YESU ALIISHI KABLA YA DUNIA KUUMBWA

0
5K
1. Yesu asema kabla ya Abraham kuwepo yeye aliishi
2. Yesu aendelea kusema kuwa kabla ya dunia kuumbwa yeye alikuwepo.
 
Yesu anasema kuwa kabla ya Abraham kuwepo yeye alikuwepo "Niko" HEBU tusome kwanza hiyo aya:
Yohana 8: 58 Yesu akawaambia, ‘‘Amin, amin, nawaambia, kabla Abrahamu hajakuwako, ‘Mimi niko’.
 
Yesu katika Yohana 8 aya 58 anakiri na au tuambia kuwa yeye aliishi kabla ya kuzaliwa. Hivi kama kweli Yesu ni binadamu wa kawaida, itakuwaje aishi kabla ya Abraham? Hakuna Nabii au Mtume au mtu yeyote yule aliye dai kuwa aliishi kabla ya kuumbwa.
 
Endelea kusoma:
 
Yohana 17:5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.
 
Katika aya hapo juu tunasoma kuwa Yesu aliishi kabla ya kuumbwa ulimwengu. Kumbuka katika Yohana 8:58 ALISEMA KUWA ALIISHI KABLA YA ABRAHAM. Hapoa sasa anasema kwa undani zaiid, kuwa hata kabla ya kuumbwa dunia, yeye alikuwepo.
 
Kumbe basi Yesu si Nabii tuu kama ambavyo na wanavyo dai Waislam kuwa eti, Yesu ni Nabii tu na si zaidi ya hapo. Kumbe Yesu ni zaidi ya Nabii, maana aliishi kabla ya kuzaliwa.
 
Ndugu zanguni, nani aliye ishi kabla ya Uumbaji? Hata Koran inakiri kuwa, kabla ya kuumbwa kwa vitu vyote, alikuwepo Mungu. YESU ANASEMA KUWA, ALIISHI KABLA YA UUMBAJI. (Yohana 17:5).
 
Kumbe basi, Yesu ni Mungu maana alikuwepo wakati wa uumbaji. Wakolosai 1: 16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
 
Tumesoma katika Wakolosai kuwa katika Yesu kila kitu kiliumbwa na tunasoma kuwa Yesu alikuwapo kabla ya kuumbwa kwa vitu vyote, kama ilivyo semwa katika Yohana 17:5.
 
Yohana 1: 3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Katika hii aya nayo inatuambia kuwa, katika Yesu vyote vilifanyika.
 
Ndugu zanguni, ni nani huyu mwenye mamlaka haya kama sie Mungu? Iweje Yesu aishi kabla ya kuumbwa Dunia? Iweje kila kitu kiliumbwa kupitia Yesu?
 
Biblia inatuambia kuwa Mungu ndie muumbaji wa kila kitu. Biblia hiyo hiyo imetuambia kuwa kupitia Yesu, kila kitu kiliumbwa. Kumbe basi Yesu ni Mungu muumbaji.
 
Leo tumejifunza kwa ufupi tu kuwa, YESU ALIISHI KABLA YA KUUMBWA DUNIA.
 
Katika huduma yake,
 
Max Shimba Ministries
Cerca
Categorie
Leggi tutto
2 SAMUEL
Verse by verse explanation of 2 Samuel 19
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 40 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 10:01:28 0 6K
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 27
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 25 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 15:18:18 0 6K
1 KINGS
Verse by verse explanation of 1 Kings 19
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 15:55:21 0 6K
2 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 2 Chronicles 11
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 27 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-01 22:15:03 0 5K
JOB
Verse by verse explanation of Job 16
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 21 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-03 03:30:21 0 5K