YESU NI PENDO

0
5K
Shetani anataka tuamini nini kuhusu jinsi Yesu anavyotuona, lakini Yesu anatuhakikishia nini?
Hata hivyo, swali muhimu linazuka: Je, Mungu anampenda kila mmoja wetu?
Baadhi ya watu wanakubali kwamba Mungu anawapenda wanadamu kwa ujumla kama andiko la Yohana 3:16 linavyosema. Lakini wanahisi hivi: ‘Mungu hawezi kamwe kunipenda mimi.’ Shetani Ibilisi anataka sana tuamini kwamba Yesu hatupendi wala hatuthamini. Kwa upande mwingine, Yesu anatuhakikishia kuwa anamthamini kila mmoja wa watumishi wake waaminifu hata kama tunafikiri hatupendwi au hatuthaminiwi.
 
Kwa mfano, fikiria maneno ya Yesu kwenye Mathayo 10:29-31. Yesu alitoa mfano huu ili kuonyesha kwamba wanafunzi wake wana thamani: “Je, shore wawili hawauzwi kwa sarafu ya thamani ndogo? Na bado hakuna hata mmoja wao atakayeanguka kwenye ardhi bila Baba yenu kujua. Lakini nywele zenyewe za kichwa chenu zimehesabiwa zote. Kwa hiyo msiwe na hofu: nyinyi ni bora zaidi kuliko shore wengi.” Hebu fikiria jinsi wasikilizaji wa Yesu katika karne ya kwanza walivyoyaelewa maneno hayo.
 
Katika siku za Yesu, shore alikuwa ndege wa bei rahisi sana aliyenunuliwa ili kuliwa. Mtu aliyelipa sarafu moja ya thamani ndogo sana, alipewa shore wawili. Lakini kulingana na andiko la Luka 12:6, 7, baadaye Yesu alisema kwamba mtu aliyelipa sarafu mbili, alipewa shore watano badala ya shore wanne. Shore mmoja aliongezwa kana kwamba hakuwa na thamani yoyote. Huenda ndege hao hawakuwa na thamani machoni pa wanadamu, lakini Muumba aliwaonaje? Yesu alisema: “Hakuna hata mmoja wao [hata yule aliyeongezwa] hupata kusahaulika mbele ya Mungu.” Sasa huenda tumeanza kuelewa alilomaanisha Yesu. Ikiwa Mungu anamthamini sana shore mmoja, namna gani mwanadamu! Kama Yesu alivyosema, Mungu Baba anatujua vizuri sana. Kwani, hata nywele za kichwa chetu zimehesabiwa zote!
 
Kwa nini tunaweza kuwa na hakika kwamba Yesu hakutia chumvi aliposema kwamba nywele za kichwa chetu zimehesabiwa?
Huenda wengine wakafikiri kwamba Yesu alitia chumvi. Hata hivyo, hebu fikiria ufufuo. Ni lazima Mungu Baba awe anatujua vizuri sana ili aweze kutuumba upya! Anatuthamini sana hivi kwamba anakumbuka kila jambo, hata chembe zetu za urithi, kumbukumbu, na ujuzi wetu wote. Kichwa cha mtu huwa na nywele 100,000 hivi, kwa hiyo kuhesabu nywele za vichwa vyetu ni jambo rahisi sana ikilinganishwa na kukumbuka mambo hayo yote. Bila shaka, maneno hayo ya Yesu yanatuhakikishia kabisa kwamba Mungu Baba anamjali kila mmoja wetu.
 
Kisa cha Mfalme Yehoshafati kinaonyeshaje kwamba Mungu hutafuta mema ndani yetu ingawa sisi si wakamilifu?
Biblia hufunua jambo lingine linalotuhakikishia kwamba Mungu anatupenda. Yeye hutafuta na huthamini mema yaliyo ndani yetu. Kwa mfano, fikiria Mfalme Yehoshafati aliyekuwa mwema. Mfalme huyo alipotenda jambo la kipumbavu, nabii wa Mungu alimwambia hivi: “Kwa ajili ya hayo ghadhabu i juu yako itokayo kwa BWANA.” Ulikuwa ujumbe wenye kuogofya kama nini! Lakini ujumbe wa Mungu haukukomea hapo. Uliendelea kusema hivi: “Walakini yameonekana mema ndani yako.” (2 Mambo ya Nyakati 19:1-3) Kwa hiyo, hasira adilifu ya Mungu haikumzuia asione “mema” yaliyokuwa ndani ya Yehoshafati. Inatia moyo sana kujua kwamba Mungu wetu hutafuta mema ndani yetu hata ingawa sisi si wakamilifu.
 
