Allah kuwa na Mwana. Allah anasema kuwa, yeye hana Mwana kwasababu hana MKE. Ikiimanisha kuwa, Allah hana uwezo wa kuwa na Mwana bila ya kufanya tendo la ndo na Mwnamke. Huu ni ushahid tosha kuwa, Allah sio mjuzi wa yote, maana hawezi kuwa na mwana bila ya mke. 

Hebu tuangalie aya zingine za Biblia zinasema nini kuhusu Yesu.
1. Mathayo 17:5 ….Huyu ni mwanangu mpendwa wangu…
2. Malaika wa Mungu alisema hivi.
Luka 1:30-31,35
Malaika akamwambia usiogope Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu.

Hivyo Isa siyo Mwana Mungu lakini Yesu ni mwana wa Mungu. Kwa hivyo Yesu siyo Isa.

Leo tumejifuinza kwa mara nyingine tena kuwa Isa wa Quran sio Yesu wa Biblia kwa kuwa Isa wa Quran yeye sio Mwana wa Mungu.
Katika huduma yake,
UTHIBITISHO WA 4
Je, Mama wa Isa ndiye wa Yesu Kristo?
Hapo awali tumeona kuwa mama wa Isa anaitwa Maryamu, Surah 3:45 na pia mama wa Yesu anaitwa Mariamu Mathayo 1: 18-21, Marko 6: 3-4 lakini kufanana kwa majina hakuwezi kamwe kumaanisha kuwa ni mtu mmoja, kwani walio na jina hilo ni wengi. Biblia inatufundisha hivi.
 
Yohana 19:25 – Na penye Msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama, Mamaye, na ubu la mamaye Mariamu wa Klopa na Mariamu Magdalena.
 
Hapa tunaona Mariamu watatu. Ili kutambua tofauti baina ya Mariamu mama wa Isa na mama wa Yesu, lazima tulinganishe ujumbe wa Qurani na Biblia. Qurani inasimulia kuhusu baba na kaka wa Mariamu mama wa Isa hivi.
 
Suratul 66:12 – Na Maryamu mtoto wa Imrani aliyejihifadhi nafsi yake na tukampuliza humo roho yetu, (inayotokana na sisi) na akayasadikisha maneno ya mola wake, na vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu (wakubwa).
Surah 19:28 – Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati.
 
Hapa tunaona kuwa Maryamu mama wa Isa, baba yake ni Imrani na kaka yake aliitwa Haruni. Tusomapo Biblia inatueleza kuwa Amrani aliwazaa hawa:-
Hesabu 26:59 – Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni, na Musa, na Miriamu umbu lao.
Pia soma 1 Nyakati 6: 1-3 na Kutoka 6:20.

Huyo Amrani aliishi miaka mingi kabla ya Yesu na tena ametokana na kizazi cha Lawi mtoto wa watu wa mzee Yakobo. Mwanzo 29:34; Kutoka2:1-10
Ikiwa Mariamu wa Qurani baba yake ni Imrani basi atakuwa ameishi miaka 1500 kabla mama yake Yesu wa Biblia hajazaliwa!
 
Je, Mariamu mama wa Yesu ametokana na kizazi gani?Tunaposoma Biblia tunaona kwamba Yesu anaitwa mwana wa Daudi Mathayo 1:1; Marko 10:47 na Luka 1:27, 32, ndiyo maana pia Yesu anaitwa Simba wa Yuda Ufunuo 5:5. Hivyo basi ukoo aliyetoka Yusufu na Mariamu wa Yesu ni mmoja.
 
Hivyo basi Maryam wa Quran ambaye aliishi miaka 1500 kabla ya Mariam wa Biblia hakuwa mama yake Yesu. Zaidi ya hapo, Maryam wa Quran ni daya ya Musa na Haruni ambao waliishi Misri.
Leo tumeendelea kujifunza kuwa Maryam wa Quran sio na ni tofauti na Mariam wa kwenye Biblia.
Mungu awabariki sana na tuendelee kujifunza tofauti katika ya Isa wa Quran na Yesu wa Biblia.
UTHIBITISHO WA 5
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Isa wa Quran na Yesu wa Biblia. Quran inakiri kuwa Isa wake si chochote bali ni mtume tu .
 
ISA WA QURAN SI CHOCHOTE ILA NI MTUME TU
1.Qurani inasimulia kuhusu Isa bin Maryamu hivi.
Qurani 5;75 Suratul Al Maidah (Meza)
Masihi bin Maryamu “si chochote ila mtume (tu).” (Na) bila shaka mitume wengi wamepita kabla yake (Hawajaona?) na mamake ni mwanamke mkweli (na) wote wawili walikuwa wakila chakula (na kwenda choo. Basi waungu gani wanaokula na kwenda choo?) Tazama jinsi tunavyo wabainishia aya, kisha tazama jinsi wanavyogeuzwa (kuacha haki).
Hapa tunaona Quran inasimulia kuwa masihi Isa si chochote ila mtume tu. Huu ndio mtego ambao Allah anautumia kwa Waislam, eti Isa ni Yesu na Yesu si chochote bali ni mtume tu. Ili kujua kama Allah anasema ukweli, lazima tulinganishe na maneno ya Biblia ambayo ndio yana mamlaka zaidi ya Quran na yalisemwa miaka 632 kabla ya Quran kuandikwa.
 
YESU ANAMAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI
Biblia inatuambia katika Injili kutokana na Matayo kuwa:
Mathayo 28:18
Yesu akaja kwao akasema nao akawambia, “nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Yesu kwa mdomo wake anakiri kuwa Mamlaka yote ya Mbinguni na duniani amepewa yeye na haya madai ni kinyume kabisa na madai ya Allah ambayo yanasema kuwa eti Yesu si chochote kile bali ni Nabii tu. Kumbuka Yesu alisema haya maneno takribani ya miaka 632 kabla ya Allah kuja na kudai kuwa Yesu si chochote kile. Sasa, Allah alikuwa wapi miaka yote hii 632 ? Kwanini Allah asinge sema haya madai kwenye Injir na akasubiri miaka 632 baadae? Hakika Isa wa Quran sio Yesu wa Biblia.
 
Malaika Gabrieli naye anashuhudia kuwa, Yesu ni Mkuu na Mwana aliye juu.
Luka 1:30-33
Malaika akamwambia, “Usiogope Mariamu kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama utachukuwa mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyu atakuwa mkuu ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. Atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
 
Yesu na yeye anaendelea kusema kuwa, Baba alimpa Mamlaka ya wote wenye Mwili na zaidi ya hapo Yesu anakiri kuwa anao utukufu kama wa Baba yake:
Yohana 17:1-2
Maneno hayo aliyasema Yesu;akainua mikono yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba saa imekwisha kufika Mtukuze mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; kama vile ulivyompa Mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.
 
Warumi 14:9
Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii awamiliki waliokufa na walio hai pia.
Ushahdi wa aya hizo hapo juu unatuambia kuwa Yesu ana mamlaka kwa watu wote wenye mwili na pia ni mfalme wa milele. Haya madai ni kinyume kabisa na madai ya Allah katika Quran kuwa eti Yesu Kristo si chochote kile.
 
Leo tumejifuinza kwa mara nyingine tena kuwa Isa wa Quran sio Yesu wa Biblia kwa kuwa Isa wa Quran yeye si chochote ila ni mtume tu.
البحث
الأقسام
إقرأ المزيد
1 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 1 Chronicles 11
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 35 questions at the...
بواسطة THE HOLY BIBLE 2022-03-20 04:52:06 0 5كيلو بايت
FORM 1
ENGLISH : FORM 1
List of all topics in English for form 1 class: CLICK HERE TO DOWNLOAD. LISTENING TO AND...
بواسطة PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-31 17:01:23 0 6كيلو بايت
Injili Ya Yesu Kristo
YAFAHAMU MAFUNDISHO YA UONGO
(basi roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani wakiyasikiliza...
بواسطة GOSPEL PREACHER 2021-12-22 01:41:05 0 5كيلو بايت
Injili Ya Yesu Kristo
JIHADHARI USIMKATAE MUNGU KATIKA FAHAMU ZAKO
Shalom, leo nipe muda nikuonyeshe jambo muhimu sana katika safari yetu ya wokovu hapa dunia...
بواسطة GOSPEL PREACHER 2021-11-23 13:02:56 0 5كيلو بايت
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 21
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 33 questions at the...
بواسطة THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:57:57 0 5كيلو بايت