Huruma ni sehemu nyingine ya upendo wa Yesu.
 
Huruma ni nini? Katika Biblia, huruma na rehema zinahusiana sana. Maneno kadhaa ya Kiebrania na Kigiriki yanadokeza sifa ya huruma yenye upendo. Kwa mfano, mara nyingi kitenzi cha Kiebrania ra·chamʹ hutafsiriwa “onyesha rehema” au “sikitikia.” Neno hilo la Kiebrania, ambalo Yesu anatumia kujihusu, linahusiana na neno linalomaanisha “tumbo la uzazi” linaloweza kufasiriwa kuwa “huruma ya mama.”
 
Biblia inatumia hisia ambazo mama huwa nazo kwa mtoto wake mchanga kutufundisha kuhusu huruma ya Yesu. Andiko la Isaya 49:15 linasema: “Je! mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie [ra·chamʹ] mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.” Ni vigumu kuwazia kwamba mama anaweza kusahau kumnyonyesha na kumtunza mtoto wake mchanga. Kwa kweli, mtoto mchanga ni dhaifu; anahitaji kupendwa na kutunzwa na mama yake usiku na mchana. Ingawa hivyo, inasikitisha kupata habari kuhusu akina mama wanaowatupa watoto wao, hasa katika ‘nyakati hizi za hatari.’ (2 Timotheo 3:1, 3) “Lakini mimi sitakusahau wewe,” atangaza Mungu. Huruma nyororo ya Yesu ni yenye nguvu zaidi ya hisia yenye nguvu tunayoweza kuwazia, yaani, huruma ambayo kwa kawaida mama humwonyesha mtoto wake mchanga.
 
Waisraeli walipatwa na nini katika nchi ya Misri ya kale, naye Mungu aliitikiaje kilio chao?
Mungu huonyeshaje sifa ya huruma akiwa kama mzazi mwenye upendo? Sifa hiyo ya huruma inaonekana wazi kutokana na jinsi alivyolitendea taifa la Israeli la kale. Kufikia mwisho wa karne ya 16 K.W.K., mamilioni ya Waisraeli waliteswa sana walipokuwa watumwa huko Misri. (Kutoka 1:11, 14) Waisraeli walimlilia Mungu awasaidie walipokuwa wakiteseka. Je, Mungu mwenye huruma nyororo aliitikiaje?
 
Mungu aliwahurumia. Akasema: “Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao . . . maana nayajua maumivu yao.” (Kutoka 3:7) Mungu hangeweza kuwatazama watu wake wakiteseka au kusikia vilio vyao na asiwahurumie. Yehova ni Mungu mwenye hisia-mwenzi. Nayo hisia-mwenzi, yaani, sifa ya kuguswa moyo na uchungu wa wengine, inahusiana sana na huruma. Lakini Mungu hakuwahurumia tu watu wake; alichochewa kuwasaidia. Andiko la Isaya 63:9 linasema: “Kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe.” Mungu wa Israel aliwaokoa Waisraeli kutoka Misri kwa “mkono hodari.” (Kumbukumbu la Torati 4:34) Baadaye, aliwalisha kimuujiza na kuwapa nchi yenye rutuba.
 
(a) Maneno ya mtunga-zaburi yanatuhakikishiaje kwamba Mungu anamjali sana kila mmoja wetu? 
(b) Mungu hutusaidia katika njia gani mbalimbali?
Mungu hawahurumii watumishi wake tu wakiwa kikundi. Mungu wetu mwenye upendo anamjali sana kila mmoja wetu. Anajua kabisa mateso yoyote yanayoweza kutupata. Mtunga-zaburi alisema: “Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, na masikio yake hukielekea kilio chao. BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, na waliopondeka roho huwaokoa.” (Zaburi 34:15, 18) Mungu anamsaidiaje kila mmoja wetu? Si lazima aondoe jambo linalofanya tuteseke. Lakini yeye amewapa maandalizi tele wale wanaomwomba msaada. Neno lake lina mashauri yanayofaa ambayo yanaweza kutusaidia sana. Katika kutaniko, Mungu ameweka waangalizi wanaostahili kiroho, ambao hujitahidi kuwa na huruma kama yeye wanapowasaidia waabudu wenzao. (Yakobo 5:14, 15) Akiwa “Msikiaji wa sala,” Mungu huwapa “Roho Mtakatifu wale wanaomwomba.” (Zaburi 65:2, NW; Luka 11:13) Maandalizi hayo yote ni uthibitisho wa “huruma nyororo ya Mungu wetu.”—Luka 1:78.
 
Utaitikiaje upendo wa Yesu?
Je, si jambo lenye kusisimua kutafakari juu ya upendo wa Baba yetu wa mbinguni? Katika makala iliyotangulia, tulikumbushwa kwamba Baba Mungu ameonyesha nguvu, haki, na hekima yake kwa njia ya upendo ili kutunufaisha. Na katika makala hii tumeona kwamba kwa njia ya pekee, Mungu ameonyesha upendo wake moja kwa moja kwa kila mmoja wetu na kwa wanadamu kwa ujumla. Sasa kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza, ‘Nitaitikiaje upendo wa Yesu?’ Na uitikie kwa kumpenda kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote. (Marko 12:29, 30) Maisha yako ya kila siku na yaonyeshe kwamba una tamaa ya kutoka moyoni ya kumkaribia Mungu hata zaidi. Na Yesu, Mungu ambaye ni upendo, na akukaribie hata zaidi—milele!—Yakobo 4:8.
 
Yesu ni Mungu Aliye “Tayari Kukusamehe Dhambi”
Tunapofanya dhambi tunakuwa na hisia gani zenye kulemea, lakini tunaweza kunufaikaje na msamaha wa Yesu?
 
Tunapofanya dhambi, sisi huona aibu, hukata tamaa, na kuhisi hatia na huenda hali hiyo ikafanya tufikiri kwamba hatustahili kabisa kumtumikia Mungu. Hata hivyo, kumbuka kwamba Mungu ‘amekuwa tayari kusamehe.’ (Zaburi 86:5) Naam, Yesu anaweza kutusamehe dhambi zetu tunapotubu na kujitahidi kabisa kutozirudia. Ona jinsi Biblia inavyofafanua sehemu hiyo yenye kuvutia ya upendo wa Yehova.
 
Yesu Kristo anayo amri na mamlaka ya kusamehe dhambi
 
Kuna jambo lililowahi kutokea hadi likawashangaza watu; hebu fatilia kisa hiki. Biblia Takatifu inasema kwamba:
 
“Wakaja watu wakimleta mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. Na walipokuwa hawawezi kumkaribia (Yesu) kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Na baadhi ya waandishi waliokuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?
 
Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?
 
Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi – Akamwambia yule mwenye kupooza,

Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.
Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe.” (Marko 2:3-12)
 
Kwa Wayahudi uponyaji haukuwa kitu kigeni kwao kwani hata manabii enzi za Agano la Kale nao walitumia nguvu za Mungu kuponya wagonjwa; lakini, jambo lililoonekana geni kwa Wayahudi ni kusikia Yesu amesema 
“...Umesamehewa dhambi zako...” (Marko 2:5) Kauli hiyo ya Yesu iliwafanya waone kwamba Yesu AMEKUFURU kwa maana mwenye mamlaka ya kusamehe dhambi ni Mungu pekee. Watu hao walidhani Yesu amekufuru kwa sababu hawakujua kuwa Yesu ni Mungu ingawa alikuwa ameuvaa mwili wa kibinadamu kama sisi.

Ukimpokea Yesu; anakusamehe dhambi zako zote. Haijalishi umetenda dhambi nyingi kiasi gani; haijalishi hali uliyonayo hivi sasa. Fahamu kwamba Yesu anakupenda. Neno la Mungu linasema kwamba:

“...asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji...” (Isaya 1:18)
 
Mungu huweka dhambi zetu mbali nasi kadiri gani?
Mtunga-Zaburi Daudi alitumia usemi mwingine ulio wazi zaidi kufafanua msamaha wa Mungu: “Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.” (Zaburi 103:12, italiki ni zetu.) Mashariki ni mbali kadiri gani kutoka magharibi? Katika maana fulani, sikuzote mashariki huwa mbali kabisa na magharibi; pande hizo mbili haziwezi kamwe kukutana. Msomi mmoja anasema kwamba usemi huo unamaanisha “mbali iwezekanavyo; mbali kabisa.” Maneno ya Daudi yaliyoongozwa na Roho ya Mungu yanatuambia kwamba Mungu anapotusamehe, anaweka dhambi zetu mbali kabisa nasi.
 
Kwa nini tunaweza kuwa na hakika kwamba Mungu hutuona kuwa safi baada ya kutusamehe dhambi zetu?
Je, umewahi kujaribu kuondoa doa katika nguo nyeupe? Huenda hukufaulu kuondoa doa hilo ingawa ulijitahidi kadiri unavyoweza. Ona jinsi Mungu anavyoeleza msamaha wake: “Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.” (Isaya 1:18, italiki ni zetu.) Usemi “nyekundu sana” unaonyesha kwamba rangi hiyo ni nyangavu.* Rangi “nyekundu” ilikuwa mojawapo ya rangi zilizotiwa kwenye nguo. Hatuwezi kamwe kuondoa doa la dhambi kwa jitihada zetu. Lakini Yesu anaweza kuondoa dhambi ambazo ni nyekundu sana na kuzifanya kuwa nyeupe kama theluji au sufu isiyotiwa rangi. Kwa hiyo, Yesu anapotusamehe dhambi zetu, hatupaswi kuhisi kwamba tuna hatia ya dhambi hizo maisha yetu yote.
 
Ni katika maana gani Mungu hutupa dhambi zetu nyuma yake?
Hezekia alimwambia Mungu hivi katika wimbo wa shukrani wenye kugusa moyo ambao alitunga baada ya kuponywa ugonjwa wa kufisha: “Umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.” (Isaya 38:17, italiki ni zetu.) Ni kana kwamba Mungu anachukua dhambi za mtenda-dhambi mwenye kutubu na kuzitupa nyuma Yake ambako Hawezi tena kuziona wala kuzikazia fikira. Kichapo kimoja cha kitaalamu kinasema kwamba andiko hilo linaweza kuelezwa hivi: ‘Umefanya iwe ni kana kwamba sikufanya dhambi.’ Je, hilo si jambo lenye kufariji?
 
Nabii Mika anaonyeshaje kwamba Mungu anapotusamehe Anafutilia mbali dhambi zetu daima dawamu?
Katika ahadi ya urudisho, nabii Mika alieleza usadikisho wake kwamba Mungu Yehova angewasamehe watu wake wenye kutubu: “Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye . . . kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? . . . Nawe utazitupa dhambi zao zote katika vilindi vya bahari.” (Mika 7:18, 19, italiki ni zetu.) Hebu fikiria maana ya maneno hayo kwa watu walioishi nyakati za Biblia. Haingewezekana kupata tena kitu kilichotupwa “katika vilindi vya bahari.” Kwa hiyo maneno ya Mika yanamaanisha kwamba Yesu anapotusamehe, anafutilia mbali dhambi zetu daima dawamu.
 
Yesu ni Mungu, endapo ukimpokea atakusamehe dhambi zote ulizozitenda. Yesu anakupenda sana. Hebu leo mpe Yesu maisha yako ayatawale; Yesu ataiondoa kiu hiyo ya kutenda dhambi ikufanyayo ushindwe kujizuia kuwaka tamaa mbaya za mwili wako; Yesu atakupatia ulinzi ambao utazuia pepo wachafu wasiingilie maisha yako; Yesu atakubariki na kufungua tumbo lako lililokosa mtoto kwa muda mrefu wote huo unaotaabika hata sasa; Yesu atawarejesha kwako watoto wako ambao wamekataa kukutii hata wametoweka kwako; Yesu atakupatia uzima na kuyaondoa magonjwa yote hayo yanayokutesa hata sasa; Yesu atakubariki na kukupatia uzima wa milele.

Kwa kweli nashindwa kuuelezea kwa ufasaha zaidi upendo wa Yesu juu yako kwa maana wewe ni wathamani kubwa sana mbele za Mungu. Mimi nachoweza kukwambia ni kwamba: Yesu anakupenda tena hataki upotee. Mpe Yesu maisha yako sasa ili ufurahie uzuri wa pendo Lake.
 
Ndugu yangu, wajua yakwamba Yesu Kristo anakupenda ? Wajuwa yakwamba alisulubiwa kwa ajili ya watu wote: Wanaume na Wanawake, Watoto, Vijana na Wazee?  Yesu Kristo alikufa kwa ajili yako.

Yesu anakupenda sana, inawezekana kuna mtu anakupenda sana ila Yesu anakupenda zaidi ya wote duniani hivyo nakushauri ukate shauri umfuate yeye maana atakupa kustarehe milele na kuurithi ufalme wa mbinguni pamoja naye.

TAFAKARI: “Yesu anakupenda upeo, amepoteza kila kitu, na kufa kifo cha aibu ili asikupoteze.”

JE, WEWE UPO KATIKA KUNDI HILI?
…Wewe ni mnyanganyi, mwizi, mwongo, muuaji, usiye kuwa na ukweli? Yesu anakupenda na anataka kukuponya.

JE, WEWE UPO KATIKA KUNDI HILI?
…Wewe ni mlozi mkubwa mwenye kutumikia Shetani, tangu ujana wako unazuru wanadamu wengine, unaua watoto, wanawake hata wanaume, unaharibu mavuno, unatawanya magonjwa toka jamaa kwa ingine, unaua hapa na pale.Unapopita ni woga mtupu na kukimbia mbali sababu ya mapepo mabaya yako. Mara na mara unajiuliza nini ulikuja kufanya hapa duniani, ukitafuta kujua sababu ya mabaya yote unayoyatenda. Unajiuliza namna gani uliweza kufikia hapo. Fahamu neno moja tu, hata unaishi mabaya haya yote : Yesu anakupenda na anataka kukuponya.

JE, WEWE UPO KATIKA KUNDI HILI?
…Wewe ni mkoma,tangu miguu hadi kichwani. Ulipoteza vidole, sikio, pua, ukageuka kilema kwa namna fulani; fahamu jambo hili: Yesu anakupenda na anataka kukuponya.

JE, WEWE UPO KATIKA KUNDI HILI?
… Wewe ni msichana, waonekana kuwa ni mrembo sana na wakati wako wote unavunja jamaa za wengine. Unapotosha rafiki zako za darasa, za shule lako, za ofisi ao za mtaa wako. Mara nyingine ulitoa mimba, ulitafuta kupatia wengine sumu, ao uligonganisha wapenzi wako: wamoja wafariki ao wangali wagonjwa sana sababu yako, sababu ya unyofu wako, na sura yako nzuri sana. Sasa wajiuliza mengi kuhusu maisha yako: uliweza kutambua mabaya yote uliyotenda na unajiuliza nini Mungu atakayokutendea.

 Unapatwa na woga wakati unawaza haya yote sababu unaambiwa yakuwa siku moja Mungu atahukumu matendo ya watu.Unaishi katika uasi, unajua ya kwamba JEHENAMU ndiyo inakungojea na unajifariji ukisema kwamba ni maneno yasiyokuwa na msingi hata unasema : Mungu hayuko!

…Wewe ni kijana uliyetenda mambo sawasawa na yale na mwisho ukafikia kusema hivyo. Unajitia kwa mstari ya wale wasiosadiki kuwa Mungu yuko, ili ujitulize.

Ndugu yangu, rafiki yangu, Shetani anakupoteza. Unajuwa ni nini inayokungojea. Hata ikiwa hivyo, ninataka kukujulisha ya kwamba wakati ungali wa kugeuza yale yote, kwani katika upendo wake Mungu alituma Mwana wake wa pekee ili akuondoshe katika maisha yale. Yesu anakupenda, anataka akuokowe kwa damu yake na uwe safi mbele ya Mungu.

…Wewe ni mwanaume, mwanamke, mtoto unayelala kitandani katika hospitali sababu ya ugonjwa, ya msiba wa barabarani, ya ulozi; ili ujue neno hili: Yesu ni karibu yako na anakupenda na anataka akuponye.

… Ulifanya kosa fulani na kwa sasa unapatikana katika mateso ya gereza: Yesu anapatikana hapo kwa kukuponya.
…Wewe ni mtumishi, kiongozi, uliyepata cheo kikubwa kwa njia ya madawa na ulozi, kuua na kusengenya, uongo na vibaruwa vya uongo: ulipita juu ya wengine ili ufikiye pahali ulipo, sasa maneno haya ni mkononi mwako: usifikiliye ni kwa bahati tu. Yesu anakuambia ya kwamba anakupenda hata ulipitia kwa njia hizo. Ulisoma mistari hii na unashangaa ukigundua kwamba hata ukiwa mwenye kutenda mabaya kama hayo, Yesu anakupenda pia.
Sikiliza anayosema Mwokozi wako:

“Watu wenye afia njema hawahitaji muganga, ila wenye ugonjwa tu.. Sikuja kuita wenye haki bali wenye zambi”( Marko 2.17) .
Unasikia hayo? Yesu anasema ya kwamba alikuja kwa ajili ya watu kama wewe.Unaona mlango wa kutoka mahali ulipo sasa, ni Yesu Kristo mwenyewe.

…Mara nyingine wasema: mimi si Muisraeli anayeambiwa maneno hayo ya Yesu ! Mimi ni Muafrika, Muasia,Muamerika…jua ya kwamba maneno hayo ni kwako pia na usikilize asemayo:
“Muniangalie, na muokolewe, miisho yote ya dunia;kwani mimi ni Mungu,na hapana mwengine.” ( Isaya 45:22).

Wasikia zaidi ya hayo? Ulizani kwamba ulifikia mwisho, ukitesa wanadamu wengine, unajisikia hakuna tena kukaribia Mungu. Ulisema haya na yale kuhusu zambi zako. Na Yesu anakuambia:
“Leo kama mtasikia sauti yangu, msifanye migumu mioyo yenu.”( Waebrania 4.7).

Una maneno haya mkononi mwako, jua ya kwamba ndiyo “leo” yako hii na Mungu anasema: Usifanye moyo wako kuwa mgumu.
Kwa kumaliza, Roho Mtakatifu anakupa ujumbe huu:

“Basisisi,! Tutapona namna gani, tusipochunga wokovu mkubwa namna huu?” (Waebrania 2.3).

Ndugu, rafiki, wajua sasa ya kwamba Mungu anakupenda, wajuwa kuwa Mwana wake Yesu ni tayari kukuponya. Haupatikane tena katika kutokujua. Mungu anataka kukufungua macho kwa maneno haya na anasema:

“Kwa maana Mungu alivyopenda ulimwengu, hata kutoa Mwana wake wa pekee, ili kila mtu akimwamini asipotee, bali apate uzima wa milele” (Yoane 3.16).

Chaguo ni lako: amini na uokolewe ao kutoamini na kuhukumiwa. Ndiyo, katika neema yake kubwa, Mungu anakuonyesha wazi njia ya kupitia. Anasema:

“Nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; kwa hivi chagua uzima ili uwe hai.” (Kumbukumbu la torati 30.19).
Unapenda kumusikia Mungu? Ama kama asemavyo mtume Paulo:
“Ao unazarau utajiri wa wema wake na saburi na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu unakupeleka kwa toba? Lakini kwa ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya asira kwa siku ile ya asira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu” (Warumi 2.4-5), na inaandikiwa tena “Basi, zamani wakati huu wa ujinga, Mungu hakuangalia ; lakini sasa anaamuru watu wote wa kila mahali watubu. Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki,kwa mtu yule aliyemuweka kwa kazi hii; naye amewapa watu wote hakika ya mambo haya kwa kumfufua toka wafu” (Matendo ya mitume 17.30-31).

Pamoja na mtume Paulo:
“Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kama kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu” (2 Wakorintho 5.20) kabla wakati haujapita.

Pokea upatanishi unaopewa na Mungu. Kwa hivyo unaombwa kukiri makosa yako, ukitambua ya kwamba wewe ni mwenye zambi.
 
Damu ya Yesu inamamlaka ya kusafisha dhambi zako zote.
 
Mpokee Yesu sasa na upate msamaha wa dhambi.
 
Yesu anakupenda.
Site içinde arama yapın
Kategoriler
Read More
NDOA KIBIBLIA
MWANAUME UKIKOSA UNYENYEKEVU MKE ATAKUSHINDA
Unyenyekevu ni tabia ya kujishusha na kuvaa kiatu cha aliye chini yako; unavua heshima na utukufu...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-08 00:12:34 3 6K
Injili Ya Yesu Kristo
KUANDAA MAHUBIRI
Malengo ya mada. Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi ataweza. Kueleza maana yamahubiri. Kueleza...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-06 08:55:11 0 8K
MASWALI & MAJIBU
Nini Maana Ya Kusali Kwa Kupayuka Payuka?
Swali linaendelea…..Na Je, nisali kwa namna gani ili maombi yangu yasionekane kuwa ni ya...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-13 08:11:49 0 5K
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Deuteronomy 28
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 73 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 06:45:59 0 6K
NDOA KIBIBLIA
KUISHI NA MWANAMKE ALIYEKUZIDI KIPATO, MALI AU CHEO.
Hiki ni kipindi cha hatari sana, wanawake wengi wanapigania haki sawa. Harakati za wanawake...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-06 12:53:27 0 5K